Thursday, April 19, 2007

Kibira Films bado wanamtafuta 'Juma'!

Bado actor anatafutwa kwa ajili ya kuigiza kama mhusika mkuu wa sinema ya Bongoland 2!

WHERE IN THE WORLD IS JUMA.....

We cannot find him and this is why this weekend on Saturday April 21, 2007 we are conducting a screen test.A screen test of the would be Juma - the lead actor for the movie...Bongoland II. If you are game and think you can act here is the venue...Holy Trinity Lutheran Church in Minneapolis - the address is 27 EAST 31st Street.

The screen test will start at 10:00 AM. Please check our site for the updates on the outcome.


Kwa habari zaidi bonyeza hapa: BONGOLAND 2

Kwaheri Sanjaya!









American Idol Judges Randy Jackson, Simon Cowell, & Paula Abdul

Kwa wapenzi wa American Idol naomba maoni yenu. Huyu kijana Sanjaya aliwezaje kukaa kwenye American Idol kwa muda wote huo? Jana alivyotolewa nilibakia nashabikia kwa furaha maana hakustahili kufika hadi kuwa namba 7 kati ya waimbaji kumi na wawili bora.

Sanjaya ni shombe wa kihindi kutoka Washington State. Ana miaka 17. Mama yake ni mzungu na baba yake ni mhindi. Ana nywele nyingi nyeusi, na sauti yake ni ndogo na ya kike kike kama ya Michael Jackson. Anaweza kuimba nyimbo za stevie wonder vizuri. Akiimba wasichana wadogo wadogo wanaanza kulia shauri ya kuingiliwa na kiwewe fulani. Watu wanasema baba yake kamfanyia dawa za kihindi maana hana sauti ya kuwa American Idol.

Watu kama Howard Stern na wengine wenye chuki walifanya kampeni za kupata watu wa kumpigia kura ili ashinde. Mungu ni mwema na wameshindwa! Sanjaya katoka jana kwa majonzi. Alivyoambiwa ndo siku yake ya mwisho, alibakia analia kama mtoto mdogo.
Kitu kilichowafanya wasichana wadogo wadogo wampende ni, kutabasamu kwake, nywele nyingi (kila wiki alibadilisha staili ya nywele), na eti ana sura nzuri yaani handsome. Lakini kuimba hawezi. Watu waliokuwa wanaimba vizuri kama Stephanie Edwards, Brandon na Gina Glocksen walitolewa kabla yake.

Picha aliyepiga dada yake, Shyamali, akiwa uchi huko anapiga gitaa ilimsaidia pia. Shyamali aliwahi kufanya kazi kwenye restaurant ya Hooters. Alitolewa zamani wakati walivyobakia waimbaji 48.
Bora hakushinda maana kuendelea kuwepo kwake ungehatarisha maisha yake, maana nchi hii kuna vichaa. Angepigwa risasi na mtu mwenye chuki eti kawa nini Sanjaya anaharibu show.

Na leo naamini kuwa producers wa American Idol wanapumua vizuri. Maana Sanjaya angeshinda ingekuwa mwisho wa American Idol maana ushindi wake ungehibitisha kuwa American idol siyo kamchagua anayejua kuimba, bali anayependwa na watu.

Lakini huo si mwisho wa Sanjaya. Kwa vile kapendwa sana lazima tutamwona kwenye matangazo ya TV, au akiigiza kwenye sinema za mateenager.

Wednesday, April 18, 2007

Mauji Chuo Kikuu cha Virginia Tech


Sura ya Muaji Cho Seung-Hui

Poleni waKorea wote. Sasa asante Cho Seung-Hui, itakuwa vigumu wapate visa za kuja kusoma Marekani bila kuchambuliwa kila kitu toka walichofanya toka wazaliwe mpaka wanakunya saa ngapi.

WaMarekani waoga sana na wabaguzi sana na sasa wamepata kisingizio cha kunyanyasa waKorea wote Marekani. Msisahau kabla ya 9/11 jinsi waarabu walivyokuwa wanathaminiwa Marekani shauri ya pesa zao.

Kama hamjasikia, vituko na visa vya kijana, Cho Seung-Hui, mwenye miaka 23, na mwanafunzi aliyekuwa anasoma Chuo Kikuu cha Virginia Tech nitawasimulia kwa ufupi. Siku ya jumatatu akili zilimruka na aliua wanafunzi na walimu wa chuoni hapo. Watu 32, walioamka na kufanya shughuli zao kama kawaida siku hiyo walipoteza maisha yao.

Cha ajabu, watu walijua kuwa huyo jamaa ni mwendawazimu siku nyingi. Hata mwalimu wake alienda polisi kumshitaki kuwa ana wasiwasi naye. Lakini polisi hawakufanya kitu.
Na wote tunajua mweusi angekuwa na vituko kama vyake, angefukuzwa shule zamani. Cho alikuwa anadika michezo ya kuigiza na mashairi zenye plots za kutisha kama kubaka, kuua, na kujiua.

Nani asiyejue kuwa waMarekani wanasema kuwa hao wenye asili ya Asia wana akili sana. Na si ajabu ndo maana huyo Bwana John Markell, alimwuzia bastola bila maswali mengi. Alisema, “he looked like a clean cut College student”, yaani alionekana hana matatizo. Je, kijana mweusi anayesoma Chuo Kikuu angeweza kununua bastola kwenye duka lake kwa urahisi hivyo? Na leo asubuhi nilikuwa nabishana na bosi wangu kuhusu hiyo swala, nikamwambia, huyo Markell asingeniuzia mimi mwanamke mweusi hiyo bastola, lazima angetafuta kisingizio cha kutokuniuzia maana sionekani kama clean cut college student au clean cut period.

Kati ya hao waliouliwa siku ya jumatatu kulikuwa na weusi kadhaa. Mmoja ni Ryan Clark, aliyekuwa na akili sana na kusoma Major tatu (haya nyie wazungu mnaosema kuwa weusi hawana akili). http://www.wrdw.com/news/headlines/7071667.html

Na jambo lingine kinachoniudhi. Wansema kuwa haya ndo mauaji makuu yaliyowahi kutokea nchini Marekani. Wamekosea, au wansema hivyo kwa vile weusi siyo watu kwao. Miaka ya nyuma huko Florida (1923) walikuwa mamia ya weusi, na mauaji ya weusi yalitokea Arkansas (1919) na Oklahoma (1921) pia.

Karibuni mtoe maoni yenu.

Saturday, April 14, 2007

Marudio - Acheni Ushamba

Hii ni kati ya posts zangu za mwanzo:

Tuesday, October 18, 2005

Acheni Ushamba! Jamani, jamani, jamani! Siku hizi nikiona vijana waBongo hapa mitaani Boston nakimbia! Hao vijana siyo wale wa miaka ya nyuma waliokuwa tayari kufanya kazi mbili/tatu ili waweze kuishi vizuri na kupeleka zawadi nyumbani. Hapana vijana wa siku hizi wanataka vya dezo!

Wamekuja Marekani wakidhania maisha USA ni kama vile kwenye video za Rap. Hapana vijana, maisha siyo hivyo kabisa. Hapa USA kama hukuja na hela zako basi uwe tayari kuchapa hizo kazi mbili/tatu, utafanikiwa! Lakini kinacho niudhi hasa ni hao vijana wanaoenda madukani na kuiba, yaani shoplifting! Yaani mtu anaingia dukani anasomba vitu, tia ma-cap kichwani halafu wanatoka nje ya duka. Wanakamatwa halafu unaombwa uwawekee dhamana! Si waliiba wao wacha wakome huko jela! Tena jela za Boston ni nzuri kuliko kupelekwa Keko! Nasema hao vijana ni washamba maana ukiwauliza kwa nini waliiba, watasema, “Oh, sikujua kama wananiona!” Hawakuoni???? Heh!

