Tuesday, July 31, 2007

Mahojiano na Kaka Michuzi juu ya site yake kuwa Hacked!





Yawezekana umeshapata ujumbe uliosambazwa na Issa Michuzi mwenyewe au ule ambao Da’Chemi wa Swahili Times blog ameusambaza ikiwa ni tahadhari kuhusu e-mail ya kitapeli ambayo ilisambaa jana na bado inaendelea kusambaa hivi sasa ikidai Issa Michuzi amekwama hotelini huko nchini Nigeria na hivyo anaomba msaada wa kifedha.

Tungeweza kuipuuzia tu e-mail kama hiyo.Tatizo ni kwamba sio tu ni ya kitapeli,bali hivi sasa imemfanya Issa Michuzi ashindwe hata ku-update blog yake maarufu. Kimsingi e-mail ya issamichuzi at gmail ambayo ndio aliyokuwa akiitumia kuingia ndani ya blog yake haipo mikononi mwake tena! Ndio maana kama mnavyoweza kuona ukiitembelea blog yake tangu jana hajaweza kuweka picha mpya,jambo ambalo sio kawaida yake kabisa.

BongoCelebrity imewasiliana na Michuzi na kufanya naye mahojiano yafuatayo. Yasome na kisha mkumbushe na mwenzio kuhusu kwamba aipuuzie tu e-mail kama hiyo. Hapa Michuzi anaelezea nini kilitokea,lini ataweza tena kuendelea ku-update blog yake(archives zote bado zipo na zinapatikana online),vipi unaweza kuepuka yasikukute yaliyomkuta na anapatikana kwa njia gani hivi sasa? Majibu haya hapa chini;


BC:Nini hasa kimetokea? Ilikuwaje?

MICHUZI: Jana mnamo saa tatu na robo usiku nilifungua mtandao nyumbani na kupost picha kama nane hivi, ikiwa ni pamoja na za Rais mstaafu wa Marekani Bill Clinton na kumalizia na ya mafuvu ya wahanga wa mauaji ya kimbari kule Rwanda ambayo kuna mdau alinitumia. Kisha kama kawaida nikaingia kwenye issamichuzi at gmail.com ili kupitia maoni kama kawaida kwani issamichuzi.blogspot.com nimeitegesha kwamba maoni hayaendi moja kwa moja bali yanapita kwanza kwenye email yangu ndipo kama naona yanafaa nayaruhusu na kama hayafai nayazuia. Basi bwana, kwenye saa tano kasorobo hivi, ukaingia ujumbe ukidai unatoka kwa ‘Gmail Team’ unaofanya censor kutokana na malalamiko kwamba gmail siku hizi bomu kwa kuwa watu wamekuwa wengi, hivyo ujumbe ukanieleza jaza details zako ndani ya siku saba kama hutaki account yako kufutwa toka gmail.

Siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Na mimi ujumbe kama huo sio mara ya kwanza lakini wa safari hii, kama ningekuwa naamini juju-nangai ningesema jamaa wamepulizia maana nikajikuta najaza jina langu, umri na hata password na kusend. Huo ndio ukawa mwisho wa issamichuzi at gmail.com kwani nusu saa baadaye nikawa siwezi kuingia kwenye gmail tena.

BC:Uligundua vipi na saa ngapi kwamba e-mail yako imekuwa hacked?


MICHUZI: Niligundua niko hacked kwenye saa sita kasoro kumi wakati Da’Chemi aliponipigia kutoka Marekani na kuniuliza nimeenda lini Nigeria naye alipoondoka aliniacha Dar? Nikajua nimeshaumia baada ya kunieleza kwamba kuna mtu kaiba email yangu ya Gmail na anasambaza ujumbe wa kuomba msaada wa pesa kila mahali. Tukaingia kazini mimi na Chemi kuanza kuarifu watu wote tulioweza kuwafikia. Yeye kupitia blog yake ya Swahili Times nami kwa simu ya mkono na email yangu ya yahoo. Kwa kweli imenisaidia sana la sivyo saa hizi tungekuwa tunaongea mengine kwani wengi wangeamini ni mimi na kutaka kutuma pesa. Tena jamaa walivyokuwa hawana haya ati wamendikia hata mimi mwenyewe kupitia anuani yangu ya yahoo kuomba msaada wa pesa. Hahahaaaa!

