Tuesday, November 04, 2008

Uchaguzi Leo!


Leo mamilioni ya waMarekani wanapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria. Huenda Mmarekani mweusi (Barack Obama) atashinda urais kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii. Au huenda mzee kuliko marais (John McCain) wote atashinda na mwanamke (Sarah Palin) atakuwa wa kwanza kuwa makamu rais.

Tutajua matokeo jioni. Leo kila ukipita foleni za watu wanaongojea kupiga kura ni ndefu.

Mungu azidi kumlinda Barack Obama na familia yake!

No comments: