Monday, May 18, 2009

Mambo ya ZIFF Mwaka Huu!

Zanzibar International Film Festival/Tamasha la Nchi za Jahazi kwa muda mrefu sasa limekua likitoa nafasi za mafunzo ya muda mfupi (Training Workshops) kwa wadau wa filamu nchini na pia kutoa nafasi kwa soko la filamu la Africa mashariki kwa ulimwengu.

Ikiwa sasa tuko katika Tamasha la 12 la nchi za majahazi, ZIFF imeendelea kunadi na kukuza soko hili la filamu, ZIFF inatambua mahitaji ya kiwanda kizima cha filamu ili kikue na kufikia malengo tuyatakayo. Lakini kumekuwa na mwamko mdogo sana kwa wadau ama washiriki wa fani hii, ukiangalia kiwanda hichi hakina watu wenye ujuzi upasao (Professionalism) na ndio maana kimekua kikizalisha ilimradi kazi tena zisizo na ubora.

Mwaka huu tena ZIFF inatoa nafasi ya mafunzo ya muda mfupi kwa wadau na washiriki wa soko/kiwanda cha filamu. Tunaomba watu wajitokeze kutuma maombi yao ili kuweza kushiriki. Pia tunaomba wadau/washiriki wasisite kuuliza maswali pale wapohisi hawajaelewa au panawatatiza.

Naambatanisha Tangazo la Warsha za Mafunzo ya muda mfupi ili kuwajulisha wadau/washiriki nini kinaendelea katika ZIFF 2009 na pia kuwaomba washiriki.

Nashukuru kwa vyombo vya habari kwa kuwa mstari wa mble kuzungumzia soko na kiwanda cha filamu kwa upana lakini tukumbuke bila elimu kiwanda hichi kitakufa.


WORKSHOP/CONFERENCE/FORUMS AT ZIFF 2009 \

27th June – 3rd July, 2009 - Film Production for Children Workshop by DFI15 Participants (10 From Mainland, 5 Zanzibar), Application Deadline 25th May, 2009For Film Makers/Producers Only.

28th June – 5th July, 09 - Screenwriting Workshop by Maisha Film Lab9 Participants: Application Deadline 21st May, 2009For Script Writers Only.

2nd July, 2009 - Acting for Camera by Ntare Mwine and Danny Glover (USA)20 Participants (15 from Tanzania Mainland/East Africa, 5 from ZanzibarFor Actors Only.Application Deadline 25th May, 2009.

2nd- 3rd July 09 - Tourism Conference by ZIFFFor All Tour Operators in Tanzania (Zanzibar and Mainland)Apply now for this special opportunity.
Deadline for Application 1st June, 2009

3rd July, 2009 - African Film Makers/Producers Forum by ZIFF/TAIPAFor East African Film Makers/Producers
Application Deadline 1st June, 2009

3rd July, 2009 - Wild Life filming by South African WildlifeFor all Wildlife Film Makers/Producers Application Deadline 1st June, 2009

4th July, 2009 – Development Film Workshop by GTZFor All Film Makers/Producers/Media Houses.25 Participants (15 from Mainland, 10 from Zanzibar and East Africa)Application Deadline 1st May, 2009

Wako katika Filamu,

Daniel NyalusiEvents Coordinator/Film Programs
Zanzibar International Film Festival 2009

No comments: