Thursday, May 28, 2009

WAPI Zanzibar

Muhula wa Pili wa WaPi Zanzibar umewadia....

WaPi ni tamasha la sanaa linalofanyika kila mwezi. Tukio hili linakusudia kutoa nafasi kwa wasanii wanaochipukia kushiriki na kuthibitisha vipaji vyao.

Katika Muhula huu tunakusudia kuanza kulipeleka tuko hili katika baadhi ya shule ili kuchochea ushiriki wa wanafunzi zaidi katika mijadala na sanaa.
Tunatarajia pia kushirikiana na baadhi ya taasisi mbalimbali ili kutoa nafasi za kujiendeleza kitaaluma na kisanii kwa wale watakaoonyesha juhudi na mwelekeo mzuri.

Tukio jingine jipya katika muhula huu ambalo litawezeshwa kama kawaida na BRITISH COUNCIL ni ubunifu na usanifu mitindo.

Mada ya safari hii katika WaPi ni ANGUKO LA UCHUMI DUNIANI.... Tunatarajia kushirikisha wadau mbalimbali katika kujadili athari za mtikisiko wa uchumi hapa kwetu. Pia hii ni nafasi muhimu ya kuangalia ni kwa jinsi gani jamii ina uelewa katika tatizo hili na namna ya kukabiliana nalo.

PROGRAMU ITASHIRIKISHA:

Waongozaji wa tukio kutoka WaPi Zanzibar

DJ Cool Para

Jukwaa la sanaa za Mikono

Mwl Muchi kutoka Nyumba ya Sanaa Zanzibar atasimamia warsha fupi juu ya sanaa ya uchoraji kwenye Kona ya MAARIFA

NEW GENERATION katika uchezaji na sarakasi

Mjadala wa mada

USHINDANI WA MAEMSII

Kimanumanu Kidumbak

Wamo Sanaa group katika Ngoma asilia

Pamoja na wasanii anaokuja juu katika Hip Hop Zanzibar..Chaby Six na Mr Mvuto

Mengineyo ni pamoja na Tenzi, Upambaji, Uchezaji na upigaji wa ala mbalimbali...

MAHALI NI NGOME KONGWE

Alhamisi tarehe 28-05-2009 kuanzia saa 9 alasiri hadi 2 usiku

Hamna kiingilio

English

The second term of WaPi Zanzibar has arrived.....

WaPi is an artistic event taking place every month. This event aims in offering a chance to underground talents in proving themselves artistically.

During this term we are planning to take WaPi events to various school in order to encourage more students participation in art and dialogues.
We will also be working hand in hand with other stakeholders to make sure that artists who shows improvements are supported in getting regular short term sponsorship to attend workshops and courses.

Through an extra support from BRITISH COUNCIL we will be adding another element which will be fashion designing and shows.

This time the theme will be WORLD ECONOMIC DOWNTURN..we will be discussing together about the effects in our society..how far does a normal local understand it?

THE PROGRAM:

Introduction from WaPi MC

DJ Cool Para

Fine art

Mwl Muchi from Nyumba ya Sanaa will facilitate a short drawing workshop...KONA YA MAARIFA

NEW GENERATION in dance and acrobatics

Theme discussions

Battle of MCs

Kimanumanu Kidumbak

Ngoma time (traditional rythms and dance) by WaMo Sanaa group

Up and strong coming Hip Hop talents Chaby Six and Mr mvuto will also hit a stage!!

VENUE: OLD FORT

Thursday 28th May 2009 from 3pm til 8pm

FREE ENTRY!!!

No comments: