Blogs in Kiswahili, the main African language of EAST AFRICA.
Saturday, February 02, 2008
Hollywood in Bostwana!
Tanzania tujifunze kutoka Botswana. Serikali ya Botswana imetoa baraka zote kwa ajili ya kutengeneza hii sinema huko. Hata mawaziri na viongozi wa dini wana acti kwenye hii filamu!
Nashukuru sana kwa kazi nzuri ya kutupa fununu na kutuweka katika mwangu kuhusu mambo mbalimbali hasa ya kuhusu mambo ya filamu. Mimi huwa napendelea sana kusoma huu ukurasa wako, maana nina mabinti ambao hupendelea kuigiza. Huwezi jua mara iko siku nikawa mgeni wako huko Boston.
Kwakweli leo umenikuna na nimefurahishwa sana na hiki kipande cha Ma Ramotswe. Huwezi amini nimesoma vitabu vyake vyote viko saba kama sikosei. Nilikuwa nacheka sana wakati nikisoma na vilikuwa ni vitabu rahisi sana kusoma na kuona picha yote. Maana mimi napenda kuona picha katikati ya mistari. Kesi zake zote ingawa si kama James Bond, au J. H. Chase, huwa ni rahisi kutatua na zina mafundisho mazuri tu. Na vile anavyofikiria ana mzidi hata Kojak yaani ni kama tu mimi na wewe tunavyofikiri, raha tupu... Na hata anavyofagilia Botswana na wanawake wenye maumbo ya kiafrika kama mimi, yaani utapenda na ndio maana serikali yake pia imetoa msaada mkubwa. Mwandishi wa vitabu hivyo ni Alexander McCall Smith, yeye ni kutoka Scotland ila hata mimi sielewi amewezaje kukamata hiyo mandhari na fikira za kiafrika asili. Tunahitaji vitabu kama hivyo ili kuwafundisha na kuwapa moyo watoto wetu hasa wale waliokulia katika nchi za magharibi, ili waelewe kiundani nini maana ya kuwa wa-Afrika na waweze kujivunia uafrika wao.
Naomba unidodose wakati sinema ikitoka, maana naingojea kwa hamu.
I worked for Tanzania's Daily News for 11 years leaving as a Senior Reporter. I love acting, films, short story writing and cooking. I blog in English and Swahili. I am a member of the Screen Actors Guild (SAG) and AFTRA.
You can contact me at chemiche3@yahoo.com.
2 comments:
Da Chemi,
Nakutakia heri ya mwaka mpya 2008.
Nashukuru sana kwa kazi nzuri ya kutupa fununu na kutuweka katika mwangu kuhusu mambo mbalimbali hasa ya kuhusu mambo ya filamu. Mimi huwa napendelea sana kusoma huu ukurasa wako, maana nina mabinti ambao hupendelea kuigiza. Huwezi jua mara iko siku nikawa mgeni wako huko Boston.
Kwakweli leo umenikuna na nimefurahishwa sana na hiki kipande cha Ma Ramotswe. Huwezi amini nimesoma vitabu vyake vyote viko saba kama sikosei. Nilikuwa nacheka sana wakati nikisoma na vilikuwa ni vitabu rahisi sana kusoma na kuona picha yote. Maana mimi napenda kuona picha katikati ya mistari. Kesi zake zote ingawa si kama James Bond, au J. H. Chase, huwa ni rahisi kutatua na zina mafundisho mazuri tu. Na vile anavyofikiria ana mzidi hata Kojak yaani ni kama tu mimi na wewe tunavyofikiri, raha tupu... Na hata anavyofagilia Botswana na wanawake wenye maumbo ya kiafrika kama mimi, yaani utapenda na ndio maana serikali yake pia imetoa msaada mkubwa. Mwandishi wa vitabu hivyo ni Alexander McCall Smith, yeye ni kutoka Scotland ila hata mimi sielewi amewezaje kukamata hiyo mandhari na fikira za kiafrika asili. Tunahitaji vitabu kama hivyo ili kuwafundisha na kuwapa moyo watoto wetu hasa wale waliokulia katika nchi za magharibi, ili waelewe kiundani nini maana ya kuwa wa-Afrika na waweze kujivunia uafrika wao.
Naomba unidodose wakati sinema ikitoka, maana naingojea kwa hamu.
Ubarikiwe.
Lilly, UK
Kweli hii lazima itakuwa sinema nzuri sana. Nangojea kwa hamu!
Post a Comment