Monday, November 12, 2007

Mama yake mzazi Kanye West Amefariki


Kanye West na mama yake, Dr. Donda West

Kuna habari ya kusikitisha na ya kushangaza....mama yake mzazi, mwimba rap, Kanye West, amefariki dunia ghafla siku ya jumamosi.

Mama yake, Dr. Donda West, alikuwa na miaka 58. Habari za kuaminikia zinasema alikufa baada ya kufanyiwa opresheni ya urembo, lakini hawakusema ilikuwa ni opresheni ya aina gani.

Huenda ilikuwa ya kupunguza matiti, matako, uso, liposuction (kupunguza mafuta).

Mama yake alikuwa meneja wake. Alistaafu kazi ya kufundisha kiingereza Chuo Kikuu cha Chicago kusudi awe na mwanae.
Mungu amlaze mahali pema mbinguni. AMEN.

Kwa habari zaidi someni:



Friday, November 09, 2007

Binti MKenya ajiunga na jeshi la Bush sasa marehemu

Marehemu Christine Ndururi


Hapa USA wahamiaji wengi wanajiunga na jeshi la Marekani kusudi wapate Green Card, uraia na hela za kulipia masomo. Kuna hata waBongo waliojiunga, waKenya, waGanda na wahamiaji kutoka karibu kila nchi ya dunia katika jeshi la Marekani. Kutokana na upungufu wa waMarekani wanaotaka kujiunga kwa hiari siku hizi ukionyesha moyo wa kujiunga wanakuchukua. Hata wahalifu waliotakiwa kuwa jela wanachukuliwa asante vita vya Iraq.

Jana tulisikia kwenye taarifa ya habari, habari ya kusikitisha. Msichana wa KiKenya mwenye miaka 21 kutoka Lowell, Massachusetts, Christine Ndururi, amefariki dunia akiwa safarini kwenda Iraq. Jeshi linasema kuwa alifariki Kuwait kwa, "Non-related Combat Illness". Yaani ugonjwa usiohusika na mambo ya kupigana.

Sasa ni kitendawili. Wazazi wake walimwona akiwa kambini kwake Texas wiki mbili zilizopita, alikuwa mzima. Jumatatu wiki hii saa tatu za asubuhi (9:00AMEST) waliongea naye kwa simu alikuwa mzima na hakusema anaumwa. Jumanne jioni saa tatu (9:00PM EST) walipigiwa simu na jeshi kuwa amefariki kwa ugonjwa!

Huyo binti alihamia Marekani na familia yake akiwa na miaka 16. Baba yake mzazi alikuwa ni polisi Kenya na alihamia hapa na familia yake. Sasa anaendesha malori. Kaka zake wote pia walijuinga na jeshi la Marekani.

Akiwa anasoma High School alijiunga na Army Reserves. Baada ya kumaliza masomo yake aliendelea kukaa jeshini kwa vile alitaka hela za kusomea unesi. Alikuwa amepangiwa kupelekwa Korea, lakini badala yake jumatatu alishutukia anapelekwa Iraq, ndipo alipiga simu kwa wazazi wake. Familia yake wanasema alikosa raha aliposikia hizo habari.

Na watu sasa wanauliza jeshi la Marekani kinaficha nini kuhusiana na kifo cha huyo binti?

Mungu amlaze mahali pema mbinguni. AMEN.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.eagletribune.com/punews/local_story_312093852

http://www.thebostonchannel.com/news/14544601/detail.html

Thursday, November 08, 2007

Marudio - Kukosa Nguvu za Kiume si Mwisho wa Dunia!

Kutoka 1/21/06.


Jamani, jamani, jamani, kuna jirani yangu kafa hivi majuzi. Alikuwa ni baba wa makamu, mmarekani mweusi. Alikuwa mcheshi na ilikuwa kila tukionana lazima tusalimiane. Mara ananinunulia kahawa halafu tunakaa namsimulia kuhusu Afrika. Yule baba, alionekana mzima na mwenye afya fiti kabisa. Nilibakia kushangaa kusikia kafa na si kwa ajali. Mke wake alifariki mwaka juzi, lakini miezi ya karibuni alikuwa anaonekana mwenye furaha kwa vile alipata mpenzi, dada mwenye miaka 25 hivi.

Story niliyoskia ni hivi: Kumbe jamaa alikuwa na matatizo ya moyo. Alifia kitandani akiwa kwenye shughuli ya kufanya tendo la ndoa na mpenzi wake. Tena wanasema alifariki mara alipofikia kilele cha tendo. Navyosikia ilikuwa ni ‘massive heart attack’. Kama ni massive bila shaka na utamu wa shughuli hakujua kuwa yuko hatarini.

Nasikia huyo mpenzi wake alipiga sana makelele majirani walipigia simu polisi 911 kwa vile walidhania wameingiliwa na majambazi. Wanasema baba wa watu kamwangukia yule dada na kafa macho wazi.Lakini bado nilikuwa nashangaa maana kama nilivyosema awali, jamaa alionekana kuwa na afya. Kumbe jamaa alikuwa mtumizi wa Viagra, yaani vile vidonge vya kuongeza uume, na kumpa mwanaume uweza wa kufanya tendo la ndoa.

Ndugu zake wanalamika kweli, maana hakuzipata kwa prescription ya daktari, alizaiagiza kwenye mtandao (internet). Kwa kumwangalia alivyofiti nisingefikiria kuwa ana matatizo ya nguvu za kiume. Kumbe mtazame mtu, matatizo yake anayajua mwenyewe na daktari wake.Nikawa najiuliza kama jamaa alijua ana matatizo ya moyo, kwa nini alitumia Viagra. Maana hata tangaza kwenye TV na magazeti wanaonyo kuwa kabla ya kutumia. Halafu pia wanaonya kuwa mwanaume anaweza kupofuka kama anatumia. Lakini wanaume bado wanazitumia!

Na siku hizi dawa za kuongeza nguvu za kiume ziko nyingi kuna Ciallis, Levitra, Yohimbine na mengine. Hizo dawa zina side effects kama kuumwa kichwa, kuharisha, pua kuziba, macho mekundu, tumbo kuumwa na mengine mengi. Pamoja na side effects bado zina soko kubwa. Na zikipigwa marufuku nina amini kuwa watu watatajirika kwa kuzifanyia magendo.

Kwa kweli wanaume wako tayari kufa kama wakishindwa kufanya tendo la ndoa. Nashindwa kuelewa sababu. Yaani tendo la ndoa ni tamu kiasi hicho au wanahofia kuwa kwa vile hawa ‘function’ tena ndo basi si wanaume? Mtu anakuwa tayari kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kufanya tendo la ndoa.

Mwanaume anaambiwa anaweza kupofuka akitumia hiyo dawa lakini bado yuko tayari kuchukua risk. Halafu mwanaume akiitwa ‘hanithi’ yuko tayari kupigana au kuua. Sijui bila kusimamisha anajiona si mtu tena…sielewi kabisa! Nikawa najadiili na marafiki zangu juzi na tulikubaliana kuwa wanaume wako tayari kuchukua ‘risks’ kuliko wanawake.

Yaani mwanaume anaweza kufanya tendo la ndoa hata akijua kuwa kuna hatari ya mwenzake kuwa na ugonjwa wa zinaa na ataambukizwa. Bongo, walikuwa wanasema eti, ‘Ajali Kazini’! Hiyo ajali inaweza kukuua! Sijui hiyo ume ikisimama ndo basi tena, akili zote zinahamia hapo. Nauliza tena, tendo la ndoa ni tamu kiasi kwamba mko tayari kuhatarisha maisha yenu? Kukosa nguvu za kiume zi mwisho wa dunia jamani. Bado tunawahitaji!Lakini nikirudi kwa marehemu jirani yangu, uwongo mbaya, alikuwa anatabasamu ndani ya jeneza lake!

Noti - Nyie wanaume mnaotaka kutumia hizo dawa kawaone daktari wenu kabla ya kuanza kuzitumia.

Msanii Ernest Mtaya anaoa kwa staili aina yake!





Ninamfahamu msanii na mchoraji, Ernest Mtaya tangu ni kijana mdogo. Alikuwa anatusaidia TAMWA katika mambo ya uchoraji katika magazeti na vitabu yetu. Sasa ni mwalimu maarufu wa uchoraji. Amewahi kupata zawadi ya uchoraji kutoka Mfuko wa Utamaduni Tanzania.

Pia alishiriki katika sinema ya Maangamizi the Ancient One. Picha zake nyingi zilitumika kwenye hiyo sinema, iliyowakilisha Tanzania katika mashindano ya Oscars Hollywood mwaka 2001.

Ernest na Juddy HONGERA! Nawatakieni maisha mema ya ndoa.

Dada Chemi

***********************************************************************************
Ndugu zangu na marafiki zangu,Natumaini wote ni wazima na kama wapo ambao wanaugua au wanauguliwa naombaMUNGU awasaidie katika matatizo hayo. Mie ni Ernest Mtaya (pichani) na maelezo yangu zaidi yanapatikana katika http://www.ernest.4mg.com/

Madhumuni ya barua hii ni kuwafahamisha natarajia kuoa tarehe 17 Novemba 2007 saa 10 kamili katika kanisa linalojulikana kama st.Peter's church liliopo Oysterbay karibu na shule ya Mbuyuni hapa Dar Es Salaam. Baada ya hapo kutakuwa na msafara wa BAJAJI sita kuelekea eneo la sherehe ambalo ni kijiji cha Makumbusho tena nje chini mwembe.

Sherehe hii itakuwa na vionjo vya kitamaduni zaidi ya "uzungu" katika msafara wa Bajaji tutakapofika eneo la Victoria tutabadilisha usafiri na kupanda GUTA lililotengenezwa kiustadi kabisa na kuitambua Bajaji nitakayokuwa na mtarajiwa wangu itakuwa imepambwakwa makuti.
Sherehe itashereheshwa na msanii maarufu wa jukwqaa Mrisho Mpoto kwa wasiomfahamu ni yule muimbaji wa wimbo wa SALAMU KWA MJOMBA pia kutakuwa na msanii maalufu wa Afro Reggae Jhiko Manyika ambaye amerudi juzi tu kutoka ziara yake ya kimuziki ya Ulaya.
Mtumbuizaji mwingine ambaye atakuwa msimamizi wa mtarajiwa wangu ni muimbaji na mtunzi maarufu anayeitwa Karola Kinasha ambaye mbali na shughuli ya usimamizi kama Matron pia atatumbuiza kwa nyimbo zake tamu na sauti nzuri. keki , shampeni na jukwaa utamaduni wetu wa Afrika utapewa hadhi.

Cha muhimu ndugu na marafiki ni hii sherehe ya watoto ambayo nimefikiri niifanye ili watoto kwa mara ya kwanza washiriki katika sherehe ya Arusi la kwa nia ya kuwaaunganisha na kusaidiana na kutambua matatizo ya watoto wengine wenye shida zaidi yao.

Hivyo basi siku ya pili ya sherehe yaani 18 Novemba 2007 kwa niaba ya mchumba wangu JUDDY nimeandaa sherehe ya watoto ambapo nimeawaarika watoto wa mataifa mbalimbali nia kubwa ikiwa ni kuwaaunganisha watoto wote bila kujali misingi ya rangi, dini na utabaka waaina yoyote, pia kuwafanya watambue matatizo ya watoto wengine ili wakue wakijua kuna watoto wenzao wenye shida zaidi yao na wawe na moyo wakuwasaidia kupitia wazazi wao, pia kuwafanya wafurahi kwa kucheza ,kuimba na chochote chema ili mradi wafurahi.

Hapa tutafanya utafiti wa kugundua vipaji vya watoto na kuwasiliana na wazazi ili kuona mwelekeo wa kuweza kuwasaidiakatika siku za mbele ambapo Mungu akinijalia nategemea kuanzisha taasisi itakayohusika na shughuli za watoto.

Nimewaalika watoto yatima wa Kurasini ili waweze kufurahi na wenzao na kama kuna yoyote atayeweza kusaidia kwa chochote kile hasa kwa walengwa wakuu ambao ni hawa watoto yatima anakaribishwa kusaidia anaweza kupiga simu hii 0713-23 31 74 .

Michango itapokelewa hata baada ya sherehe kwani baad ya sherehe mimi na Juddy tutaelekea Zanzibar kwa mapumziko ingawa tutatumia mapumziko yetu kutembelea vituo vya watoto wenye shida na nyumba za kutunzia wazee.

Tayari kwa niaba ya Juddy nawashukuru Duka la vifaa vya elimu lilopo Upanga la KALL KWIK Bookshop kwa zawadi zao ambazo zitatolewa kwa watoto wote wataohudhuria sherehe hii.
Pia wale walioahidi kusaidia nitawaandika mara nitakapopokea zawadi zao. nawashukuru pia wazazi ambao tayari wamechangia sherehe hii na napenda kuwaahidi michango yao itasaidia kuwaalika watoto yatima na itatumika kwa madhumuni yaliyotajwa kwenye kadi tu.
Nashukuru kwa kuniamini na naahidi sitawaangusha tufanye huu ni mwanzo tu.

Ahsante na MUNGU awabariki wote na kuwajalia imani na huruma.

Ernest kwa niaba ya Juddy

Tuesday, November 06, 2007

MaChifu wa WaNgoni

Hii picha ilipigwa kwenye 1890's. Ni MaChifu wa waNgoni German East Africa. Sijui kama ni kweli lakini eti wote walinyongwa na waJerumani? Ninaomba sana kama kuna mtu anayejua
majina ya hao maChifu anijulishe. Asanteni.

Maoni - Falsafa za Watawala wetu na ulinzi wa kikatiba


Falsafa za Watawala wetu na ulinzi wa kikatiba

Imeandikwa na msomaji Ipyana Mwakamela



Ni mambo mengi sana yamejiri tangu Serikali ya awamu ya nne iingie madarakani dhidi ya ile ya awamu tatu juu ya uborongaji uliotawala katika uongozi wa kipindi cha miaka kumi cha Rais Benjamini William Mkapa.

Mengi yamesemwa na tuhuma kedekede dhidi ya Mkapa sasa zimeanikwa wazi juani kwa kila mwenye uchu wa kutaka kuzijua na afanye hivyo. Ninafurahi binanfsi kwamba kila ambacho kiongozi aliye madarakani alidhani amefanya kwa siri huwa kinakuwa peupe peee amalizapo muhula. Labda huo ndio ule tunaita ukomavu wa kisiasa na demokrasia ama uhuru wa kutoa mawazo kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Imeandikwa magazetini, imeongolewa katika vyombo vyote vya habari na hata katika vikao vya kahawa juu ya ufisadi uliotawala katika kipindi cha serikali ya awamu ya tatu. Kibaya ama kizuri zaidi, itategemea na kila mtu atakavyotafsiri ni kwamba Mzee Ben ameamua kukaa kimya kitu ambacho ama kinafanya uthibitisho wa tuhuma dhidi yake, kuendeleza tafsiri ya ubabe aliyokwishabatizwa nayo, kudharau vilio vya majeraha aliyotuacha nayo ama ni ujivuni wa kinga ambayo viongozi wakuu wastaafu wamewekewa na katiba yetu.

Mzee Ben aliwambia waandishi wa habari waliomtaka kuthibitisha ukweli wa tuhuma dhidi yake kuwa amestaafu siasa aachwe apumzike. Hii naifananisha kabisa na kauli ya Kikwete mwenyewe pale awali aliposema “Muacheni Mzee Mkapa apumzike”

Nashindwa kutafsiri maana halisi ya kauli hiyo ya Kiongozi aliyeshika dola kwa sasa kama ilimtoka kwa bahati mbaya, woga wa kutekleleza majukumu aliyoaminiwa ama ni kuimarisha ulinzi dhidi yake pale atakapokuwa amestaafu.

Ni mkanganyiko mkubwa maana wao pia wote waliona alichokifanya Fredrick Chiluba wa Zambia dhidi ya muasisi wa taifa hilo Kenneth Kaunda na hatimaye Levy Mwanawasa kumbadilishia kibao pale alipokaa nje ya madaraka.

Pengine ingekuwa vyema na busara zaidi kama Viongozi wetu wa Afrika wangejitahidi kuhakikisha macho yao yote mawili yanafanya kazi sawia kwa kuyazungusha kushoto na kulia huku wakiyapima kwa kutazama vitu vilivyo karibu yao na hata vile vya mbali na pale walipo. Hii ingewasaidia kujua yaliyotokea, yaliyopo kuwazunguka wao na hata yale ya baadaye yanayotazamiwa kuwafika. Wangelitekeleza hili hapana shaka hata utekelezaji wa ahadi zao wanazozitoa kwa waajiri wao zingelitimia.

Ninachojifunza kwa viongozi wetu ni kushindwa kabisa kutekeleza usemi wa “Ukila na kipofu msimshike mkono”. Wanatushika mikono yetu huku wakiendelea kusokomeza chakula chote midomoni mwao tena milo yote ya siku….hii ni kasheshe maana kipofu keshagundua kwamba anadhulumiwa na hatimaye atakufa kwa njaa kama akifanya utani.

Kwa mtazamo wangu Rais Mkapa naye alifanya mengi tu ya kukumbukwa tofauti na tunavyoichukulia kwamba ni mmoja kati ya viongozi waliotawala nchi ambao hawakutakiwa kabisa kuingia madarakani.

Baba yetu wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifanya mengi sana ya kujivunia katika nchi hii na ndio maana anakumbukwa mpaka leo hii na tungependa viongozi wetu wengine wote wanaofuata waige mfano wake. Lakini kama binadam Mwalimu Nyerere pia hakuyatimiza yote kikamilifu na hata yeye mwenyewe alikubali pale alipojikwaa. Hapa pia tukumbuke kwamba ni ngumu sana kwa viongozi waliofuata kufanya kikamilifu kabisa kama Mwalimu alivyotaka iwe. Wanawe tu wa kuwazaa hawajatimiza matakwa hayo sembuse wa urithi?

Baada ya Mwalimu kuachia madaraka alichukua Mzee wetu Ali Hasan Mwinyi ambaye aliongoza nchi kwa kipindi cha miaka kumi ambacho Hayati Baba wa Taifa alikuwa hai na akikemea kila alipodhani hapakua sawa. Tunakumbuka maneno kama ikulu kuwa pango la walanguzi, mtu kuongoza nchi na mkewe na mengine yafananayo na hayo ambazo ni kauli alizitoa Mwalimu kwa kutoridhishwa na uongozi wa Mzee Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa.

Si muafaka kumuongelea Mzee Ruksa kwa kuwa hakuwahi kujibu hata tuhuma moja dhidi yake katika zile alizotwishwa hata kama zilimdharirisha kiasi gani. Pengine ndiye aliyemshauri kijana wake Mkapa kwa kumuasa kukaa kimya kama alivyofanya yeye inaweza kuwa dawa mbadala.

Ninachojiuliza ni kwamba kama amemsihi hivyo aligeuza macho yake pande zote na kuangalia ni mwanga kiasi gani unamulika kwa viongozi kama wao sasa akilinganisha na wakati alioachia ngazi yeye?. Nadhani hapa panahitaji tafakari ya kutosha kabla hatujapandisha mori.

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete yu madarakani sasa, ndiye aliyeshika usukani wa nchi. Kizuri zaidi ni kwamba katika serikali zote mbili kabla yake alikuwamo ndani ya Serikali na hivyo si mgeni sana na mambo yaliyotendeka na pengine yanayoendelea kutendeka.

Labda linalonichanganya mimi sana ni hili: Je Rais atakuwa tayari kuruhusu mabadiliko ya katiba ili vile vipengele vinavyowalinda watu kama yeye waondokapo madarakani vinafutwa ili wakimaliza madaraka yao washitakiwe kwa kila walichotenda kinyume na kiapo walichokula, ama kwa lugha nyingine wahukumiwe sawa na matendo yao?.

Naomba Rais atujibu katika hili ili sasa tuanze kumuona jinsi gani alivyojiandaa kuwa safi katika utawala wake na wala si kufanya mambo kama waliyoyafanya wenziwe waliomtangulia na hivyo kuendeleza Utanzania wa kushupalia mambo wakati muhusika hayupo ama kutoa sifa kwa maiti ambaye hana la kufanya tena kwa wakati huo anapokuwa ndani ya jeneza.

Mheshimiwa Kikwete aliahidi kwamba atafuatailia kwa makini mikataba yote iliyosainiwa ya madini ili kuhakikisha kwamba kila kilichokwenda mrama kinarekebishwa kwa manufaa ya nchi na si kama ilivyofanyika hapo awali. Siwezi kuchimba kiundani kabisa kujua ni kwa kiwango gani mikataba hiyo tayari imekwisha pitiwa na hata kuruhusu kusainiwa kwa mikataba mingine kama ya Buzwagi inayopigiwa kelele kwa sasa na kuiingiza Serikali ya Chama cha Mapinduzi matatani dhidi ya kambi ya upinzani.

Kinacholindwa sana hapa katika mkataba wa Buzwagi hata kupelekea Mh. Zito Kabwe akasimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge, Mheshimiwa Lowasa kuiwekea ngao kila anapoulizwa na jeuri ya Karamagi kutojiuzulu kwa kashfa kama alivyofanya Mbilinyi na Mpologomyi enzi za Serikali ya awamu ya tatu ni nini?.

Mheshimiwa Rais alituahidi kwamba Waziri atakayevurunda hataweza kumaliza hata temu ya kwanza ya miaka mitano. Ni nani anathibitisha uvundo wa waziri?, ni mpaka Rais mwenyewe aseme ama kilio cha Wananchi walio wengi ndio chachu ya Rais kujua kiwango ambacho Waziri kavurunda?

Yupo Mheshimiwa Kapuya aliyetumia ndege ya Jeshi kwa safari binafsi na watu wakapiga kelele sana mpaka kwenye vyombo vya habari lakini sisi kama waajiri wakuu wa viongozi hao hatujafahamu hasa nini kilifuata baada ya pale na kelele za vyombo vya habari zilichukuliwa vipi na mkuu wa kaya hii.

Palikuwa na suala la Richmond ambalo lilifukuta na kufuka moshi mzito lakini hatimaye ikaja eksitigwisha ya Dowans ambayo ikauzima moto huo huku na yenyewe ikiwa bado na madhara na inaendelea kutafuna kama kutu inavyokula chuma.

Profesa Maghembe na Wizara yake ya Maliasili, macho yake hayakuzungushwa pande zote na sasa amefanikiwa kupandisha mbao kwa asilimia 700. Hakutazama mlaji mdogo anawezaje kununua ubao mmoja kwa shilingi 9000 kutoka bei ya awali ya shilingi 2000.

Bajeti ya Serikali ya 2007/2008 imepitishwa kwa mabavu pasipo kuzingatia maisha halisi ya Mtanzania na mfumuko wa bei ya vitu wakati tungali na mahubiri ya Maisha bora kwa kila mtanzania. Hakuna asiyejua gharama ya maisha imepanda kwa kiasi gani mpaka hivi sasa na huku mshahara wa kima cha chini wa serikali ukiwa chini ya shilingi laki moja kwa mwezi.

Pamekuja suala la malipo ya wafanyakazi wa majumbani maarufu kama House Girls na House Boys kwamba wanatakiwa kulipwa kima cha chini kabisa shilingi 65000 kutoka katika mfuko wa mfanyakazi anayelipwa shilingi 85000 kwa mwezi. Mahubiri yetu yangali “ maisha bora kwa kila mtanzania.

Kuna mradi wa ugawaji wa viwanja wa Serikali unaitwa viwanja vya bei nafuu lakini unaongelea kwenye malaki kama si mamilioni ya shilingi. Saruji imefikia kiasi cha shilingi 16000 kwenda juu kwa hapa jijini Dar es Salaam kwa mfuko mmoja wa kilogram 50. Tunavyo viwanda vitatu nchini Twiga Cement kilichopo Wazo jijini Dar es Salaam, Tanga Cement kinachozalisha Cement ya Simba na Mbeya Cement kinachozalisha Cement ya Tembo. Nani atajenga hapa ni kila Mtanzania ama tabaka fulani tu la watu?.

Nimeona katika vyombo vya habari matangazo ya Tanga Cement juu ya bei halali ya kununulia Cement yao kwa mikoa yote nchini. Najiuliza utekelezaji wake utakuwa vipi na ni nani atatutetea kuhakikisha bidhaa zinapatikana kwa bei inayotambulika. Sitamani hata kidogo kurudi katika enzi za “Duka la kaya”, nani atakuwa Sokoine wetu wa leo kupambana na uhujumu uchumi unaokuja kwa kasi ya ajabu.

Kikubwa katika haya yote ni kwanini tunawaangalia panya, mende, mchwa, dumizi, nzige na wadudu wengine wanaoingia kwenye boksi la mheshimiwa Kikwete huku wakifanya uharibifu kwa uhuru na viburi tena katika boksi jipya tulilolinunua jana kwa bei ghali zaidi na badala yake tunalishughulikia boksi la Mkapa ambalo tayari limekwisha chanika na hatuna jinsi ya kuliokoa leo.

Ufisadi unaotangazwa leo katika nchi yetu hautaisha kama hatutaacha unafiki wetu kwa wanaokalia madaraka leo ili tuwasubiri kesho watakapokuwa wametoka. Nani atakuwa Raisi wetu jasiri atakayetekeleza kwa dhati kila anayoahidi kuyafanya?.

Wapi Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na kwa nini imebakia nadharia tu na hakuna ukweli halisi wa kwa nini vitendo vyake vimebaki kuwa ndoto. Cha ajabu na kinachotia kichefuchefu ni kwamba kila panapotajwa jina la muasisi wake Wasomi, Wanadiplomasia, Viongozi mashuhuri hawaishi kutaja Azimio la Arusha na mengine mengi yaliyoasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kuna sababu gani ya msingi inayofanya kila mtawala aje na falsafa yake ikiwa falsafa zilizotumiwa na watawala waliotangulia hazina matatizo yoyote. Hapana shaka hapa nitapata waliobobea katika tafakari wanisaidie kupata uchambuzi wa hili tena ulio yakinifu.

Najuliza sana ni wapi “Fagio la chuma” lilikopotelea baada ya Mzee Ali Hassan Mwinyi kuondoka madarakani. Ni kwa nini falsafa yake haikutekelezeka kivitendo hata kwake yeye mwenyewe ikaendelea kubaki kinadharia peke yake na hatimaye kuzikwa kabisa baada ya Serikali ya awamu ya tatu kuingia madarakani. Kama ilikuwa ni falsafa nzuri yenye matunda kwanini haikurithiwa ama hata kuzungumziwa katika Serikali zilizofuata.

Kama pangekuwa na “Ukweli na Uwazi” aliotuletea Mzee Benjamin William Mkapa na ukatekelezeka kama ulivyokusudiwa na kupokelewa na umma wa watanzania walio wengi sidhani Mkapa angekuwa na jina baya machoni na masikioni mwa Wananchi aliowaoongoza kwa miaka kumi. Lakini hali kadhalika mazingira ya nadharia katika falsafa za watawala wetu yameendelea kutukuka na hii pia ilimshinda aliyeiasisi. Leo hii amekalia kaa la moto.

Kibaya zaidi ni kwamba kila inapokuwa mchana na usiku jina la tarehe, siku, mwezi na mwaka hubadilika. Sasa leo kuna mashindano ya viongozi bora wa Afrika wanaopata tuzo za heshima na kuvuna donge kubwa la fedha. Mfanyabiashara Mo Ibrahim amejitolea kutoa tuzo hiyo katika kuonyesha ama kutafuta njia mbadala ya kuwafunda watawala wa Afrika jinsi ya kuwatawala Waafrika wenzao.

Mzee Ben akadondoka kama kiongozi wa Tanzania na huku Joaqim Chissano akivuna alichopanda katika utawala wake. Hata hivyo mimi sikushutumu sana kwa hili kwani angalau ulimkaribia Chissano ukilinganisha na wenzio kumi na mmoja. Kumbuka unashutumiwa tu kwa kuwa tulihitaji kuwa na furaha waliyonayo Msumbiji leo hii…..pole sana mzee Ben labda Kikwete atajifunza kutoka kwako ili aje atutoe kimasomaso siku za mbele katika “ishu” kama hiyo.

Imeshika hatamu kubwa sasa “Kasi mpya, Nguvu mpya na Ari mpya” kwa kuwa ndiyo iliyo madarakani sasa. Ewe Mweny-enzi Mungu tunusuru na hili lisije bakia nadharia kama yaliyopita. Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete tunaona utekelezaji hafifu wa falsafa yako hasa ukizingatia kuwa bado upo katika hatua za awali za uongozi wa nchi ambayo ina kiu kubwa kabisa ya kuona mabadiliko ya kimaisha ili kauli mbiu yako “Maisha bora kwa kila Mtanzania” iweze kufikia lengo.

Hii habari ya badilisha huku kwenda kule kwa watendaji wako inakuharibia kabisa na inazidi kutia giza katika juhudi za kutekeleza kwa vitendo falsafa yako. Hii kwa kukuibia siri tu ndio chanzo cha kuanguka kwa falsafa za wenzi wako waliotangulia. Ikiwa huwa mnafanya hayo kwa makusudi yenu binafsi basi lipa fadhila ama ua nyani kwa kumtazama usoni kisha uone haya.

Boksi la uliyempokea kijiti li tafrani kabisa, limeliwa na wale wadudu aliowafuga kwa muda mrefu na kuwaacha wazaliane huko. Tayari boksi lako limeingia wadudu wale wale kwa kuwa hukulichoma moto boksi la Mkapa bali umeliweka karibu na hilo la kwako jipya na wameanza mapema kulitoboa lakini halahala maana sasa hivi madawa ya kuwaangamiza wadudu hao ni mengi tu ni wewe kwenda sokoni na kununua. Ukiwa mvivu dawa yake itakuwa ni kuchoma nyumba nzima ili hata wale walijificha katika kenchi na kona zisizo fikika waweze kuteketea.

Hatuhitaji mbwembwe na ujuvi wa kuibua falsafa zaidi kinachohitajika na Watanzania wote ni “Utekelezaji kwa vitendo wa falsafa zenu”. Nakumbushia tu, tumeyafumbua macho yetu kwa ung`avu kabisa na hatutalala tena.

Ipyana Mwakamela
P.O. Box 17132
Dar es Salaam
Barua pepe: nakumbushia_tu@yahoo.com

Monday, November 05, 2007

Aliyeigiza kama Shaka Zulu Amefariki!




Mwigizaji maarufu wa Afrika Kusini, Henry Cele, amefariki dunia kwao Durban. Wengi tunamfahamu kama SHAKA ZULU.
Habari zinasema kuwa alifariki jana baada ya kuuguua ugonjwa wa kifua. Alikuwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi kwa zaidi ya wiki mbili. Habari za kusikitisha zinasema aliugua muda mrefu na hapo mwisho alikuwa anatukana na kupiga watu ovyo mpaka ilibidi afungwe na kamba kwenye kitanda chake cha hospitali.
Henry Cele aliigiza kwenye sinema kadhaa lakini hakupta umaarufu aliyotegemea. Agent wake anasema kuwa hapo mwisho offa za kazi zilianza kuingia lakini Cele alikuwa ni mgonjwa hivyo hakuweza kuzifanya.

Alifanya kazi nzuri mno kuigiza maisha ya mfalme maarufu ya huko Afrika Kusini, Shaka Zulu. Hiyo sinema inajulikana kama sinema bora na inayoonyesha maisha ya Shaka Zulu kutoka upande wa mwafrika. Na Shaka Zulu mwisho wa maisha yake alikuwa kama kichaa maana alikuwa anaua watu ovyo na kusababisha maelfu ya wafrika kusini kukimbia kwao.

Kabla ya kuingia kwenye dunia ya uigizaji, Henry Cele, alikuwa ni mcheza mpira maarufu wa Afrika Kusini. Alikuwa anaitwa, The Black Cat. (Paka Mweusi) kwa sababu alikuwa ni mweusi sana kulinganisha na wafrika kusini wengine.