Mjue mkifika kwenye mall tena parking lot, mnaanza kuchgunguzwa na makamera yaliofichawa kila mahala isipokuwa chooni! Yale mapambo na magololi yanayoing’inia si urembo tu, bali ni masecurity camera. Hivyo huwezi kusema, “Oh sikuiba!” huko store detective anakutolea kanda ya video ambacho wewe ndo star!

Wanaona kwa vile mlango huko wazi hakuna security, au watu wengi basi ni free for all. Kitu kingine hao vijana,utasikia wanaongea, sijui vitu gani, wakidhania English! Wanajaribu kuiga ma-slang wanaosikia kwenye movies. Nyie! Watu hawaongei hivyo!

Ukitaka kazi ya maana ujfinze kuongea English! Yaani inatisha maana huwezi hata kuelewa ansemaje na Slang zake zenye Bongo accent! Na acheni kuvaa kama gangsta! Kwanza ukikosea rangi utapigwa risasi na ma-gang au utasumbuliwa na polisi wakidhania wewe ni gang banga!

Na poleni vijana ambao wanashuka kwenye ndege wakidhania wanaenda kuishi kwenye nyumba inayofanana na ya P. Diddy, lakini wanakuta wanaenda kubanana watu 10 kwenye chumba kimoja.

Na kuna wengine wanafanya uhalifu kama kuingia kwenye biashara haramu ili wapate pesa za haraka. Sijui ni kwa kuwa hawajui au hawajali,lakini wanhatarish maisha yao na za familia na marafiki zao!

Ngoja niishie hapa ...maana!

Bongoland 2


(Photos courtesy of Muhidini Michuzi)

Naona Kibira Films International inasonga mbele na maandalizi ya kupiga picha ya Bongoland 2, Tanzania mwezi Julai. Wasanii nchini Tanzania wanatoka kwa wingi kujaribu kupata nafasi ya kuigiza katika hiyo sinema. Katika picha za juu, ni baadhi ya wasanii waliotokea kwenye Casting Call.
Sinema itakuwa sehemu ya pili kuhusu maisha ya Juma Pondamali, ambaye katika sinema ya Bongoland, alishindwa na maisha ya Marekani. Hatimaye aliamua kurudi zake Tanzania, tena baada ya waBongo wenzake kumchangia nauli ya tiketi. Je, alivyorudi maisha yake yalikuaje?
Kibira Films, inaongozwa na Bwana Josiah Kibira, wa Minneapolis, Minnesota. Kampuni hiyo ilitengenza sinema ya Tusamehe. Mimi naigiza katika sinema hiyo kama Mama Kurusumu.

Wednesday, April 11, 2007

Sinema ya ROOTS




Tangu jumapili TVOne, wamekuwa wakionyesha sinema kabambe ya ROOTS. Hiyo sinema ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mwaka 1977 na kuingia katika vitabu vya historia kwa watazamaji wengi. Zaidi ya watu 130 milioni nchini Marekani walitazama.

Nasifia sana hiyo sinema maana inakumbusha watu na hasa waMarekani weusi kuwa wametoka mbali. Inaonyesha kuwa waafrika walikuwa na utamaduni na mzungu alijaribu kuifuta kwa kuzuia watumwa kutoongea lugha zao, kuchukua majina ya kizungu, na walizuiliwa kufanya kitu chochote cha kiaafrika. Katika Roots unamsikia binti Fanta, akisema mimi nimesahau kila kitu cha Afrika, nia yangu niishi. Na utasikia watumwa waliozaliwa Marekani wanavyowakashifu watumwa waliotoka Afrika. Watumwa wanajiona bora kuliko wale waafrika.
Roots ilitungwa na marehemu Alex Haley. Inahusu historia ya familia yake na inaanzia kijiji huko Gambia, na kuzaliwa kwa Kunta Kinte. Kunta anakamtawa na kuletwa Marekani. Ukiona walivyokuwa wanasafirisha weusi utalia. Huko nakumbuka dada moja mmarekani mweusi kaniambia eti kafurahi kuwa mababu zake waliletwa kama watumwa kutoka Marekani maana ana maisha bora na hashindi njaa. Pia inasikitisha ukiona Kunta Kitne kafungwa cheni shingoni na wanam-pat kichwani kama mbwa!
Huko mashuleni Marekani ni lazima vijana watazame sinema ya Schindler's List kusudi waelewe wayehudi walivyouliwa na Hitler wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Sasa kwa nini isiwe lazima watazame ROOTS kusudi waelewe history ya mwafrika Marekani na mateso waliopata.
Ukitazama Roots, pia utaweza kuelewa vizuri zaidi matatizo yanayowakabili wamarekani weusi kwa sasa. Matatizo mengi yanatokana na historia yao ya utumwa. Na kwa maoni yangu wengi bado wana mawazo ya kitumwa.
Leo wataonyesha tena TVone sehemu ya nne. Itatoka kwenye DVD May 22.
Karibuni mtoe maoni yenu.

Tuesday, April 10, 2007

Awatukana eti ni Malaya wenye nywele za kipilipili!

Captain wa Timu ya Rutgers, Essence Carson, akiongea na waandishi wa habari leo 4/10/07.

Mbaguzi Don Imus

Ubaguzi hauishi Marekani. Wiki iliyopita kuna huyo mtangazaji maarufu wa Marekani, Donald Imus, kasema eti wasichana wanaocheza basketball kwenye timu ya Chuo Kikuu cha Rutgers ni nappy headed hos (malaya wenye nywele za kipilipili). Alikuwa anaongea na meneja wake kwenye hicho kipindi na walizidi kusema wamejaa matatoo na pia wamekaa kidumedume. Kisa timu ya Chuo Kikuu cha Tennessee iliwashinda katika mashindano ya Basketball ya wanawake.

Mazungumzo enyewe ni hayo:

Imus started the firestorm after the Rutgers team, which includes eight black women, lost the NCAA women's championship game to Tennessee. He was speaking with producer Bernard McGuirk and said "that's some rough girls from Rutgers. Man, they got tattoos . . ."

"Some hardcore hos," McGuirk said.

"That's some nappy-headed hos there, I'm going to tell you that," Imus said.
Pia walisema kuwa eti hiyo timu ya Rutgers inafanana na timu wa wanaume ya NBA, The Toronto Raptors!"

Jana alikutana na Reverend Al Sharpton kuomba msamaha lakini Sharpton alikasirika baada ya Imus kusema, "You People!" (Nyinyi watu weusi). Na Reverend Jesse Jackson naye amekasirika ana anataka Imus afukuzwe kazi. Jackson kasema hiyo siyo 'Slip of the Lip' (Utelezi wa ulimi).

Lakini kwa hapa Marekani kusema kuwa mtu mweusi ana nywele za kipilipili ni tusi kubwa mno! Hii inatokana na asili ya utumwa Marekani. Pia nywele za kilipili inahusishswa na watu wesui hasa weusi tii. Na kama unataka kuelewa kwe undani zaidi ni kuwa hapa USA, unavyozidi kwa weusi ndo unavyoshushwa kwenye hadhi ya ubinadamu. Insikitisha! Weusi wenyewe wanadharau weusi na hasa weusi tii. Unasikia, "You Too black" yaani wewe ni mweusi mno. Ama kweli Imus, kachokoza watu.

