Bila shaka wadau wengi mmesoma vitabu vya African Writers Series. Hivyo jina la Sembene Ousmane si ngeni kwenu. Alikuwa ni MSenegal. Alitunga vitabu vingi vikiwemo, God's Bits of Wood, na Xala.
Zaidi ya kuandika vitabu, marehemu Sembene alikuwa ni muongoza sinema maarufu barani Afrika. Alikuwa anaitwa, " The Father of African Cinema" yaani baba wa sinema Afrika. Hiyo ni kwa sababu alikuwa ni mwafrika wa kwanza kujulikana katika viwanjavya sinema vya kimataifa kama Hollywood. Huenda mmeona sinema zake za Xala, Faat Kine, Black Girl na Moolaade. Aliongoza kama sinema kumi na tano. Huko Afrika Magharibi hasa nchi zilizotawaliwa na Mfaransa (francophone) zimeendelea sana katika sinema kuliko nchi zilizotawaliwa na Mwingereza. Sinema zao huwa zina ubora zaidi kuliko za Anglophone.
Kwa kweli sijui kama alifariki mpaka jana nilipokuwa naangalia sherehe za Academy Awards (Oscars). Katika kumbukumbu ya waliofariki mwaka uliyopita alikuwemo. Mbona nilishutuka.
Sembene Ousamane alifariki nyumbani kwake Dakar, Senegal, mwezi Juni mwaka jana. Alikuwa na miaka 84.
REPOSE EN PAIX - REST IN PEACE
4 comments:
umenistua maana hii habari ni ya mwaka jana nikajiuliza walikuwa wawili ila ahsante kwa kutukumbusha.uzuri dada yangu unaleta mambo mapya ambayo hayapo kwenye blogu nyingine maana sasa kila mtu anataka kuwa kama michuzi basi wana copy na ku paste kama zilivyo inaboa sana Big Up
Na mimi sikujua kuwa amefariki. Asante kwa taarifa ingawa aliondoka siku nyingi kidogo. nakumbuka niliandika essay juu ya Gods Bits of Wood nikiwa A level.
REPOSE AN PAIX!
He was a great author and filmaker!
Ile sinema ya XALA nzuri kweli. Blockbuster wanayo.
Post a Comment