Wednesday, February 13, 2008

Kipanya Anasema...


Duh! Nimeblow na hii! Yaani anamwita PM 'Beast'? Kweli kuna uhuru wa vyombo vya habari Bongo siku hizi maana Mwalimu asingevumilia. Wadau mnasemaje?

16 comments:

Anonymous said...

Kweli Kipanya anagepelekwa pale pahala Oyster Bay na kiminywa. Baada ya hapao asingethubutu kuchora kitu kama hicho tena.

Anonymous said...

Adabu hamna!!

Anonymous said...

Da Chemi nimecheka kweli! hiyo Torture chamber ya Mwalimu imehamia Kunduchi haiko Oyster Bay tena! Kweli Kipanya kakosa adabu leo!

Anonymous said...

Haya ndio matatizo ya uhuru wa habari, vyombo vingi vya habari ikiwemo clouds fm watangazaji wake si watu wanaoheshimu taaluma yao na kutoa habari kwa kuzingatia maadili ya jamii yetu ya kitanzania, mara nyingi wanaropoka tu!!!

Pengine ni tatizo la malezi sana, huko walikolelewa hasa wazazi wao!! wanayosema ni kama wameishi maisha kama chokoraa tu!! pasipo kuwa na wazazi wa kuwakanya na kuwafundisha kuheshimu watu wote, hasa wanaowazidi umri, masudi, fina na wenzao hapo clouds, maneno yao mengi hayafai kusikiliza wala hayajengi ustaarabu.

Tafadhali kipanya muombe radhi mzee pinda, kikwete na mashabiki wa kazi zako, yeye ni sawa na baba yako!! taaluma yako haiwezi kuvuka mipaka hiyo!!

Anonymous said...

ndio tunahita uhuru huo sasa kwani uongo alichoandika au nyie vipofu

Anonymous said...

Kuminywa! Tunacheka lakini watu waliminywa kweli enzi za Mwalimu Nyerere. Kuna njemba moja pale UDSM jina nahifadhi, alikamatwa, kafunkiwa kichwa kazungushwa kwenye gari kama masaa matatu kusudi asijue anapelekwa wapi. Kumbe ni hapo oystabei. Basi njemba kahojiwa siku mbili na kuminywa hata maji ya kunywa hakupewa. Mwisho walimpa hamburger na soda. Walimfunika kichwa na kumtia kwenye gari lao halafu walimrudisha pale UDSM bwenini kwake usiku wa manane. baada ya hapo jamaa kimya! Mwalimu alikuwa anadhibiti midomo ya watu.

Anonymous said...

Sijafurahishwa na utani wa kipanya kwa kweli..Yeye ana uzuri gani wa kumsema mwenzake namna hii.Jokes nyingine sio fresh kweli kabisa

Anonymous said...

Said umesema kweli,Its not fair.Pamoja na kwamba yeye anaona ni kichekesho lakini haileti picha nzuri kumtania mtu kutokana na maumbile yake au jinsi alivyo.
Kipanya huwa anaropoka sana,this in not good,just imagine mzee pinda atajisikiaje au watoto wake watajisikiaje baba yao kuitwa Beast.
By the way kipanya mwenyewe sura yake iko matatani hata sijui mamiss wanampendea nini.

Anonymous said...

Hata mimi sijapenda kabisa, Kipanya hana adabu kabisa. Amekosa heshima kwa wakubwa zake na siyo wakubwa tu na hata angekuwa kijana mdogo sijapenda kabisa kuchora vile mtu mzima wa kumzaa. Aombe radhi kwa kweli.

Anonymous said...

Kwanza aliposema the beauty alikuwa anamzungumzia nani ? Kama ni Kikwete basi matusi makubwa kwani hata siku moja uwezi kumlabel mwanaume kama Mrembo unless una maana nyingine.
Huyu KP analack exposure ndio maana anafanya mambo yasiyo na kichwa wala miguu. Pamoja na kuwa tuna uhuru wa vyombo vya habari lakini lazima pia tuheshimu utamaduni wetu !

Anonymous said...

Kwani hao watangazaji wa mawingu Fm wanataaluma ya Uandishi na utangazaji basi wako pale kutokana na sauti labda kujilakana kwao na mmliki wa radio au midomo yao kutokuwa na break.

Kipanya mwenyewe anatisha, ukimlinganisha Kipanya (ambaeni 30+) na PM ambae anamiaka 60 nani anatisha kama sio kipanya?

Yule mzee (pm) sio mbaya bali anamakunyanzi yasioyo na sababu lakini ni wa kawaida tu, hivi mnaweza kumlinganisha na Pius Msekwa? Arap Moi, Obasanjo?

Kipaya kanenepa kidogo nakupata shavu anajiona Hb lakini hanma kitu dogo anatisha, angalia nyusi zake zilivyonyanyuka kama anazitinda vile.

Hata mimi hajanifurahisha kabisa.

Anonymous said...

Kipanya ana elimu gani jamani ? Dada chemi naomba unijibu hilo...

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 7:18PM, kwa kweli sijawahi kuona Resume/CV ya Kipanya hivyo siwezi kukujibu. Labda ungemwuliza kaka Michuzi.

Anonymous said...

Tatizo ni shule.Hamna kitu kichwani,na ni wengi hasa pale Clouds FM.Vile vile kama anony hapo juu,malezi ya wazazi yanachangia kwa sana fanya utafiti, nadhani kipanya atakuwa na kasoro kwa wazazi wake.

Anonymous said...

Mwaka 1990 tulifukuzwa UDSM, na sababu mojawapo (licha ya mgomo) ni kuwa kuna mtu alikuwa anajiita Mzee Punch alibandika katuni ambayo Chancellor wa wakati huo (Rais mstaafu Mzee Ruksa) aliielezea kama "matusi ya nguoni". Tulifukuzwa kama mbwa koko, na watu mitaani wakaandamana nchi nzima kuunga mkono kufukuzwa kwetu (hii maandamano ilikuwa propaganda of course). Watu siku hizi wana uhuru bwana, mwacheni Kipanya ajinome na uhuru wake!

Anonymous said...

UHURU LAKINI UUTUMIE KWA BUSARA. HAPO KIPANYA HAJAFANYA BUSARA HATA KIDOGO NA NYIE WAANDISHI WAKONGWE MSHAURINI. SIO SUALA LA ENZI YA NYERERE LAKINI KWENYE SUALA LA MAUMBILE MUNGU NDIO HULIPA!!! hapo hatanii anamaanisha.