Thursday, November 08, 2007

Marudio - Kukosa Nguvu za Kiume si Mwisho wa Dunia!

Kutoka 1/21/06.


Jamani, jamani, jamani, kuna jirani yangu kafa hivi majuzi. Alikuwa ni baba wa makamu, mmarekani mweusi. Alikuwa mcheshi na ilikuwa kila tukionana lazima tusalimiane. Mara ananinunulia kahawa halafu tunakaa namsimulia kuhusu Afrika. Yule baba, alionekana mzima na mwenye afya fiti kabisa. Nilibakia kushangaa kusikia kafa na si kwa ajali. Mke wake alifariki mwaka juzi, lakini miezi ya karibuni alikuwa anaonekana mwenye furaha kwa vile alipata mpenzi, dada mwenye miaka 25 hivi.

Story niliyoskia ni hivi: Kumbe jamaa alikuwa na matatizo ya moyo. Alifia kitandani akiwa kwenye shughuli ya kufanya tendo la ndoa na mpenzi wake. Tena wanasema alifariki mara alipofikia kilele cha tendo. Navyosikia ilikuwa ni ‘massive heart attack’. Kama ni massive bila shaka na utamu wa shughuli hakujua kuwa yuko hatarini.

Nasikia huyo mpenzi wake alipiga sana makelele majirani walipigia simu polisi 911 kwa vile walidhania wameingiliwa na majambazi. Wanasema baba wa watu kamwangukia yule dada na kafa macho wazi.Lakini bado nilikuwa nashangaa maana kama nilivyosema awali, jamaa alionekana kuwa na afya. Kumbe jamaa alikuwa mtumizi wa Viagra, yaani vile vidonge vya kuongeza uume, na kumpa mwanaume uweza wa kufanya tendo la ndoa.

Ndugu zake wanalamika kweli, maana hakuzipata kwa prescription ya daktari, alizaiagiza kwenye mtandao (internet). Kwa kumwangalia alivyofiti nisingefikiria kuwa ana matatizo ya nguvu za kiume. Kumbe mtazame mtu, matatizo yake anayajua mwenyewe na daktari wake.Nikawa najiuliza kama jamaa alijua ana matatizo ya moyo, kwa nini alitumia Viagra. Maana hata tangaza kwenye TV na magazeti wanaonyo kuwa kabla ya kutumia. Halafu pia wanaonya kuwa mwanaume anaweza kupofuka kama anatumia. Lakini wanaume bado wanazitumia!

Na siku hizi dawa za kuongeza nguvu za kiume ziko nyingi kuna Ciallis, Levitra, Yohimbine na mengine. Hizo dawa zina side effects kama kuumwa kichwa, kuharisha, pua kuziba, macho mekundu, tumbo kuumwa na mengine mengi. Pamoja na side effects bado zina soko kubwa. Na zikipigwa marufuku nina amini kuwa watu watatajirika kwa kuzifanyia magendo.

Kwa kweli wanaume wako tayari kufa kama wakishindwa kufanya tendo la ndoa. Nashindwa kuelewa sababu. Yaani tendo la ndoa ni tamu kiasi hicho au wanahofia kuwa kwa vile hawa ‘function’ tena ndo basi si wanaume? Mtu anakuwa tayari kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kufanya tendo la ndoa.

Mwanaume anaambiwa anaweza kupofuka akitumia hiyo dawa lakini bado yuko tayari kuchukua risk. Halafu mwanaume akiitwa ‘hanithi’ yuko tayari kupigana au kuua. Sijui bila kusimamisha anajiona si mtu tena…sielewi kabisa! Nikawa najadiili na marafiki zangu juzi na tulikubaliana kuwa wanaume wako tayari kuchukua ‘risks’ kuliko wanawake.

Yaani mwanaume anaweza kufanya tendo la ndoa hata akijua kuwa kuna hatari ya mwenzake kuwa na ugonjwa wa zinaa na ataambukizwa. Bongo, walikuwa wanasema eti, ‘Ajali Kazini’! Hiyo ajali inaweza kukuua! Sijui hiyo ume ikisimama ndo basi tena, akili zote zinahamia hapo. Nauliza tena, tendo la ndoa ni tamu kiasi kwamba mko tayari kuhatarisha maisha yenu? Kukosa nguvu za kiume zi mwisho wa dunia jamani. Bado tunawahitaji!Lakini nikirudi kwa marehemu jirani yangu, uwongo mbaya, alikuwa anatabasamu ndani ya jeneza lake!

Noti - Nyie wanaume mnaotaka kutumia hizo dawa kawaone daktari wenu kabla ya kuanza kuzitumia.

8 comments:

Anonymous said...

