Monday, February 23, 2009

Mkutano Dallas


Jumuia ya Watanzania Dallas
Ndugu Wajumuia,

Kwa niaba ya mwenyekiti wa muda ndugu Simon Nkanda, napenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha kuwepo kwa mkutano mkuu utakaofanyika Jumamosi ya tarehe 28, Februari 2009, kwenye ukumbi wa 12727 Hillcrest Dallas TX 75230. Mkutano huu utaanza saa kumi na moja jioni mpaka saa nne usiku. Tukio hili kubwa na la kihistoria lina nia na madhumuni ya kuimarisha jumuia ya Watanzania waishio jijini Dallas na vitongoji vyake. Katika harakati zake za kuunda jumuia hii mwenyekiti, katibu, na viongozi wa kamati mbalimbali wa muda walichaguliwa. Vilevile hatua nyingine ya kihistoria iliyochukuliwa ni kuundwa kwa katiba ambayo jumuia hii itafuata mwenendo, taratibu na muelekeo wa kimaendeleo. Mkutano huu utachukua fursa ya kutambulisha jumuia ya Watanzania hapa Dallas na vitongoji vyake umuhimu wa kuwa na amani, upendo, ushirikiano, umoja na kufuata tararatibu ambazo zitaimarisha jumuia hii. Katika mkutano huu, mwenyekiti, katibu, na viongozi wa kamati mbalimbali watatambulishwa. Vile vile katika jitihada za kuimarisha jumuia hii, hatua zimechukuliwa za kusajili jumuia hii, kuanzishwa mfuko wa dharura, kuanzishwa mtandao mpya, kutumia njia ya teknohama ili kuimarisha mawasiliano na kuutaarifu ubalozi wa Tanzania hapa Marekani tukio hili la kihistoria. Kiongozi wa ubalozi wa Tanzania huko Washington D.C. , Dr Mkama atahudhuria mkutano huu. Kijiweni restaurant wanafadhili mkutano huu na watatoa huduma ya chakula.. Kutakuwa na wageni kuoma miji mingine hapa Marekani ambao watahudhuria mkutano huu. Tunaomba Watanzania wote mliopo Dallas na vitongoji vyake mjitokeze kwa wingi ili tukamilishe jitihada hizi. Tukumbuke tena, “Our real values are expressed in our actions, in what we do and how we do it”.

Kwa maelezo zaidi tunaomba muwasiliane na:

Ndugu Simon Nkanda Ndugu Abdul Amiri
Phone: 469-585-8476 Phone: 214-535-6329
(Mwenyekiti wa muda) ( Katibu wa muda)

No comments: