Kuna Mdau ameniletea hii Kitendawili:
kuna msafiri alikuwa anasafiri kwa farasi enzi hizo na akafika katika kitongoji cha mbali na kuomba hifadhi ya kulala. watu wawili wakajitokeza kumfanyia ikramu. pamoja na malazi, mmoja akatoa mikate mitatu na mwengine mikate mitano jumla ilikuwa mikate minane.
kila mkate ukakatwa vipande vitatu na kufanya vipande ishirini na nne kwa mikate minane. watu wale wawili na mgeni wao mmoja ambao jumla ni watu watatu wakala mikate ile sawa kwa sawa ambapo kila mmoja alikula vipande vinane vya mikate.
siku ya pili kulipopambazuka, mgeni aliwashukuru watu wale waliomkirimu na kuwapa riyali ( fedha za mji huo enzi hizo) nane kwa wema waliomfanyia na kuchukuwa farasi wake na kuaga.
kimbembe kiliibuka baina ya wale watu wawili waliopewa zile pesa.
yule aliyetoa mikate mitano alitaka kuchukuwa riyali tano na kumpa mwenziwe aliyetoa mikate mitatu riyali tatu. kwa upande mwengine yule aliyetowa mikate mitatu aliona ameonewa na akataka kugawana kila mtu riyali nne sawa kwa sawa. upande wa pili nao haukukubali rai hiyo.
swali langu lipo hapa jee ni upi uamuzi sahihi na halali, kugawana sawa kwa sawa au aliyetowa mikate mitano achukuwe riyali tano na aliyetowa mikate mitatu achukuwe riyali tatu au wote wawili hawapo sahihi?
na kama hawapo sahihi usahihi ni kuzigawa vipi hizo riyali nane walizopewa na mgeni ambae ameshaondoka?
naomba jibu wadau. nitatoa jawabu sahihi baada ya wadau kutoa jawabu zao.
Tuesday, April 15, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
7 comments:
ize..Ni 4-4..haikuwa bizinesi ilikuwa Hospitaliti...Ukiingiza proportionaliti unaleta bizinesi.
WOTE WAWILI WAMEKOSEA.
JIBU NI KWAMBA:-
ALIYETOA MIKATE 5 APEWE RIYALI 7;
ALIYETOA MIKATE 3 APEWE RIYALI 1
KWASABABU MIKATE 5 ILITOA VIPANDE 15 (5X3) HALAFU AKALA VIPANDE 8 NA KUBAKISHA VIPANDE 7 ALIVYOKULA YULE MGENI.
VILEVILE MIKATE 3 ILITOA VIPANDE 9 (3X3) HALAFU AKALA VIPANDE 8 NA KUBAKISHA VIPANDE 1 ALICHOKULA YULE MGENI.
Dada Chemi mimi nilikwenda shule na sikuogopa umande. Jibu lako ni kwamba huyo jamaa alietoa mikate mitano anatakiwa kupata riyali 7 na huyo alietoa mikate mitatu anapata riyali 1. Hii ni kwasababu mikate mingine walikula wenyewe. Vipande alivyokula huyo mgeni vilikua vinane tu.
Subira
Wagawane nusu kwa nusu hizo riyali, kwa vile wote waliamua kumkarimu mgeni; na ukarimu hauna kipimo wala bei.
Mie naona hizo riali 8 wamuongezee Balaljai au Chenge kwenye account yake! Yanini kugombania hela wakati walifanya ukarimu?!
WAGAWANE SAWA KWA SAWA KWA KUWA WALIKULA WOTE VIPANDE NANE KILA MMOJA REGARDLESS YA NANI KATOA VIPANDE VINGAPI VYA MKATE.
ule ulikuwa ukarimu wangekuwa na busara wasingepokea hizo riyali 8 kwani nao wameshiriki katika kula wangemuacha aondoke nazo huenda zingemsaidia mbele ya safari
Post a Comment