Wednesday, January 23, 2008

Mapigano katika sinema ya Bongoland II


Peter Omari na Charles Magali wakifanya mazoezi kabla ya kushuti scene

Jason Hilton coaches Shaffi & Mzee Olotu for a fight scene
Jason Hilton coaches Mzee Olotu on how to fall during a fight scene
Jason Hilton plays 'Kung Fu' with curious neighborhood kids while filiming in Manzese
Josiah Kibira discusses with Jason Hilton and Shafii on the logisitics of a fight scene

Watu wanangojea kwa hamu sinema ya Bongoland II.

Kwenye crew ya Bongoland II kulikuwa na mtaalamu wa mambo ya stunts (kupigana, kuanguka nk katika sinema) anaitwa Jason Hilton. Nilivyokuwa Bongo niliwaambia baadhi ya wasanii kuwa wawe makini kujifunza maana alikuwa anatoa somo bure. Hapa Marekani ukitaka masomo ya stunt unalipia hasa.

Kwa kweli kuna umuhimu wa mwalimu wa kufundisha stunts kwa wasanii Bongo. Nilishangaa sana nilipoambiwa kuwa eti katika sinema za Bongo, ukiona watu wanapigana au mtu kazabwa kibao basi wanafanya kweli hadi kuumizana! Hollywood mnaona watu wanapigana kumbe hakuna mtu aliyeguswa. Mfano kwenye ile sine ya Aftershock:Beyond the Civil War ambayo nimo, utadhani jamaa wanapigana kweli. Kumbe jamaa hakuguswa hata kidogo. Nakumbuka walivyoifilm na final product nikashangaa kweli utadhani jamaa kaua!

Website ya Jason Hilton ni: http://www.tumblemonster.com/pages/gallery.html

Hapa mnaweza kuona clip fupi ya mapingano kutoka sinema ya Bongoland II.

Note inachukua muda ku-load.

http://www.tumblemonster.com/video/TMPStuntSchoolReel.mov

4 comments:

Anonymous said...

Kumbe Kibira alienda na wataalam Bongo wa filamu. Doh! Ni kweli ulivyosema watu alitakiwa wajifunze kutoka kwao. Sasa Da Chemi hiyo sinema tutaiona lini. Sasa kweli nina hamu ya kuiona.

Anonymous said...

Chemi hizi sinema zenu zinaonyeshwa katika Sayari gani? Mbona mimi sijawahi kuziona? Huku nilipo, Helsinki sijawahi kuziona na kama ungefanya utaratibu wa kueneza soko zitufikie na sisi tutashukuru.

Anonymous said...

This looks like it will be an interesting film. Congratulations to Mr. Kibira and crew.

Anonymous said...

Hivi hakuna mtu aliyeumia kweli kwenye hiyo sinema? Mapigano ni makali kweli kweli!