BC: Umejifunza nini kutokana na tukio hili? Unawaambia nini wanablog wengine ili wajihadhari na tukio kama hili?

MICHUZI: Nimejifunza mengi sana, lakini kubwa na ambalo limenigusa sana moyoni ni kwamba wadau wananithamini na hakuna aliyesita kuniunga mkono na kuweka wazi kuwa tupo pamoja katika wakati huu mgumu.

La pili nililojifunza ni kwamba mtu usi-panic kwenye aina yoyote ya emergency, keep cool and ponder each and everything in its own perspective otherwise you will compromise your judgement the way your email address has. Usikurupuke.

Tatu na mwisho ni kuhakikisha una plan B katika kila ufanyacho kwenye maisha, hata kama yamekunyookea vipi. Kwa lugha nyingine hata kama blog itakufa leo (na haifi) nina plan B ambayo ni kubwa pengine kuliko blog.

BC: Unawaambia nini wadau wako.Lini site itarudi hewani?

MICHUZI: Asante kwa swali hili kwani wengi wametafsiri kwamba mtandao wa Michuzi ume-kuwa hacked na umekufa ama hauko hewani. Ukweli mtandao haujaguswa na wala hao jamaa hawajaingia huko. Wao wameingia kwenye email yangu ya Gmail na kuiba password kwa nia ya kutapeli watu. Uzuri wabongo sio mazezeta kama hawa jamaa wa ki-Nigeria wanavyodhani. Hivyo kukujibu lini narudi hewani ni kwamba kwa muda mfupi nitaacha ku-posti picha kwani ni hadi google watakaponipa password mpya pamoja ndipo nitaanza tena. Lakini kama unavyoona ukisearch issamichuzi.blogspot.com ama uki-google ‘michuzi’ unaipata blog yako kama kawaida kwani bado iko hewani.

BC: Unawaambia nini wadau,ndugu, jamaa na marafiki ambao walikuwa kwenye e-mail list yako? Wachukue tahadhari gani?

MICHUZI: nawaambia waachane kabisa kabisa na issamichuzi at gmail.com na watumie jina hilo hilo katika yahoo.com
BC: Wanaotaka kuwasiliana nawe hivi sasa watumie njia gani?


MICHUZI: issamichuzi at yahoo.com
Kama bado hujaisoma e-mail yenyewe ya kitapeli unaweza kuisoma pale Swahili Times.
Developing story…
Michuzi hivi sasa anapatikana katika http://isamichuzi.blogspot.com/
Tofauti yake na ile blog ya zamani ni “s” iliyopo kwenye issa,badala ya s mbili weka moja.

Bongoland II - Manzese


Picha hizi zinatoka Kwenye site ya Sam Fischer, ambaye ni Cameraman kwenye sinema ya Bongoland II. http://web.mac.com/samfischer/iWeb/Site/Africa%20Photos%202.html
Hapo juu Star wa Bongoland II Peter Omari, na actor mwingine wanajiandaa kuacti scene kwenye gari.
Scene inapangwa. Hapa Sam Fischer anapanga jinsi atakavyopiga picha ya scene ya kupigana.

Stunt Coordinator, Jason Hilton, akicheza Kung Fu na watoto wa Manzese.


Hapa wanapadisha camera kwenye crane.



Akina Sam walitengeneza Crane kwa ajili yakupandisha camera na kupiga scene kutoka juu. Ila bahati mbaya crane ilivunjika na haikuweza kutumika.




Uchochoro wa Manzese. Amini msiamini, zamani hii ilikuwa barabara ambayo magari yalikuwa yanapita. Baba mdogo alikuwa ana drive hapo na kupaki gari yake kwenye gereji yake. Sasa asante ujenzi holela hakuna barabara tena.



