Wednesday, May 06, 2009

Maafa Mbagala



(Picha kwa Hisani ya Global Publishers. Kwa Picha zaidi Bofya Hapa)

Idadi rasmi ya waliokufa kwa ajali ya mabomu Mbagala ni 23. Lakini watu wanadai waliokufa huenda ikafika zaidi ya mia! Serikali inasema itawalipa fidia watu waliopoteza mali katika ajali huo.

Nina swali. Je, serikali na jeshi wanachukua hatua gani kuhakikisha jambo kama hilo halitokee tena?

Na samahani, lakini watu Bongo wanahitaji kuelimishwa. Mnaona hiyo picha ambayo watu wameshika kipande cha kombora? Si ingelipuka watu zaidi wangekufa. Watu wakimbie siyo wakimbilie! Hizo silaha siyo toy. Na si ajabu kuna watu wameweka vitu wasivyovijua majumbani mwao, tutasikia oh, sijui alitaka kutengeza nini, alivyoigonga ikalipuka.

**************************************************************************
Kutoka Ippmedia.com

Ni vilio tu!

2009-05-05

Na Emmanuel Lengwa na Moshi Lusonzo

Wakati hadi sasa taarifa rasmi juu ya idadi kamili ya watu waliopoteza maisha katika mlipuko wa mabomu uliotokea wiki iliyopita Jijini Dar es Salaam ni 23, baadhi ya wananchi wa maeneo ya Mbagala, wanadai kuwa idadi ya waliokufa ni kubwa zaidi na kwamba miili yao huenda imekwama kwenye tope la mto Kizinga.

Kadhalika madiwani wa kata za Mbagala na Mbagala Kuu wameonyesha wasiwasi wao wakidai kuwa, wana hofu kwamba watu kadhaa wakiwemo watoto ambao walitoweka tangu siku ya tukio hilo la mlipuko, wakawa wamefia kwenye mto huo.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova amesema hadi sasa jumla ya watoto 19 wakazi wa Mbagala, tangu siku ulipotokea mlipuko huo, hawajulikani waliko.

Kufuatia hofu hiyo, jana Baraza la Madiwani la Manispaa ya Temeke liliitisha kikao cha dharura kujadili hali hiyo.

Katika kikao hicho, Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, ambapo ndipo lilipotokea tukio hilo, Bw. Anderson Charles alisema kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo watoto wengi waliozama ndani ya mto Kizinga na kuwa miili yao imekwama kwenye tope la mto huo.

Akasema kasi ya uokoaji inayoendelea kufanywa na wananchi kwa kushirikiana na Polisi ni ndogo, hivyo akaomba Jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ, kufanya operesheni maalum kusaka miili ya watoto hao na kuiopoa mtoni.

Hoja ya Bw. Charles iliungwa mkono na Diwani wa Kata ya Mbagala, Bw. Peter Osoro aliyesema kuwa baada ya milipuko, watoto wengi walikimbia na kuingia mtoni, wakiwa na nia ya kuvuka mto Kizinga kwenda ng\'ambo maeneo ya Yombo.

Kwa mujibu wa diwani huyo, watoto wengi walizama mtoni katika maeneo ya Kingugi na Bugudadi mahali ambapo wengi wao walitaka kuvuka wakidhani maji ya mto ni machache, lakini wakajikuta wakizama kwenye tope na kupoteza maisha.

Aidha Bw. Osoro akasema kuwa hadi sasa kuna familia nyingi zinahaha kutafuta ndugu, jamaa pamoja na watoto wao, na hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kupeleka kikosi cha JWTZ kufanya operesheni maalum.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Bw. Steven Kongwa aliwahakikishia madiwani hao ambao wengi wao walikuwa wakibubujikwa machozi kuwa, juhudi kubwa za kuwasaidia wahanga wa tukio hilo zinaendelea na hivyo akawataka waheshimiwa madiwani wasiwe na huzuni sana.

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Temeke, Bw. Jerome Bwanausi, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maafa hayo, alisema kamati yake iko imara na wahanga wote wanapewa misaada.

Akasema mazishi ya maiti zote za ajali hiyo yamegharimiwa na kamati ya maafa ya mkoa wa Dares Salaam ambayo iko chini ya Mkuu wa Mkoa, Bw. William Lukuvi.

Madiwani hao walimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kutembelea majeruhi na wahanga wa tukio hilo.

Aidha waliwashukuru watu wote waliotoa misaada ya hali na mali kusaidia wahanga wa tukio hilo.

Katika hatua nyingine, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kuwa watoto 19 ambao hawajulikani waliko wanahisiwa kuwa wamekimbilia maeneo mbalimbali na wengine wamehifadhiwa majumbani na wasamaria wema.

Ametoa wito kwa watu wanaowahifadhi watoto wasio wao majumbani au wale wanaojua walipo, watoe taarifa ili juhudi za kuwakutanisha na wazazi wao ziweze kufanyika.

``Kuna watoto wamekimbilia maeneo ya mbali, wapo waliofika hadi Arusha, lakini pia kuna wengine wamehifadhiwa na wasamaria wema, nawaomba wote wajitokeze kutoa taarifa zao ili tuwakutanishe na wazazi wao,`` akasema Kamanda Kova.

Ameonya kuwa miongoni mwa watoto hao wamo watoto wa kike na wanafunzi, hivyo kutotoa taarifa zao inaweza kuleta hisia mbaya baadaye na ikawa shida.

SOURCE: Alasiri

Kwa habari zaidi someni:

http://thecitizen.co.tz/newe.php?id=12244

http://www.thisday.co.tz/News/5685.html

http://www.upi.com/Top_News/2009/04/30/Tanzania-munitions-dump-explodes/UPI-26051241071540/

3 comments:

Anonymous said...

Doh! Kweli tumfichwa mengi. Asante sana Da Chemi kwa kuposti linki ya global publisher.

Anonymous said...

NAFURAHI CHE-MPONDA UMEJIPIGA NA KUTUWEKEA PICHA HIZI ANGALAU TUJIONEE YALIYOWAKUMBA WAHANGA WA MBAGALA.
SINA CHA KUKUPA KWANI UMESIKIA KILIO CHETU NA KUWEKA HIZO PICHA KAMA NILIVYOKUOMBA KWENYE HABARI YAKO YA KWANZA YA MABOMU ULIYOITOA.
TUKIO HILI LINGETOKEA KWA WENZETU, LINGEKUWA GUMZO LA WIKI,MWEZI HATA MIEZI KWANI PRESS SI KWA AJILI YA WANYONYAJI, BALI WANYWONYWAJI.
I DON'T KNOW MICHUZI ANA KIPAJI GANI CHA KUHABARISHA WATU KWA PICHA.SIJUI ANATAKA PICHA ZA AINA GANI NDIYO AFUATILIE. HALAFU ANAJIFAFANYA ANAJUA NA HATAKI KUAMBIWA! ANAJIONA YUKO JUU KULIKO MTU MWINGINE YEYOTE.
KAMA UNA KIJIMUDA TAFUTA WAPIGA PICHA WANAOSAKA CELEBRITIES NA KUJIPATIA MAELFU YA DOLAS KWA SIKU WAKUPE STORY FUPI TU YA WAO KUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA KAZI YAO. UTAJIFUNZA MENGI MNO.
NILIPATA BAHATI YA KUMTEMBELEA MMOJA WA MAPAPARAZI NIKAMFUNGULIA BLOG YA MICHUZI. NIKAMWONYESHA PICHA ALIZOPIGA MICHUZI; ZA MPIRANI, KWENYE HAFLA, ZA VIONGOZI NA NYINGI TAKEN BY MICHUZI-NIKAJIGAMBA KWA KUSEMA HUYU NI MMOJA WA WAPIGA PICHA WA JUU BONGO-JAMAA ALICHEKA SANA,SANA YAANI SANA. ALIDHANI NI PICHA ZILIZOPIGWA NA MTOTO PRIMARY SKUL AKIJIFURAHISHA NA KIKAMERA CHAKE. ANYWAY NDIIYO UJUZI ALIONAO HUWEZI KUMLAUMU.

Anonymous said...

Dada Chemi una pointi. Watu hawataki kusikia. Ni kweli hayo mabaki ni hatari na tutasikia habari zaidi za ajali kutokana ana hayo mabaki.