Friday, February 08, 2008

Waziri Mkuu Mpya ni Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda!


Maelezo mafupi ya Mh. Pinda Bungeni leo:


WAZIRI MKUU MTEULE MH. PINDA AMESEMA YEYE NI MTOTO WA KWANZA KWENYE FAMILIA YAO NA ANA SHAHADA YA SHERIA YA CHUO KIKUU NA KWAMBA AMEFANYA KAZI KAMA MSAIDIZI WA RAIS IKULU TOKA ENZI ZA MWALIMU KWA MIAKA 7, KWA ALHAJI MWINYI MIAKA 10 YOTE NA MIAKA KAMA MITANO KWA MH. MKAPA KABLA YA KWENDA JIMBONI KWAKE MPANDA KUOMBA KURA KUWA MBNGE MWAKA 2005.

7 comments:

Anonymous said...

Khaa! Hongera kwa Waziri Mkuu mpya lakini mbona ana sura mbaya?

Anonymous said...

Wewe anon hapo juu hata kama jamaa ana sura mbaya hii kazi ataiweza. Ana uzoefu wa miaka mingi sana!

Anonymous said...

Sifa za Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri(TAMISEMI) Mh.Mizengo Kayanda Pinda(MB) kuwa waziri mkuu mpya.Sababu ni hivi zifuatazo.
1.Kitaaluma ni mwanasheria hivyo naamini anaweza kutumia taaluma yake kubaini mambo mengi ambayo yataonekana kuwa yanakinzana na sheria za nchi na hivyo kuepusha kuliingiza taifa kwenye matatizo yasiyokuwa ya lazima.
2.Amewahi kuwa afisa mwandamizi wa idara ya usalama wa taifa pale Ikulu kabla ya kwenda kugombea ubunge kwao huo Mpanda mwaka 1995.Kuwa katika idara hii ni imani kutamuweza kuwa upeo mkubwa wa kushushtua dili fekifeki mapema na kuchukua hatua haraka.
3.Alipochaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya kwanza 1995,Rais Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI chini ya waziri mzee Kingunge.Hapa ndipo wafuatiliaji wa mambo tulipogundua kuwa anaonyesha dalili za kuja kuwa kiongozi makini sana kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao katika kujenga hoja alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge.
4.Mwaka 2000 aliteuliwa tena kuendelea na nafasi yake hiyo hiyo chini ya Mh.Brig.Ngwilizi.Kwa kuwa tayari alishakuwa na uzoefu wa miaka 5 katika wizara hiyo,Mh.Pinda alizidi kuonyesha uwezo mkubwa sana kiasi ambacho wachambuzi wa siasa tuligundua kuwa alikuwa na uwezo hata kumzidi waziri wake.
5.2005 Rais JK kwakuwa alikuwa ameshauona uwezo wake kwa kipindi cha miaka 10,kama naibu waziri,akampandisha kuwa waziri kamili.
6.Sasa hoja yangu ni kwamba kwa wanaojua dhamana ya waziri mkuu katika mfumo wa serikali yetu,ni kwamba yeye ndiye msimamizi mkuu wa sera za serikali.Na sera za serikali zinatekelezwa kwa asilimia 90 na TAMISEMI.Kwa hiyomuhimu sana kuwa na mtu mwenye uzoefu na masuala ya serikali za mitaa na tawala za mikoa.Kwa lugha nyepesi,TAMISEMI ndio serikali yenyewe.Hakuna wizara isiyofanya kazi na TAMISEMIukiondoa,mambo ya nje,Ulinzi,na mambo ya ndani.

Naomba kuwakilisha,
Pinda jr.

Anonymous said...

Wewe Anony hapo juu ni mshenzi wa tabia! Suala la sura nzuri hapa halina nafasi.... Cha msingi tunataka waziri mkuu mchapa kazi ambaye atasaidia kulikomboa taifa letu dhidi ya umaskini.Kama Ndugu Mizengo Pinda anasifa ambazo watanzania tunazihitaji katika kipindi hiki kigumu basi hatuna shaka! Tumechoka kuongozwa na "wauza sura" ambao hawana maana yeyote!! Je Baba yako ana sura nzuri???! sina uhusiano wowote na Mizengo Pinda ila umenikera sana na hoja zako za kipuuzi..

Anonymous said...

Da Chemi, nimekuwa na nitaendelea kuwa mpenzi wa blog yako ila bila nia mbaya yaliyomhusu Mr wako ni kasoro ndogo imetokea na hawo watu wa Obama wako kwenye pressure all the time especially campaign perfomance not exceeding to their expectations. I know it's kinda hard to let it go because of the party involved , keep up good work.

Anonymous said...

Pamoja na jedwali lililopo hapo chini, pia nimefanikiwa kuelewa mambo haya kumhusu Mh. Mizengo KPP (ikiwa nimekosea, samahani, haya yote nimeyatoa kwenye maandishi tofauti tofauti mtandaoni).

Amefanya kazi na marehemu Raisi Julius Kambarage Nyerere katika ofisi yake kwa kipindi cha miaka 7
Amefanya kazi na Raisi mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa kipindi chote cha miaka 10 raisi
Amefanya kazi na Raisi mstaafu Benjamin William Mkapa kwa kipindi cha miaka 5
Amefanya kazi na Raisi Jakaya Mrisho Kikwete kwa kipindi cha miaka 2

Kitaaluma ni mwanasheria.
Kikazi: Amewahi kuwa afisa mwandamizi Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu.
Aligombea Ubunge huko Mpanda mwaka 1995 na kuchaguliwa.
Mwaka 1995 Rais mstaafu B.W. Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI chini ya Waziri mzoefu Mh. Kingunge Ngombale Mwiru.
Mwaka 2000 aliteuliwa tena kuendelea na nafasi yake hiyo chini ya uongozi wa Mh.Brigadia, Hassan Ngwilizi.
Mwaka 2005 Rais JKikwete kaliujua uwezo wake kama Naibu waziri kwa kipindi cha miaka 10, akampatia Uwaziri kamili.
Mwaka 2008, Raisi JKikwete amemteua kuwa kuwa Waziri Mkuu na Bunge limethibitisha hatua hiyo.
Kwa kuwa Waziri Mkuu ndiye msimamizi mkuu wa sera za Serikali, kwa kuwa sera za Serikali hutekelezwa kwa karibu asilimia tisini na Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM -TAMISEMI) ( isipokuwa wizara za Ulinzi, Mambo ya nje na Mambo ya ndani), na kwa kuwa mh. MKPP aliwahi kufanya kazi katikaOWM -TAMISEMI kwa kipindi cha miaka 5, na kwa kuwa sasa yeye ni WM, basi ninalazimika kuamini kuwa uzoefu alioupata katika ngazi zote hizo za kiutendaji zitamwezesha kutumia vyema uzoefu, busara na hekima aliyojipatia katika kutekeleza majukumu na kusimamia shughuli zote zitakazomwezesha MTanzania kuishi kama binadamu wenye haki na uhuru wa kutumia vyema rasilimali za nchi waliyotunukiwa na Mwenyezi Mungu kwa faida yao na maendeleo ya nchi yao kwa vizazi vya baadaye.

Mtu uliyejaliwa kufanya kazi kwa karibu kabisa na Maraisi wenye mchakato tofauti katika kuiongoza Tanzania, tangu nchi ijue kujitawala yenyewe, lazima utakuwa una makabrasha ya kuweza kuchambua mafanikio na mapungufu ya awamu zote tatu na sasa ya nne na hivyo kuweza kutushauri vyema kuhusu lipi litakalotupotezea muda na lipi litakalotusaidia kupata ahueni na kisha mafanikio.

Kazi si yako peke yako au yetu peke yetu, WaTanzania tunataka kufanya kazi kwa umoja wetu, tutaelekezana na kuchambuana tukiendelea kutekeleza majukumu yetu hadi kila kila Mtanzania apate maji safi, lishe yenye afya, malazi bora na elimu ya kutosha kujikimu katika maisha ya kawaida, Inshaallah, ziada ikiwepo ni kwa faida ya baadaye.

Mungu uibariki Tanzania.
Mungu uibariki Afrika.
Mungu uwabariki WaTanzania.
Salam zangu,
Subi

Anonymous said...

imenishangaza sana kuona watu wanafatilia sura badala ya utendaji kazi.hivi sura inasaidia nini kawa utendaji ni mbovu? watanzania tubadilike na tuelimike jamani tutaenda hivi mpaka lini? bwana huyu mzee hana mchezo wangukua wote wako hivi Tanzania isingi kua hapa ilipo na nampa big up sana tu.ni agatha a.k.a Agy