Muongozaji na Mwandishi wa sinema ya Bongoland II, Josiah Kibira, akifika kwenye nyumba ya Manzese.




Hapa Timu ya Bongoland II wana survey kama nyumba itafaa kwenye filamu. Nyumba hiyo ni ya marehemu baba yangu mdogo, Prof. Crispin Hauli. Na inatumika kwenye sinema ya Bongoland II kama nyumba ya 'Uncle'.

Forodhani


Nimeona hii picha kwenye internet iliyopigwa mwaka 1905 enzi za Mjerumani kutawala Tanganyika Territory. Naona kama ni eneo la Forodhani Secondary School, St. Joseph Convent pale Posta ya zamani au?

Blogu Mpya ya Michuzi

Nawataarifu kuwa Kaka Michuzi amehamisha site yake:

Anwani mpya ni: http://isamichuzi.blogspot.com/

KARIBUNI!

Monday, July 30, 2007

Konyagi Part II

Kaka Michuzi alinipiga picha na chupa ya Konyagi. Nilitoka kuinunua kwenye kiosk pale City Centre. Duh, hizo chupa kubwa za Konyagi mbona zilikuwa adimu safari hii. Niliona chupa ndogo nyingi lakini kubwa mmmhh sikuziona!

Konyagi Juu!

Kwa habari zaidi ya Konyagi, kinywaji kikali cha aina ya pekee bofya hapa:

KONYAGI

Siti Binti Saad

Siti Binti Saad 1880-1950

Kama kungekuwa na uwezekano wa kurudi nyuma katika miaka na kukutana na mtu maarufu ambaye aliwahi kuishi duniani, ningependa sana nikutane na Bibi Siti Binti Saad.

Bila shaka kwa sasa kuna watu wengi Tanzania ambao hawajawahi kumsikia, lakini Bibi Siti Binti Saad ni mwanzilishi wa Taarab, Tanzania. Siti alizaliwa katika familia maskini huko Zanzibar, lakini aliweza kuchukua muziki iliyokuwa unaimbwa kwa kiarabu na kuanza kutunga nyimbo zake na kuimba kwa Kiswahili. Pia zamani taarab ulikuwa kwa ajili ya matajiri tu, lakini aliufanya uwe kwa ajili ya wote.

Bibi Siti pia alisafiri hadi India kurekodi santuri kadhaa. Mwanafunzi maarufu wa Bibi Siti, bado yu hai, naye ni mpendwa Bibi yetu, Bi Kidude.

Nina website kuhusu maisha ya Siti Binti Saad. Na ni:

http://groups.msn.com/SitiBintiSaad/tributetositibintisaad.msnw


Karibuni.

Sofia Records

CCrew ya Bongoland II wakiburudika na Coca-Cola nje ya ofisi za Sofia Records.

Sofia Records ni kampuni inayohusika na mambo ya filamu na muziki, inayomilikiwa na Bwana Mussa Kissoky. Makao makuu ya kampuni hiyo iko Mwananyamala Komakoma, mjini Dar es Salaam. Kampuni hiyo ilitoa mchango mkubwa katika kutengeneza filamu ya Bongoland II hasa kwa masuala ya Usafiri na kutafuta sehemu za kufanya filming (locations).

Kichekesho:


Kuna siku nilipanda hiyo gari ya Sofia Records kusudi tukanunue bidhaa fulani. Nilikaa kiti cha mbele.

Basi wakati tunangojea traffic kweneye ile barabara ya Mabibo kusudi tuingie Morogoro Road kijana aka approach gari. Aliniamkia vizuri. "Shikamoo Mama Sofia!" Huko nimesahau gari imeandikwaje, kwa mshangao niliitika,"Marahaba" maana sina mtoto ambaye anaitwa Sofia.

Kijana kaanza, "Mimi nina leseni ya kuendesha gari Grade C, na pia nimesomea udereva, naomba sana unitafutie kazi."

Huko bado nashangaa nikamwambia, "Sawa nikisikia kuna kazi sehemu nitakujulisha". Jamaa kanitajia na jina na wapi pa kumpata.

