Thursday, February 19, 2009

Katuni ya Kibaguzi?


Wadau naomba maoni yenu. Hii katuni ilitoka jana kwenye gazeti la The New York Post. Imechorwa na msanii Sean Delonas. Viongozi wa weusi Marekani wanasema kuwa hii katuni ni ya kibaguzi na kuwa jamaa anataka Rais Obama auliwe! Bwana Delonas anakataa tena anacheka huko akisema kuwa alikuwa na maana ya kesi ya yule nyani aliyeuawawa huko Connecticut juzi.
Nampinga kwa sababu, polisi anasema "itabidi wamtafute mtu mwingine kuandika stimulus bill". Aliyeandika stimulus bill ya sasa ni Rais Obama na siyo nyani. Hapa Marekani tangu zamani watu weusi wanafananishwa na manyani. Hata kwenye kampeni wabaguzi walikuwa na sanamu za nyani na kusema ni Obama. Na yule nyani wa Connecticut alihusika nini na stimulus bill?
Wadau, Marekani ina rais mweusi lakini ubaguzi bado upo!
Soma maoni ya Roland Martin wa CNN juu ya hii katuni HAPA:

10 comments:

Unknown said...

Hili si jambo la ajabu, Wamerikani katu hawataacha desturi yao ya kubagua dhidi ya watu weusi, hata kama rais wao ana asili ya kiafrika. Muhimu ni kwamba misingi ya nchi hii inampa fursa mtu yeyote kutimiza ndoto yake ya kukuwa chenye anataka kwa kutumia mbinu mbalimbali yaliomo humu. Wacha waseme na wachora watakavyo hakitabadilisha chochote.

Anonymous said...

Jamaa kajichongea kweli. Asingetaja habari ya stimulus basi. Nalaumu editors kwa kukubali kuprint.

Anonymous said...

America is a country where white men with criminal records are more likely to be considered for a job than black men with no criminal past. What can we expect? Racism is in white folks blood.

Anonymous said...

wanajisumbua tu hao mbona Obama hafi ng'o ktk jina la Yesu

Anonymous said...

Whether they draw it in pictures or say it aloud, racists will always be there. Racism is a manifestation of inferiority complex

Anonymous said...

nasikitika na watu wengine hapa badala ya kumsapot president obama katika harakat za kufufua uchum,bado wanafikira za ubaguz,ukiwa na ubaguz ata kama utasali na kumuabudu mungu ni kaz bure,yesu alituasa tuwe na upendo dunian

Anonymous said...

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema dhambi ya ubaguzi ni mbaya kama ya kula nyama ya mtu. Huu ubaguzi utapungua na kuchukua sure tofauti lakini hautaisha.
Nakubaliana na Martini hapo juu kuwa hawawezi kubadilisha chochote, maana wameshampa nchi mtu mweusi, ambaye pia inabidi awaonyeshe kuwa mtu atahukumiwa kwa 'contentof their character and not color of their skin' kama alivyosema Martin Luther

Anonymous said...

UBAGUZI NI UDHAIFU, LAKINI NA NINYI SI MNAKWENU, HUKO MLIPO VIBARUA , KAZI MFANYAZO NI ZA UDHALILISHAJI, SASA KWA NINI MSIBAGULIWE KAMA MLISHAJIBAGUA. RUDINI TZ.

Anonymous said...

Huyo cartoonist anasema chinicini kuwa anataka Obama apigwe risasi!Kwa nini hajakamatwa na Secret Service?

Unknown said...

Da Chemi ni lini hao jamaa weupe watakubli kuwa sasa white house kuna black family??
na kuwa iwe isiwe hata kama Obama watamuua leo hii tayari amekweisha weka historia ambayo hakuna kiumbe chochote kitakuja ibadili hata kiama kije???


yawezekana wangali na hasira kwanini Barack anawaongoza, yawezekana wanadhani kuwa wako ndotoni na kuwa wataamka na kukuta sivy, lakini hawana uwezo wa kubadili lililoandikwa na Mwenyezi MUNGU nalo ni kuwa mwaka 2009 na kuendelea WAREKANI WATAONGOZWA NA MWEUSI, watake wasitake hivyo ndivyo ilivyo.

Lakini pia si ni wao ndo walomchagua tena kwa kura nyingi zisizo na utata hata kidogo ka wakti wa Kichaka mwaka 2000?

CIAO.