Saturday, March 15, 2008

Mwanamke akaa kwenye choo miaka miwili!

Trailer ya Tukio huko Wichita, Kansas


Wadau hii story itakutia kichefuchefu, hivyo halahala mkisoma.
Juzi tulisikia habari ya mwanamke fulani huko Kansas aliyekutwa amekaa kwenye choo miaka miwili. Pam Babcock (35) alikutwa kwenye choo ndani ya trela ya boyfriend wake. EMT's walipofika kumhudumia walikuta trela inanuka harufu mbaya mno na huyo Pam kaganda kwenye choo hawezi hata kuinuka! Kumbe nyama ya matako yake ilianza kuota kuzunguka hiyo kiti cha choo!
EMT's walipofika alikataa kuhudumiwa akisema ni mzima na hana shida. Baadaye alikubali msaada wao.

Ilibidi wabandue kiti kwenye choo na kumpeleka hospitalini hivyo hivyo imenasa matakoni! Wanasema kuwa huyo mama aliuwa hajaoga wala hajaosha nywele zake muda wote huo hivyo harufu ilikuwa balaa.
Pia matako yake yalikuwa yamejaa vidonda! Madaktari wanasema kuwa miguu yake ime 'atrophy' yaani misuli imekwisha maana alikuwa hatembee. Wanasema huenda hatatembea tena na itabidi atembee kwa kiti maalum.
Boyfriend wake alisema kuwa eti alikuwa anatoka kwenye choo anaoga na kubadilisha nguo zake, lakini kwa hali wale EMT's na polisi waliyokuta wanampinga! Boyfriend wake anasema kuwa alikuwa anamwomba atoke chooni kila siku na alikuwa anajibu, "labda kesho". Ina maana alikuwa anakula chakula na kulala hapo hapo kwenye choo!

Sasa jamani, hicho choo kilikuwa hakisafishwi hivyo ilikuwa imejaa vinyesi na wadudu! Huyo boyfriend wake alikuwa anajisaidia wapi miaka yote miwili?

Huenda huyo boyfriend atafunguliwa mashitaka kwa kutomkutafutia huyo mwanamke msaada mapema!
Kwa habari zaidi someni:


Kuona video BOFYA HAPA

4 comments:

Anonymous said...

Huyo mama lazima ana ugonjwa wa akili! Si bure.

Anonymous said...

Once again guiness has sthg to add in their book.

Think even tht beau has a mental breakdown, he needs a medical attention.

Anonymous said...

ufisadi mwingine bongo
BAADA ya taifa kutikiswa na ufisadi wa kutisha wa uporaji fedha za umma uliosababisha kuyumba kwa uchumi, mtiririko wa matukio hayo umegeuka, na sasa umeanza kutishia uhai wa Watanzania.
Taarifa za karibuni zilizothibitishwa na viongozi wa juu serikalini zinasema kuwa mamilioni ya Watanzania waliopima maambukizi ya virusi vya ukimwi majibu yao si sahihi kwa sababu vifaa vilivyotumika kuwapima havikuwa na ubora unastahili.

Wakati serikali ikitangaza hatari hiyo, taarifa nyingine kutoka ndani ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASCO) zimeeleza kuwa zaidi ya Watanzania milioni 15 wanaotumia maji yanayosambazwa kutoka mtambo wa Ruvu Chini wako hatarini kupoteza maisha baada ya baadhi ya wafanyakazi wa mtambo huo kutangaza azma yao ya kuweka sumu katika mitambo inayosambaza maji kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Kitisho hiki, pia kimethibitishwa na Menejimenti ya DAWASCO iliyokiri kupokea barua ya wafanyakazi wa mtambo huo, inayomtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Mark Mwandosya kuwarudisha kazini katika kipindi cha wiki moja wenzao waliofukuzwa kwa tuhuma za kukiuka taratibu za kazi, kabla hawajatia sumu kwenye mitambo inayosambaza maji hayo.

Matukio haya mawili makubwa yalitokea mwishoni mwa wiki hii.

Tukio la kwanza, serikali imekiri kuwa mashine za kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) zinazofahamika kitaalamu kwa majina ya ‘Capillus na Cyflow CD4’ hazina ubora unaotakikana, hivyo waliopima majibu yao si sahihi.

Kauli hiyo ya serikali ilitolewa jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa kwa waandishi wa habari ikiwa ni siku chache baada ya kupokea majibu ya tume iliyochunguza vifaa hivyo.

Prof. Mwakyusa alilazimika kuunda tume hiyo baada ya mzabuni aliyeleta vifaa hivyo kuituhumu wizara yake kuwa ilipokea rushwa ili vifaa hivyo vionekane batili na zabuni hiyo itolewe kwa mtu mwingine.