Basi tukaendelea na safari, ndo watu kwenye gari wakaniuliza kama nilielewa ilikuaje. Waliambia kuwa yule kijana alidhania mimi nahusika na hiyo kampuni na alikuwa anaomba kazi. Ama kweli jet lag kitu kibaya. Maana kama ningemwelewa mara moja ningemwambia mimi ni pasenja tu kwenye hiyo gari na salamu zake ningefikisha kwa mwenye hiyo kampuni.

Kwa sasa naona kijana kaona kuwa "Mama Sofia" kamwangusha.

Friday, July 27, 2007

Michuzi Blog & E-mail is Hacked! ONYO!

TANGAZO MUHIMU
Wanablogu, nimegundua sasa hivi kuwa Blogu na e-mail ya Muhidini Michuzi imekuwa hacked!

Kuna Tapeli Nigeria amefanya hivyo!

Nimeongea na Michuzi sasa hivi na anaomba watu wasambaze habari kuwa site imekuwa hacked na hiyo e-mail kuwa anaomba hela haitoki kwake.

Kwa sasa mnaweza kumpata kwenye e-mail issamichuzi@yahoo.com.

******************************************************************************************* E-mail iiyokuwa hacked ni hii: muhidin michuzi [issamichuzi@gmail.com]

How are you doing today? I am sorry i didn't inform you about my traveling to Africa for a program called "Empowering Youth to Fight Racism, HIV/AIDS, Poverty and Lack of Education, the program is taking place in three major countries in Africa which is Ghana, South Africa and Nigeria.

It as been a very sad and bad moment for me, the present condition that i found myself is very hard for me to explain. I am really stranded in Nigeria because I forgot my little bag in the Taxi where my money, passport, documents and other valuable things were kept on my way to the Hotel am staying, I am facing a hard time here because i have no money on me. I am now owning a hotel bill of $ 1550 and they wanted me to pay the bill soon else they will have to seize my bag and hand me over to the Hotel Management.,

I need this help from you urgently to help me back home, I need you to help me with the hotel bill and i will also need $1600 to feed and help myself back home so please can you help me with a sum of $3500 to sort out my problems here? I need this help so much and on time because i am in a terrible and tight situation here, I don't even have money to feed myself for a day which means i had been starving so please understand how urgent i needed your help.

I am sending you this e-mail from the city Library and I only have 30 min, I will appreciate what so ever you can afford to send me for now and I promise to pay back your money as soon as i return home so please let me know on time so that i can forward you the details you need to transfer the money through Money Gram or Western Union.

Thanks.

Muhidin Michuzi.

****************************************

NAWAKUMBUSHA KUWA HII HABARI NI UWONGO NA UNATOKA KWA TAPELI HUKO NIGERIA!

Picha zaidi za Bongoland II Film Shoot Dar es Salaam

Cameraman and Cinematographer Sam Fischer, akifanya vitu vyake mitaani Dar es Salaam.
Moja wa Interns kutoka kampuni ya Sofia Records akirekodi somo kuhusu film editing kwenye shoot ya Magomeni.

Some of the UCLA interns at the shoot at Manzese. Manzese was the location for Uncles's house.



Mama Thecla Mjatta akisome script kabla ya scene huko Tanki Bovu.



Gayle alikuwa in charge kwenye msawala ya chakula. Hapa yuko Manzese.
Bwana Kibira alimdraftio baba yangu kuwa extra kwenye scene. Nyuma ni Mzee Olutu na Mama Thecla Mjatta .


Mbele ni mcheza sinema maarufu wa Bongo, Shafii. anaposi na interns wa UCLA, baba yangu na Peter Omari.


Mama Mjatta na Mzee Olotu wakipata maelezo kutoka kwa Mwuongoza sinema, Josiah Kibira kabla ya kufanya scene Manzese.


Stelingi Peter Omari, kama Juma, ambaye ni mhusika mkuu katika sinema ya Bongokand II.