Haya mambo ya nywele ni mjadala mkubwa maana utasikia weusi wanasema, yulekichwa chake kimejaa 'naps' (Kipilipili), na yule ana good hair (nywele nzuri), zimekaa kizunguzungu. Biashara ya ku-perm na ku-relz nywele kusudi zinyoke kama mzungu imeshamiri duniani. Hata Bongo watu hawaridhiki na nywele waliozaliwa nayo, unatukuta watu wanakimbilia saluni kupata 'relaxer'.

Na huyo Captain wa timu leo kaonekana na nywele ambazo zimetiwa Relaxer! Zimenyoka kabisa. Ningemheshimu zaidi kama angetoka na Afro. Ni kama vile wanaona haya kuwa na nywele za kiafrika.

Tangu enzi za utumwa hapa Marekani wanasema kama una hata tone moja ya damu nyeusi basi wewe ni mweusi. Unakuta watu ambao ungedhania ni wazungu lakini la, ni weusi! Na kama umetazama ile sinema ya School Daze ya Spike Lee, utaona mgogoro kati ya wanafunzi weusi. Weupe wanajiona bora kuliko wale ambao ni weusi zaidi.

Haya sasa Imus amesimamishwa kutangaza redioni kwa kipindi cha wiki mbili. Watu wanataka afukuzwe maana wanasema kuwa si mara yake ya kwanza kuongea mambo ya kibaguzi. Siku zijazo tutasikia hii 'issue' inaishia wapi.

Kwa habari zaidi mnaweza kusoma hii tukio:



Tuesday, April 03, 2007

TAMWA

Bila shaka mmesikia majina kama Fatma Alloo, Leila Sheikh, Edda Sanga, Maria Shaba, Pili Mtambalike, Wema Kalokola (marehemu), na Ananilea Nkya. Hao ni kati ya waanzalishi wa chama cha waandishi wa habari wanawake nchini Tanzania, TAMWA. Na mimi ni mmoja wa waanzalishi wa TAMWA (Tanzania Media Women's Association).

Tulitoka mbali maana mwanzoni tulipata pingamizi nyingi kutoka kwa wanawake na wanaume. Tulitukanwa na kuitwa majina ya ajabu kama, 'frustrated women, na malesbo'. Hivi sasa wanaume wakisikia jina la TAMWA wanatetemeka. TAMWA imefanya mengi kutetea haki za akina mama nchini Tanzania na inaendelea kwa nguvu! Tulianzisha kwa ajili ya kusaidia akina mama waliokuwa waandishi wa habari lakini ilikuwa mpaka kutetetea haki za akina mama Tanzania.

TAMWA Oyee!

Hii picha ilipigwa mwaka 1992. Tulikuwa kwenye safari Zanzibar na wageni wetu kutoka vyama vya akina mama mbalimbali barani Afrika. Mimi niko kushoto kabisa na miwani! Pia wamo Edda Sanga (3rd from left, Maria Shaba 5th from left, Halima Shariff 2nd from right). Wengine ni wageni kutoka nje.
Ndo baada ya hii safari iliyofana ilitokea kasheshe kubwa kutokana na picha fulani aliyopiga Muhidini Michuzi, na kuwekwa kwenye front page ya gazeti ya Daily News mpaka ilibidi viongozi wa TAMWA warudi Zanzibar kuomba radhi. Picha eneyewe ilipigwa kwenye shughuli ya mpendwa somo na kungwi mkuu wa Tanzania, Bi Kidude.
Kwa habari zaidi kuhusu TAMWA someni:

Afungwa Marekani kwa kutokuvaa Mask! Anaumwa Kifua Kikuu!


Jamani, leo nimeshutushwa na habari ya Mrusi kufungwa jela tangu mwezi Julai mwaka jana kwa ajili ya kutokuvaa mask hadharani. Jamaa amefungwa huko Pheonix, Arizona. Anaitwa Robert Daniels, na ana miaka 27. Anaumwa ugonjwa hatari wa kifua kikuu (Tuberculosis au TB). Kisa cha kumfunga ni kuwa anaumwa aina ya TB inaitwa XDR-TB. Wanasema kuwa ni drug resistant na haitibiki.

Mahakama ya huko Phoenix, inasema kuwa ilibidi Daniels afungwe kwe vile akikataa kuvaa mask (kizuio kwenye mdomo na pua), akitoka nje na kuwa na watu wengine. Walisema kuwa ana nia mbaya ya kutaka kuambukiza watu huo ugonjwa wa TB kwa maksudi.

Habari zinasema kuwa haijulikani atafungwa mpaka lini na huenda atafungwa mpaka anafia huko jela. Baada ya kusoma hivyo nikasema ni kweli wana haki ya kumfunga hasa kama hiyo TB haina tiba. Wakubwa wanasema kuwa kama watu wengine watapatikana na huo ugonjwa itabidi nao wafungwe.

Wataalam wa afya wanasema kuwa kama mtu anaumwa HIVAIDS (UKIMWI) na akipata huo ugonjwa atakufa siku 25 tu, baada ya kuambukizwa. DUH!

Na walivyo na woga na huo ugonjwa jamaa haruhusiwi kuoga kwenye shower. Anatumia wipes (vifutio). Hana TV, simu wala redio. Anasema kuwa maisha yake huko jela ni mabaya kuliko ya mtu alifungwa kwa kosa la jinai.

Chumba chake kina ventilation ya peke yake na filters za chumba zinachomwa moto, na watu waliojifunika kama vile astronauts! Ama kweli waMarekani hawataki huo ugonjwa usambae na siwalaumu.

Mnasemaje wapendwa wasomaji?

Kwa habari zaidi ya kufungwa kwa Robert Daniels mnawaeza kusoma:


Wednesday, March 28, 2007

Unawafahamu Cavemen?

Original Cavemen:
And Now the Geico Cavemen!


Kama uko Marekani, lazima mmeona yale matangazo ya Geico insurance yenye Cavemen. Cavemen ni aina ya binadamu walioishi hapo zamani za kale. Yaani wale wa mwanzo kabisa baada ya enzi za dinosaurs.

Sasa kwenye hayo matangazo hao Cavemen ni wa kisasa, na mambo yao ni ya kisasa hasa. Huwa matangazo yao yanafurahisha kweli kweli. Kuna ile ambao wanamhoji Caveman fulani na ana kasirika, anavyokasirika mama moja anasema, "Seems like someone woke up on the wrong side of the rock!"

Kuna habari kuwa wanapata TV show yao mwaka kesho. Kwa kweli watu wamefurahi sana kusika habari hizo na wanangojea kwa hamu.

Kwa sasa unaweza kwenda kuwatembelea nyumbani kwao, sijui Manhattan, sijui ni Los Angeles hapo.


From Variety Magazine:

"Cavemen" will revolve around three neanderthals who must battle prejudice as they attempt to live as normal thirtysomethings in modern Atlanta.

Tuesday, March 27, 2007

Tendo la Ndoa




Nina swali. Ile tendo la kukutana mwanume na mwanamke na kufanya mapenzi ina majina mbalimbali. Wengine wanasema ‘ngono’, wengine’ kut-mbana’, wengine ‘majambo’, wengine ‘kufanya’, ‘vituuz’ na majina mengi. Lakini jina nacho shangaa ni hiyo, ‘tendo la ndoa’. Ndo jina la heshima au sijui ndo kuweza kusema bila aibu. Au ndio wamisionari walituletea hiyo jina.

Lakini watu wanaita ‘tendo la ndoa’ wakati tunajua kuwa watu wengi wanafanya kabla hawajafunga ndoa. Na watu ambao hawajafunga ndoa, wanafanya. Mungu sijui aliumbaje binadamu lakini kuvumulia mpaka kufunga ndoa si rahisi, katika jamii zote za dunia. Wanataka wasichana watunze bikra zao (lakini hiyo ni topiki nyingine). Pia watu wanafanya na watu ambao si wake, waume zao, sasa ndo ni tendo la ndoa?

Au wanaita tendo la ndoa kusudi watu wajisikie vibaya wakifanya bila ndoa? Au wanataka walazimaishe wafunge ndoa? Ndoa ni hatua kubwa katika maisha ya bindamu. Na kwa kweli ukifunga ndoa ndo unafanya mapenzi na mwenzako kwa halali. Lakini wengine wanatembea nje ya ndoa zao.

Je huko gesti au hotelini watu wanaombwa cheti cha ndo kabla ya kupewa chumba? Miili ya watu inacheka, eti hatuwezi kufanya mapenzi mpaka tufunge ndoa. Na nadhani ni vigumu sana wanaume waweze kuvumulia mpaka wafunge ndoa, maana mwili unafika ile peak ya ‘maturity’ kabla hawajafika miaka 19. Hebu someni vitabu vya biologia.

Uwongo mbaya, watu wataendelea kufanya bila ndoa. Ile ume ya mwanaume ikisimama akili anakosa mpaka anapata kitu cha kumpooza! Na kuna wanawake nao kuna kipindi fulani wanashindwa kuvumulia lazima wapate kitu tena hali hiyo inatokea bila kufunga ndoa!

Nafungua mjadala, karibuni mtoe maoni yenu.

Monday, March 26, 2007

Marudio - Miaka Baada ya tukio kaniomba Msamaha!

Naona, kuna 'Anonymous' fulani kagusia hii swala ya yalionipata nikiwa jeshini JKT. Watu wengi wamenitumia e-mail kuulizia details. Nimeamua kuibandika tena. Ni posti ya kutoka April 2006. Lakini mjue enzi za JKT, wasichana wengi walinyanyaswa kijinsia, mimi nilikuwa na bahati maana nafahamu wasichana waliokuwa gang raped. Dada fulani, alimkubali afande, alivyomaliza kaita wenzake kwa kusema, "Njooni, Mboga hii hapa!" Yule dada hakuweza kutembea vizuri kama wmezi baada ya hapo!

*****************************************************************************

Nilipokuwa Jeshi ya Kujenga Taifa (JKT) karibu nibakwe na afande Fulani (jina nahifadhi). Lazima niseme kuwa katika kipindi hicho wanaume wengi waliona makambi ya JKT kama ‘buffet’ ya wasichana. Si maafande wa jeshi tu, bali hata viongozi wa serikali walikuwa wanapitia makambi ya JKT kula tani yao!

Mimi nilikuwa Masange JKT, Tabora. Wakati huo huyo jamaa alikuwa ni Kepiteni wa JKT. Nadhani alidhania kwa vile yeye ni kepiteni basi alikuwa na haki ya kutembea na yeyote aliyemtaka. Kwangu aligonga ukuta! Bila shaka alikuwa hajawahi ‘kunyimwa’ mpaka siku hiyo alipokutana na mimi.

Miaka baada ya tukio nikiwa nafanya kazi Daily News mara nyingi nilikuwa napishana naye Posta Mpya. Basi ananisemesha, na mimi namnunia halafu napita zangu kimya bila kumjibu kwa hasira. Siku moja kanisimamisha kaniambia, "Chemi, naomba msamaha, nisemahe tafadhali, kweli nilikukosea!” Aliongeza kuwa miaka mingi imepita hivyo sina sababu ya kuwa na hasira naye! Na mimi nilimjibu, “Mshenzi sana wewe!” nikaenda zangu.

Ikapita kama mwaka mwiingine. Jamaa anaendelea kunisalimia kila nikimpita njiani na mimi kwa uchungu bado nikashindwa kusema kitu. Basi nikafikiria alichoniambia Posta Mpya. Lakini niliona kama jambo hilo linamsumbua. Na nikasema kama Bwana Yesu aliweza kusamehe watu kwa madhambi yao kwa nini mimi nisimsamehe. Basi baada ya hapo ikiwa nikimwona na akinisalimia naitika na naendelea zangu na nikaona kidogo hata yeye alikuwa na raha.

Lakini bado najiuliza kama kitendo chake kilimsumbua miaka na miaka kama ilivyonisumbua mimi.Unauliza ilikuaje mpaka nikajikuta kwenye situation ya kubakwa. Au mnasema nilitaka mwenyewe. Ngoja niwaelezee ilivyokuwa.

Nilikuwa mhudumu Officer’s Mess, mpishi na msafishaji. Huyo jamaa alikuwa ni mgeni kutoka Makao Makuu ya JKT Dar es Salaam. Kwa kweli sikutaka kufanya kazi pale Mess lakini tulichaguliwa special na Matron, mimi kwa vile niijua kupika vyakula mbalimbali hasa za kizungu. Lakini uzuri wa hiyo kazi ni kuwa uanambulia mabaki ya vyakula (leftovers), na mara nyingine kulikuwa hakuna.

Basi huyo Afande alikaa kambini wiki kadhaa. Katika kumhudumia tukawa tunaongea na mimi nikawa namheshimu kama kaka vile. Wala sikusikia mapenzi yoyote kwake. Basi jioni fulani, kanialika chumbani kwake kunywa soda na biskuti na kwa Maongezi zaidi. Sasa kama ulienda jeshi unajua njaa kali unayokuwa nayo. Nikaenda, kanikaribisha vizuri, nilipewa soda na tukawa tunaongea. Basi nikaona mwenzangu anabadilika ghafla! Mara ananikumbatia kwa nguvu, na kunibusu na mengine. Nikajaribu kuaga lakini jamaa hakuniachia. Baada ya ku-plead naye aniachie, kaniachia. Kaomba msamaha na kaniomba niendelee kukaa nimalize hizo soda alizoninulia.

Kama mjinga nikamwamini, nikakaa nakunywa hizo soda. Tukaendelea na Maongezi, kukaa kidogo huyo kanirukia, najaribu kusimama huyo, kanivuta na kuniangusha kitandani! Mimi saa hizo nikawa naogopa kabisa nia yake!Kaniambia eti, “ukipiga makelele najua nitasema nini! Nyamaza! Huna sababu ya kunikatalia!” LOH! Kanizaba kibao! Nikamwuliza kwa nini anaifanyia hivyo, na mimi nilikuwa namwona kama kaka yangu!Hapo sasa ikaniingia. Nabakwa! Loh!

Nilimpiga mangumi na mateke lakini jamaa alikuwa na nguvu huyo kachana chupi yangu! Baada ya hapo, jamaa kashika miguu yangu huko anafoka kwa sauti kama vile anatoa amri “panua miguu! PANUA MIGUU!” Huko katoa ume wake uliyosimama kwenye suruali! Basi kuona sipanui jamaa kaongeza makofi na kafanikiwa kupanua miguu yangu! Kuona kafanikiwa kupanua huyo kajaribu kupenya. Ilipogusa kwangu nilipiga kelele cha kufa! Nikasema, “Nakuufaaaa!”

Heh! Ghafla jamaa kaniachia kaniambia niende. Alisema, “Nimeigusa na ume wangu, unatosha!” Nenda zako! Na ukimwambia mtu najua nitasema nini!”Loh nilikimbia bwenini na giza lile la Masange huko nalia. Wenzangu wananiuliza vipi, nikashindwa niseme nini! Kwanza niliona haya! Fikiria, niliona haya (shame)!Kesho yake nikaenda dispensary na kujiandikisha mgonjwa. Sikwenda kazini Officer's Mess bali nililala bwenini.

Siku iliyofuatia huyo Afande mshenzi kapita bwenini kwetu kaulizia hali yangu, na mimi huko natetemeka kwa woga nikashindwa niseme nini. Alininunulia Orange squash na biskuti na kuzileta bwenini. Sitasahau alivyonitazama! Ilikuwa kama vile anapanga jinsi gani atanipata. Baada ya hapo alimwopoa msichana mwingine na huyo alimkubali kabisa. Akawa analala kabisa huko Officer’s Mess. Hakuna anayemsumbua wakijua ni bibi wa Afisa. Basi, siku za yule jamaa kukaa kambini zikaisha, na yule binti alienda naye Tabora mjini kwa siku kadhaa. Halafu jamaa karudi zake DSM. Yule binti karudi zake kambini! Kumbe alienda bila pass. Alidhania kwa vile yuko na mkubwa hana haja ya pass. Na yule Afande ndo kaondoka kimoja! Maafande waliobakia wacha wamtese huyo binti alivyorudi kambini! Walimtesa kwa Extra drill na mengine mpaka ikabidi Military Police waombe wakuu wamsamehe la sivyo atakufa. Raha yake iliishia kwa suluba! Sijui yule binti alidhania jamaa atamwoa! Kwa nini alimkubali yule mshenzi.

Anyway, kila mtu na vyake. Alivyotoka kwenye suluba tulimwuguza! Siku haizkupita na mimi nilitolewa kazi Officer’s Mess na kupelekwa kwenye kikosi cha Ujenzi na lazima nisema hapo nilifurahi sana. Basi miaka ilipita. Mimi nilikuwa mwandishi wa habari Daily News, tena nilijenga jina. Sasa nikawa napishana na yule jamaa huko kapandishwa cheo na yuko JWTZ. Jamaa anajaribu kunisalimia na mimi napita zangu kimya, namnunia kabisa.

Nilimwona mshenzi, mnyama, na kila kitu kibaya ndo ilikuwa yeye! Angefanikiwa kuingiza na kunimwagia uchafu wake ningejiona mchafu mpaka leo! Miaka kama 20 imepita sasa na bado nina uchungu naye.Jamani nyie wanaume nawaambia kubaka kinaathari zake kwa wanawake. Unataka raha ya dakika na unamwachia mwenzio na uchungu wa maisha! Wengine mpaka wanakuwa wagonjwa wa akili.

Kwa nini nimeamua kuzungumzia kubakwa kwangu hapa, ni kwa sababu naona wasichana wengi wanabakwa, halafu wanaamua kunyamaza kimya. Kisa wakienda polisi na hospitali wanahofia kuambiwa ni Malaya au walitaka wenyewe! Hata mwamanke mwenzako anaweza kukufokea kuwa ulitaka mwenyewe. Tanzania, wanaume walikuwa na usemi wao kuhusu wanawake na ngono. Walisema eti ukimwomba mwanamke halafu akijibu ndiyo, manake ndiyo atafanya. Akisema labda, manake atafanya, akisema hapana, manake hapana. Lakini jamani tendo si inakuwa tamu kama wote mmekubali? Na kama angefanikiwa kuingiza si angeniumiza sana!

Wengine wanasema ningemshitaki. Je, ningemshitaki ingekuaje? Kwanza jeshini mimi ningepewa Extra Drill mpaka niumie au kufungwa jela ya jeshi iliyojaa maji na mbu kusudi niteswe. Kumbuka ilikuwa Tanzania na yule alikuwa ni Kepiteni wakati huo na mimi nilikuwa Private. Hakuna ambaye angekuwa tayari kunisikia zaidi ya wenzangu maPrivate, na yeye alijua hivyo. SHENZI TAIPU!

Thursday, March 22, 2007

Sinema ya '21'



Wapendwa wasomaji, nimepata bahati ya kuwa katika sinema ya '21'. Wahusika wakuu ni Laurence Fishburne na Kevin Spacey. Kwa habari zaidi mnaweza kusoma hapa:

http://www.imdb.com/title/tt0478087/

Naigiza kama mhudumu wa hoteli ya Planet Hollywood. Nitawapa habari zaidi siku nyingine.

Friday, March 16, 2007

Waziri wa Liberia Ajiuzulu baada ya Skandali kumpata!




AIBU KUBWA JAMANI!

Huyo baba mweupe kwenye picha si mcheza sinema, wala porn star. Ni mtu mwenye wadhifa kubwa Afrika!



Huenda mmesikia mkasa uliyompata Waziri wa Mambo ya Rais (Minister of Presidential Affairs) huko Liberia, Afrika Magharibi. Bwana Willie Knuckles, amejiuzulu baada ya picha ya ajabu ya yeye akiwa uchi wa nyama, tena anafanya tendo la ngono na wanawake wawili, kuwekwa kwenye internet! Yaani tendo enyewe infaaa kuwa kwenye sinema ya pono! Picha enyewe inaonekana kama ilipigwa siku nyingi, na huenda waliyoitoa walikuwa na kisa naye.

Picha nimekata (cropping), lakini kwa kusimulia, kuna wanawake wanafanya tendo la kishoga. Kuna mwanamke kalala chale na kuchezea matiti yake mwenyewe huko mwanamke mwingine ananyonya uke wa huyo aliyelala na kupanua miguu, huko huyo Bwana Knuckles anamwingia kwa nyuma (huyo anayemnyonya mwenzake), mtindo wa chuma mboga au dogi!

Ni aibu kwake na familia yake. Kafunga ndoa na mke wake miaka 37 sasa. Je, mke wake atamvumulia baada ya picha hiyo ya matusi kunonekena karibu dunia nzima? Nasema shauri zake! Mke wake akimwacha ana haki maana yeye asingevumilia kuona picha ya mke wake akiwa kwenye shughuli na mwanaume mwingine.

Nashukuru Bwana Knuckles amejiuzulu. Viongozi wanatakiwa kuwa mifano kwa wananchi. Kwa kweli amejiangusha mwenyewe. Natoa pole kwa Rais wa Liberia, Mama Ellen Johnson-Sirleaf kwa kumpoteza mfanyakazi mzuri, na aibu yaliyopata uongozi wake.

Nalaani tabia mbaya na chafu ya wanaume huko Afrika. Kwanza wanaume waafrika wamezidi kupenda ngono, na tena kutoheshimu ndoa zao. Kutembea nje ya ndoa ni sifa na wanajigamba huko kwa wanaume wenzao…oh nimetafuna yule na yule! Khah! Wanaona sifa kutembea na wanawake wengi, eti inawafanya wanaume! Na wanaume walivyo washenzi badala ya kusutana, wana pongezana! Halafu watu wanashangaa kwa nini magonjwa kama UKIMWI yanasambaa kwa kasi. Si siri kuwa kuna viongozi wetu waliofanya maajabu na wanawake wasio wake zao wakiwa katika uongozi. Wakisafiri, wanasema, oh siwezi kulala mwenyewe! Kisa! Na hiyo misafara ya Mwenge enzi zile ndo usiseme, maana ilitembea kila kona ya nchi, mchana shughuli za Mwenge, jioni ‘ngonofest’!

