Friday, January 18, 2008

Mtoto wa Osama Bin Laden anataka Amani


Mtoto wa Osama bin Laden (26), Omar Osama bin Laden anasema anataka 'Amani' duniani. Huyo mtoto ni tofauti kabisa na baba yake ambaye ameua maelfu ya watu duniani bila huruma wala majuto na kudai ataua maelfu zaidi.
Osama bin Laden ndiye ali-organize kulipuliwa kwa ubalozi za Marekani katika miji ya Dar es Salaam na Nairobi. Pia ndiye ali-organize matukio ya Septemba 11, 2001 ambayo yalisababisha vifo vya watu karibu elfu nne siku hiyo.
Omar anasema anataka kuwa Balozi wa Amani kati ya nchi za kiislam na nchi za Magharibi.
Mke wa Omar ni mwingereza, Jane Felix-Browne mwenye miaka 52. Kwa sasa wanakaa Misri.
Kwa habari zaidi someni:

6 comments:

Anonymous said...

Now,if he could only convince his dad...

Anonymous said...

Chemi inabidi uwe makini unapoandika,kwani Bin Laden hajathibitishwa kuwa ndiye aliyepanga mashambulizi ya dar es salaan na nairobi, ndio maana siku zote anaitwa mtuhumiwa wa ugaidi. sina maana kuwa mtu mzuri,bali naona kama unapotosha kusema alipanga yale mashambulizi,inabidi ufahamu kuwa matawi mengi ya al-qaida ambayo hata Bin Laden mwenyewe hayajui, na siku zote yanafanya ugaidi kwa jina hilo. Sijui kama unakumbuka hata baada ya september 11, Bin Laden aliweka wazi kuwa alifurahishwa na lile tukio lakini hausiki kwa namna yoyote. Ila ukweli unabaki kuwa itikadi ya Bin Laden imewavutia watu wengi na imeleta maafa mengi ya watu wasio na hatia

Anonymous said...

Nimeona kipindi cha TV hapa UK kinachomzungumzia huyo kijana. Anasema anampenda sana baba yake. Huyo mkewe naye ni msanii fulani, walioana baada ya kufahamiana siku 2 tu! Ni mama fulani hivi mpenda ngono, ana miaka 52, keshaolewa mara kibao na kote huwa anafuata ngono tu, sasa amemngangania huyo kijana wa watu mwenye miaka 30 tu ili ajipatie pia umaarufu kwa sababu ya jina la huyo Osama. Keshatengeneza hela kibao kutokana na documentary za TV.

Anonymous said...

dada chemi wewe ni mwandishi inabidi hizi habari uwe unazifuatilia, huyu ana mke wa kwanza mwarabu na mama muingereza alikuwa mke wa pili ambaye hata hivyo wametalikiana kwa sababu ambazo huyo omar alisema ni za kiusalama kwake na kwa huyo mama.. huyo mama hiyo ni ndoa yake ya 6 ni msanii sana na sasa eti anavaa ninja akiwa hapa uk na anasaini autograph kama celebrity fulani hivi, alijipatia millions kutoka the sun baada ya kuuza habari huko, ila katika documentary ya huyo mama ambayo ni ya mwaka jana mwishoni alisema kuwa ana imani kuna sikuwatarudiana....

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 11:35am, hizo habari za huyo mama kuwa na waume wengi na huyo mzungu ni mke wa pili tena walifunga ndoa baada ya siku mbizi tu za kujuana, nilijua. Lakini skuona haja ya kuzisema hapo. Pointi ilikuwa kuwa mtoto anataka kuwa Balozi wa Amani. Mengine tunaweza kujadili baadaye.

Anonymous said...

Chemi ni mwandishi by cheti (ana cheti cha uandishi) lakini her ineptitude in that professional beggars belief.

Lakini haya si matatizo yake, ni matatizo ya kitaifa. Nyumbani watu wanasoma siyo ili waelimike bali wapate kuajiriwa. Ndo maana wakishapata kazi tuu, elimu haina matumizi tena.