Thursday, February 12, 2009

Msiba Boston - Mzee Leonard Merere

Ndugu,Jamaa na Marafiki,

Tunapenda kuwajulisha ya kuwa Mzee Leonard NJ Merere ambaye pia ni baba mzazi wa ndugu zetu Naomi na Jacob[JJ] Merere wa Boston-Masachusetts amefariki dunia siku ya Jumanne [Feb 10th 2009] asubuhi hapa Boston,USA.

Marehemu alikuwa na umri wa miaka 73, ameacha mjane,watoto watatu na wajukuu wanne. Taratibu na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es salaam kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa watoto wake huko Boston-Masachusetts. Kila mmoja wetu anaombwa kuchangia fedha kwa ajili ya kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi.

Gharama za kuhifadhi mwili,kusafirisha mwili,Jeneza pamoja na ticket ya atakaye kwenda pamoja na mwili ni dola elfu ishirini[$.20,000]. Ni mzigo mkubwa sana ambao kila mmoja wetu anombwa kusadia ili kukamilisha shughuli hii hasa ukizingatia ya kuwa kwa kadri mwili unavyokaa funeral-home ndio gharama zinavyozidi kuongezeka.

Mwili utasafirishwa punde zitakapopatikana fedha za kulipia gharama.

Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account ya wafiwa kama ifuatavyo:

NAOMI MERERE
BANK OF AMERICA,
ROUTE NUMBER :011000138
ACCOUNT NUMBER:009441233628

Au kwa adress hii:
Jacob & Anna Merere
510 Skylinedrive suite # 11
Dracut,MA 01826.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:

Jacob & Anna Merere [JJ]-978-726-2227 au 978-957-2153.
Naomi Merere-978-413-3722 au 978-632-9823.
Juma Malika-781-244-7353
Saimon Twalipo-978-423-1192
Pastor Abisalom Nasua-214-554-7381

Email-Adress:- RambiRambi@Yahoo.com

Tafadhali chukua muda kuwafariji wafiwa na kuwaombea Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa kuwasaidia familia Merere !

Mbarikiwe, Mch.Abisalum Nasua,Jackson Mollel
Michango-Kwa Niaba ya Marafiki wa Familia ya Merere.

2 comments:

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Nawapa pole kwa msiba huu.

Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya mpendwa wetu mahala pema peponi.Amina

Anonymous said...

Poleni sana familia ya Merere. Mungu amlaze mahala pema mbinguni. AMEN.