Navyoona ni vizuri vijana waelemishwe kuhusu mabadiliko mwilini mwao. Pia kuepusha mimba wakiwa na umri mdogo na kuambukizwa magonjwa ya zinaa. Kwa vijana wanaokaa mijini wanaelimishwe na vijana wenzao na mara nyingi wanapotoshwa. Oh hutapata mimba kama ukitia sabuni huko. Au, kijana anaamibwa hawezi kutia msichana mimba kama atamwaga nje! **********************************************Nadhani mzungu ameandika hii, lugha si ya Bongo.Kutoka BBCKubalehe
Kubalehe ni sehemu moja muhimu ya maisha yetu. Wakati huo mwili na akili hukumbwa na mabadiliko makubwa ya kukua kutoka utotoni kuelekea ujanani na hatimae utu uzimani.
Wakati huo viungo vya uzazi hukua na kuimarika kujitayarisha kwa uzazi.
Miili ya watu hubadilika kwa kiwango tofauti. Wengine huanza mapema na kuimarika haraka, wengine ikawa ni kwa polepole. Kwa wengi kubaleghe hutokea kati ya miaka 8 na 16, lakini kila mtu ni tofauti. Umri wa wastani kwa wasichana ni kati ya miaka 9 hadi 13 na kwa wavulana ni kuanzia miaka 10 hadi 12.
Vijana wengi hukumbwa na wasiwasi wasijue jinsi ya kukabiliana na mabadiliko hayo... lakini mara nyingi kiwango chochote cha mabadiliko yanayotokea wakati huo huwa ni kawaida na sawa kabisa.
Ni nini hasa kinachotokea?
Mwili huzalisha chembe chembe ziitwazo hormones kwa kiingereza. Wasichana hutoa homoni ziitwazo oestrogen ilhali wavulana wanakatoa homoni ziitwazo testosterone.
Chembe chembe za mwili ndizo ndizo zinazoanjisha utaratibu wote wa hatua za kubaleghe. Huenda pia kukawa na mabadiliko ya hisia mbali yale ya ndani na nje ya mwili.
--------------------------------------------------------------------------------
Swala la kufanya ngono
Je niko tayari kufanya mapenzi?
Swala la kushiriki katika ngono ni swala zito linalohitaji uamzi mkubwa na wa makini. Wasichana na wanawake chipukizi hukumbwa na shinikizo kubwa kutoka kwa marafiki zao na wapenzi wao wa kiume. Lakini kanuni kuu muhimu ni kwamba usifanye kitendo ambacho hujisikii au hutaki kukifanya.
TAYOMwili ni wako, na ni muhimu kudhibiti yale yanayotokea maishani mwako hasa yale yanayoweza kuathiri afya yako ya uzazi , hasa kuhusiana na hatari za kupata mimba, na kuambikizwa magonjwa ya zinaa ikuwemo ukimwi.
Basi lini ntakuwa tayari kufanya mapenzi?
Watu wengine hukimbilia kufanya mapenzi bila ya kufikiria kwa makini swala hilo, na baadae kujutia na kutamani wangedumu katika ubikira kwa muda mrefu zaidi.
Kuwa tayari, ni kuwa na hakika kwamba unaelewa ngono ina maana gani, na matokeo au madhara yake yanavyoweza kuwa nini, ili usije kujutia baadaye.
Kumbuka matatizo ya kupata mimba sizizohitajika, magonjwa ya zinaa ikiwemo kuambukizwa virusi vya HIV hutokana na vitendo kama hivi.
Nitajuaje basi kama niko tayari?Utajua kwa hakika, tu iwapo huo utakua uamuzi wako binafsi.
Utajua uko tayari tu iwapo una uhakika kuwa unaelewa vyema maswala ya ngono na hasahasa afya ya uzazi, na vipi kitendo hicho kinaweza kuathiri maisha yako.