Kwa kweli nashukuru kuwa nilipata nafasi ya kushiriki katika sinema ya Bongoland II. Ninamshukuru hasa Bwana Josiah Kibira, kwa kuandika script nyingine safi na kufanikisha kutengeneza kwenye sehemu halisi (authentic location) Dar es Salaam. Kwa kweli safari ilikuwa ndefu mpaka kukamilisha lakini yeye na timu yake walikamilisha.

Natumaini sinema ya Bongoland II ikitoka mtaifurahia mno.

Hizi ni picha zaidi na bado sijasafisha mikanda mingine.


Kwa habari zaidi za Bongoland II someni:

Mimi na Mcheza Sinema wa Marekani Cory Tyler

CoryTyler appearing on a USA TV Show.
Kushoto ni baba yangu, Dr. Aleck Che-Mponda, Kuwana Hausley (mchumba wa Cory), Cory, Mama yangu na mama Nancy Macha.

Tulipata bahati ya kutembelewa nyumbani, Tanki Bovu, na mcheza sinema kutoka Marekani, Cory Tyler. Alikuja na Mchumba wake, Bi Kuwana Hausley. Wanatembelea Bongo kwa mwaliko wa serikali kuona jinsi watakvyoweza kutangaza Utalii Tanzania.

Cory alianza kucheza katika televison na sinema za Marekani akiwa mtoto mdogo kabisa. Nilimtambua kwa vile alicheza kama 'Terrance' katika ile show, A Different World iliyohusu maisha katika Chuo Kikuu fulani Hillman College. Show ilianzishwa na Bill Cosby.

Pia Cory amecheza katika televison shows zingine kama Beverly Hills 90210, na Moesha. Kwa habari zaidi za Cory Tyler, nenda:

http://www.imdb.com/name/nm0878798/

Mimi na Michuzi

Tanzanian Photojournalist, Muhidini Issa Michuzi, akiburudika baada ya kazi ngumu huko Safari Carnivore, Mlalakuwa.

Mimi na Michuzi huko Safari Carnivore, Mlalakuwa. Michuzi alinipa offa, kwa kweli nyama choma pale ni tamu sana.
Michuzi naye anajua kuselebuka! Hapa yuko kwenye arusi huko Dar. Aliniambia anaalikwa kwenye arusi nyingi sana na anashindwa kuhudhuria zote, kwa siku anaweza kualikwa arusi hata tano! Kweli Michuzi amekuwa 'Popular'! (photo from Jiachie Blog)

Thursday, July 26, 2007

Mjue Msanii Mkongwe wa Bongo Mzee Godwin Kaduma

Mzee Kaduma akiburudika na sigara, huko akitoa mawaidha juu ya fani ya kutengeneza filamu. Mzee Kaduma alicheza kama Sekondo, katika sinema ya Arusi ya Mariamu. (1985)
http://www.grisgrisfilms.com/html/marriage_of_mariamu.html
Mzee Kaduma ndani ya Theater anayojenga. Anasema atakuwa anafundisha kozi za usanii hapo. Kwa kweli ni jengo safi sana. Bado haijaisha lakini.

Nilivyofika kwa Mzee Kaduma, niliburudika na soda baridi. Tulikuwa na manongezi marefu sana juu ya fani ya sinema Bongo, script development, na mambo mengi ya usanii. Nilifurahi sana siku hiyo kupata ushauri kuhusu filamu kutoka kwa Mzee Kaduma. Tulikuwa tumemwomba Mzee Kaduma acheza kama 'Uncle' kama sinema ya Bongoland II, lakini alikataa kutokana na majukumu mengine.


Mzee Kaduma na mbwa wake Tommy. Utashangaa Mzee Kaduma anavyoongea na Tommy na jinsi Tommy anayotii amri.



Hii ndo View kutoka backyard ya Mzee Kaduma.

Utengenezaji wa Sinema ya Bongoland II mjini Dar es Salaam

Msaidizi wa Josiah Kibira, Chris Audet kutoka Minnesota, akipanga mambo ya shoot. Hapa ni Manzese.

Mama Thecla Mjata anayecheza kama Mama yaka Juma, na Mzee Olotu anayecheza kama Uncle, akitoka kwa hasira ndani ya nyumba. Hapo ni eneo la Tenki Bovu.

