Wednesday, October 08, 2008

Magofu Yanabomolewa Tanga



Picha na maelezo kutoka Jiachie Blog:

Sio Dar tu majumba makuu kuu yanakula nyundo kupisha majengo mengine mapya na ya kisasa,la hasha hata kwa wagosi wa kaya nako kazi ni moja tu,kusafisha majumba yalijichokea na kuleta mapya yatakayoleta sura iliochangamka na ya kuvutia katika mji wa Tanga.Tatizo katika ubomojai wamajumba haya ni kwamba wameyabomoa kidogo sijui kuwatisha wenye nyumba/wapangaji waondoke halafu wameyaacha hivyo hivyo,kutokana na hali ya hayo majengo baadhi ya wakazi wa tanga wameanza kulalama kwamba kama wahusika wameamua kuyabomoa majumba hayo basi wayabomoe na si kuyaacha kama yanavyoonekana pichan kwani yanatishia usalama wa wapita njia.
********************************************************
Hivi wadau, kuna Historial Preservation society huko Tanga? Wasiwe wanabomoa majengo ya kihistoria. Sawa ni 2008, lazima twende na wakati lakini pia history ya mji usifutwe kabisa!

1 comment:

Anonymous said...

hakuna kitu kama kuhifadhi historia ya mjii katika tanganyika.ikiwa jumba la makumbusho dar wameuza na kuiba kila kitu cha historia?usishangae ukakuta hata mlima wa kilimanjaro utakua umeuzwa kwa george bush...bongo tambarare kwa kufisadi na kujisahau kwa kila kitu mpqka waje wadhamini..si tumezoea rushwa na kujiiibia sisi wenyewe.kalaga baho...mpaka mitihani inauzwa na vyeti vya jchuo kikuu vyote tender ,hiyo ndio nchi yetu kurudi nyuma kimaendeleo ndio kasi mpya na awamu ya christopher columbus..