Sunday, February 08, 2009
Bill Gates aachia Mbu kwenye Mkutano wa Wazungu!
Juzi, tajiri na mataalam wa kompyuta, Bill Gates, alifungua kopo la mbu kwenye mkutano wa Design Conference California. Wanaohudhuria huo mkutano ni wataalam wa hali ya ju katika fani zao, wanasiasa, mastaa na hata wafalme! Hao watu walihaha kweli kwa hofu kuwa wataambukizwa malaria. Nasikia watu wengine walilia.
Akifungua kopo la mbu alisema, " Ugonjwa wa malaria unasambazwa na mbu, nimeleta mbu wachache hapa sasa nawaachia huru hapa watembee. Hakuna sababu ya watu maskini tu kuumwa ungonjwa wa malaria!" Baadaye aliwwambia kuwa watu wasiwe na hofu maana hao mbu hawana malaria, bali ni mbu aina ya anopheles wanaobeba ugonjwa huo. Hata hivyo ujumbe wake uliwafikia! Lazima niseme ni shujaa kwa tando aliyofanya.
Wadau, hapa Marekani ukisema malaria watu wanaugopa kweli. Bora mtu useme una UKIMWI kuliko malaria. Nafahamu watu walioenda Bongo wakapata malaria na walivyorudi na kuwaambia wanaumwa ugonjwa huo waliachishwa kazi. Wengine wanatengwa huko hospitalini (quarantine). MBongo mwingine aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi!
Rais Bush alijitahidi sana kusaidia Afrika na tatizo la malaria a UKIMWI. Kama wameweza kufuta ugonjwa huo sehemu nyingi duniani kwa nini wasiweze kufuta Afrika? Na kama pale Dar wakisema kuwa kila mtu atie mchanga/udongo kwenye madimbwi ya machafu karibu na nyumba zao, si itasaidia kupunguza.
Wadau, mnakumbuka miaka ya 80 waJapan walianzisha mradi chini ya Halmashauri ya jiji kupuliza dawa ya kuua mbu jijini. Huo mradi ulisaidia sana kupunguza mbu, ila baada ya miezi sita na waJapani kuondoka na kuachia waBongo uligueka mradi wa mtu. Nakumbuka mtu alifika nyumbani na kusema kama unataka dawa lazima ulipe! Wakati waJapani walikuwepo ulikuwa bure! Jamani!
Kwa habari zaidi someni:
http://www.americanthinker.com/2009/02/the_bill_gates_mosquito_circus.html
http://www.guardian.co.uk/technology/blog/2009/feb/07/bill-gates-ted-mosquitoes
http://www.sfgate.com/cgi-bin/article.cgi?f=/c/a/2009/02/07/BULG15OVGP.DTL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Gates kawakomesha! Lazima kuna waliojikojolea kwa hofu ya kupata malaria.
Post a Comment