Nami nakemea vikali hiyo tabia ya wanaume kujisaidia hapa na pale bila hata kujali nani anapita au watoto watacheza hapo!
*******************************************************************************
DC akoromea Wanaosumbua wenzao kwa Mikesha
2008-04-08
Na Abdul Mitumba, Magomeni
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Jijini, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, ameagiza watu wote wanaokesha wakipiga na kucheza muziki wa rusha roho na aina nyingine za muziki kwa sauti ya juu kiasi cha kuwasumbua wengine wakome kufanya hivyo na kwamba kuanzia sasa wawe wakiburuzwa kortini kwani wanavunja sheria za nchi.
Kadhalika, DC Massawe amechukizwa na tabia ya wanaume wengi kujisaidia aja ndogo kila sehemu akisema ni baadhi ya dalili za kuporomoka kwa maadili miongoni mwa jamii. Bw. Massawe ameyasema hayo wakati wa mkutano wake mmoja na wananchi wa Kata ya Ndugumbi hivi karibuni.
Mkuu huyo amesema sheria za namna watu wanavyoweza kufanya sherehe majumbani mwao na hata zile zinazoelezea utaratibu wa shughuli za starehe ziko wazi na kila mmoja anapaswa kuzifuata. Akasema kamwe hairuhusiwi watu kukesha wakicheza muziki usiku kucha, tena kwa sauti ya juu kiasi cha kuwasumbua wengine.
Mbali na hayo, DC Massawe pia alikemea tabia ya baadhi ya watu wanaotiririsha maji machafu na kinyesi katika mifereji ya mvua. ``Matukio yote hayo ni mwanzo wa matatizo katika jamii. Kupiga muziki usiku kucha katika makazi ya watu ni tatizo linalokemewa kila siku na ninasisitiza kuwa sasa sheria zifuatwe... kujisaidia ovyo mitaani ni aibu nyingine ambayo jamii inapaswa kuikemea ili kujenga kuwa na kizazi kilichostaarabika,`` akasema DC Massawe.
Agizo la Kanali Massawe limekuja kufuatia baadhi ya wananchi kutoa kero mkutanoni hapo, ambapo kero iliyotawala mkutano ni tabia ya baadhi ya watu kukesha wakipiga muziki katika makazi ya watu.
SOURCE: Alasiri

11 comments:
Loh Da Chemi utasutwa! Acha umbea, alokwambia huyo anakojoa nani? Unaushahidi gani kwamba huo ni mkojo? umeona uume unaotoa mkojo hapo? Kama anakichupa cha maji jee anakikamua? Dont judge a book by its cover...
tuliza mpira uwanja uwanja mkubwa tena mpira wenyewe hata hautangazwi redioni
we unaona yuko mashambani hata kama anakojoa kwa akili yako unadhani kutakuwa na choo hapo?
be realistic onyesha picha yenye choo hapo halafu mtu anakojoa pembeni kwenye majani halafu ndo ukorome
Yaani wanaume wamezidi. Wanatoa dudu lao popote na kukojoa bila hata haya!
Wewe anony 719, Sasa kama ni shamba ndo ruksa kukojoa ovyo! Watu si wanakula matunda ya shambani? AU wewe unapenda kula vinyesi na mikojo?
Sema Da Chemi! Usiogope Sema!
Inasemekana hii global warming imezidi, kwa sababu moja kwamba watu hawafanyi haja zao vichakani kama hapo zamani, kuwezesha hii mimea kupata rutuba, e.g. mbolea inayotokana na mkojo kama sulphur, na rutuba nyingi inayopatikana na kinyesi vya watu na wanyama.
Kwa hiyo mimea inakufa kama tunavyoona hivi sasa, na hivyo kusababisha global warming.
LOL
sitetei tabia hiyo mbaya, lakini ukosefu mkubwa wa vyoo hasa maeneo ya mjini nao unachangia kwa kiasi kubwa kwa watu kujisaidia maeneo yasiyohusika. na wanawake wengi wanashindwa kujisaidia hadharani kwa sababu za kimaumbile.
Wee chemi kaa kimya,sababu inayowafanya wanawake wasikojoe mahala kama hapo ni kwamba hawawezi kukojoa wima, wao mpaka wachuchumae.
Mwagilia shamba hilo kamanda juu hapo.
Si wasifii wafanyao hivyo hapa !
Ila ukweli ni rahisi kwa wanaume kujisitiri popote haja ndogo kuliko wanawake, labda ndio maana wanaonekana zaidi.
Na vyoo vingine ukiingia, labda uwe umebeba Perfume yako, la sivyo unaanza kunukia choo.
Cha kusikitisha ni kwamba watu hujisaidia mpaka kwenye vyanzo vya maji kitu kisababishacho uchafuzi wa maji hat ya kupikia dagaa nyumbani.
Mikojo na Vinyesi ya binadamu inaunguza mimea! Hebu tazama shemeu ambazo watu wanatumia ovyo. Mimea imekufa!
Kukojoa au kunya njiani au kwenye kuta za nyumba huo ni uchafu, tabia hiyo ikomeshwe kwani ina hatarisha afya za watu hasa watoto.
Huo si mkojo ni sehemu ya mmea! Keshamaliza umebakia wa kudondoka dondoka!
Huku kwetu vijijini, kama huko kwenu vijijini, hatukuwa na vyoo! Na kama kuna kitu kizuri kuhusu Vijiji vya Ujamaa, mbali na kulinda usalama wa raia, ni kule kuwalazimisha watu wachimbe vyoo na wavitumie!
Vijiji raised the level of environmental sanitation kwa kiasi kikubwa!
Post a Comment