Bado sijajua jina la huyo mwanamke ila ana miaka 20. Alienda supermarket na huyo jamaa kamfuata huko na kumpiga risasi kichwani. Kwa bahati risasi haikupenya kichwani shauri ya kukumbana na weave!!!! DUH! Ila dada mwenyewe anasema alisikia joto la risasi. Anasema alitumia hela nyingi kuweka hiyo weave kichwani bora imekuwa na faida kwake! Polisi walivyokuja walikuta risasi imenasa ndani ya weave.
Wazungu wamenichekesha kwenye taarifa ya habari leo. Wanauliza hiyo weave ni nini na inatengenezwa na nini! Je, inatumia gundi au chuma?
Kwa habari zaidi na kuona kideo, bofya chini:
7 comments:
Ana bahati kweli! Saaa hizi ingekuwa kilio.
yaani wewe chemi ni pumbaf sana. unapenda sana kuchemka na pumba zako. kwani hizo weaving zenu mnazovaa watu weusi zinatengenezwa na nani? wazungu au weusi? Kwanini wewe huna akili kiasi hicho? hata usipoibandika hii lakini ujumbe umeshaupata.
Doh! Mungu kmalinda. Mimi mwanauma lakini nitatafuta weave.
Ilikuwa na pande za chuma nini? Ashukuru Mungu!
duh na kweli. Yaani nyinyi mnaovaa wieve mnajifanya mnazijua kuliko wao wazungu wanaozitengeneza.
Wewe anony uliyemtukana Chemi hapo juu hii blog sio zeutamu, nenda huko ukatoe hasira zako za maisha. Alichokifanya Chemi ni kuwasilisha kilichotokea kama una bifu zako binafsi hapa si mahala pake, toa dukuduku lako kunakohusika au mwandikie Chemi personal email.!!
Issue sio suala kuwa tunazijua weaving kuliko wazungu wanaozitengeneza, kwani kwasababu ni wazugu lazima wajue kila kitu, mimi navaa wigs mara kibao na kila ukienda kuna wazungu hapa US wanakuambia nice hair cut! unabaki unashangaa, kumbe wewe unajua umevaa wig, wengi wao bado hawawezi kutofautisha real hair na weaving bado kwa hiyo mnachoshangaa ni kitu gani, rasta tu zenyewe kuna wazungu bado wanadhani ni nywele original za mtu. Kuwajibu swali lenu NDIO blacks wanajua weaving zaidi kuliko mzungu aliyezitengeneza!!
Post a Comment