Wednesday, November 19, 2008

Al Qaeda wamtishia Obama

Barack Obama ni rais mteule wa Marekani hata hajaapishwa, na tayari Al Qaeda wanamtumia vitisho! Doh! Wanamtukana na kusema kuwa ingawa baba yake ni mwislamu na kakulia kikristo anawaabudu wayehudi!

Unaweza kupata habari zote CNN.

http://www.cnn.com/2008/US/11/19/obama.alqaeda/index.html

Vitisho vinazidi juu ya maisha ya Barack Obama na familia yake. Kuna wazungu wachache wenye hasira kwa vile kashinda. Wanaona kuwa nguvu ya mzungu Marekani umepungua. Na nasema acha ipungue weusi na watu wengi wasio wazungu wamenyanyaswa kweli hapa Marekani. Hii nchi ina historia chafu na mbaya mno kwa upande wa ubaguzi.

Wataalamu wanasema kuwa Sarah Palin alichochochea huo ubaguzi ambayo tunaiona leo. Watoto wadogo wanasema "Mwue Obama", Misalaba inachomwa kwenye nyumba za weusi, nyumba na magari ya weusi zinachorwa na maneno ya kukashifu weusi na matukio mengi.

Mnaweza kusoma habari zaidi hapa: http://www.timesonline.co.uk/tol/news/world/us_and_americas/us_elections/article5172285.ece
Mimi nadhani Obama atakuwa ni rais mzuri kuliko wote hapa Marekani. Kwanza hapa USA ukiwa mweusi ni lazima uchape kazi mara nne ya mzungu. Hivyo tayari tunajua atachapa kazi zaidi. Watu wana matumaini makubwa juu yake. Obama ana kazi kubwa sana ya kujenga nchi aliyobomoa Bush.

Na naomba kuuliza, Bush yuko wapi siku hizi? Hata zile hotoba zake za kila wiki kwenye redio zimezidi kuwa fupi. Bush kachoka na nadhani siku akiondoka White House atafurahi sana.

No comments: