Thursday, November 08, 2007

Msanii Ernest Mtaya anaoa kwa staili aina yake!





Ninamfahamu msanii na mchoraji, Ernest Mtaya tangu ni kijana mdogo. Alikuwa anatusaidia TAMWA katika mambo ya uchoraji katika magazeti na vitabu yetu. Sasa ni mwalimu maarufu wa uchoraji. Amewahi kupata zawadi ya uchoraji kutoka Mfuko wa Utamaduni Tanzania.

Pia alishiriki katika sinema ya Maangamizi the Ancient One. Picha zake nyingi zilitumika kwenye hiyo sinema, iliyowakilisha Tanzania katika mashindano ya Oscars Hollywood mwaka 2001.

Ernest na Juddy HONGERA! Nawatakieni maisha mema ya ndoa.

Dada Chemi

***********************************************************************************
Ndugu zangu na marafiki zangu,Natumaini wote ni wazima na kama wapo ambao wanaugua au wanauguliwa naombaMUNGU awasaidie katika matatizo hayo. Mie ni Ernest Mtaya (pichani) na maelezo yangu zaidi yanapatikana katika http://www.ernest.4mg.com/

Madhumuni ya barua hii ni kuwafahamisha natarajia kuoa tarehe 17 Novemba 2007 saa 10 kamili katika kanisa linalojulikana kama st.Peter's church liliopo Oysterbay karibu na shule ya Mbuyuni hapa Dar Es Salaam. Baada ya hapo kutakuwa na msafara wa BAJAJI sita kuelekea eneo la sherehe ambalo ni kijiji cha Makumbusho tena nje chini mwembe.

Sherehe hii itakuwa na vionjo vya kitamaduni zaidi ya "uzungu" katika msafara wa Bajaji tutakapofika eneo la Victoria tutabadilisha usafiri na kupanda GUTA lililotengenezwa kiustadi kabisa na kuitambua Bajaji nitakayokuwa na mtarajiwa wangu itakuwa imepambwakwa makuti.
Sherehe itashereheshwa na msanii maarufu wa jukwqaa Mrisho Mpoto kwa wasiomfahamu ni yule muimbaji wa wimbo wa SALAMU KWA MJOMBA pia kutakuwa na msanii maalufu wa Afro Reggae Jhiko Manyika ambaye amerudi juzi tu kutoka ziara yake ya kimuziki ya Ulaya.
Mtumbuizaji mwingine ambaye atakuwa msimamizi wa mtarajiwa wangu ni muimbaji na mtunzi maarufu anayeitwa Karola Kinasha ambaye mbali na shughuli ya usimamizi kama Matron pia atatumbuiza kwa nyimbo zake tamu na sauti nzuri. keki , shampeni na jukwaa utamaduni wetu wa Afrika utapewa hadhi.

Cha muhimu ndugu na marafiki ni hii sherehe ya watoto ambayo nimefikiri niifanye ili watoto kwa mara ya kwanza washiriki katika sherehe ya Arusi la kwa nia ya kuwaaunganisha na kusaidiana na kutambua matatizo ya watoto wengine wenye shida zaidi yao.

Hivyo basi siku ya pili ya sherehe yaani 18 Novemba 2007 kwa niaba ya mchumba wangu JUDDY nimeandaa sherehe ya watoto ambapo nimeawaarika watoto wa mataifa mbalimbali nia kubwa ikiwa ni kuwaaunganisha watoto wote bila kujali misingi ya rangi, dini na utabaka waaina yoyote, pia kuwafanya watambue matatizo ya watoto wengine ili wakue wakijua kuna watoto wenzao wenye shida zaidi yao na wawe na moyo wakuwasaidia kupitia wazazi wao, pia kuwafanya wafurahi kwa kucheza ,kuimba na chochote chema ili mradi wafurahi.

Hapa tutafanya utafiti wa kugundua vipaji vya watoto na kuwasiliana na wazazi ili kuona mwelekeo wa kuweza kuwasaidiakatika siku za mbele ambapo Mungu akinijalia nategemea kuanzisha taasisi itakayohusika na shughuli za watoto.

Nimewaalika watoto yatima wa Kurasini ili waweze kufurahi na wenzao na kama kuna yoyote atayeweza kusaidia kwa chochote kile hasa kwa walengwa wakuu ambao ni hawa watoto yatima anakaribishwa kusaidia anaweza kupiga simu hii 0713-23 31 74 .

Michango itapokelewa hata baada ya sherehe kwani baad ya sherehe mimi na Juddy tutaelekea Zanzibar kwa mapumziko ingawa tutatumia mapumziko yetu kutembelea vituo vya watoto wenye shida na nyumba za kutunzia wazee.

Tayari kwa niaba ya Juddy nawashukuru Duka la vifaa vya elimu lilopo Upanga la KALL KWIK Bookshop kwa zawadi zao ambazo zitatolewa kwa watoto wote wataohudhuria sherehe hii.
Pia wale walioahidi kusaidia nitawaandika mara nitakapopokea zawadi zao. nawashukuru pia wazazi ambao tayari wamechangia sherehe hii na napenda kuwaahidi michango yao itasaidia kuwaalika watoto yatima na itatumika kwa madhumuni yaliyotajwa kwenye kadi tu.
Nashukuru kwa kuniamini na naahidi sitawaangusha tufanye huu ni mwanzo tu.

Ahsante na MUNGU awabariki wote na kuwajalia imani na huruma.

Ernest kwa niaba ya Juddy

2 comments:

Anonymous said...

Hongera Ernest na Juddy!

Anonymous said...

kaka ernest hongera sana mon! hakika nimefurahi sana leo hii kuona habari zako ktk mitandao ya watanzania
ee bwana nimekukumbuka sana wakati ule mimi ,wewe ,ndunguru,walter lema ,robert mwampembwa,ntilo,dada poni,na wengine wengi wakati wetu wa shughuli za uchoraji pale dsm
mungu awabariki sana kwenye ufungaji wa piongu za maisha
just so you know my love for burning spear,mutabaruka is still the same agwan lisen fe dem mon!
tafadhali tuwasiliane .
hivi sasa naendelea na uchoraji lakini ni ktk mambo ya kuchora kwa mwanga yaani mambo ya film making na cartoon animations
nayakumbuka sana yale mashindano ya uchoraji pale don boscomiaka ya 89 hivi wakati ule mimi nasoma forodhani sec,vipi ile taasisi yako ya uchoraji kwa watoto inaendeleaje? you can contact me through mhandom@yahoo.com
Gibbons Mlowe
RACEZNOBAR
edmonton,canada