Friday, February 08, 2008

Nani atakuwa Waziri Mkuu sasa?

Mara Mh. Lowassa alipotangaza kujiuzulu kwake, wananchi walianza kuulizana na kutabiri nai atakuwa Waziri Mkuu mpya.

Je, ingefaa arudishwe mtu mwenye uzoefu na hiyo kazi nzito. Wapo Mzee Malecela , Mzee Sumaye na Mzee Warioba. Je, Mzee Salim Ahmed Salim?

Je, Rais Kikwete atamchagua mtu mgeni kabisa? Je atamchagua mwanamke?

Kuna maswali mengi na kuna watu ambao watashikwa na homa wakiwaza mrithi wa Lowassa.

Nacho weza kusema ni kuwa wananchi na TZ Diaspora watamweka chini ya darubini (microscope).

Mungu ambariki na kumpa nguvu atakayeteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya.

Mungu Ibariki Tanzania na Watu Wake.

****************************************************************************

Kutoka ippmedia.com

Wananchi wanong`ona wanaofaa kumrithi Lowassa '

2008-02-08

Na Mwandishi Wetu

Kufuatia Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa, kutangaza kujiuzulu, wananchi wamekuwa na shauku kubwa ya kujua nani atakayemrithi endapo Rais Kikwete atamkubalia. Hata hivyo, kumekuwa na majina ya mawaziri kadhaa wa kuchaguliwa yaliyokuwa yakizungumzwa zungumzwa kwamba wanafaa kumrithi Bw. Lowassa.

Miongoni mwa majina hayo ni pamoja na la Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Bernard Membe, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. John Magufuli na Waziri wa TAMISEMI Bw. Mizengo Pinda.

Mwingine aliyetajwa ni mbunge wa Sumbawanga, Bw. Paul Kimiti.

Aidha wananchi wengi walizungumzia kuwepo haja ya kuteuliwa Waziri Mkuu mwanamke. Wanawake waliotajwa ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Getrude Mongela na Anne Kilango Malecela.

SOURCE: Nipashe

No comments: