Tuesday, October 30, 2007

Wazungu wakamatwa Chad wakijaribu kutorosha watoto 100!




Kuna kundi la wazungu wamekamatwa nchini Chad wakijaribu kutorosha watoto zaidi ya mia moja. WaChad wanadai kuwa hao watoto ni raia wa Chad. Hao wazungu wanasema ni yatima kutoka Sudan na walikuwa wanapelekwa Ufaransa kukaa na familia kadhaa kule.

Kuna kundi la ufaransa inaitwa Zoe's Ark, ndo ilikuwa imeleta ndege ya kusafirisha hao watoto.

Sasa hao wazungu wanaweza kufungwa kwenye gereza la Chad kwa miaka 20 na kufanyishwa kazi ngumu. Pia wameshika raia wawili wa Chad.

Baadhi ya hao watoto walidai kuwa walitekwa na hao wazungu. Walipewa pipi na biskuti na walijikuta wanatoroshwa.

Inasemekana familia kadhaa huko Ufaransa walilipa kati ya Euro 2,800 hadi 6,000 kumpata mtoto yatima kutoka Sudan.

Kwa habari zaidi someni:




Video

2 comments:

Anonymous said...

Kama kweli ni yatima basi waende France kupata maisha mazuri. Kama kweli walikamatwa kama wanyama kwa bait ya biskuti na pipi basi hao wazungu wachukuliwe hatu kali. Hao marubani waachiwe huru maana hawana makosa.

Anonymous said...

JAMANI DA CHEMI! HII NI HATARI SANA NI VIZURI U-WAPE HIZI HABARI WATU WA TAMWA AU VYOMBO VINGINE VYA HABARI USIKUTE HATA HAPA NYUMBANI TANZANIA HIZI NDEGE ZIPO NA ZINAONDOKA NA WANETU ATA!! KWANI ILE KASHFA YA SANGARA MWANZA TULIJUA SI HADI FILAMU ILETE MZOZO