Monday, September 29, 2008

Athumani Hamisi yuko South Africa kwa Matibabu



Kutoka Lukwangule Blog:

TAARIFA ambazo nimezipata leo mchana ni kuwa Athumani Hamisi ,pichani,ameshaanza kupata matibabu katika hospitali aliyofikishwa, nchini Afrika Kusini.

Matibabu hayo ni pamoja na vipimo vya muhimu kabla ya kumfanyika upasuaji.

Kwa mujibu wa mtu aliyekuwa ananipa habari hizi Athumani ameongezwa damu kwa siku ya leo kwa kuwa aliyokuwa nayo ilionyesha kuwa tatizo kwa madaktari wake.Vinginevyo wamesema hali ni shwari.Nitawapatia maelezo hali ya mpiganaji huyu kwa jinsi inavyowezekana lakini si mara zote.

************************

Wadau tuendelee kumwombea kaka Athumani apate nafuu na aweza kurudi kazini na kuendelea na maisha yake kama hapo awali.

2 comments:

Anonymous said...

Pole sana kaka Athumani. Bora upate tiba South Africa.

Anonymous said...

jamani kwani kapatwa na nini kaka huyu?