Akitoa taarifa ya uchunguzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya Muhimbili (MUHAS), alisema umebaini kuwa vifaa hivyo havina ubora, hivyo kuwapo kwa uwezekano mkubwa kwa wagonjwa waliopimwa ukimwi na VVU kwa kutumia vifaa hivyo au waliopima CD4, kupewa majibu yasiyo sahihi.

Prof. Mwakyusa alisema baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi uliofanywa na MUHAS aliamua kuunda tume ya kuchunguza tuhuma hizo kwa uzito wake kuwa kama ni za kweli, basi maisha ya maelfu ya Watanzania wanaougua ugonjwa huo yalikuwa hatarini.

Aliwataja wajumbe wa tume hiyo kuwa ni Profesa Philip Hiza, Mganga Mkuu wa Serikali mstaafu, Profesa Raphael Lema, Consultant Pathologist mstaafu, Dk. Juma Madati, Mkemia Mkuu wa Serikali mstaafu.

Alisema tume aliyoiunda ilianza kazi kwa kuzifanyia kazi tuhuma zilizotolewa na mzabuni wa vifaa hivyo, Roland Gohde, aliyeingiza vifaa hivyo nchini kwa kushirikiana na mtoto wake, Wolfang Gohde pamoja na Mtanzania mmoja aliyetajwa kwa jina la Dk. Mbawala mkazi wa Dar es Salaam.

Prof Mwakyusa alisema taarifa ya tume hiyo ilionyesha kuwa, vifaa hivyo havikuwa feki bali viliharibika baada ya kuwekwa sehemu yenye joto kwa muda mrefu.

Aidha, tume hiyo pia ilibaini kuwa historia ya Prof. Gohde ilionyesha kuwa ni mstaafu wa Chuo Kikuu cha Muster cha nchini Ujerumani ni mshauri wa Kampuni ya Partec inayotengeneza kifaa cha Cyflow na pia ndiye aliyeleta vifaa hivyo hapa nchini wakati akiwa hana utaalamu wa kutengeza kifaa hicho.

Kwamba historia hiyo ilionyesha wazi kuwa Prof. Gohde hakuwa na sifa ya kuwa mshauri wa kampuni hiyo kwa sababu si mtaalamu wa vifaa hivyo, hivyo hakuwa na sifa ya kuvileta.

Alisema ripoti ya tume hiyo ilibainisha kuwa, tuhuma ilizotupiwa wizara za kucheleweshwa kwa makusudi kwa vifaa hivyo hadi vikaharibika si za kweli kwa sababu viliagizwa nchini kwa jina la Katibu Mkuu aliyepita (hakumtaja jina) na si wizara.

“Hata hivyo, tume ilichunguza na kuona kuwa kuna ukweli ndani yake, vifaa hivyo vilicheleweshwa mara mbili, lakini ni kutokana na kuingizwa nchini kwa jina la mtu binafsi na si kiofisi ndiyo vilicheleweshwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa zaidi ya miezi miwili jambo lililosababisha viharibike.

“Kutokana na hilo, taarifa za ujio wa vifaa hivyo zilichelewa kutolewa tangu vilipoingia uwanja wa ndege, kwenda wizarani hadi kufika katika bohari la serikali la kuhifadhi dawa (MSD) ambalo ndiyo ‘Clearing agent’ wa wizara,” alisema Prof Mwakyusa.

Alisema ucheleweshwaji wa pili ulichukua miezi saba baada ya mashine kufikishwa MUHAS ambako zilikaa bila kuchunguzwa kwa kukosa vitendanishi hadi vilipowasilishwa vikiwa vimechelewa.

Alikanusha uzembe huo kufanywa na wataalamu wa MUHAS na kueleza kuwa lilikuwa jukumu la wasambazaji wa vifaa na Bodi ya Maabara ya Umma (PHLB) iliyokuwa na jukumu la kuleta vitendanishi.

“Hata hivyo, baada ya vitendanishi kuwasili, iligundulika kwamba vifaa hivyo vilikuwa na kasoro ambayo ilibidi Mhandisi wa Partec aitwe kutoka Nairobi Kenya kuja kuvirekebisha, jambo lililochangia ucheleweshwaji kuvichunguza,” aliendelea kufafanua Prof Mwakyusa.

Sababu nyingine ya kuchelewesha kufanyika kwa utafiti wa vifaa hivyo iliyotolewa na Prof. Mwakyusa ni uchunguzi wake kuchukua wiki sita kukamilika na kwamba mwakilishi wa Kampuni ya Partec, Dk. Mbawala, aliwaudhi wanasayansi kwa sababu ya kutojiamini hali iliyomfanya kwenda kila wakati katika maabara vilikohifadhiwa vifaa hivyo.

