Wednesday, January 30, 2008

Mnenguaji Aisha Masinda anahitaji Msaada!

Wapendwa wadau,

Nimepokea hiii e-mail kuhusu Mnenguaji maarufu, Aisha Madinda, wa African Stars Band- Twanga Pepeta.

**********************************************************************

Habari yako, ukiwa kama mmmoja wa wazalendo naamini kabisa kwa namna moja ama nyingine utaguswa na ugonjwa unaomuandama Aisha MAdinda!

Aisha anahitaji msaada ili aweze kumudu matibabu anayoendelea nayo katika Hospital ya Taifa Muhimbili hivyo basi kama nawe utaguswa katika hili unaweza kwa kumsaidia kubandika habari hii niliyokutumia katika blog yako ili ujumbe huu uweze kusambaa zaidi!


Natanguliza shukurani zangu kwa kukubali kubandika habari hii!

Asante,
Tulizo Kilaga



****************************************************************************

Ugonjwa wa Aisha Madinda "Ngoma Nzito"


Ugonjwa wa Mnenguaji maarufu wa Bendi ya African Stars International, Aisha Madinda (27) hivi karibuni ulidhihilisha kuwa ni "ngoma nzito" kutokana na vipimo vya awali kuonesha asumbuliwi na ugonjwa wowote huku miguu ikiendelea kumvimba kila kukicha.

Aisha Madinda hivi karibuni alinukuliwa na gazeti moja la michezo nchini akisema kuwa, hali yake bado iko vile vile na miguu bado inamsumbua licha ya kufanyiwa uchunguzi wa awali.
Mnenguaji huyo aliongeza kuwa, kushindikana kuonekana ugonjwa wake kumesababisha madaktari bingwa wa moyo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam juzi (Jumatatu) mchana kuanza kumfanyia uchunguzi wa kina.

"Uchunguzi wa awali umeshindwa kubainisha ugonjwa wangu ndio wamenirudisha kwa madaktari bingwa wanifanyie uchunguzi zaidi, miguu imevimba na sijisikii vizuri, lakini kinachonisikitisha zaidi ni kutoonekana kwa maradhi yanayonisumbua. Nawaachia wataalam, nina imani kama kuna kitu hawa hawawezi kushindwa na suluhu ya tatizo langu itapatikana mapema, Mungu ni wa wote na naamini kwamba atanisaidia na hii ni hali ya kawaida tu kwenye maisha, wala siamini maneno ya watu kuwa nimepigwa juju," alisema Aisha.

Aisha Madinda ambaye ni mama wa watoto wawili wanaosoma sekondari, amekuwa nje ya jukwaa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa.

Mnenguaji huyo, amewaomba wadau mbalimbali na mashabiki wa muziki nchini kuendelea kumsaidia kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na kugharamia matibabu yake kupitia namba 0717 555557 ambayo ni ya meneja wake.


Kutoa ni moyo si utajili mimi nimeanza kwa kumchangia kwa kuusambaza ujumbe huu!!

11 comments:

Anonymous said...

Dah! Pole sana Aisha Madinda. Sasa huo ugonjwa wa ngoma nzito si UKIMWI kweli?

Anonymous said...

dawa yake achakuneng'ua sasa halafu huu unaweza kuwa utapeli

Anonymous said...

