Kutoka ippmedia.com
Taasisi ya Saratani ya jijini Ocean Road imeanza kuzidiwa
2009-01-24 12:04:06
Na ITV Habari
Taasisi ya Saratani ya jijini Ocean Road imeanza kuzidiwa kutoa huduma za tiba hiyo kwa wagonjwa wapya kutokana na idadi ya wagonjwa hao kuongezeka kila mwaka na kufikia wagonjwa elfu arobaini wanaohitaji tiba hiyo kwa mwaka .
Wakizumgumza baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku tatu kujadili mikakati ya kuthibiti ugonjwa wa saratani uliohudhuriwa na wataalam wa tiba na madkatari wa saratani nchini baadhi ya washiriki wamesema kuna haja ya kuongeza jitihada katika kuwahamasisha wanajamii wa maeneo ya vijijini umuhimu wa kuwahi tiba ya saratani ikiwa kwenye awamu za mwanzoni wakati bado kuna matumaini ya mgonjwa huyo kupona.
SOURCE: ITV
3 comments:
Vyakula tunavyokula vimeathiri sana afya zetu!!, tumeacha uji wa ulezi, chai na mihogo, viazi na ufuta, mayai ya kienyeji, kuku wa kienyeji. Hivi vya asili tumeviacha na kushabikia visivyo asili. Leo ukila chai kwa muhogo unaonekana 'choka mbaya', angalia hata kinga ya maradhi inavyop[oromaka. Nadhani magonjwa mengi pia yana uhusiano na mabadiliko ya vyakula kwa siku hizi.
Mi naona sio vyakula tu,haya mambo kama mawasiliano-wireless, Mabomu ya kisasa yaangushwayo hapa na pale na jamani mnakumbuka zile habari za kutupwa masalio ya nyuklia huko Afrika? na yakichangia haya mambo ya makulaji basi tena
KILI, bg
...must the paragraphs be single sentences? I mean ina eleweka lakini nimetahamaki tu. Yeah, unfortunately cancer is spreading in Africa. Pia, nashuku ni vile siku hizi wananchi wanaelimishwa kwa kiasi kikubwa kuliko zamani na kutafuta huduma zaidi wakiona ishara zisizofahamika mwilini mwao.
Post a Comment