Kwa kweli yaliyompata Bwana Knuckles iwe fundisho kwa watu. Siku hizi kuna internet na unaweza kudhalalishwa dunia mzima katika dakika chache! Kuna picha za cell phone, na vicamera vidogo vidogo, unaweza kupigwa picha na huna habari. Nafahamu jamaa alipanga chumba kwenye hoteli fulani hapa States, kachukua demu wakafanya mambo yao huko, kumbe kuna mfanyakazi wa hoteli alificha video camera huko chumbani. Hawakuwa na habari. Baada ya miaka miwili yule mfanyakazi alikamatwa na kanda nyingi za watu mbalimbali wakiwa kwenye tendo. Bahati nzuri hakuwa anaaziuza bali anazitazamma mwenyewe. Je angekuwa anaziuza. Fikiria unanunua kanda ya X video au DVD, unaanza kutazama na unatambua watu waliyoomo.. DUH!

Duniani kuna mambo ya ajabu.



Kwa habari zaidi mneweza kusoma:





Saturday, March 10, 2007

Wasio na Makaratasi wakamatwa Massachusetts

Jamani, wiki hii wasio na makaratasi wana haha hapa Massachusetts. Ni hivi, siku ya jumatatu walivamia kampuni fulani huko New Bedford and kukamata wasio na makaratasi karibu 400! Tena wengi wao walisafirishwa kwa ndege na kupelekwa kwenye makambi ya wasio na makaratasi huko Texas. Watarudishwa kwao (Deported)!

Cha kusikitisha ni kuwa wengi ya waliokamatwa walikuwa na watoto wadogo. Wamebaki bila wazazi, bila mama au baba. Kuna watu ambao wanawaonea huruma na wengine wanasema shauri zao, maana walivunja sheria kwa kukaa USA bila makaratasi. Na mbaya zaidi, waligundua kuna duka iliyokuwa inauza vyeti feki (social security card na green card) kwa dola $120! Wanaesema wakuu wa hiyo kampuni walishirikiana na wenye duka kuwapatia hao wafanyakazi makaratasi feki!

Lakini jamani, walikuwa wanafanya kazi kwa hela ndogo, na kufanya kazi ngumu. Wanaofanya kazi pale wanasema hata ruksa ya kwenda chooni ni shida. Ukichelewa kazini dakika tano unakatwa mshahara. Hiyo kampuni ilikuwa inatengeneza vifaa vya jeshi.

Wengi ya waliokamatwa wanatoka Guetemala, na El Salvador. Sijasikia kama mwafrika alikuwemo.

Unaweza kusoma habari zaidi hapa:

http://business.bostonherald.com/businessNews/view.bg?articleid=187373&srvc=biz

http://biz.yahoo.com/ap/070306/ma_immigration_arrests.html?.v=1

Thursday, March 08, 2007

Ni Ubaguzi, Uonevu au Upendeleo?

UPDATE: ANTONELLA KATOLEWA ALHAMISI. Alilia kweli. Lakini amepata offers za kupiga picha uchi Playboy magazine na ku-host Girls Gone Wild. Frenchie ata sue American Idol kwa uonevu!
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@



Kwa wapenzi wa American Idol, naomba maoni yenu. Mnakumbuka mwaka 2003, (msimu wa pili aliyoshinda Ruben Studdard) kulikuwa na dada fulani, Frenchie Davis. Huyo dada ni mweusi, mnene na ana zinga la sauti. Yaani anaimba huyo si mchezo, Jennifer Hudson alie kwake.

Kwa bahati mbaya, Frenchie aliwaambia Producers kuwa akiwa mwanafunzi, alipiga picha nusu uchi (topless) kwa ajili ya kupata pesa za kumsaidia kulipia masomo yake Howard University. Producers waliamua kumfukuza kwenye show. Mungu ni mwema na Frenchie sasa ni mwimbaji maarufu kwenye mchezo wa kuigiza, Rent, huko Broadway, New York.

Msimu huu wa American Idol kuna dada fulani, Antonella Barba, ambaye naye ali picha za uchi kwenye internet. Hajafukuzwa na bado yumo. Amepiga picha za uchi kabisa. Kwenye picha zingine anamfurahisha mwanaume kwa kumnyonya ume wake! Zingine kapanua miguu. Loh! Ajabu hajafukuzwa kwenye American Idol.

Sasa imekuwa issue, mpaka Rosie O’Donell anaongelea kwenye show yake The View, yeye anasema kuwa eti ni ubaguzi. Pia wiki hii kulikuwa na maandamano mbele ya Kodak Theater Hollywood kupinga Antonella kuendelea kuwa kwenye show wakati Frenchie alitolewa.
Na Frenchie mwenyewe sasa anataka maelezo kutoka kwa Producers wa American Idol. Anasema kuwa anamtakia huyo Antonella mema lakini ni lazima wamweleze kwa nini alitolewa na kudhalalishwa wakati ule na picha zake siyo mbaya kama za Antonella.

FYI- Producers wanajitetea kwa kusema eti Frenchie alilipwa hela kwa ajili ya zile picha wakati za Antonella zilibandikwa na boyfriend wake.

Mimi navyoona ni ubaguzi. Frenchie ni mweusi na ni mnene. Huyo Antonella ni mwembamba na wanasifia uzuri wake. Lakini jamani uwongo mbaya, Antonella hawezi kuimba.

Mnasemaje wasomaji?

Kwa habari zaidi soma hapa:

http://www.showbuzz.cbsnews.com/stories/2007/03/06/tv_realty_tv/main2540578.shtml?source=RSSattr=Entertainment_2540578

Monday, February 26, 2007

Sinema ya 'Maangamizi' itaonyeshwa Toronto, Canada March 9th


Mimi na-acti katika hiyo sinema kama Nurse Malika. Karibuni Kwa habari zaidi kuhusu sinema ya Maangamizi: the Ancient One, bonyeza hapa. http://www.grisgrisfilms.com

***********************************************************************************

Friends of Alternative and Complementary Therapies presents a special screening of Maangamizi: The Ancient One on Friday March 9th, 2007.


This multi-award-winning film about healing trauma from a traditionalAfrican perspective is a Tanzanian-U.S. co-production (2001), co-directed by Martin Mhando and Ron Mulvihill and executive produced by Jonathan Demme.According to American author Alice Walker, "MAANGAMIZI - The AncientOne...is more than a movie. It is a look at how we've been torn at our roots; severed from nourishment at the source...Those of us who can remember and honor who we have been over eons of time, will be able to inspire the whole world to greater heights of compassion."


This powerful film about the role ancestor spirits play in healing will be followed by a panel discussion , moderated by Cameron Bailey, film critic and programmer of Planet Africa for the Toronto International Film Festival.


Panel members include: Ainajugoh Taylor is a traditional African healer from Sierra Leone who is currently helping the government of her home country draft legislation to formally recognize and register traditional healers there according to WHO criteria. She is also a recipient of the Michael Clemons Community Leadership Award for such activities as introducing live African music to Toronto and establishing the health-care team that lobbied the College of Physicians and Surgeons to acknowledge the credentials of foreign graduates in medicine and nursing.


Rebecca Rogerson, born in Toronto, was trained in Soweto, South Africa and is a registered sangoma. After 10 years of work in Southern Africa, she returned to Toronto where she continues her practice as a traditional healer and pursues graduate studies in medical anthropology.


Dr. Ted Lo is a community psychiatrist, Assistant Professor consulting to the Culture, Community and Health Studies Program at the University of Toronto.


