Monday, January 28, 2008

Academy Awards wanaijua Tanzania







Mwaka 2001, Tanzania ilipeleka sinema, Maangamizi The Ancient One, kushindana katika, 74th Academy Awards. Ilishindana katika kipengo cha 'Foreign Language' (Lugha za kigeni). Sinema hiyo ilikuwa ya kwanza kutoka Tanzania kupelekwa. Ilikuwa kati ya sinema 51, zilizopelekwa na nchi kadhaa huko mwaka huo.

Hatimaye haikufika katika sinema tano bora zilioingia katika raundi ya mwisho kupewa tuzo ya Oscar. Mwaka huo sinema ya 'No Man's Land' kutoka Bosnia Herzegovina, ilishinda.

Ili sinema ifike Academy Awards ni lazima iwe na sifa kadhaa. Sinema ya Maangamizi ilikuwa na sifa zote.

Je, sinema ya Bongoland II, itakuwa sinema ya pili kutoka Tanzania kupelekwa Academy Awards?

Mnaweza kusoma Press Release ya Academy Awards 2001, hapa:

Tutaona mambo yatakavyokuwa.

1 comment:

Anonymous said...

Mbona Oscar ya Kanumba haifanani na hiyo kwenye picha?