Tuesday, February 17, 2009

Nyumba ya Mugabe huko Hong Kong

Wakati waZimbabwe wanakufa kutokana na njaa kukosa maji safi na magonjwa kama kipindupindu kuna habari kuwa familia ya Rais Mugabe wanaishi maisha ya kifahari huko Hong Kong! Asante Mdau Born Again Pagan kwa kuleta habari hizi.






Habari za Reuters zilizoandikwa kutoka London zinaeleza kuwa jumba hilo hapo JC Castle, kasikazini ya Tai Po District, mjini Hong Kong, limenunuliwa kwa $ milioni tano na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe. Inasemekana kuwa kuwa ni mojawapo ya majumba ya Rais Mugabe huko Asia ya Mbali. Bintiye, mwenye umri wa miaka 20, anasoma Chuo Kikuu cha Hong Kong, na mkewe amekuwa akifanya safari za “shopping” ile mbaya huko Hong Kong na Bangkok.

7 comments:

Anonymous said...

Kwa nini unashangaa? Mugabe amefilisi Zimbabwe!

Anonymous said...

Ninyi pilipili msizokula zinakuwashieni nini? Toeni za Watanzania na mafisadi wake.Hayo waachieni Wazimbabwe wenyewe

KILI
BG

Anonymous said...

mbona wetu wa bongo wanazo kubwa tu kuliko hizo

Anonymous said...

Hong Kong nyumba ni bei ghali!Ardhi ni adimu! Hiyo nyumba Marekani inaweza kuwa $800,000 lakini Hong Kong ni $5 million.

Anonymous said...

KAMA UNAZO ZA WA-TANZANIA, NA ENDAPO ZA WA-TANZANIA PIA ZIKIJULIKANA WAZI, TUTAZIWEKA BLOGUNI!

KAMA UNAZIJUA, USIFICHE!

Anonymous said...

Gabriel Mugabe? Dachemi sasa kweli vacation haikutosha

Anonymous said...

Mugabe kwani ndiyo Rais wetu?Mbona watanzania wanazo numba walizopata kwa ufisadi hamzisemi.Mfano nasikia Mkapa ana hoteli ya kitalii Afrika ya kusini NK