When: Friday, March 9th at 7:30 p.m.


Where: Workman Theatre, CAMH 1001 Queen St. W. at OssingtonTickets: $10 (book early to reserve a seat)


Advance Tickets: Send cheque to FACT, 375 Bay Mills Road, # 516, TorontoOn M1T 2G6Payment must be received by Friday, Feb. 23, 2007.


Same day Tickets go on sale at the Workman theatre 30 minutes prior to the screening.For more information, call FACT 416-299-5113 or see http://www.the/ facts.orgFor further details, please see the attached poster. And thanks for passing this on to anyone else who might be interested.FACT is a non-profit

Tuesday, February 20, 2007

Marudio - Wapenzi wa Matako Makubwa



Naona blog ya 'Matako Makubwa' ilikuwa na hits nyingi sana, nilibandika kwanza 12/2005. Hivyo nimeamua kuirudia.

Nimesikia wazungu wakisema hiyo kupenda matako makubwa eti ni 'cultural thing' kwa watu weusi, na hawajakosea. Ni mila na desturi ya mwafrika kupenda matako makubwa. Na kuyasifia. Hata wengi wa waMarekani weusi wanapenda mpaka kutunga nyimbo za 'bootylicious'. Huwa nacheka nikiona mzungu anasifia mwanamke ambaye huko nyuma kapigwa pasi. Yaani fleti. Lakini kuna wesui ambao wamekuwa 'zungunized' na wanapenda matako fleti. Shauri zao!

Matako Makubwa Oyee!



************************************************************************

From my 12/2005 Blog:


Wapenzi wasomaji, leo nimeamua kuzungumzia suala ya matako makubwa. Tafadhali msione kama ni matusi lakini hapa USA ni issue kubwa, maana watu wanayachukia!

Nimeona nizungumzie suala ya matako makubwa kwa vile jana kazini, mzungu aliyekondeana mno kasema ni mnene na akila keki eti yote itaenda matakoni. Nilishangaa na kusikitika sana.Uzuri kwa wazungu ni kuwa na matako fleti kama vile yamepigwa pasi. Sijui kwa nini. Mtu anashepu ya mbao, mwanamke hana hips kakaa kama dume vile eti ndo uzuri. Kumbe ni kwa sababu hao models na wacheza sinema wako hivyo!

Basi wasichana na akina mama wanajinyima chakula kusudi wakonde na eti wapendeze. Ndo maana magonjwa kama Bulimia na Anorexia zimeshamiri hapa. Lakini ukitazama sinema za miaka ya nyuma kama za 1930's na 1940's, wanawake walikuwa na shepu na walikuwa wamejaa na hata wanaume wa kizungu walikuwa wanasifia. Mpaka 1950's kulikuwa na mcheza sinema Marilyn Monroe, alikuwa na zinga la figure 8, na wanaume wote walikuwa wanampapatikia. Ama kweli mambo yanabadilika. Hivi sasa wanasema eti walikuwa ni obese yaani wanene!

Mbona mimi naona matako fleti kama chapati ni mabaya na hayapendezi? Au ni kwa sababu nimekulia Africa? Brothas (waMarekani Weusi) wanapenda mwanamke awe na matako ya maana! Akipita mwanamke mwenye mbarikio utasikia brothas wakisifia, "umm, umm umm!" Kuna siku nilisikia wanaume wa kizungu wakijadili sababu ya wanaume weusi kupenda matako makubwa, walisema ni "cultural thing". Kwa kweli ni culture yaani utamaduni! Kama umekulia katika mazingara ya kupenda kitu utakipenda. Na ndo maana kuna weusi USA wanataka kuwa na shepu iliyokondeana kama mzungu kumbe haiko katika 'genes' zake. Wajitahidi kupunguza mzigo lakini wapi, iko pale pale.

Sisi wanawake wenye asili ya Afrika tumebarikiwa huko nyuma. Yaani boxi, siha, wowowo, booty, na nasikia waGhana wanaita yokohama, matako makubwa yana majina mengi. Waafrika tunaona kama ni urembo, lakini wazungu na waliokulia uzunguni wanaona kinyaa. Wanasema eti ni dalili ya ulafi na uvivu! Lakini kama ni dalili ya ulafi mbona hata mwanamke mwembamba mwafrika anaweza kuwa na kamzigo huko nyuma?

Ubaya mwenye matako makubwa anaweza kubaguliwa kwa vile bosi anaweza kuona kuwa ni 'ugly' (mbay) na mwenye nacho anachafua mazingira ya ofisi. Kweli kabisa!Hayo matako makubwa ni 'genes' za sisi waafrika. Lakini ajabu kuna siku nilisikia wazungu wakisema eti waafrika tuna matako makubwa kwa sababu ya utumwa. Eti mabibi zetu walinyimwa chakula hivyo matako ndo ilikuwa 'godown' ya mafuta ya akiba. Nadhani ni uzushi kama ile ya ngamia kuweka maji kwenye nundu zake!

Mimi mara nyingi nimeambiwa nina matako makubwa, niyapunguze kwa kwenda gym kufanya mazoezi. Hayo mazoezi haisadii kitu ni makubwa vile vile! Lakini msione kama naona haya, wala! Mtu akiniambia nina matako makubwa namwambia mbona kama ni madogo, na ningependa yawe makubwa zaidi! Wanabakia kushangaa hasa nikiwaambia kuwa Afrika, matako makubwa ni uzuri.Na amini usiamini kuna opresheni ya kuyapunguza inaitwa Liposuction. Wanawake wengi weusi na wazungu wamefanya hiyo liposuction ya matako, akiwemo mwimbaji Janet Jackson. Ubaya, ni kuwa ukishafanya hiyo liposuction, mafuta yataenda kwingine mwilini, hivyo utakuwa na shepu ya ajabu!

Sisi waafrika tunapenda kuringia huo mbarikio wa matako makubwa. Nilipokuwa nacheza ngoma shuleni na jeshini, tulikuwa tunatia nguo ndani ya bukta kusudi tuonekana na matako makubwa kweli kweli! Lakini, mara nyingi mitaani hapa USA, nimesikia akina dada wakifokewa, "You got a big a-s!" Kuna siku nilikuwa kwenye kituo cha Subway hapa Boston, kapita mama fualni Mganda, aisei alikuwa amejaliwa kweli huko nyuma, mpaka nikaona wivu. Basi ungeona wazungu walivyokuwa wanamtazama kwa mshangao ungecheka. Ila nilishuhudia baba fulani Mmarekani Mweusi akimtazama kwa furaha na kawa kama vile anamezea mate.

Nampenda sana mecheza sinema, Whoopi Goldberg. Nilikuwa nasoma jinsi akienda kwenye audition au akiwa kwenye movie shoot, wazungu wanamwambia kuwa ana matako makubwa au avae nguo ya kuzificha. Yeye alichoka, na mwishowe kusema, " Mimi ni mwanamke mweusi, nina matako makubwa niache kama nilivyo!" Wanawake wote tungedai heshima kama Whoopi nadhani wazungu wangeheshimu matako yetu makubwa.

Tatizo linigine la kuwa na matako makubwa USA ni kupata nguo. Ukienda kununua sketi au gauni uanweza kukuta mbele refu nyuma umepanda. Au unavaa hiyo nguo lakini kwenye hips na matako haipiti! Hii ni kwa sababu nguo imeshonwa kwa ajili ya wazungu wenye matako fleti. Na kupata Jeans inayofiti ni vigumu. Mtu ambaye atatengeneza nguo 'molded for the black woman' atapata wateja kweli kweli, maana tunalilia nguo kama hizo.

