Monday, February 02, 2009

Safarini Anguilla

Wadau, niko safarini Blowing Point, Anguilla. Ni kisiwa katika bahari ya Caribbean.

Niliondoka Boston asubuhi sana. Nilipanda ndege hadi kisiwa cha St. Maarten. Kutoka huko nilipanda ferry kuja Anguilla. Customs yao uwanja wa ndege ni kama Bongo ulivyokuwa enzi za Mwalimu. Bahati nzuri hawakunisumbua sana.

Nina picha kibao, lakini sina access nzuri ya internet. Nitazibandika nikirudi Boston wiki ijayo.

Kuna wazungu wengi wenyeji wa visiwa hizi. Wamepikwa na jua. Wengine wana rangi ya brown, na wengine wekunduuu! Yaani baada ya kuzoea kuona wazungu weupe kama karatasi huko Boston lazima niseme niliwatazama hawa wa hapa mara mbili kuhakikisha kuwa ni wazungu.

14 comments:

MICHUZI BLOG said...

NAKUTAKIA VEKESHENI NJEMA. TUNASUBIRI HIZO PICHA.

Anonymous said...

wekundu kama damu au wanaelekea kwenye uwekundu

Anonymous said...

Vacation njema

Anonymous said...

Nakutakia mapumziko mema, Da Chemi, tuko pamoja.
Apfle.

Anonymous said...

Una maana gani enzi za Mwalimu.Sifa na hadhi ya Tanzania ilikuwa juu sana enzi hizo unazozibeza.Tulikuwa nuru kwa yote mazuri Africa.Kulikuwa hakuna ukabila,rushwa.Watu walisoma bure ikiwa pamoja na wewe.Usihadaike na wingi wa golgate.Utu wa mtanzania umepungua sana tokea enzi hizo.Ukiwa na shilingi mia ya mmasai na simba ilikuwa inatosha kununua vitu vingi tu.Tulikuwa na viwanda na vyote vimeuzwa au kufa.

Anonymous said...

enjoy your stay dada,tumekumiss siku hizi mbili mtandaoni.
likizo njema
mdau
thessaloniki,ugiriki

PASSION4FASHION.TZ said...

vekesheni njema dada yetu, enjoy the sun.

Anonymous said...

Da Chemi tumekuelewa vizuri sana. Enzi za Mwalimu ukitoka ng'ambo kupitia Airpost Dar unatetemeka kwa jinsi watu wa customs wanavyokusumbua! Una nini? Kama una sharti jipya au kitu kipya utakoma, unatozwa kodi kubwa!Wanataka kukunyanganya vitu vyako. Walikuwa wezi kweli pale DIA. Sanduku unaweza usipate au una nusu! Watu wamesahau! Tumekuelewa!

Simon Kitururu said...

Safari njema na mapumziko mema!

Subi Nukta said...

Tunasubiri zawadi, ahadi ni deni. Safari njema na ya salama!

Unknown said...

Dada Chemi huko ni wapi kusiko na mtandao? maana tunakumiss.

Anyway safari Njema.

Chemi Che-Mponda said...

Bongo Pixs, mtandao upo, lakini sikuja na lap top. Pia nina shughuli nyingi za kufanya katika muda mfupi. Blog itarudi full speed jumatatu ijayo.

Anonymous said...

siku moja fanya safari kama hiyo kwenu MANDA- LUDEWA-IRINGA TANZANIA kuna mandhali nzuri ya ziwa nyasa au umeisahau?dagaa ,mbasa mbelele bado kwa wingi bila kusahau "mpunga"ulimwao kandokando ya mto nchuchuma

Chemi Che-Mponda said...

Anony wa 6:28pm, kwetu sijapasahau. Ugali wa muhogo na dagaa wa ziwa Nyasa...weeee! Nilifungasha kifurushi cha unga wa muhogo na dagaa na kuleta Boston nlivyokuwa huko mwaka jana.