Cameraman Sam Fischer, wakiandaa kufanya scene barabarani na Thecla Mjatta na Mzee Olotu.

Hapa ni Manzese. Tulipiga sinema kwenye maeneo hayo. Utatuona tunkimbia maeneo la uchochoroni, hapo ni sehemu moja tulipokimbia. Huyo baba ni Baba Saidi, mjumbe wa eneo hilo la Manzese. Pia alikuwa anakaanga samaki safi sana waliotoka freshi Ferry.


Josiah Kibira akimwelezea actor kuhusu scene ya 'chooni'.

Bongo Child Superstar Liz Michael Kimemeta alicheza kama mtoto muuza chapati. Liz alitueleza kuhusu ndoto yake ya kuja kuacti kwenye sinema za Hollywood. Kwa kweli mtoto ana kipaji. Nilimowna akihosti kipindi cha watoto kwenye TV Bongo.


Hapa wanashoot scene ya 'chooni' hapo Magomeni Mikumi.

Hapa wako Tanki Bovu nyumabni kwa wazee wangu.


Hapa Peter Omari anayecheza kama mhusika mkuu, Juma, akifanya scene na landlady wake anachezwa na mcheza sinema maarufu wa Bongo, Bi Hindu.

Mimi na Steven Kanumba


Siku ya kwanza kwenye shoot ya Bongoland II huko Magomeni Mikumi, tulibahatika kutembelewa na maSuperstar wa Bongo. Kulia kwangu ni mcheza sinema maarufu wa Bongo Steven Kanumba. Kushoto ni Emmanuel Myamba ambaye naye ni Bongo Superstar.

Kwa kweli nilifurahi sana kuwaona, hasa Steven maan nilikuwa nimesikia sifa zake na hasa habari ya sinema ya Dar 2 Lagos. Bado sijaiona lakini.
Kwa habari zaidi za Steven Kanumba soma:

WaKenya wajanjaruka na kufanya utapeli wa KiNigeria USA!


Hii story ni babukubwa! Maana itasababisha hata waTanzania wapate matatizo sasa. Waafrika wengi wanafanya hizi kazi za kuosha wazee na mataira. Sasa hii kesi itafanya tukose hata hiyo kazi!

Kwa miaka mingi waafrika hasa kutoka Afrika Mashariki waliweza kukaa USA bila makaratasi na kutokusumbuliwa sana. Ila baada ya hiyo tukio, lazima msako mkali ya East Africans USA inakuja.

*************************************************************************************
Grand Jury Indicts 17 People
UPDATED: 5:41 pm CDT July 19, 2007
E-mail this story Print this story

KANSAS CITY, Mo. -- A federal grand jury has indicted 17 people for allegedly using the identities of Kansas City-area nursing home residents to file bogus tax returns across the country.

They allegedly sought $13.1 million in refunds.

In an indictment returned Wednesday and unsealed Thursday, prosecutors charge the defendants with stealing the personal information of around 300 individuals and using it to file at least 365 fraudulent federal tax returns beginning as far back as February 2005.

U.S. Attorney John Wood told reporters the conspirators also filed fraudulent tax returns in 27 states.

Wood said some of the refunds paid to the defendants were cashed and transferred to the African nation of Kenya, where 12 were either born or held citizenship.

"We're seeing identity thieves using more complex and sophisticated methods to commit their crimes than ever before," Wood said.

The indictment names as defendants Loretta Wavinya, 30; Ervin Somba, 26; Edwin Nyumu Sila, 25; Lillian Nzongi, 26; Moses Ndubai, 33; Bernard Nyemba, 39; Jeanette Alexander, 38; Michael Anderson, 46; Rashira Lewis, 20; and Parker S. Willingham, 23, all of Kansas City; Vincent Niagwara Ogega, 23, of Independence; Aaron Mutavi, 28, of Overland Park, Kan.; Kenneth Njagi, 31, of Lenexa, Kan.; Mary Githia, 25, of San Francisco; Ernest Kangara, 40, of Santa Rosa, Calif.; Paul Kilungya Nyumu, 41, address unknown; and Karingithi Kamau, age and address unknown.
Prosecutors said 10 of the defendants are in custody and being held pending a hearing, three are believed to be living in Kenya and four are unaccounted for. Wood said his office is working with officials in Kenya to try and find the defendants there.
According to the indictment, Wavinya and seven other defendants worked in Kansas City-area nursing homes and hospitals and had access to patient information.
"Frankly, it's not hard to get identity information in an institutional situation," said assistant U.S. Attorney J. Kurt Bohling.