Kwa hivyo usikubali chochote wanachokwambia marafiki zako, ama shinikizo la mpenzi wako wa kiume. Utakuwa na hakika pale utakapokuwa na ufahamu mzuri wa kuelewa ngono ni nini, na jinsi kitendo hicho kitakavyobadilisha uhusiano wako.
Mbali na hayo, ni vyema pia ujue mbinu za kuzuia mimba (iwapo huko tayari kupata mimba) na jinsi ya kufanya mapenzi kwa usalama. Utakuwa na msimamo wa hakika, na hutakuwa na tashwishi yoyote. Utakuwa unaelewa hali halisi ya maisha kwa hivyo hutatarajia iwe kama mifano kwenye sinema. Kama huna hakika na hayo basi huko tayari!
Na je nikiamua niko tayari?Zungumza na mpenzi wako, na mhakikishie kwamba nyote mko tayari. Jadilianeni kuhusu mapenzi salama na kubalianeni kuhusu njia za kuzuia mimba iwapo hamuko tayari kupata mtoto.
Pangeni ni wakati gani na wapi mtatekeleza haja yenu. Ni vyema pia kujiwekea viwango, mipaka na vima – yaani zungumzeni juu ya jinsi kila mmoja anavyojisikia kuhusiana na mambo kama punyeto, mapenzi ya kunyonyana sehemu za siri, na yale yakuingiliana kupitia sehemu ya haja kubwa.
Kama hamuwezi kuzungumza kwa uwazi na kwa kuaminiana kuhusu maswala haya, basi mwapasa kubadilisha fikra zenu kuhusu kufanya mapenzi.
Kumbuka iwapo utabadili nia na msimamo wako wakati mkijitayarisha kufanya ngono, katika kiwango au hatua yoyote ambayo utakuwa umefikia, una haki ya kutoendelea na kitendo hicho. Pia iwapo umefanya mapenzi mara moja, haimaanishi uendelee kufanya mapenzi! La muhimu ni kuwa uwe ni uamuzi wako, ili usije kulaumu baadae.
Na je, kama nafikiria siko tayari?Basi usifanye mapenzi, Una haki ya kusema La, na hupasi kujisikia kuwa umekosea, umemkosea mtu unaefanya nae mapenzi au kuwa na hatia kuhusu uamzi wako.
Kumbuka lolote unalofanya ni uamuzi wako - Tafakari juu ya maadili ulojiwekea, juu msimamo wako, juu ya viwango ulivyojiwekea - Je unaonelea ni sawa kubusiana? Kupapaswa? Kunyonyana? Hakikisha mpenzi wako anajua msimamo wako, maoni yako na anaheshimu uamuzi wako.
Umri unaoruhusiwa kisheria kufanya ngono.
Ni kinyume cha sheria kufanya mapenzi kama uko chini ya umri wa miaka 18, lakini si hatia kisheria usipofanya mapenzi hata kwa umri wako wote!
--------------------------------------------------------------------------------
UsengeUhusiano wa kimapenzi kati ya mwanamume na mwanamke huitwa heterosexual, kwa kimombo wengi huuita uhusiano wa kawaida.
Lakini uhusiano wa kimapenzi kwa watu wa jinsia moja yaani mume kwa mume au mke kwa mke huitwa Homosexual kwa kimombo, kiswahili ni usenge kwa wanaume (au gay) na usagaji kwa wanawake, pia wakiitwa Lesbians kwa kimombo.
Wasenge na wasagaji ni watu wa kawaida ila wanamapendeleo tofauti ya kingono.
Hata hivyo maisha ya wasenge na wasagaji yanaweza kuwa magumu sana kwa vile watu wengi wana itikadi kali za kuchukia mienendo hiyo kimapenzi.
Hapa tungesema tu kuwa watu hao wanatimiza aina ya ngono wanayoonelea yawafaa .
Utajuaje kama u-msenge au msagaji?
Hakuna anayezaliwa akijijua yeye atakuwa nani maishani, na atakuwa na uhusiano wa kingono wa aina gani baadae maishani.