Kwa habari zaidi someni:


Oprah Jihadari!


Hii skandali ya shule ya Oprah sasa unaingia kwenye ukurasa mpya. Kuna baadhi ya wa South Africa wanamwonya Oprah kuwa awe mwangalifu. Wanasema amezidi kuleta umarekani na ufahari kwa hao wasichana waliotoka kwenye familia maskini.

Wanasema ni kawaida wasichana na hata wavulana waliokosa nidhamu kuchapwa kwa mila zao. Wengine wanasema kuwa wana wasiwasi kuwa madai ya unyanyasaji ya hao wasichana si ya kweli. Wana hofia kuwa msichana akimchukia mkubwa basi watasema uwongo juu yao na kwa vile Oprah ni mtu mzito mtuhumiwa hatasikilizwa.

Wengine wanasema kuwa Sangoma (waganga wa kienyeji) zao wana dawa kali, Oprah anaweza kuamka siku moja ajikute kichaa au kapofuka.

Oprah alifungua shule kwa nia nzuri mwanzoni mwa mwaka huu. Watu wanacho hofia ni kuwa ametenga hao wasichana anaowaita binti zake na kuwalea kifahari mno. Pia watu wana hofu watakosa kulelewa kikwao.

Majuzi Oprah alimpa kila msichana wa shule hiyo, simu ya mkononi enye 'feature' inayomwezesha kupiga simu moja kwa moja Oprah Marekani.

Mmoja wa matron wa shule hiyo, Tiny Virginia Makopo, amefunguliwa mashtaka ya kupiga wasichana 15. Pia wasichana wandai kuwa alitaka kufanya ngono ya kishoga nao.
Mwalimu Mkuu, wa shule hiyo, Dr Mbulelo Mzimane, naye amefukuzwa kazi na Oprah kwa madai kuwa hakusikiliza malalamiko ya wasichana wa shule hiyo.

Oprah ametuma 'Trauma Specialist' kutoka Marekani kwenda kutoa tiba kwa hao wasichana kusudi wasipate majeraha ya fikra ya kudumu.



Tangazo kwa wenye magazeti ya Lance Spearman


Kuna mdau anatafuta makala, magazeti/majarida yenye habari za Lance Spearman ambaye alikuwa muhusika wa makala/tamthiliya za picha (photo novel/photo play/photo comic) zilizochapishwa kati ya miaka ya 1960 na 1970 na magazeti ya Afrika Kusini "Drum Publications Ltd".

Mhusika huyu pia alikuwa anajulikana kama "The Spear" au "Spia"Pia kwa Afrika Mashariki kuna magazeti yaliyochapishwa Kenya yanayoitwa "Film" au "African Film" yaliyokuwa na mhusika huyu.

Pia kuna wahusika wengine kama "Fearless Fang", an African "Tarzan" na wengineo pia kama kuna mtu mwenye kumbukumbu zozote hizo pia zinahitajika.

Mdau huyu yuko tayari kununua nakala hizo zilizotumika zitakazopatikana kwa ajili ya kuweka kumbukumbu katika maktaba.

Kulingana na ubora na idadi mdau yuko tayari kulipa Euro 5 mpaka 20 Kwa watu wanaofahamu jarida/gazeti linaloitwa "Film Tanzania" na kama kuna mtu analijua na upatikanaji wake mdau anaomba amfahamishe kupitia vicensiashule@hotmail.com.

Sunday, November 04, 2007

Apiga Maiti Kanisani! Mwingine afanya ngono na maiti!

Timothy Cleary

Leo nimesikia mpya! Kwa kawaida watu wanaogopa maiati. Lakini kichaa fulani wa kizungu aliingia kwenye kanisa ambapo marehemu alikuwa anaagwa na kuanza kumpiga mangumi. Jeneza ilikuwa wazi kusudi waombolezaji waweze kumwona kwa mara ya mwisho. Watu waliokuwa huko kanisani kumwombea marehemu waliita polisi huko Harvest Baptist Church.

Polisi walimtambua kichaa kama, Timothy Cleary, wa Apopka, Florida karibu na Orlando. Haijaeleweka sababu ya kupiga maiti lakini jaji ameamuru apime akili.

Na huko Teaneck, New Jersey kijana wa miaka 24 amekamatwa kwa kufanya ngono na maiti ya Bi Kizee wa miaka 92!

Polisi wanasema kuwa huyo kijana ni Anthony Merino na ni mfanyakazi wa hospitali ya Holy Name alipofia huyo bi kizee. Wanasema amefanya kazi pale siku 14 tu na alikuwa mfanyakazi wa kulipwa per diem, si mfanyakazi wa kudumu. Aliingia kwenye mortuary ya hospitali ndipo alipovamia maiti.

Baada ya maovu yake kugundulika alikamtwa na polisi na nudgu wa marehemu waliaarifiwa.

Merino yuko jela kwa sasa. Jaji ameamuru apimwe akili. Dhamana yake imepangwa dola $400,000. Akipatikana na hatia anaweza kufungwa gerezani kwa miaka 10.

Kwa habari zaidi soma:

Aliypeiga maiti:

http://www.shortnews.com/start.cfm?id=66217


Aliyefanya ngono na maiti:

http://www.local6.com/news/14466884/detail.html


Friday, November 02, 2007

Rose Muhando atafanya Concert Detroit, Michigan



WaBongo wa US Midwest mtafaidi sasa! Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, Rose Muhando atakuwa Detroit.

DATE: NOVEMBER 11th, 2007

TIME: FROM 12:00PM (Noon)


Kwa habari zaidi contact: Mrs. Malaniese Zeigler 1-313-921-3100

Bishop Milton Woods @ 1-313-921-7209

Thursday, November 01, 2007

Wimbi la Ajali za barabarani Tanzania!


Nimetumiwa haya maoni na msomaji Born Again Pagan:

*******************************************************************************
Born Again Pagan said...
Chemi, naomba uruhusu haya yangu kuhusu Ajali Barabarani Nchini:


Hivi karibuni, katika mojawapo ya blogu nyingi mashuhuri za wa-Tanzania, niliahidi kwa kuwaomba wanakijiji kujipa muda wa tutafakuri na kuchangia suala la ajali barabarani na jinsi ambavyo tunaweza kupunguza “balaa” hili ambalo linaendelea kutusibu siku hadi siku, mchana na usiku.

Ingawa ni wanakijiji kama wawili hivi walichangia, sikukata tamaa. Nazidi kuwaombeni tujaze blogu hizi kwa maoni yetu kuhusu maafa ya ajali barabarani. Blogu hizi zinasomwa na wengi, wakiwemo viongozi wa serikali, wabunge wetu, viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya serikali.

Napenda kurudia mchango wangu wa awali kuhusu ajali nchini mwetu, ikiwa ni sehemu ya maombolezo ya kutokwa na Naibu Waziri Salome Mbatia. Mhariri wa gazeti maarufu nchini la kila siku aliandika, “…taifa limeghubikwa na majonzi makubwa kufuatia kifo (cha Naibu Waziri Salome Mbatia) kilichotokana na ajali ya gari eneo la Kibena, Njombe mkoani Iringa Alhamisi.”

Lakini yatubidi kuzingatia kwamba si Salome Mbatia peke yake aliyekufa katika ajali hiyo. Dereva wake na utingo wa lori nao walikufa. Na sio ajali hiyo tu iliyotokea siku hiyo na kusababisha mauaji! Karibu watu kama kumi hivi walikufa kwa ajali barabarani siku hiyo! Lakini kifo cha Naibu Waziri Salome Mbatia kimepewa kipaumbele zaidi ya vifo vya wengine. Sababu zinaeleweka; sina haja ya kuzirudia.

Mhariri huyo alitoa tahadhari kali kuitaka “Serikali na vyombo husika na sekta ya usafirishaji” kudhibiti ajali: “[Y]afaa tatizo hili la ajali za barabarani zinazotokana na uzebe na mwendo wa kasi litizamwe tena kwa makini. Bado linapoteza maisha ya watu wengi wasio na hatia wakati zinaweza kuepukwa.

Madereva wengi bado wamekuwa ni vichwa maji katika uendeshaji wao barabarani.”Kauli kama hiyo ya mhariri, sambamba na kauli nyingi za umma zisizotangazwa, inaitaka serikali yetu kamwe isingoje “kifo cha mzaliwa wa kwanza”, kama mtawala Firauni wa Misri, ndipo iamke na kufanya lolote dhidi ya “janga” hili ambalo hudonoa maisha ya wa-Tanzania wetu!

Tumezoea kusema, “Ajali haina kinga!” Lakini ukweli ni kwamba ajali inaweza ikakingika! Wengine husema, “Ngoja ajali ziwamalize kwa kumwonea Kabwe Zubeir Zitto!”

Hili nitalizungumzia kwa kifupi:Katika magazeti na blogu nyingi kumeibuka tabaka la washirikina au niwaite “wanajimu wabaya, watabiri mabaya, wenye ndoto mbaya, wenye maono” wenye kungojea “kiyama” kiikumbe serikali na CCM yake.

Wenzetu wanamwomba m-Bunge wetu “kijana” Zitto Zubeir Kabwe aombe miungu ya huko kwao Kigoma kuweka breki ili isiwamalize wote wale waliomnyoshea kidole - mizimu ya Kigoma inalipa kisasi!

Wanaoanisha msululu wa ajali ambazo zimetokea kwa baadhi ya viongozi wa CCM kufuatia mzozo wa m-Bunge wetu “kijana” Zitto Zubeir Kabwe eti zinatokana na “kumwonea Zitto”!

Natarajia kuchangia hili la mzozo wa Zitto, kulingana na maoni ya wasomi wetu wawili: Prof. Gidion Shoo (Zitto Hakuwatendea Mema Wananchi,” kwa mujibu wa “Kanuni za Bunge”.

Msomi mwingine ni Prof. Shivji (Zitto Kabwe’s Suspension an Episode or an Epitah?) Kero ya Zitto yaonyesha jinsi ambavyo nchi yetu imejigawa. Kuna ukweli kwamba wote hatuimbi, “Tanzania, Tanzania,
nakupenda kwa moyo wote;
nilalapo nakuota,
jina lako ni tamu sana”!

Ni lazima kuna sababu zake, mbali ya vitendo vya rushwa na ufisadi!Kuna baadhi yetu ambao wamegeuka washirikina na kuonyesha hali ya chini kabisa. Hawa wanaomba mabaya zaidi yawapate wana-CCM, kwa jumla, na hasa wale viongozi waliojeruhiwa katika ajali mbali mbali!Sioni kama hili ni ombi la kiungwana!