The indictment claims Wavinya, who worked as a tax preparer at H&R Block Inc. in late 2002 and early 2003, and others prepared and filed false tax returns under the victim's names, listing jobs and income the victims had never had and claiming thousands of dollars in tax refunds. The returns were filed electronically, sometimes using public Internet portals, such as those in coffee shops, or by piggybacking on someone else's wireless Internet signal.

The refunds were deposited in bank accounts allegedly opened by the defendants, who then used a series of "runners" to withdraw the money in increments less than $10,000 each in an attempt to avoid federal scrutiny, the indictment claims. In some cases, Wood said, bank officials or the IRS grew suspicious and froze the accounts.

Some of the money was wired to banks in Kenya or withdrawn through ATM machines there. In other cases, the refunds were electronically deposited on prepaid debit-style cards obtained anonymously over the Internet.

Besides the overall conspiracy charge, the indictment charges 14 of the defendants with wire fraud, charges Wavinya with two counts of aggravated identity theft and charges Nzongi with money laundering.

Wood said some of the defendants may have been in the country on expired visas.

KWA HABARI ZAIDI SOMENI:

http://allafrica.com/stories/200707230039.html

http://www.usdoj.gov/usao/mow/


DAILY
NATION


The arrests sent shock waves among Kenyans living in Kansas City, many of
whom have taken up nursing jobs who now fear that employers might be wary of
hiring them.

Tuesday, July 24, 2007

Niko Dubai Tena




Haya ndugu wasomaji wapendwa, niko njiani kurudi USA. Niko Dubai Airport ni midnight (Saa sita za usiku) nangojea flight ya kwenda New York.

Samahani nilibanwa sana kwenye shghuli za sinema, lakini nadhani mtapenda sinema enyewe. Itatoka hivi karibuni. Hiyo Emirates ni ndege safi sana. Wanachukua soko ya British Airways / KLM etc. naona na Qatar Airways wameingia na bei nafuu za tiketi.

Mengine Kesho kutwa.

Na kwa yule aliyekuwa na wasiwasi....mbona nilikuwa na simu Bongo.

Monday, July 16, 2007

Bagamoyo Road

Leo nimekwenda mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Barabara safi kabisa. Ila magari yanaenda kwa kasi na wana overtake hata kwenye maeneo ya solid lines. Mji wa Bagamoyo unapanuka kweli, na hapajalala kama zamani.

Anayecheza kama Juma, Peter Omari amefiwa na alienda kuzika, hivyo nilikuwa na mapumziko kidogo.

Sunday, July 15, 2007

Maendeleo Bongoland II

Tunapiga hatua katika shooting ya sinema, Bongoland II. Juzi tulipiga scene ya Car Chase Manzese, na watu kukimbia kwenye vichochoro vya huko. Authentic hasa. Wacha nikanyage maji machafu ya bafuni, si mnajua Manzese hakuna sewage system!

Sinema ina mapenzi, lakini kwa sasa sisemi ni kati ya nani na nani. Mtaona wenyewe.

Bwana Kibira amekutana na problem ya actors wa Bongo kutaka kuigiza kama zile sinema za Nigeria. Kuna mikasa mpaka unaweza kuanguka chini kwa vicheko. Hivyo actors wengine wa awali wamebadilishwa. Lakini anajitahidi sana kuwapa training ya style anayotaka kwanza, wakishindwa ndo kwa heri. Mama Mjatta na Mzee Olotu ni A+ actors.

Watu wamekuwa freshi kweli kila sehemu tukienda ku-acti. Na picha zimepigwa kibao.

Juzi cameraman wetu Sam Fischer, alianguka na kuteguka mguu. Alikuwa analia kwa maumizu, ikabidi apelekwe hospitli. Lakini mzungu wa ajabu huyo hajaomba evacuation, anabaki na kuendelea kushuti na magongo yake.

Kichekesho. Tuko na mabinti wa chuo kikuu cha UCLA, sasa hivi wamebakia wawili tu., tulianza na kumi. Wanataka kula maisha tu. Bwana Kibira alienda Slipway kwenye shughuli fulani. Huko si ndo kakutana na moja wa hao mabinti akishuka kwenye boti akitokea sijui kisiwa gani. Kibira kamwuliza kwa nini hakwenda kwenye seti. Yule binti alikuwa hana la kusema. Pia tuna interns wa Bongo wanaotoka kampuni ya Sofia Records.

Thursday, July 12, 2007

Dar es Salaam

Salamu nyingi sana kutoka Dar es Salaam. Kwa kweli hali ya hewa siyo joto kama iliyokuwa nilivyokujwa mwaka jana Novemba. Kwa sasa hali ya hewa siyo mbaya. Kwa mara ya kwanza umeme umekatika hapa kwetu Mbezi Beach. Hii cafe wana generator, ila air condition haifanyi kazi ni joto balaa.

Ila bado kuna mavumbi na msongamano wa magari umezidi kuwa mbaya mno. (TRAFFIC JAMS). Nimekwisha shuhudia accident za magari kama nne hivi. Bahati hakuna aliyeumia, ila magari yao ndo yaliumia.

Filmming ya Bongoland II inaenda vizuri sana. Tuko na wasanni maarufu wa hapa Mzee Olutu, Shafii, na mama mjatta. Wanafanya kazi nzuri sana. Bongoland II itakuwa safi sana.

Ila bado nalalamika, internet connection nayo tumia ni mbaya. Niko Mbezi Squre, Silver cafe, na naona kila mtu anapta shida kufungua site wanazotaka, mpaka watu wana hama hama computa. Bado sijaweza kufungua site ya Michuzi, na site yangu ila naingia kupitia blogu moderation.

Nina picha nyingi za kubandika. Haya siku nyingine. Leo nilikuwa na mapumziko kidogo. Kesho naendelea na shooting ya Bongoland II.

Sunday, July 08, 2007

Niko Dar na nina mengi ya kuwaelezea. Ila internet connection shida. filiming ya Bongoland II ilianza Ijumaa iliyopita.

Leo nilitembelea Saba Saba.

Nina picha na habari nyingi tu. Natafuta connection nzuri.

Thursday, July 05, 2007

Safarini Tanzania

Kwa sasa niko Dubai. Natumia keyboard enye maandishi ya kiarabu. Bahati nzuri najua keys ziko wapi. Airport ya Dubai ni safi sana. Hata bathrooms nu safu kuliko za JFK New York. Duty Free nzuri pia.
Ila joto. Air condition haifanyi kazi vizuri.

See you in Dar soon.

Tuesday, July 03, 2007

Wazazi Wangu safarini Boston

Kutoka Kushoto, Mhesimiwa Frederick Sumaye, Dr. Aleck Che-Mponda, mimi na mama yangu. Tulienda kumsalimia Mheshimwa Sumaye, ambaye kwa kweli alikuwa mkarimu sana. Msaidizi wake alitupikia mishikaki mitamu kama nyumbani. Mheshimiwa Sumaye amemaliza masomo yake Harvard University hivi karibuni.


Baba akiagana na Mheshimiwa Sumaye ambaye alikuwa jirani yangu hapa Cambridge, Ma. Ndo siku nilikabidhi kanda za sinema ya Tusamehe na Bongoland.

Baba na Mama wakiwa South Station, Boston Ma. kuelekea New York City ambapo walienda kusalimia ndugu na marafiki.


Dr. Aleck Che-Mponda akicheki sanamu ya mbwa aina ya St. Bernard huko Mohegan Sun.