“Kwenda kwenda kila mara MUHAS wakati uchunguzi ukiendelea, jambo hilo liliwaudhi wanasayansi hao kwa kuwa si utaratibu wala kanuni zinazozingatiwa katika kufanya uchunguzi huo,” alisema Prof Mwakyusa.

Aliendelea kueleza kuwa, tume iligundua kuwa kulikuwa na vitendanishi vya aina tatu ambavyo ni Calibration beads vilivyoisha muda wake tangu Oktoba mwaka 2005, Dilution Buffer vilivyoisha muda tangu Desemba 2005 na Easy Count CD4PE vilivyoisha muda wake tangu Februari 2006.

Kwamba uchunguzi kwa kutumia vitendanishi ulikamilika Septemba 30 mwaka 2005 jambo linaloonyesha kuwa vilikuwa bado ndani ya muda ila vifaa havikuwa salama.

Alisema matokeo ya tume hiyo pia yalibaini udhaifu kwa Patrec ambao ni wazalishaji wa vifaa hivyo kuwa hawakuwa makini katika kufuatilia usafirishaji na utunzaji wake kutoka vilipotumwa hadi kuwasili maabara ya uchunguzi.

Alieleza wasiwasi na mshangao kwa nchi zinazotengeneza vifaa hivyo kupenda kuingiza vifaa hivyo kwa wingi katika nchi zinazoendelea.

“Mimi nashangaa kwa nini vipimo hivi viwepo katika nchi zinazoendelea kwa wingi - Nigeria, Ghana, Uganda na Sudan na si katika nchi zilizoendelea za bara la Ulaya. Hapa kuna walakini kidogo,” alisema.

Alisema kutokana na shaka iliyojionyesha kuhusu vifaa hivyo, serikali imepiga marufuku uingizwaji wake hapa nchini na kuongeza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wanaoviingiza kinyume cha taratibu.

Wakati hali ikiwa hivyo katika Wizara ya Afya, huko Dawasco nako, tishio hilo la wafanyakazi lililofikishwa mezani kwa Waziri Mwandosya, linakuja wakati taifa likipita katika kipindi kigumu cha kukabiliana na kashfa mbili kubwa zilizogharimu uchumi wa taifa, Richmond na EPA.

Wafanyakazi walioandika barua pasipo kuweka majina yao wanasema kufukuzwa kwa wenzao hao hakukuwa kwa utaratibu maalumu, bali kulitokana na mipango iliyopangwa na Mkurugenzi Mkuu wa DAWASCO makao makuu, akishirikiana na Meneja wa Mtambo huo.

Katika barua hiyo, walieleza kuwa, iwapo waziri hataizingatia atashuhudia matokeo ya kuwapoteza Watanzania wengi wasio na hatia kutokana na utendaji mbovu wa meneja wa mtambo pamoja na mkurugenzi wake.

Katika barua hiyo, wafanyakazi hao walidai kuwa, baada ya wenzao kufukuzwa wamekuwa wakifuatilia jambo hilo na kubaini kuwa ni njama za Mkurugenzi Mkuu wa DAWASCO za kutaka kuwaondoa wafanyakazi wote wa zamani wenye ajira ya kudumu.

Kwa mujibu wa wafanyakazi hao, habari walizonazo zinaeleza kuwa mameneja waliopewa kazi hiyo wameahidiwa kulipwa zawadi ya shilingi milioni tano kama akiikamilisha kazi hiyo.

“Kilichobaki ni kulipiza kisasi, tunajua ndugu zetu watakufa, lakini kwa hili heri lawama kuliko fedheha. Vyombo vya habari vitaripoti ni lazima tuweke sumu, hatuna mzaha vinginevyo wenzetu warudishwe kazini,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Akizungumza na maofisa kutoka DAWASCO makao makuu waliokuwa wameambatana na makachero kadhaa wa polisi, Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Joseph Bamwezaki alisema alikuwa hana taarifa juu ya barua hiyo.

Naye Meneja wa DAWASCO makao makuu, Elias Kasitila alisema kuwa, mkurugenzi wake amepata barua hiyo juzi na kwamba siku hiyo hiyo walimuomba ofisa upelelezi kwenda naye eneo la tukio ili kuona ni jinsi gani wataimarisha ulinzi kuokoa maisha ya Watanzania.

Meneja uhusiano wa DAWASCO, Badra Masoud alieleza kuwa, taarifa hizo zimekwishaufikia uongozi wa juu wa mamlaka hiyo na umekwishawasiliana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuhakikisha jambo hilo halitokei.

Anonymous said...

sasa alikuwa anakula vipi,wallaah dunia hadaa ulimwengu shujaa.