President Bush is leaving a lasting impression on multitudes of Tanzanians. He has not put on airs and has even evaded his security to meet, shake hands and hug common people! It sounds like he is enjoying his trip to Tanzania immensely!
*********************************************
From ippmedia.com
Rais Bush apagawisha
2008-02-18
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Licha ya kutoka katika taifa lenye nguvu kubwa zaidi za kiuchumi duniani, Rais George W. Bush wa Marekani ameweza kujichanganya na Wabongo Jijini na kuwapagawisha maelfu ya waliofika kumpokea.
Bush, aliyewasili Jijini tangia Jumamosi jioni kwa ajili ya ziara ya kitaifa ya siku nne nchini, amefanya jambo hilo lisilokuwa la kawaida kwa marais wa taifa hilo walio madarakani na kuwashangaza hata maafisa wake wa Kikosi cha FBI.
Kwa ujumla, mambo yenyewe aliyoyafanya Rais Bush mara tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kuwapagawisha watu ni kama haya:
Ajitosa uswazi:
Awali ya yote, alipotua pale kwenye `terminal one`, Bush alitoa mpya wakati alipositisha ghafla zoezi lake la kupungia mkono watu waliokuja kumpokea na kisha kujichanganya nao kwa muda.
Ilianza kama masihara vile, Bush alichomoka ghafla toka kwenye kapeti kali jekundu alilokuwa akipitishwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Jakaya Kikwete.
Kisha kwa mastaajabu ya wengi, akamuendea mama mmoja aliyekuwa miongoni mwa watu tele waliokuwa wakimpungia na kukumbatiana naye. Jambo hilo liliamsha hisia kali za furaha na nderemo.
Jana, Bush akaendelea kujichanganya `uswazi`, kunako mitaa ya Buguruni na Ilala ambako, ingawa alikuwa akilindwa vikali, aliweza kutimiza ratiba yake ya kuzindua majengo mapya katika Hospitali ya Amana, yaliyofadhiliwa na Serikali yake.
Atema Kiswahili.
Wakati alipopewa fursa ya kuzungumza pale katika viwanja vya Ikulu, ambako yeye na mwenyeji wake walikutana na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, Rais Bush alibonga Kiswahili kwa namna isiyotarajiwa.
Alikamata mic, kisha akasalimia kwa kusema `Mambo viipiii!``
``Alinishangaza. Kamwe sikujua kama Rais Bush anaweza kutusalimia kwa Kiswahili,`` amesema Bw. John Jacob, mkazi wa Manzese Jijini.
Amwaga Mapesa
Pamoja na kuwapagawisha Wabongo kwa staili ya ujio wake na mivifaa ya kisasa ya kumlinda ikiwa ni pamoja na midege na migari myeusi ya bei mbaya, Rais Bush amewaletea neema Wabongo.
Yeye na mwenyeji wake, Rais Kikwete, wamesaini mkataba utakaoiwezesha Tanzania kupata msaada wa dola za Kimarekani Milioni 698 sawa na pesa za Kitanzania bilioni 800. Haijapata kutokea!
Pesa hizo zitatumika kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kujengea miundombinu ya barabara.
Aidha, mke wa Rais Bush, Bi. Laura Bush, amemwaga msaada wa dola za Kimarekani Milioni 43 kwa mradi unaokwenda kwa jina la `Pamoja Inawezekana`, ulio chini ya Mama Salma Kikwete, kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima nchini.
- SOURCE: Alasiri
2 comments:
Mbona wagonjwa wachache?Au waliambiwa wasifike hospitalini siku hiyo!
Nawezaje kuomba kazi hapo Amana. nataka kazi ya uuguzi. Au kazi zote zitaenda kwa ndugu wa watu?
Post a Comment