Kuelekea kwenye set ya filamu huko Burlington, Massachusetts. Hayo mabango ya njano ya kuelekeza pa kwenda.
Baadhi ya Extras wakisubiri kuitwa kwenye set. Huyo dada alicheza kama karani kwenye ofisi ya Uhamiaji
Hao akina dada nilikaa nao meza moja. Hao wawili weusi ni mamodo (models).
Baadhi ya Extras wakisubiri kuitwa kwenye set. Huyo dada alicheza kama karani kwenye ofisi ya Uhamiaji
Hao akina dada nilikaa nao meza moja. Hao wawili weusi ni mamodo (models).
Baada ya kusibiri muda mrefu watu wanaanza kuwa Bored.
Lunch time. Kwenye set ya sinema za Hollywood huwa watu wanalishwa vizuri sana. Huyu bibi mwenye nywele nyeupe ndiye anacheza kwenye ile commericial ya Joe Kennedy ya watu maskiniwanaohitaji misaada ya mafuta kwa ajili ya kupasha joto nyumba zao.
Lunch time. Kwenye set ya sinema za Hollywood huwa watu wanalishwa vizuri sana. Huyu bibi mwenye nywele nyeupe ndiye anacheza kwenye ile commericial ya Joe Kennedy ya watu maskiniwanaohitaji misaada ya mafuta kwa ajili ya kupasha joto nyumba zao.
Hivi huyo caterer kakosea njia maana Burlington siyo Hollywood na huyo ni caterer wa Hollywood. Ni hivi kwa sasa sinema nyingi zinapigwa Boston hivyo wanaita watu kutoka majimbo mengine kusaidia.
Huyo ni mcheza sinema na mwimbaji Doug Weeks, aliwahi kucheza kama Pilato (Pontius Pilate) kwenye Jesus Christ Superstar ilivyokluwa Broadway.
Huyo ni mcheza sinema na mwimbaji Doug Weeks, aliwahi kucheza kama Pilato (Pontius Pilate) kwenye Jesus Christ Superstar ilivyokluwa Broadway.
**************************************
Wadau, leo nilibahatika kucheza kama mhamiaji wa kiafrika katika sinema, The Proposal. Stelingi wake ni Sandra Bullock. Bahati mbaya sikumwona kwenye set. Scene ilikuwa kwenye ofisi ya uhamiaji. Nilibahatika kuambiwa niongee kiswahili. Sasa huyo mama ambaye nilikuwa naongea naye alikuwa hajui hata neno moja la kiswahili ilikuwa kichekesho.
16 comments:
unaboa unajua usilete ishu zako za kujifagilia hapa tupe habari mbalimbali kila siku na misinema yako ya uongo hapa
Hongera sana Dada Chemi. Kuna siku utakuwa na mafanikio makubwa katika sinema za Hollywood.. Unavuofanya ni safi maana unajifunza undani wa industry.
Ndoto zako zaelekea kuwa kweli dada keep it up.
Da Chemi achana na wivu wa waswahili. Endelea na kazi nzuri unayofanya!
Chemi, kweli umekomaa sana katika anga za habari na uandishi. Unajua sikutegemea comment ya kwanza ungeitunza na kuionesha. Nimesema hivyo si kwmba namsifia mtoa maoni, lah hasha. Nimekuwa nikitembelea na ku comment kwa akina Michuzi, Mjengwa na kidogo kwa Michuzi Jr. Michuzi kakomaa sana, yeye kazoea mitusi hata kejeli. Michuzi anachotoa (futa) ni matusi anayotukanwa mtu mwingine, kama katukanwa yeye, anaacha tu. Mjengwa ameanza kukomaa, mwanzoni alikuwa anabishana na wadau, sasa hivi naona Misupu kajitahidi kumfundisha, anavumilia. Bado huyu bwana mdogo, na yeye siku moja atakuwa tu, Micuzi Jr. Huyu dogo ana tatizo la "H". Sehemu isiyotakiwa anaweka na panapotakiwa haweki. Mfano anaweza kuandika "wengi wenu mtakuwa mnapakumbuka vyema hapa, wakati huo palikuwa maharufu sana, nimepita leo mchana hapa,daa kwa sasa hakuna tena ile hali yake ya mwanzo kutokana na upanuzi wa barabara ya Sam Nujoma
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, April 07, 2008 | | Permalink | Maoni 2 " Mimi nilimwandkia maoni mazuri tu ya kurekebisha hicho Kiswahili KIBOVU, cha ajabu akabana maoni yangu, kweli nadhani kama hawezi kukubali ukweli, hatajifunza na hataenda. Hongera
Chemi Iam always happy 4 u sister ,great great siku moja tutasema yule dada mtanzania ni actress
Manka
Hongera Da Chemi!
Hongera sana! Tujulishe sinema ikitoka.
anony wa kwanza huna haya,hii blog yake si umekuja mwenyewe sasa kama anakuboa si ufungue yako.
Da Chemi sina budi kukupongeza kwa kuchakarika kwako,mh kuna siku utapata role kubwa zaidi ya hiyo jinsi unavyokwenda.Hongera dada usijali makunyanzi songa mbele.Haters will always be haters
dada chemi, hivi wewe na dully sykes ni ndugu? kama mmefanana vile?
Mdau wa 8:49 PM, asante kwa maoni. Sina undugu na akina Sykes.
Asanteni wote kwa maoni yenu na motisha.
huna haya wewe mdududu wa sikio mi natoa maoni,kama wewe unamsifia msifie kimpango wako..umepewa pesa umfagilie?ndiyo anaboa..na huko ni kubabaikia vitu vya kijinga wewe april 9 10:30
anony wa kwanza ushawahi sikia "cha mtu mavi".Piga ua hii ni blog yake da chemi atafanya atakalo.Da chemi mi ningekuwa uko uliko Wallah nisingekuacha,maana mara kibao watangaza wapi kuna hizi auditions,(mkiaudition Bongo land 3 hapa tz sichezi mbali)sasa anayetaka naye aende asiyetaka basi.Allah akujaalie Dadangu.
da chemi hivi una habari za John Mashaka.Du huyu kaka natisha yaani mpaka kwenye Tv za huko ulaya ,yani ana moyo Mkubwa Mungu atamzidishia mara dufu.Nawe da chemi kwamtaji huo hollywood producers watakuja Bongo kushoot,maana dada kila audition ikatangazwa humo.Napenda jinsi jinsi usivyokata tamaa.mie yaani kwa kutatamaa ndo namba moja.Kwa kweli unanifanya nijaribu zaidi .Asante dada wanawake na maendeleo.
Chemi ungepunguza unene kidogo wangekuwa wanakuchukua zaidi maana du lakini naona kama umepungua kidogo sasa hivi ukilinganisha na siku za nyuma sio
Mdau wa 8:14am, asante kwa maoni yako. Unasema kuwa ningepungua wangekuwa wananichukua. Ukweli ni kuwa kuna competition kubwa sana katika sinema za Hollywood na hao wembamba ni wengi mno. Parts ambazo napata, ninapata kwa sababu ya jinsi nilivyo.
Hata hiyo juzi nilivyoitwa ku-audition kwa ajili ya sinema ya Bruce Willis (ambayo niliigiza kumpiga risasi kichwani) ilikuwa kwa sababu walitaka mama 'heavyset'. Nangojea kuona nani atapata hiyo role, huenda watamwita Mo'nique! Siku hizi wanataka watu ambao ni 'true representation of the population'. kila mtu si mwembamba kama sindano.
Post a Comment