Ni matakwa ya wendawazimu kwani endapo CCM inafanya mabaya, kuitakia mabaya nako ni vibaya! Makosa mawili hayajengi au hayazai haki!Kumtakia mwenzako kifo ni sawa na kumwua tu. Leo tunatakiana vifo; kesho tutauana kimacho macho!

Kuna wengine wenye kuamini kuwa ajali “Ni mipango ya Mungu - Mungu kapenda; siku yako ya kufa ikifika, imefika!” Hili pia yanataka ufafanuzi: Je, maisha yetu yamewekewa“blinkers” za “determinism”? Je, hakuna lolote tunaloweza kufanya kuepusha hiyo “determinism”? Mbona tunataka kuingilia kati nguvu za asili (nature) kwa kualika nchini “wachawi wa mvua” kutoka Thailand?

Maisha yanajengeka kutokana na kuoana kwa akili zetu na maingilio ya mazingira tuliyomo. Tunaweza kuyabadili kwa kupata elimu tosheleza na hekima ya kuweza kutafukari na kutafuta njia za kusuluhisha au kutanzua tatizo la ajali barabarani. Wengine, hasa wadini walokoke huamini kuwa Mungu huadhibu kwa sababu ya dhambi. Hii sio kwa wa-Tanzania tu bali pia wahubiri wengi walokoke duniani, hususani, Marekani.

Mhubiri mmoja mlokoke wa Amerika aliwahi kutamka kuwa Jimbo la Florida lilipatwa na madhara ya kuwaka moto kutokana na dhambi za kisenge na kishoga. Mlokoke huyo huyo alimshutumu Waziri Mkuu wa Israel kwa kupatwa na mshituko uliomlemaza kuwa ni kwa sababu kagawa nchi ya Palestine - nchi ya Mungu - kwa Wapalestina!

Kisa kingine cha hivi karibuni: Jaji wa “federal” hapa Amerika ameamuru kanisa moja la Ki-Baptist la Westboro - kanisa lenye kuhubiri na kueneza chuki - kulipa faini ya dola millioni 10.9 kwa kushangilia kifo na kukielezea kifo hicho cha askari Lance Cpl Matthew Snyder vitani Iraq Machi 2006 kuwa ni adhabu kutoka kwa Mungu.

Washirika walokoke wengi wa hapa Amerika wanahubiri ‘injili ya chuki” dhidi ya ushoga na kubagua mazishi ya watu waliokufa kwa ukimwi. Walokole wengine wanaamini kuwa Amerika inapata majanga, kama hilo la 911, kwa sababu wameacha kumcha Mungu! Je, Mungu anatuadhibu na hizo ajali zitokeazo barabarani?Pengine hilo la ajali na kudra za Mwenyenzi Mungu nalo linahitaji muda wake maalum wa kutafukari kwa undani, hasa kwa wale wenye kutaka kujua kutoka kwa wanaolielewa vizuri.

Kuna baadhi yetu wenye kuziona na kuzitafukari ajali barabarani na kwinginepo, kama matukio ya kawaida tu. Tusitekwe nyara na fikra za kufungwa macho yetu na akili zetu kuamini kwamba ajali haina kinga; ajali ni adhabu ya Mungu, au ni matakwa mengine ya ushirikina.

Ajali husababishwa na/au mchanganyiko wa haya matatu:dereva, gari na barabara. Kuna Ripoti ya Mwaka 1994 inayoelezea rasmi na kwa undani kuhusu usafiri nchini. Sijui ni wangapi kati ya matrafiki husika, wamiliki wa magari, maderera na abiria wa kawaida wameipitia ripoti hii?

Kuna vitu vitatu muhimu katika njia za usafiri wa nchi kavu kwa kutumia magari barabarani: dereva, gari na barabara. Kila kimoja kina masharti yake sawa na “social environment”: mshiriki (actor/participant), kusudi (purpose), sheria (rules and regulations), mipaka (boundaries), maadili (morality), siasa (what is to be done), na lugha (technical language).

Dereva: Kulingana na Ripoti hiyo, sababu kubwa ya ajali nchini mwetu hutokana na madreva wenyewe. Ajali za namna hii ni kiasi cha asilimia 76. Napenda kuongezea kuwa u-mahiri na u-makini wa kuendesha unatokana na mafunzo tosheleza na utahini usiopendelea; dereva kujiandaa vya kutosha kabla ya safari; asiendeshe huku amelewa au amechoka; afuate sheria za barabarani; na uwezo wa dereva kubaini endapo gari lake lina udhaifu au kasoro.

Ajali nyingi za mabasi, malori yetu na magari madogo yetu kugongana vichwa kwa vichwa, kama ajali hiyo iliyotokea na na kuchukua maisha ya wakina Waziri Mbatia, dereva na utingo wa lori. Hii ina maana kuwa sababu kubwa ni pale dereva wa gari linalofuata kutaka ku-“overtake” lililotangulia karibu na mwisho wa kilima au kwenye kona kali bila kujua kuwa kuna gari lingine linakuja mbele.

Wakati mwingine gari hupata kasoro na dereva kushindwa kuliongoza. Sababu nyingine ni kwa dereva kuchoka na kusinzia sinzia na mwisho kupoteza saiti yake. Madereva wengine huendesha kulingana na wimbo wa mapenzi wa Daudi Kabaka (Kenya), ambapo abiria anamsihi dereva wa basi aongeze spidi ili abiria afike au awahi “date” yake:

Dereva,Choma gari moto;
Nifike upesiNikaone mtoto.
Mtoto ananingojaStendi ya basi;
Fanya haraka!

Kuna pia baadhi ya abiria wenye kutaka kufika mapema kungali na jua kule waendapo. Abiria kama hao huimiza dereva aendeshe kwa kasi. mMadereva wengine nao wanapenda sana kuendesha kwa kasi ili wapate muda wa kupumzika, na kupata angalau “moja baridi” au kuwaona wapenzi wao huko waendapo au mwisho wa safari.

Madereva wengine ni walevi; hupenda kunywa vileo kabla ya safari na wakati mwingine kupumzika safarini kwenye visima vya ulevi. Ukiwa Dar es Salaam, mabasi ya kwenda katika mikoa mingine yanaitwa “mabasi ya kwenda mikoani”, kana kwamba Dar es Salaam si mkoa.

Kuna mabasi mengine, kwa mfano, huondoka Dar kwenda Mwanza kupitia Nairobi (Kenya) huwa yana madereva wawili tu. Kuna pia mabasi yanayoondoka Dar es Salaam kwenda Lubumbashi huko Kongo (Kinshasa) kupitia Kitwe (Zambia). Habari za kuaminika zinaeleza kuwa wakati mwingi madereva huchoka kuendesha na kuanza kusinzia sinzia na huku wakiendesha.

Kuna madereva wengine wenye ka-tabia ka kuendesha magari kana kwamba wana-“enjoy the cruising moment.”Madereva wengine vichwamaji huwazuia wenzao wasipite; ni kama umewatukana. Hivyo huendesha kwa ujeuri kana kwamba kuna ugomvi au vita.

Madereva wengine, hasa kwenye barabara zetu zisizo na lami, wanapenda sana kutangulia kuepuka au kuogopa mavumbi yanayoachwa na gari liliotangulia. Huwa ni mashindano. Kuna wengine, hasa wamiliki, hupenda sana kushindana kuwa wa kwanza kuchukua abiria au shehena kabla ya wenzao. Tabia hii ni ya kawaida kwenye barabara zetu nyingi.

Dereva wa basi ataliendesha basi lake kwa “ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya” ili awahi kuchuma. Na mara nyingine basi linaweza kupata ajali.Barabara nyingi hazina maafisa wa trafiki. Na kama wapo wengi wanahongwa; na wananyamaza, kana kwamba mambo yote ni sawia. Lakini ukificha maradhi, kifo kitakuumbua.

Wamiliki wa magari na madereva wamewaweka wakuu wa trafiki wa wilaya na mikoa mikononi. Hata kama afisa wa trafiki mdogo akimkamata mhalifu, kesi yake itafutwa na “wakubwa”.Barabara: Ripoti hiyo hiyo inaelezea kuwa ajali asili mia 7 husababishwa na matatizo ya barabara. Napenda kuongezea kuwa barabara zetu ndo hivyo tena; zilitengenezwa wakati magari yalikuwa ni ya serikali au machache kwa ajili ya abiria. Ieleweke wazi kuwa hakuna uwiano wa moja kwa moja kati ya barabara nzuri na kupungua kwa ajali.

Huko Ulaya kufika mwaka 1648, barabara zake nyingi zilizokitengenezwa tangu enzi za Warumi zilikarabatiwa kukabili mapinduzi ya viwandani yaliyoleta magari ya kukokotwa na farasi hadi mwingilio wa magari ya sasa.

Huko Ulaya, Ujerumani wakati wa Hitler ikawa ya kwanza kuwa na “autobahns” “highways”) kukidhi mahitaji wa maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo na endapo kutatokea vita. Nchi nyingi za Ulaya/Amerika na zingine zilizoendelea zina barabara nzuri na pana.

Nitatoa mfano mdogo wa hapa Amerika:New Jersey Turnpike (Highway) ipitayo karibu na Newark Liberty International Airport ina barabara zenye safu (lanes) sita za kwenda upande mmoja. Kwa hiyo barabara kuu hiyo ni kama ina barabara 12. “Highways” nyingi zina safu 3. Kwa kuwa Amerika inaendeshea mkono wa kushoto, safu ya upande wa kushoto ni kwa wale wenye kutaka kwenda kasi bila ku- “exit”.

Safu ya katikati ni kwa wale wenye kuendesha mwendo wa kawaida. Na safu ya upande wa kulia ni kwa wale wenye kutaka ku-“exit”.Pamoja na “administration and management” ya uedeshaji wa namna hiyo, kuna matrafiki wakali wa mikoa (State Troopers) wanaolinda sheria za barabarani.

Wengine hufanya kazi zao wazi wazi.Endapo msafara wa magari unakwenda kwa kasi, gari la trafiki hao litatangulia mbele na kwenda spidi inayotakiwa. Hakuna dereva atakayethubutu kuli-“overtake”! Kuna wakati madereva iliwabidi kuwasiliana kwa njia ya "Citizen Band - CB" ili kujiepusha na "State Troopers".

Wakati mwingine matrafiki hao hujificha vichakani kando ya marabara na kuwalopoa (kwa njia ya rada) wale wenye ku-“overspeed”, na wakati mwingine kufanya ukaguzi wa ghafula wa gari .Magari ya kubeba shehena (“rigs” au “long distance trucking or haulage”) haya yana sheria zake kali. Kila dereva ni lazima abebe utambulisho wa kile alichobeba, kinatoka na kwenda wapi, ameanza kuendesha saa ngapi, na amepumzika kwa kiasi gani. Gari lake pia ni lazima lionyeshe ukaguzi uliofanyika.

