Tuesday, September 02, 2008

Shukurani - Mama Ethro Yohane Gadau

MAREHEMU ETHRO YOHANE GADAU

FAMILIA YA MZEE ELEUTHERIUS JOSEPH WELLA WA MBEZI BEACH, DAR ES SALAAM, KWA MOYO MKUNJUFU, INAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KUWASHUKURU WOTE WALIYOFANIKISHA MAZISHI YA MAREHEMU ETHRO YOHANE GADAU.

SHUKRANI ZA PEKEE TUNAOMBA WAZIPOKEE WANAJUMUIYA WOTE WATANZANIA WANAOISHI MAREKANI, HUSUSANI WANAKAMATI WANAOISHI HOUSTON, TEXAS, USA – KWA MIKAKATI NA HARAKATI ZAO NYINGI WALIZOFANYA TOKA MSIBA UTOKEE TAREHE 07 AUGUST 2008 KATIKA HOSPITALI YA WEST HOUSTON MEDICAL CENTER, TEXAS. MIKAKATI HIYO ILIWEZA KUFANIKISHA KUHIFADHI MWILI HADI KUSAFIRISHA KWA GHARAMA KUBWA, KUTOKA HOUSTON HADI DAR ES SALAAM AMBAPO ILIFIKA TAREHE 16 AUGUST 2008 IKIWA IMESINDIKIZWA NA MTOTO WA MAREHEMU ANDREW E. WELLA.

AIDHA TUNAPENDA KUTOA SHUKRANI NYINGI KWA MAJIRANI WA MBEZI BEACH, NDUGU NA MARAFIKI WOTE WALIOKUWA NASI WAKITUFARIJI, KWA KIPINDI CHOTE CHA MSIBA, IKIWA PAMOJA NA MISAADA YAO MBALI MBALI YA HALI NA MALI WAKATI WA MSIBA HUU ULIOKUWA WA KIPINDI KIREFU. KWA KUWA NI VIGUMU KUMSHUKURU KILA MTU PEKEE, TUNAOMBA SHUKRANI HIZI MZIPOKEE KATIKA UJUMLA WAKE.

FAMILIA HAINA CHA KUWALIPA, BALI TUNAMWOMBA MWENYEZI MUNGU AWAJALIE NA KUWAZIDISHIA KATIKA SHUGHULI ZENU ZA KILA SIKU.

MAZISHI YALIFANYIKA KATIKA MAKABURI YA KIFANYA CATHOLIC PARISH MISSION, WILAYA YA NJOMBE, MKOA WA IRINGA, TAREHE 18 AUGUST 2008 BAADA YA MISA TAKATIFU.

MISA YA SHUKRANI KWA MUNGU KUTIMIZA SIKU 40 ITAFANYIKA TAREHE 20 SEPTEMBA 2008 KATIKA KANISA CATHOLIC LA MTAKATIFU GASPARY, MBEZI BEACH, DAR ES SALAAM.

WENYE NAFASI YA KUHUDHURIA TUNAOMBA TUJUMUIKE WOTE KUMWOMBEA MAREHEMU MAMA YETU MPENDWA ETHRO YOHANE GADAU ILI ROHO YAKE IPOKELEWE NA KUSTAREHE MAHALI PEMA PEPONI,
AMINA.

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Napenda kuwapa pole wanafamilia. Marehemu astarehe kwa amani. Amen

Anonymous said...

Rest in Peace Mama Ethro.

Unknown said...

Poleni sana kwa kufiwa na mama na jirani yetu. Tuko nanyi katika sala. From Baba na Mama Gi

Anonymous said...

Poleni sana kwa kufiwa na mama ghafla. Yote ni mapenzi ya Mungu, maana alimjalia kuwaoneni baada ya muda mrefu. RIP. Baba Gi.