Pamoja na yote haya sasa wazungu wameibuka na staili ya kuwa ka ka-butt. Yaani jeans inakuwa na pedi ndani kusudi mtu aonekana ana matako. Loh! Watu hawaridhiki! Sijui tuseme asante J-Lo (mwimbaji Jennfier Lopez) au nini. Kwanza walikuwa wanamcheka J-Lo na matako yake makubwa lakini naona watu wanaanza kuyapenda. Mpaka kuna opresheni sasa ya kuongeza matako. Wacha wafanye haitapendeza kama matako natural tulyiozaliwa nayo waafrika.

Matako Makubwa Oyee!

Sunday, February 04, 2007

Leo ni SuperBowl - Wanaume wanakuwa Wajinga!

Leo ni siku ya SuperBowl. Yaani msimu wa mchezo wa football unaisha leo. Wanaocheza ni timu za Chicago Bears na IndianapolisColts. SuperBowl inachezwa mji ambayo haina uhusiano na timu wanazoshindana, maana lazima watu wangeuana. Mwaka huu inachezwa Miami, Florida.

Mimi siyo mshabiki wa football wa Marekani. Naona kama wanaumizana, kazi kuangushana. Mara unaona mtu kazolewa kavunjika mguu, mkono au mgongo!

Lakini wanaume hapa USA wanaipenda kweli. Mpaka wasichana wanaotafuta wapenzi, mume wanaambiwa wajifunze kuelewa huo mchezo na itakuwa rahisi kumpata!

Lakini nacho shangaa ni hivi, wanaume wanakuwa wajinga hawajali nini zaidi ya mambo ya hiyo SuperBowl. Wengine wananua tiketi za kwenda huko na mshahara wa miezi kadhaa, mradi wanaenda. Pia TV Kubwa kubwa zinauzwa sana kipindihiki, wanunuzi wakuu wanaume wanaotaka kuangalia Superbowl.

Magazeti, na TV wanaongea habari ya SuperBowl tu mpaka inachosha. Ukienda Grocery store, (dukani) unakuta wanaume wamejaa huko wananunua vyakula vya party kama potato chips, nachos, salsa, chicken wings, cold cuts platters, vinywaji kama soda na bia na nyama za kufanyia barbecue. Hata kwenye baridi unakuta wanaume wako nje wanafanya barbecue. Kwenye football wanita ‘tailgating’

Ajabu wikiendi ya SuperBowl kunakuwa na seli nzuri ya chakula. Mameneja huko Corporate Offices wanakuwa na huruma na kuwapunguzia bei nini? Halafu kila sehemu utasikia kuna SuperBowl party hata majumbani mwa watu. Mabaa zenye TV zinafanya kazi nzuri kweli siku ya SuperBowl.

Niliuliza akina mama wa kizungu kwa nini wanaume wanapenda sana SuperBowl na kupika wao wenyewe siku hiyo. Wakasema ni siku ya mwanaume kuonyesha kuwa ni mwanaume bila kujali wanawake. Haya SuperBowl ikisha watatukumbuka sisi wanawake.

Mama moja kaniambia habari ya chakula fulani wanachopika hao tailgaters, inaitwa jambalaya. Hicho chakula kina wali, sausage, nyanya, vitunguu, pilipili hoho, na viungo kadhaa. Halafu wanatia vipande vya nyama ya kaa. Eti hiyo kaa inaongeza ladhaa. Ukweli eti ina harufu kwa uke wa mwanamke, ndo maana wanaishangalia. Unaona wanaume wananusa halafu wanshangalia. Fikiria mbuzi beberu anvayotanua tanua pua akitaka mambo. LOH!

Hapa Boston timu yetu New England Patriots, hawakufanikwa kwenda. Mbona wanaume walilia machozi walivyoshindwa! Haya tuone nani atashinda Colts au Bears. Na kwa mara ya kwanza timu zote mbili zina kocha mweusi.

UPDATE- Washindi ni INDIANAPOLIS COLTS

Score ilikuwa 29-17.


Huwezi kujua ajali itatokea lini

Ajali ni ajali. Hupangi itatokea lini au itatokea nini. Ukweli ukiamka huwezi kujua Mungu au shetani amekupangia nini siku hiyo.

Zaidi ya wiki mbili zilizopita nikiwa nakwenda kazini nilianguka kwenye ngazi za subway Central Square hapa Cambridge. Hata sikumbuki vizuri ilikuaje, sikuwa nakimbia wala kuwa na haraka, mwendo wa kawaida tu. Nilikuwa nateremka kwenda kwenye geti kusudi nisubiri treni. Ghalfla nilianguka, kwa bahati kuna ile sehemu pana ya katikati ndo nikaishia hapo na sikwenda chini kabisa. Ngazi zenyewe zimechongwa na mawe. Loh, magumu! Baada ya kuanguka nilishindwa kuinuka. Nikasema hayo ni malipo kwa ajili ya kucheka uile tangazo ya bi kizee akisema, “I’ve fallen and I can’t get up!) (nimeanguka na siwezi kuinuka), japo sijaiona miaka mingi. Mzungu mwanaume aliyekuwa anapanda zile ngazi alinisaidia kuinuka. Alivyokuwa ananinsaidia nikasikia maumivu makali kwenye mguu na kushindwa kutembea kabisa. Nikamwambia nadhani nimevunjika mguu. Huyo mzungu alipiga simu polisi, na polisi kaja, halafu wakaamua kuniitia ambulance.

Wale EMT (Emergency Medical Technicians) walinipakia kwenye kiti maalum ya wagonjwa na kunibeba mpaka kwenye stretcher barabarani ndo wakanipakia kwenye ambulance. Nikapelekwa hospitalini donidoni ikiwa inalia.

Basi mle ndani nikawa nalia. Niliamka mzima, sasa nimevunjika mguu! Nikawaza je, ningechelewa kidogo ningeanguka, je, ninegwahi kidogo ningeanguka? Je, nitakuwa mzima tena, je, nitaweza kucheza densi tena? Nikasema nina bahati lakini maana kuna wengine wanapata ajali ya gari na wanakufa. Au wanakatika kiungo. Fkiria mtu unaagana na mpenzi wako mtaonana au mtapigiana simu baada ya muda kadhaa, halafu simu inapigwa, mwenzako kapata ajali. Nilikuwa na mawzao mengi lakini nilishukuru kuwa sikumia kiasi cha kupoteza fahamu.

Hospitalini walinihudumia mara moja. Nilikuwa nimevaa suruali, walivyopandisha wakaona kuwa ngozi imechunwa kwenye gotii. Nilibakia kushangaa maana suruali haikuchanika. Baadaye walinipeleka X-ray. Bahati nzuri hakuna mfupa iliyovunjuika lakini nilikuwa nimeumia misuli tu kwenye goti. Wakanipa magongo, na madawa ya kupunguza maumivu na nikaenda zangu nyumbani kwa teksi. Nilikosa kazi siku mbili na bahati nzuri wikiendi ikaja. Nikapata nafasi nzuri ya kumpumzika. Baada ya hapo ikabidi nirudi kazini na magongo. Na mjue huko kwenye treni hakuna aliyenipisha kiti hata waliokaa viti maalum vya wagonjwa. Wengine wanakuaona halafu wanajidai wanasoma gazeti.

Lakini nashukuru sikuumia zaidi, na daktari kasema baada ya wiki kadhaa maumivu yatakwisha kabisa. Namshukuru Mungu kuwa sikuumia zaidi.