Na katika mabarabara ya mikoa mingi kuna “weighing stations” za kupima magari hayo yamebeba shehena ya uzito gani, pamoja na kuchunguza mambo mengine muhimu ya ki-trafiki. Dereva mwenye hatia, hutozwa faini pamoja na kupoteza pointi fulani kutoka kwa leseni yake, hadi kiasi cha kutoruhusiwa kuendesha Gari. Ripoti hiyo niliyotaja hapo juu inaeleza kwa ajali asili mia 1 husababishwa na gari lenyewe.

Napenda kuongezea kuwa baadhi yetu wanaweza kusema gari haliui; anayeua ni dereva, sawa na kusema kuwa bunduki haiui; anayeua ni mwanadamu. Gari halina budi kuwa katika hali nzuri ya kuendeshwa. Matairi yawe katika hali nzuri na kiasi cha upepo uliojazwa, na viungo vingine muhimu vya gari vichunguzwe mara kwa mara kuona na kuhakikisha kuwa havina kasoro. Gari ni lazima lifanyiwe “servicing”.Kuna ka-tabia ka kupenda kutunza pesa kwa madai kwamba gari bado linakwenda. Wamiliki hawapendelei kukarabati magari yao.Ajali nyingi zinazotokea huwa ni za mabasi mapya. Hii haina maana kuwa basi jipya halipati ajali.

Mengine huanguka kwa sababu ya spidi (ku-“overtake”) na kujaza abiria na shehena (overload). Mara nyingi mabasi ya namna hiyo hushindwa ku-“balance” kutokana na mshituko wa kona au kwa ghafla kujaribu kukwepa wakati wa ku-“overtake”.

Nchini Amerika ni Jimbo la Connecticut peke yake lenye 55 m.k.s. (majimbo mengi yanaendesha 60, 65, 70 na 75 m.k.s.). Lakini takwimu za spidi na ajali hazikubaliani. Hakuna uwiano kati ya spidi kali na kutokea kwa ajali! Pengine hii ni kwa sababu ya huduma za haraka za ambulance na hospitali katika kunusuru waliojeruhiwa. Kukosekana kwa huduma za namna hiyo nchini Tanzania kunawafanya waliojeruhiwa kutokwa damu sana.

Lakini hapa Amerika endapo itatokea ajali, basi magari huwa yanavaana nyuma kwa nyuma. Kumekuwepo na ajali nyingi za mashangigi nchini mwetu. Lakini hatuna utafiti yakini wa kuonyesha au kuelezea ni mashangigi ya aina gani au modeli gani, ua magurudumu ya aina gain hupasuka pasuka na kusababaisha ajali.

Wakati mwingine, gari au matairi yake huwa vina hitilafu ambazo madereva wengi hawazifahamu! Ajali nyingine hapa Amerika zimesababishwa na hililafu, kama nilivyoelezea hapo juu. Ikibainika kuwa aina au modeli fulani ya magari au matairi ndio yenye makosa, basi aina au modeli au matairi hayo yatarejeshwa viwandani.

Je, Tanzania itahakikishaje kuwa hitilafu kama hizo, na makosa mengineyo yanadhibitiwa? Yasemekana Tanzania yetu ni maskini haiwezi kutengeneza barabara kama za Ulaya/Amerika au kuwa na teknolojia ya kisasa ya kudhibiti nidhamu ya uendeshaji na upakizi. Nakubalina na hilo hapo juu.

Lakini kuna mengi ya kufanya kudhibiti ajali barabarani. Mabasi kutoka na kurudi Mwanza/Dar yanayopitia nchi ya jirani ingefaa yawe na madereva wanne. Mmoja kati ya Dar na Arusha (apumzikie Arusha); Arusha na Nairobi (apumzikie Nbi); Nairobi na Tarime (apumzikie Tarime); na Tarime na Mwanza (apumzikie Mwanza). Kila dereva aweze kuendesha kwa muda wa kati ya masaa manane na masaa kumi hivi. Mabasi yanayokwenda Lubumbashi (Kongo-Kinshasa) nayo yadhibitiwe kikamilifu: Dar hadi Iringa; Iringa hadi Tunduma; Tunduma hadi Kitwe. Kitwe hadi Lubumbashi.

Kuhusu madereva, sioni sababu kwa nini kusiwe na matrafiki wa tarafa au wilaya. Hawa matrafiki wetu waheshimike na wapokezane zamu toka tarafa hadi tarafa au toka wilaya hadi wilaya.Na kama madereva watathubutu kuwahonga, watahonga mpaka lini? CID, TAKUKURU. na Usalama wa Taifa viwashughulikie!

Yafaa sana mabasi yawekewe ratiba na yazifuate ili kuzuia hiyo “marathon” ya uchu wa kuchuma pesa. Tuwape madereva mafunzo bora ya usanii elekevu wao kupitia semina, majopo au mikutano sawa na “refresher courses” za kuzidi kunoa umahiri wa kuendesha. Pengine haitawezekana kuwakutanisha maderera wetu huko Ngurdoto Hotel au Bagamoyo!Lakini tunaweza kupitia kwenye restauranti za “Mama Ntilie” ili nao wapate mtaji wa kuendeleza ulishaji mijini kwa walalahoi.

Kwa wale madereva wanaoendesha wakubwa, mara nyingi kumekuwepo na malalmiko ya hao madereva kutopata muda wa kupumzika wawapo safarini. Badala ya kumwambia dereva aende akapumzike na aje amchukue wakati fulani, dereva huyo analazimika kungojea kwenye gari bosi wake amalize shughuli rasmi au za ubinafsi hadi zaidi ya usiku wa manane! Dereva anaambiwa kuanza safari ndefu asubuhi na mapema, tuseme kurudi Dar es Salaam.

Na wakati mwingine madereva hao hata posho hawapati vizuri! Tatizo la kupakia abiria na shehena nyinginezo zaidi ya kilichoruhusiwa, limesababaisha ajali kwa vyombo vetu vya usafiri si barabarani tu bali pia relini, angani na majini.

Gari la moshi lilishindwa kupanda miinuko na ghafla ku-“reverse” na kurudililipotoka. Ndege zetu nyingine zimeshindwa kuruka shauri ya uzito wa shehena (magunia ya vyakula na matunda). Meli, boti, mashua na mitumbwi yetu imezama shauri ya uchu wa pesa kutokana kujaza sana abiria na shehena. Umuhimu wa “servicing” uzingatiwe na kuelezeka kwa msemo wa mambo ya uganga, “Wakia moja ya kinga ni bora kuliko tani ya tiba.”

Tanzania si masikini; ni tajiri. Tunafuja mapesa yetu bure. Fikiria, hao mawaziri karibu sitini ya 60 ni wa nini, kama sio kuzidi kutonesha kidonda cha umasikini wetu? Hawa “mawaziri” na “wizara” zao wanamaliza mapesa kwa mishahara ya wafanyakazi, kuwapamba kwa magari ya fahari na majumba, marupurupu, ubadhirifu, ufisadi, na kurudufisha huduma.

Tulishindana na Benki Kuu ya Dunia, washauri wetu wa uchumi, kututaka tupunguze sekta ya umma (serikali) ambayo ilikuwa imetuna, mithili ya mwenye kitambi. Tukashauriwa kuipeleka “gym” ikafanye mazoezi ya kukonda; ikakonda! Lakini sasa tumerudia yale yale ya kuota kitambi, tena kikubwa zaidi! Ikiwa kitambi kwa binadamu leo hii ni “skandali”, basi hata kitambi cha serikali nacho ni “skandali”!

Najua nchi kongwe (kama Uingereza, Ujerumani, Ufaransa) zilikuwa tayari na dola (the State) kabla vyama vya siasa kuanzishwa. Nchi changa (kama Tanzania) zilikuwa ni lazima ziunde vyama vya siasa ili zijenge (the State) na State ijenga nchi. Kwa kifupi, chama tawala cha siasa ndicho kiliunda State ijenga nchi.

Matokeo ya kuota kitambi kitambi hicho yalikuwa ni mafanikio ya kujenga nchi. Leo hii eti tunaambiwa mambo yamebadilika. Kuna kuoana baina ya sekta ya ummana ya binafsi. Ndoa hiyo ndio kitovu cha maendeleo ya kujenga nchi….bado tunajenga nchi mpaka leo!

Ubinafsi tuliouona kwa darubini ya ujamaa kuwa kama dhambi, leo hii ni nyenzo muhimu ya kuleta eti maendeleo! Tunalipendelea sana Jiji la Dar es Salaam. Wengine kati yetu wanalifananisha na New York au Shanghai kwa madhari yake.

Tuliache Jiji hili lilivyo bila ya kulinyonga.Lakini Jiji la Dar limeshindwa kudhibiti wingi wa magari kwenye barabara zilizotengenezwa wakati wa Gavana akiwa ndiye mwenye gari, na wakati wa kutaka kutoka na gari hilo, barabara zilifungwa.

Mpaka sasa, serikali imekataa kuhamia Dodoma; inazidi kujenga nyumba za mawaziri mjini hapo Dar! Nchi imetumia mapesa mengi kwa ajili ya hayo “makao Makuu ya Dodoma” toka enzi za “Sir” George Clement Kahama! Na “over cost” yake inazidi kila mwaka,licha ya kutojua ni mapesa mangapi Mamlaka ya Mji wa Dodoma ilitumia kuwakopesha wafanyakazi wake kujijengea nyumba zao binafsi! Tuache kuhamia Dodoma! TAKUKURU mnayajua hayo!

Itatubidi tuunde utaratibu wetu wenyewe wa madaraka mikoani ili kuendeleza baadhi ya miji yetu mingine na kupunguza msongamano wa magari jijini Dar,ikiwa ni pamoja na watu kusafiri kwendaDar es Salaam kwa ajili ya kununua vitu na huduma. Niruhusu nifupishe orodha ya wizara zetu ziwe wizara 15 tu.

Orodha iwe fupi kama mini-sketi lakini ndefu kiasi cha kusetri huduma za lazima, kama ifuatavyo:Dar es Salaam: Fedha na Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Mipango (Mipango, Uchumi, Uwezeshaji na Kazi); Habari, Utamaduni na Michezo; Nje (Mambo ya Nje, Mashirika ya Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Mashariki); na Ulinzi na JKT.Dodoma: Uhusiano wa Ndani (Muungano, Siasa na Uhusiano wa Bunge); Elimu (Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia; Sheria (Katiba na Utawala Bora); pamoja na kuwa Makao Makuu ya Vyama vya Siasa.Arusha: Maendeleo (Makazi, Jamii, Jinsia na Watoto); Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa Nairobi na Kenya Kusini.Mwanza: Afya na Ustawi wa Jamii, na Mazingira Nishati, Madini na Miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuwa jiji la kuhudumia biashara ya Ziwa Victoria, Uganda, na sehemu za Kenya Magharibi.Kigoma: Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijana, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa biashara ya Ziwa Tanganyika, na DCR Mashariki.Mtwara: Uzalishaji (Viwanda, Biashara na Masoko).

