Wednesday, October 31, 2007

Wema wa Denzel Washington





Hivi karibuni, mcheza sinema maarufu wa hapa Marekani, Denzel Washington na familya yake walitembelea Brook Army Medical Center, mjini San Antonio, Texas (BAMC). Hiyo hospitali ni ya jeshi na inahudumia hasa wagonjwa walioungua moto. Wengi wameumia katika vita vya Iraq na wamesafirishwa kutoka Ujerumani.

Kuna nyumba kadhaa za familia za wagonjwa kukaa wakiwa wamefika kuangalia wagonjwa wao.

Mara nyingi zinakuwa zimejaa. Familia wanakaa pale kwa gharama ndogo au bila malipo kutokana na uwezo wao. Ni bei rahisi kuliko kufikia hospitalini.

Denzel aliliuliza bei ya kujenga nyumba moja ni bei gani. Aliambiwa. Alishangaza wanajeshi alipotoa andika hundi enye pesa za kutosha za kujenga nyumba moja.

Sasa watu wanashangaa. Kwa nini akina Britney Spears, Madonna, Robert Downey Jr. , Tom Curise, wakifanya vituko wanatolewa ukurasa wa kwanza wa magezeti. Denzel akitenda wema wako kimya!

5 comments:

Anonymous said...

kwa sababu, watu (hasa wamarekani) wanapenda mikasa (scandal)

Anonymous said...

It's a shame vitu vya kipuuzi ndio vinakuwa glorified. Lakini ndio hivyo, that's what sells. Go Denzel!!!!

Anonymous said...

Dada chemi habari hii ilitokea kama miaka miwili iliyopita lakini hata hivyo baadaye walikuja kugundua kuwa sio kweli...

Chemi Che-Mponda said...

Na mimi nimecheki. Ni kweli alipatembelea, lakini alikuja kutoa mchango mkubwa miezi minne baada ya kufika hospitalini. Wanasema kuwa hela ilikuwa nyingi lakini hazikutosha kujenga nyumba nzima ambayo ilikuwa zaidi ya dola milioni moja. Hivyo ni kweli alitoa mchango lakini siyo papo hapo.

Yet another 'Urban Myth'.


http://www.snopes.com/politics/military/denzel.asp

Anonymous said...

the great