Pole sana dada yangu, ila mungu ananjia nyingi za kuwafanya viumbe wake wamkumbuke, I hope huu ndo muda wako wa kutubu kama tufanyavyo wenzako (maana sote hufanya dhambi) na uaminikwamba kumbe haya maisha ya dunia ni si kitu, leo mzima kesho waweza kuwa mahtut au marehemu kabisa, ujuwe kwamba pumzi anayokupa muumba isikulevye ukafanya utakavyo mpaka ukachupa mipaka, naamini unaomuda wa kutafakar na kurekebisha pale ulipomkosea yeye alie na uzima (yeye ndo DAKTARI BINGWA sio hao wamuhimbili unaosema), Aisha jina zuri mashaallah lakini aah , hukuona kazi njema iliyobora hata kwa muumba wako, isipokuwa kazi ya kucheza uchi jukwaani (Laahaula..), kama haitoshi mtoto wakiungwana ukapiga picha za uchi ukazianika kwenye mtandao (Malipo duniani ahera kuhesabiwa). Sina nia yakukusimanga la hasha bali kukukumbusha wewe na kuikumbusha nafsi yangu. Huo ni mtihani wa mungu na yeye ndie atakae kuondolea, wengine wamekatwa mikono kwa mabaya yao wengine walikufa kwa ajili miili ikanyambuka nyambuka hata yale makalio waliokuwa wakitingisha kwa ufahari pia yakasagika(Akina SHENAZ) (sub hanna llah). Wewe na mimi mungu bado anataka turudi kwake tukiwa wasafi, ndo maana anaendelea kutuacha hai, ila anatupa mitihani tutubie. Jee huoni kuwa anakupenda?!Dada yangu Asha nahisi msaada wangu huu ni bora kuliko anaekupa hela kwa matibau, sababu kama utaufuata utapata uzima wa mguu wako kwa hapa duniani na kesho yaumul haki!
Dada Asha swali, funga na mtake msamaha Mola wako, mungu ni mwenye huruma na nimsikivu kwa wanaomuomba na kumtaka msamaha...na kwake kila kitu kinawezekana( kun fayakul) akisema kuwa huwa.Hakika nyanyuka usiku swali zungumza na mola wako, mwambie nimekuskia mungu wangu naomba uniondolee mtihani huu, kwa moyo wa unyenyekevu na utiifu mbele ya yeye alie mbora, kwa hakika mungu hasemi uongo kama amesema niombeni niwape (adduuni yastajiblakum) basi utapona Inshaallah. Namie nakuombea uzim dada yangu Mungu akupe uzima wa mwili na roho (Ameen).

Naomba dada chemi nipe nafasi japo ya mwisho (usibane)..ubarikiwe sana.

Anonymous said...

kwanza pole sana aisha madinda pili hebu tupe umri kwanza wa watoto wako maana wameandika hapa kuwa ni mama wa watoto wawili wanaosoma sekondari na wewe una umri wa 27 hao watoto uliwazaa ukiwa na umri gani? au miaka 13 au 12?

Anonymous said...

Boyfriend wangu ni daktari kaniambia huo ugonjwa wake unaitwa Kaposi sarcoma, miguu huwa inavimba halafu inakuwa migumu kama mbao. Namuombea kwa Mola amjaalie nafuu, aamin.

Anonymous said...

Jamani Kaposi Sarcoma ni dalili ya UKIMWI! Aisha weee! Pole sana. Tunakuombea upone.

Anonymous said...

ana watoto wawili wapo sekondari na yeye mwenyewe ana miaka 27 amewazaa akiwa na umri gani???

pili misaada ipelekwe kwa kupitia kwa meneja wake kwani hana mume huyu?? kama ameolewa kwanini isitolewe namba ya simu ya mumewe??

naona kama usanii hapa

Anonymous said...

kapigwa kuung'uta huyu.muharakisheni kwa mzee hainehaine bagamoyo.msisahau kwenda na nyoka mwenye kengeza

Anonymous said...

Aisha anabahati kwa kuwa anafanya/alikuwa mfanya kazi hivyo lazima atakuwa na akiba bank, vilevile kama muajiliwa wa sekta binafsi muajili wake anapaswa kusaidia matibabu (As band pesa wanayo sana tu) sio kuomba michango ya sisi walala hoi ambao hata kazi hatuna.

Sisi walalahoi ndio tunawategemea ninyi ma-star mtusaidie sio kinyume wandugu mwee!

Nionavyo mimi.

Anonymous said...

Maybe she is suffering from Elephantiasis. She is not Bewitched (uchawi).

Anonymous said...

Good Question on her marital status.

KAMA MR. MADINDA SASA HANA MSAADA HAPO BASI HATA KUBAKI NA HILO JINA HAKUNA MAANA.
AISHA WAHI MAHAKAMANI UBADILI JINA PENGINE UENDELEZE JINA LA BABA YAKO INSTEAD!

HILI SUALA LA KUBEBA JINA LA MTU AMBAYE WALA HANA MSAADA LIMEPITWA NA WAKATI.
HATA HIVYO YEYOTE ANAWEZA KUMSAIDIA PIA.