Mtwara hauna budi kupewa hadhi mpya kama mji wa huduma za mpango wa “Mtwara Corridor” (Tanzania, Malawi na Zambia na sehemu za Msumbiji Kasikazini). “Daraja la Umoja” kwenye Mto Ruvuma ili kuunganisha Tanzania na Msumbiji sasa linajengwa baada ya kulisubiri kwa miaka mingi tangu Awamu ya Kwanza – wakati Msumbiji inapata uhuru wake!

Mbeya: Ardhi, Maji, Mifugo, Kilimo, Chakula na Ushirika; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa nchi za Malawi na Zambia. Ni kitu cha kutia shime kuona kuwa uwamja wa ndege wa kimataifa unaendelea kujengwa mjini Mbeya.

Uwanja huu utasaidia pia kuinua maendeleo kwa mikoa ya kusini. Tuwe na Mawaziri Wadogo 15 tu wakisaidiwa na nyongeza ya Makatibu Wakuu, endapo italazimika. Wizara hizi zitagawanya katika mafungu matano.Kila fungu litasimamiwa na afisa mwenye sifa za nidhamu na uchapaji kazi ili kuweza kufuatililia maazimio na miradi mbali mbali ya serikali kulingana na”manifesto” ya “chama tawala” (na kudhibitiwa na “chama tawala kivuli” kikisaidiana na vyama vingine vya siasa. Afisa huyo asaidiane na tawala za mikoa.

Wakuu wa mikoa na maafisa wao wasaidizi (hadi wilayani) wafanye kazi karibu zaidi ili kufanikisha wajibu wao kwa wananchi. Naona kumekuwepo na kuteuliwa kwa maafisa wapya wa kumsaidia Waziri Mkuu katika kusimamia mipango ya sera za serikali.Hii itasaidia sana kuangalia ni vipi tunavyotekelza yale ya Hotuba Rais aliyotoa alipokifungua Bunge la Awamu ya Nne. Na itawasaidia sana Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuweza kufuatilia, kukagua na kudhibiti miradi na maazimio yaliyowekwa.Sambamba na kupunguza wingi wa wizara, juhudi ifanywe pia kupunguza idadi ya wa-Bunge wetu!

Wa-Bunge wengine “hulala sana”! Sioni sababu kwa nini kila wilaya isiwe na na m-Bunge mmoja tu wa kuiwakilisha katika Bunge la Taifa, Dodoma! Shughuli za “wa-Bunge” wa Seriali za Mitaa wapewe hadhi na majukumu makubwa ya kusimamia maendeleo katika sehemu zao za majimbo ya uchaguzi, kulingana ana usemi wa serikali za mitaa wa nchi moja iliyoendelea: “Using local people, with local knowledge to serve the local area”.

Huku tukitilia mkazo wa sera ya “madaraka mikoani” (kama kweli bado inatekelezwa), mikoa yetu haina budi kushiriki zaidi katika kupanga na kutekeleza hayo ya “maisha bora kwa kila m-Tanzania”, ikiwa ni pamoja na kudhibiti athari za ajali barabarani. Naamini Tanzania si masikini; ni tajiri! Fikiria leo hii tunajivuna kuwa tu nchi ya tatu katika Bara la Afrika kwa uzalishaji wa dhahabu!Michanga ya dhahabu inachimbwa na kusafirishwa nchi za nje.

Makapuni ya kigeni kwa muda wa miaka mitatu ya kuvuna dhahabu yetu bila kulipa kodi. Yanaweza kuichimba usiku na mchana kabla ya miaka hiyo mitatu kuisha. Miaka mitatu iishapo, ili yaanze kulipa kodi, aidha yanaweza kulalamika kuwa yatafunga migodi kutokana na uhaba au ugumu wa kuchimba dhahabu yenyewe.Au wakati mwingine makampuni hao yanatishiwa na wakubwa wenye kutaka kuila Tanzania kwa kuyalazimisha kuwahonga ili waidhinishe mikataba hiyo na kuanza kulipa kodi. Hii inayafanya makampuni hayo kuuza “business” kwa wamiliki wengine wa kigeni au kuunda kampuni mpya yenye jina tofauti!Tatizo hili lipo pia katika mikataba ya gesi yetu.

Utajiri wa madini na gesi yetu umeingiliwa na unyarubanja unaotekelezwa na wawekezaji wa kigeni Makampuni hayo yamepewa dhahabu ya bure. Mikataba tunatiliana na hao wawekezaji wageni ikiwa na kipengere cha “production sharing agreement”, psa (kugawana uzalishaji).

Lakini inaonekana kuwa wanaonufaika na kipengere hiki ni wawekezaji, ambao kila mra huongeza vikampuni vingine vya kigeni vidogo vidogo na kunufaika. Je, huo si “unyarubanja”? Hakuna hata kikampuni cha wazawa kinachonufaika na kipengere hicho, kama ilivyo katika mikataba ya madini na gesi yetu.

Labda, Tanzania iko pembeni mwa kipengere hicho! Tangu mkataba wa kwanza kusainiwa (na pengine mpaka sasa hivi) kuna kutafuta “production sharing agreement”, psa (kugawana uzalishaji). Si ajabu mzozo wa Buzwangi umetokana na “production sharing agreement”, kama ilivyo mikataba mingi ya madini na gesi yetu!

Ukifungua http://www.globeinvestor.com/servlet/story/RTGAM.20071030.wbarrick1030/GIStory/ utapata ripoti ya mgomo unaoendelea huko kwenye Mgodi wa Barrick. Mwisho wa stori hii kuna para moja juu ya vile walivyovuna mwaka uliopita: “The mine, which Barrick acquired in 1999, produced 330,000 ounces of gold last year at a total cash cost of $339 (U.S.) an ounce. It had proven and probable reserves of 11.2 million ounces as of the end of last year.” Sijui kama wameanza kulipa kodi au kutupatia 3% (royalities) zetu? Hata kama wakitupa kiasi hicho, Tanzania itapata dola ngapi? Fanya hesabu! Mwisho, naipongeza serikali kwa juhudi zake za kuwapa msasa kidogo madereva. Lakini hii haitoshi kabisa. Naomba juhudi hii isiwe ndani ya majengo tu bali huko nje barabarani ambako ajali hutokea.

Matrafiki wafanye hiyo kwa maadili ya hali ya juu (mithili ya madaktari na wahubiri dini) ili kuokoa maisha na mali ya wa-Tanzania.Hivi karibuni tulizawadishwa na serikali ya Amerika (kupitia mfuko wa Rais wa Millennium Challenge Corporation - MCC) ya zawadi (“grant”) ya dola 698 milioni kuboresha mabarabara nishati na maji nchini kwa kipindi cha miaka mitano.

Pili, kulikuwa na habari kutoka Makao Makuu ya African Development Bank mjini Tunis kuwa Benki hiyo imetoa kiasi cha dola za ki-Marekani million 92 (72%) (serikali ya Tanzania itagharimia 28%) kwa ajili ya kutengeneza mabarabara ya mikoa ya Dodoma na Singida ili kuuunganisha mikoa na mikoa ya kasikazini hadi Kenya.

Je, ki-mapatano, mapesa hayo yatatumikaje katika kudhibiti baadhi ya mienendo mibaya yetu inayosababisha ajali barabarani?

Sakata la Wafanyakazi Bongo

Nilishasema. Serikali kuongeza mishahara kwa kiwango walichoongeza kitakosesha watu kazi. Na kweli hivi majuzi tulisikia makampuni kama Urafiki waliachisha wafanyakazi kwa wingi.

Nakumbuka ma baa medi walisherkea kusikia kuwa watalipwa shs.80,000/-. Lakini wangapi watabaki na kazi? Pia mahausigeli wanatakiwa walipwa 65,000/- kwa mwezi. Je mwajiri wake analipwa shs. ngapi?

Mishahara mipya ilikuwa ianze kulipwa leo lakini serikali wamesogeza hadi januari mwakani. Ila mshahara wa mahaugeli unaanza leo.

*******************************************************************************

From ippmedia.com

Waliofukuzwa kazi warejeshwe - Serikali

2007-11-01

Na Beatrice Bandawe, Dodoma

Serikali imewaagiza waajiri wote waliowafukuza kazi wafanyakazi wao kwa madai ya tangazo la mishahara mipya kuwarudisha kazini mara moja. Tamko la serikali lilitolewa na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Bw. John Chiligati, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini hapa.

Sambamba na hilo, serikali imetangaza kuwa viwango vipya vya mishahara vya sekta binafsi vitaanza kulipwa Januari Mosi, mwakani badala ya leo kama ilivyotangazwa awali na serikali. Waziri alisema kusogezwa mbele kwa muda wa kulipa mishahara hiyo kumetokana na maombi ya waajiri wa sekta yaliyowasilishwa serikalini wakiomba muda wa kujitayarisha kwanza.

Akizungumzia kusimamishwa ama kupunguzwa wafanyakazi alisema serikali imewaagiza waajiri hao kujipanga na bajeti yao mpya ili wawalipe wafanyakazi wao mishahara mipya ifikapo Januari mosi mwakani. Alisema mwajiri atakayeshindwa kumlipa mfanyakazi katika muda uliopangwa atachukuliwa hatua.

Aliwaonya baadhi ya waajiri wanaotaka kugeuza zoezi hilo kuwa la balaa badala ya neema. Aidha, Bw. Chiligati alisema kwa waajiri wa viwandani ambao walilalamika kuwa kupanda kwa mishahara hiyo kutaathiri mapato yao na kusababisha kupanda kwa bei za bidhaa, amewaagiza wakae na bodi zao kutoa mapendekezo na kuyawasilisha serikalini ili kuangalia athari zitakazojitokeza.

Waziri aliwaomba wafanyakazi kuwa wavumilivu wakati waajiri wanaandaa mishahara yao. Aidha, alisema kuanzia sasa waajiri wa sekta binafsi watatakiwa kuwaongeza wafanyakazi mishahara kila mwaka kama ilivyo kwa watumishi wa umma. Kutangazwa kwa viwango hivyo kunafuatia sekta binafsi kukaa muda mrefu bila kuwaongezea wafanyakazi mishahara yao.

Alisema wafanyakazi katika sekta hiyo tangu mwaka 2002 hawajaongezewa mishahara na kubaki na kima kile kile kwa kipindi cha miaka mitano. Bw. Chiligati alisema Oktoba mwaka huu serikali ilitangaza viwango vipya vya mishahara ya kima cha chini kwa sekta binafsi ambapo mishahara wa chini kabisa ni Sh. 65,000 kwa wafanyakazi wa ndani kilichotakiwa kutekelezwa kuanzia leo.