Da Chemi samahani hii haihusiani na picha husika. Ila nimekurushia nakala ya tarifa hii iliyotoka vyanzo vinavyoaminika ili kila mmbongo aione na kuijadili. Naamini wewe kama mwandishi mkomavu hutasita kuiweka wazi.
Shukrani ziwaendee waliotuwezesha kuyajua haya.Waajiriwa Wa Bot

Ndugu wana tz kuna kaemail kalikua forwarded kwangu ,nilipokasoma nilipatwa na mshtuko lakini inshallah nguvu zangu zimenirudia leo na nachukua fursa hii kukawakilisha kwenu (in my own version) but i hope it will still be enjoyable to read........ enjoy!
Hii ni habari halisi na ya uhakika kutoka ndani ya BOT. Je unawajua walioajiriwa kusimamia uchumi wa nchi yetu na kutuletea mafanikio? Pokea taarifa ya wateule hawa.
Nakutajia kwanza wachache ili wewe na watanzania wenzetu watafakari kama kweli ndege yetu itaweza kupaa kama bwana Lowasa alivyosema, au tutabaki ombaomba kama Balali anavyodai!!!. Ama tunageuzwa kuwa wadanganyika!!!
Ndani ya Mtungi wa BOT walioqualify kuajiriwa kwa sifa na vigezo vinavyotambulika na BOT ni pamoja na hawa wafuatao:-

Pamella Lowassa, Filbert Frederick Sumaye, Zalia Kawawa, Harieth Lumbanga,Salama Ally Mwinyi, Rachael Muganda, Sylvia Omari Mahita, Justina James Mungai, Kenneth John Nchimbi, Blassia Blassius William Mkapa, Violeth Phillemon Luhanjo,Liku Irene Katte Kamba, Thomas Mongella,Allen Shibuda,Jabir Abdallah Kigoda,Fred Nicolas Mwanri. Hii ndio success team, hapa nani atamuwajibisha Dalali alas Balali?
Je KAPUKU MWENDE(a.k.a KAYUMBA) ATAAJIRIWA KWELI HAPO?

Hawa ni wale wenye uhusiano wa moja kwa moja na wazito wa nchi, wapo wengine ambao ni ndugu wa karibu au kabila moja na waheshimiwa. Ni vigumu kuamini kuwa hii ni bahati mbaya(mere coincidence).
Wana JF, ni juu ya watanzania kuamua kuendelea na viongozi wabovu na wenye ubinafsi au kuwaambia ukweli hata kama utawauma na kwa vile wao ndio miungu basi watatoa adhabu za kukufukuza katika bustani ya Eden.
Rhuksa kupayuka utakavyoona inafaa, na kama kuna cha kuongeza na kiko ndani ya uwezo wangu, nitakuongezea.

Anonymous said...

Ina maana hawa ndio walioajiriwa katika BENKI KUU YA TANZANIA? loh! Haya tutafika tu. Kuna usemi usemao... "Bubu husema, mambo yanapomzidia!" Naamini ipo siku "wadanganyika" nao watasema "BASI, LIWALO NA LIWE, TUMECHOKA". Huu mkutano wa juzi huko Dodoma ulikuwa ni wa kuwarudisha wale-wale ambao tulianza kuwasikia tangu tulipopata akili, na sasa tuna-wajukuu. Bado watu, sura ni zile-zile. Kustataafu ni maka mtu achukuliwe na Mwenyezi Mungu....kaaazi kweli kweli!

Anonymous said...

LOL! Viagra can kill you man! Let it be limp and live!

Anonymous said...

Du hii ishu ya viagra nzito. Unjaua sometimes wananume tunaogopa kuzungumza kwa uwazi kuhusu matatizo yetu ya nguvu za kiume. ninavyofahamu kuna maaktari ambao wa specialise kabisa kwenye erectile dysfunction if that is the problem so I do not see why people do not make an effort to seek help. Ila inavyoonekana ni kwamaba hata kama jamaa hana erectile dysfunction bado anatumia viagra ku enhance performance, ili awe ana perform kama porn star! Kuna natural foods kibao amabazo zinaweza zikaprovide stamina kwenye game, I think they are more safe than these funny drugs. But the best thing to do whenever taking any kind of medication is to seek medical advice. Sex is great but life is precious!

Anonymous said...

sigara huleta kansa nani hajui, lakini mbona hata madaktari huvuta?
NGONO ni muhimu acheni siasa Chemi! Mtu anatambulika jinsia yake kwa UUME au UKE wake; mwanaume Ni UUME wake kwa hiyo libeneke ni MUHIMU mno kuliko unavyofikiria.
Mume wako asingekuwa anafanya uneishi nae? Hao watoto hao walioko college ungetoa wapi au ungeanza UASHERATI??

Anonymous said...

Ni vyakula gani vinasaidia kuongeza nguvu na hamu ya kufanya ngono?
Naomba msaada jamani....

Anonymous said...

Mi naungana na Anonymous wa hapo juu kuhusu natural products ambazo hazina side effects na inasaidia kuongeza nguvu za kiume kwa wasio nazo kabisa na wale wa kigoli kimoja tu hoi.Kuna hizi products za Forever Living ambazo zinatengenezwa na Aloe Vera wengi wanazisifia kwa kuboresha hali kama hizo hasa hii ya forever multi maca(chungulia huku www dot flptz dot com)kwa hizo products.Mambo ya viagra na wenzake noma wabongo,thanks to dada kemi kwa info za huyo babu kwani itawashtusha wengi wabongo ambao kupima afya tu ni shida je tutajuaje tuna haya magonjwa ya moyo..

Anonymous said...

kukosa nguvu za kiume ni kama wewe Chemi uende kwa daktari akwambie uuke wako umeziba. Utakavyojisikia, ndo sisi wanaume tunavyojisikia tukikosa nguvu za kiume.