Sunday, April 27, 2008

Kwame Nkrumah wa Ghana

Kwame Nkrumah na mke wake na machifu huko Ghana siku ya Januari 20, 1963


Ule ukumbi mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, unitwa Nkrumah Hall. Ilipewa jina hiyo kwa heshima ya rais wa Kwanza wa Ghana, Kwame Nkrumah.

Ghana ilikuwa nchi ya kwanza ya weusi kupata Uhuru barani Afrika. Ilipata Uhuru mwaka 1957 kutoka Uingereza. Mwaka 1960, Nkrumah alitangaza kuwa Ghana ni Jamhuri. Mwaka 1964, alisema yeye ni rais wa maisha ya nchi hiyo. Alikataza vyama vyote vya siasa isipokuwa chama chake.

Mwaka 1966 alipokuwa safarini China, alipinduliwa. Alikufa akiwa exile nchini Romania mwaka 1972.

Nkrumah alikuwa na ndoto ya bara Afrika kuwa, UNITED STATES OF AFRICA. Wadau mnadhani kuwa bara Afrika inaweza kuwa nchi moja kama majimbo ya Marekani? Tulivyo na lugha na utamaduni tofauti na ukabila sidhani kama itawezekana kwa sasa. Labda baada ya miaka 200!

Kwa habari zaidi za Kwame Nkrumah someni:

http://www.thenagain.info/WebChron/Africa/Ghana.html

http://news.bbc.co.uk/onthisday/hi/dates/stories/march/6/newsid_2515000/2515459.stm

http://www.africanews.com/site/list_messages/16337

9 comments:

Faustine said...

Kina Nkrumah, Nyerere, Nasser, Kaunda n.k., waliona mbali wakati walipokuwa na wazo la US of Africa. Wazo hili lilipigwa vita na wazungu wakati huo katika miaka ya 60.
Sasa hivi Ulaya wana EU ambayo ina malengo mengi ikiwa pamoja na ulinzi, uchumi n.k.
Ni vyema Afrika ikaanza kufikiria wazo la kuwa na umoja wa kiuchumi. Ghadaffi amekuwa na wazo hili, lakini viongozi wenzake wamekuwa wakipinga.

Anonymous said...

faustine, get your facts right,history tells us,when nkrumah came up with this idea of united africa,it was the likes of nyerere,kenyatta who disagreed saying it was not the right time.after nkrumah had bowed out of the scene,nyerere started trumpeting this idea.To this very day historians dont really understand why nyerere was against united africa when nkrumah first proposed it

Anonymous said...

Kwanza huyo mke wa Kwame ni Mzungu? au vipi hapo? hajakaa kiafrika. Na kama alikuwa mzungu, basi simuheshimu nkrumah tena.
"Do as I say, and not as I do?"

Anonymous said...

alikuwa ameoa mzungu??

Anonymous said...

Machifu hao hao ndio waliomwangusha!

Anonymous said...

Yaani Mrs. Nkrumah alikuwa mzungu! AIII!

Anonymous said...

Mke wa Nkrumah ni m-misri kama sikosei, si mzungu hata chembe anaitwa Fadhia.

Anonymous said...

She was an African!


By Mchangiaji

Anonymous said...

Fadhia alikuwa m-Misri. Alipewa na Rais wa Misri, Gamel Abdul Nasser, ili kudumisha Afro-Asiatic Solidarity! (CHEKA)!