Hata hivyo, aliongeza kuwa baada ya kutangaza hatua hiyo, iliwastua waajiri wengi kwa kuwa hawakuwa wamejiandaa na wengine walianza kupunguza watumishi wao. Waziri alisema sekta ya viwanda, hasa ya nguo, ndiyo iliyopunguza wafanyakazi wengi na kuongeza kuwa waajiri wa sekta hiyo walipeleka malalamiko wizarani, wakisema tangazo hilo limekuja ghafla sana na kuomba wapewe muda wajitayarishe kwanza.

Alizungumzia wafanyakazi wa sekta ya kilimo, alisema kuna wale walio katika mashamba makubwa kama ya miwa, maua na tumbaku ambao walisema viwango vyao vya mishahara ya kima cha chini vimekuwa sawa na wale wanaofanya kazi kwenye mashamba madogo bila kuangalia uwezo. Alifafanua kuwa Bodi pia itakaa na sekta hiyo ili kuangalia mapendekezo yao. Bw. Chiligati alisema wafanyakazi wanaozalisha zaidi wana haki ya kulipwa vizuri ili waongeze tija kazini. Akitoa ufafanunuzi kuhusu mishahara ya wafanyakazi wa ndani, Bw. Chiligati, alisema kumekuwa na upotoshaji mkubwa kuhusu mishahara hiyo.

Alifafanua kuwa wafanyakazi wa ndani wanaofanya kwa mabalozi, mishahara yao ni Sh. 90,000, wakati wale wanaofanya kwa watumishi wa serikali wanatakiwa kulipwa Sh. 80,000 na wale walioko kwa watu wa kawaida watalipwa Sh. 65,000 lakini kama hawakai nyumbani kwa mwajiri. Alisema kwa wanaoishi nyumbani kwa mwajiri kati ya hizo Sh. 65,000, watakatwa asilimia 68 ya mshahara wake.

Kuhusu wafanyakazi hao kulipiwa michango ya Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na waajiri wao, Bw. Chiligati alisema serikali itakaa na Chama cha Wafanyakazi Mahotelini na Majumbani (CHODAWU), kujadili hilo.

Aidha, alisema sheria mpya ya kazi inakataza ajira za kienyeji na kuwataka waajiri kuhakikisha kunakuwepo na mikataba. Alitaja aina za mikataba hiyo kuwa ni ile ya muda, ya kudumu na ya kulipana kila siku.
SOURCE: Nipashe

Wednesday, October 31, 2007

Mjue Msanii wa Vichekesho Bongo Kingwendu

Tanzanian Comedian Kingwendu Kingwendulile




Kabla ya Ze Comedy kulikuwa na Kingwendu aka. Kingwendu Kingwendulile (pichani). Yeye ni mchekshaji wa siku nyingi huko Tanzania. Anavyoongea inachekesha pia. Fani la uchekeshaji kinshamiri huko Bongo siku hizi. Watu wanauliza mbona hawamwoni Kingwendu zaidi?

Nimekuta clipu kadha kwenye youtube. Yeye Kingwendu ndiye star!

YOU TUBE CLIP 1

YOU TUBE CLIP 2

YOU TUBE CLIP 3

Kazi nzuri! Na kucheka nimecheka hasa!


Huyo Polisi Vipi?




Wema wa Denzel Washington





Hivi karibuni, mcheza sinema maarufu wa hapa Marekani, Denzel Washington na familya yake walitembelea Brook Army Medical Center, mjini San Antonio, Texas (BAMC). Hiyo hospitali ni ya jeshi na inahudumia hasa wagonjwa walioungua moto. Wengi wameumia katika vita vya Iraq na wamesafirishwa kutoka Ujerumani.

Kuna nyumba kadhaa za familia za wagonjwa kukaa wakiwa wamefika kuangalia wagonjwa wao.

Mara nyingi zinakuwa zimejaa. Familia wanakaa pale kwa gharama ndogo au bila malipo kutokana na uwezo wao. Ni bei rahisi kuliko kufikia hospitalini.

Denzel aliliuliza bei ya kujenga nyumba moja ni bei gani. Aliambiwa. Alishangaza wanajeshi alipotoa andika hundi enye pesa za kutosha za kujenga nyumba moja.

Sasa watu wanashangaa. Kwa nini akina Britney Spears, Madonna, Robert Downey Jr. , Tom Curise, wakifanya vituko wanatolewa ukurasa wa kwanza wa magezeti. Denzel akitenda wema wako kimya!

Wanaume wanavyotusema sisi Wanawake!


Nimepata hii kwa e-mail:


CHAGGA WOMEN

First Date: You get to buy her Amarula (or Redds), mbuzi choma and dance the whole night. You have to buy her credit, to organize for the second date.

Second Date: You get to buy her and her girlfriends Amarula (or Redds), mbuzi choma and dance to the whole night. You exchange your expensive phone with her nokia. Third Date: You get to pay her rent. Tenth Date: She tells you she is engaged and you are a kyasaka

ZIGUA/ DIGO WOMEN

First date: She wants your home address

Second date: She comes home for the date with her brother (who is looking for a job)

Third date: She ends at the door, her mother is waiting

Fourth date: You have sex and she tells you she is pregnant and want you to take her and her baby

WAHAYA WOMEN

First Date: You both get blind drunk as you dance to Saida Karoli and later have sex.

Second Date: You both get blind drunk as you dance to Saida Karoli and later have sex.

20th Anniversary: You both get blind drunk as you dance to Saida Karoli and later have sex.


SUKUMA WOMEN

First Date: You take her to a movie and an expensive restaurant.

Second Date: You meet her parents and her Mom makes ugali and chicken.

Third Date: You have sex, she wants to marry you and insists on a 3-carat ring.

4th Anniversary: You already have 3 kids together and hate the thought of having sex.

5th Anniversary: You find yourself a girlfriend.


HEHE WOMEN

First Date: You buy her an expensive dinner, get drunk on Guinness, and have sex in the back of your car.

Second Date: She's pregnant.

Third Date: She moves in. One week later, her two sisters, her brother, all of their kids, her two cousins, her sister's boyfriend and his three kids move in ... and you get to eat rice and beans for the rest of your life in your home that used to be nice before you met her .


ZARAMO WOMEN

First date: You get to buy her dinner, but you realize nothing is going to happen.

Second date: You wait for her in the same restaurant but she gets lost on the way.

Third date: She does not even remember to pick your calls.


NYAKYUSA WOMEN

First date: After a date of drinking several bottles of Fanta, you get to kiss her goodnight.

Second date: You get to grope all over and make out.

Third date: You get to have sex, but only in the missionary position.


ZANZIBARI WOMEN

First Date: You get dynamite head.

Second Date: You get more great head.

Third Date: You tell her you'll marry her and never get head again.


MAASAI WOMEN

First date: You get to buy her an expensive dinner, but nothing happens.

Second date: You buy her an even more expensive dinner. Nothing happens again.

Third date: You don't even get to the third date and you already realized nothing is going to happen.


MAKONDE WOMEN

First date: Meet her parents.

Second date: Set the date of the wedding.

Third date: Wedding night and you get to ask her, her name


PARE WOMEN

First date: She wants sex, no food or drink

Second date: She wants more sex

Third date: She only wants chuma mboga

Tuesday, October 30, 2007

Wazungu wakamatwa Chad wakijaribu kutorosha watoto 100!




Kuna kundi la wazungu wamekamatwa nchini Chad wakijaribu kutorosha watoto zaidi ya mia moja. WaChad wanadai kuwa hao watoto ni raia wa Chad. Hao wazungu wanasema ni yatima kutoka Sudan na walikuwa wanapelekwa Ufaransa kukaa na familia kadhaa kule.

Kuna kundi la ufaransa inaitwa Zoe's Ark, ndo ilikuwa imeleta ndege ya kusafirisha hao watoto.

Sasa hao wazungu wanaweza kufungwa kwenye gereza la Chad kwa miaka 20 na kufanyishwa kazi ngumu. Pia wameshika raia wawili wa Chad.

Baadhi ya hao watoto walidai kuwa walitekwa na hao wazungu. Walipewa pipi na biskuti na walijikuta wanatoroshwa.

Inasemekana familia kadhaa huko Ufaransa walilipa kati ya Euro 2,800 hadi 6,000 kumpata mtoto yatima kutoka Sudan.

Kwa habari zaidi someni:




Video

Oprah aomba msamaha!


Mnajua ile shule ya fahari ya wasichana ya Oprah huko Afrika Kusini? Kumbe baadhi ya wasichana wamebakwa na kufanyiwa vibaya na mfanyakazi wa kike huko!

Oprah amekuwa msiri na 'details' za matukio. Huyo mama aliyetenda mabaya amefukuzwa kazi na anachunguzwa na polisi wa Afrika Kusini.

Navyosikia sheria za hiyo shule ni kali sitashangaa nikisikikia kuwa wasichana wa shule hiyo wameshikwa na ugonjwa wa 'HYSTERIA'.


***********************************************************************************

Sexual abuse claims at Oprah's school

October 30, 2007

US talkshow queen Oprah Winfrey has tearfully begged for forgiveness after a staff member at a girls' school she funds in South Africa was accused of sexual abuse.

Winfrey rushed to the Leadership Academy for Girls, near Johannesburg, after the abuse claims surfaced.

She met with parents and assured them she would do everything possible to ensure prosecution, The Independent newspaper reported.

"I've disappointed you. I'm so sorry. I'm so sorry," Winfrey told the parents who attended a meeting in a packed marquee.

One of the matrons who oversees the dormitories has been accused of abuse.
Reports said the staffer grabbed one girl by the throat and threw her against a wall. The woman, who has not been named, has also been accused of sexually fondling at least one pupil.
The claims came after a student fled the school saying the situation had become unbearable. Winfrey has sent the accused woman on leave, along with the school's principal, identified only as Dr Mzimane, and one other staffer, the Independent said.

The alleged victims have accused Dr Mzimane of failing to act after students complained of abuse.

Police and special US investigators have been called in.

Winfrey, reportedly in tears, told the meeting: "I trusted her (Dr Mzimane). When I appointed her, I thought she was passionate about the children of Africa. But I've been disappointed."
One father responded by telling Winfrey it was not her fault.

Winfrey spent millions to build the school after former South African president Nelson Mandela asked her to become involved in education programs.

Kwa habari zaidi someni:



Mjue Msanii Mkongwe wa Bongo - Mzee Kipara


Msanii wa siku nyingi Tanzania, Fundi Saidi aka. Mzee Kipara yumo kwenye sinema ya Bongoland II.
Kwa habari zake zaidi Bofya Hapa!