Ila matarajio ya wengi ni kuwa atakuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wa jinsia tofauti nae.
Lakini baadhi ya watu huvutiwa na watu wa jinsia sawa na wao. Wale wanaoendelea na kuwa na uhusiano wa kingono, yaani mume kwa mume, ni wasenge, ilhali wasagaji wana uhusiano wa kimapenzi wa mke kwa mke.
Wengine huvutiwa na wanawake na vilevile wanaume kwa hisia za viwango mbali mbali. Hawa nao wakitekeleza aina zote mbili za kingono huitwa bisexuals kwa kiengereza.
Matamanio ya kimapenzi huenda yakabadilika katika maisha yako. Hata hivyo kuwa na hisia tu, za kuvutiwa na mtu ambaye ni mume mwenzako au mke mwenzako, haimaanishi kwamba wewe ni msenge au msagaji.
Kwa wengi hali hizo haziwaathiri na huwa na uhusiano wa kawaida, ilhali wengine wao wakawa wasenge au wasagaji. Kwa bahati mbaya matabaka mengi ya watu wanapinga uhusiano wa aina hii.
Msimamo wa watu wengi na imani ya dini nyingi ni kwamba jambo hili ni mwiko, lililokatazwa, na dhambi kwa Mungu. Huku wengine huchukulia jambo hilo kuwa tisho kwa desturi na maadili yao.
Kwa hivyo kama wewe ni msenge au msagaji, hasa kama humjui mtu mwingine yeyote ambaye ni msenge au msagaji, unaweza kujikuta mpweke ukiona kwamba jamii haikuelewi kwa vile aina ya mapenzi unayofanya ni tofauti na wengine.
Ni vyema pia kujua kuwa uhusiano wa kingono wa watu wa jinsia moja, yaani usenge au usagaji, umepigwa marufuku kisheria katika mataifa mengi ya Afrika yakiwemo mataifa ya afrika mashariki.
--------------------------------------------------------------------------------
Mapenzi ya kunyonyana sehemu za siriHii ni hali ya kutumia mdomo wako na ulimi kunyonya uume au uke ili kusisimua hamu ya mapenzi.
Kwa wanaume, mpenziwe humnyonya uume (mboo) na sehemu zinazozunguka eneo hilo ilhali wanawake, mpenzi wake humnyonya mashavu ya kuma, kisimi (kinembe) na eneo linalozunguka uke.
Watu wengi hujisikia wamepata hisia za starehe kubwa katika kitendo hicho, na ni moja ya njia za kumkurubisha kimapenzi mwendani, mpenzi wako. Kuona, kunusa, kunyonya lakini mambo haya kwa kawaida huwa baina ya wapenzi walio karibu sana katika uhusiano wao.
Kwa hivyo ni kawaida kujihisi kutopendelea kufanya mambo kama hayo na mpenzi ambae si wa mda mrefu, au ambae humfahamu vyema.
Je kuna hatari gani ukifanya mapenzi ya kunyonyana sehemu za siri?
Hatari zipo. Bado unaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa, kwa hivyo, ni bora kutumia kondomu naam kondom, labda ujaribu zile zenye ladhaa ya matunda ukipendenda!
Kwani bila kufanya hivyo na ukanyonya sehemu ya siri ya mpenzi wako ilhali ameambukizwa ugonjwa wa zinaa hata kama ni virusi vya HIV, upo uwezekano wa kuambukiwa.
Na kama mvulana ananyonya uke wa msichana pengine atumie kifaa maalum kwa kufunika mdomo kinaitwa "dental dam".
La kuzingatia zaidi, katu usifanye mapenzi ya kunyonyana sehemu za siri iwapo una vidonda vya mdomo au katika sehemu za siri.
Mbali na hayo kuna hatari nyenginezo? Ni lipi lengine ninalopaswa kujua?Kama unahakika ni salama kufanya mapenzi ya kunyonyama, pia ni vyema kujitayarisha – Oga! Naam usafi wa mwili ni muhimu.
Halafu kuwa mtaratibu na mwangalifu kwani viungo vya sehemu ya siri huwa laini, nyororo na nyeti. Hivyo basi msuguano wa nguvu huenda ukaleta madhara kuliko starehe.
Zaidi ya yote mheshimu mpenzi wako, mengine ambayo kwako ni sawa huenda yasiwe sawa kwake!
--------------------------------------------------------------------------------
Kufikia kilele wakati wa kufanya mapenzi.Katika harakati za kufanya mapenzi, viungo vya uzazi husisimka na kujisikia starehe ya aina yake. Mishipa ya damu katika viungo hivyo hujaa, na kusikia moyo kupiga kwa kasi - Unapofikia kilele mishipa hushupana kwa haraka, hali hiyo huanzia mkunduni na kuenea kote katika sehemu za siri, na hata kote mwilini na kuleta tukio la kufurahisha.
Katika starehe hiyo mishipa hukakakamka na kuachilia msismko unaombatana na kutokwa kwa ghafla kwa manii kwa upande wa mwanamme (hali inayoitwa ejaculation kwa kimombo) na mwanamke nae hurishai kwa kutoa majimaji kutoka eneo la ukeni.
TAYO Hali hiyo ya kifikia kilele katika mapenzi huitwa "orgasms" kwa kiengereza. Punde mtu hujisikia mstarehe na mtulivu.
Kila mmoja vilevile ana kile kinachomsisimua zaidi- na uwezo tofauti wa kuhimili hisia za kimapenzi na mhemko.
Kitendo cha kufanya mapenzi, au hata kufanya mchezo tu au kutaniana kimapenzi kwa kushikana shikana na kutomasana na mtu ambaye unajisikia huru nae kuwa na uhusinao wa kimapenzi, kwaweza kukufanya kufikia kilele cha kusimika.
Pia watu wengine kufanya punyeto kama njia moja ya kufikia kilele cha kusimika. Ni vyema kujijua, unaweza kutimiza starehe yako unavyotaka ilmradi tu unafanya hivyo kwa njia salama kwako na kwa mpenzi wako na mradi tu huvunji sheria.
Mbona mie sijawahi kufikia kilele kama hivyo mlivyozungumzia?
Aha – usiwe na wasiwasi. Si kwamba wewe ni mtu aliye na kasoro, au asiye wa kawaida eti kwa kuwa tu hujafikia kilele wakati wa kufanya mapenzi.
Kwa kawaida ni rahisi kwa wanaume kufikia hatua hiyo kuliko kwa wanamke, lakini wanawake wanaweza kufikia kilele cha hamu ya mapenzi kwa urahisi zaidi na kujisikia mustarehe iwapo anapenda kutekeleza au kutekelezewa vitendo hivyo anavyofanyiwa wakati wa kufanya mapenzi. Ikiwa atachukizwa basi usitarajie atasisimka kimapenzi.
Lakini kwa upande wao ni vyema wawe watulivu na kujua hali ya miili yao na kile kinachowastarehesha.
Watu wengine hufikia hali hiyo pale wanapofanya punyeto. Jambo linalowaashiria kile wanachotaka katika kufanya mapenzi.
(Ni vyema kujua pia wavulana na wanaume, wakati wengine hutokwa na manii au maji maji bila hata kusisimuliwa na harakati za kufanya mapenzi. Hii hutokea zaidi wakati wanapokuwa wamelala, na hizo huitwa ndoto chepe yaani "wet-dreams" kwa kiingereza. Hii ikiwa njia mojawapo ya kuondoa mihemko mwilini.)
***************************************************************
Kwa habari zaidi tembelea:
http://www.chezasalama.com/A-Sexuality/puberty/questions_and_answers.phphttp://sw.wikipedia.org/wiki/Ubalehe