Friday, September 28, 2007

Heshima za Mwisho - Mzee Godwin Kaduma (1938-2007)

Prof. Saida Othman (kulia) Prof. Amandina Lihamba, Prof. Penina Mlama na Mama Thecla Mjatta wakiongea kabla ya heshima za mwisho kuanza.
Wazazi wangu Dr. Aleck Che-Mponda na Rita Che-Mponda wakiongea na Prof. Penina Mlama, Prof. Saida Othman na Prof. Amandina Lihamba.
Mama Thecla Mjatta (mwenye Scarf ya pinki) akiongea na waombolezaji wengine kabla ya shughuli za kuwaga Mzee Kaduma kuanza.


Mzee Masimbi akitoa maelezo kuhusu mipango ya mazishi. Mwili wa Mzee Kaduma ulipelekwa kwanza nyumbani kwake Bagamoyo halafu ulipelekwa Iringa kwa ajili ya mazishi.


Prof. Amandina Lihamba na Prof. Penina Mlama wakipita kutoa heshima za mwisho.

Mzee Masimbi akiwafariji Mama Thecla Mjatta na Prof. Penina Mlama

Thursday, September 27, 2007

Rest in Peace Mzee Godwin Kaduma (1938-2007)

Hapa Mzee Kaduma anajadili mambo ya filamu Tanzania.


Nimepata habari za kusikitisha sana. Mzee Godwin Kaduma amefariki dunia. Nilikuwa namfahamu miaka mingi sana, alikuwa na kipaji ya ajabu katika usanii. Ninalia. Mungu Amlaze mahali pema mbinguni. AMEN.

*****************************************************************************

Dear Friends,

Mzee Godwin Zilaoneka Kaduma is no longer with us. Godwin Kaduma passed away at the Muhimbili National Hospital this afternoon the 27th September 2007 due to a severe stroke. I will update you with the funeral arrangements once I get information from relatives. May God rest him in eternal peace!

Ghonche Materego.

CEO - EATI
27th September 2007

************************************************************************
Habari za kusikitisha zilizotufikia ni kwamba gwiji la sanaa za maonyesho nchini Tanzania Mzee Godwin Zilaoneka Kaduma hatunaye tena duniani.Habari hizo zinazidi kupasha kwamba mauti imemfika Mzee Kaduma katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa ajili ya matibabu zaidi.Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza(stroke).

Msiba upo nyumbani kwake Bagamoyo jirani na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo. Heshima za mwisho kwa walio Dar-es-salaam zitatolewa kesho (Ijumaa) saa nne asubuhi habari zaidi zinasema heshima za mwisho kwa marehemu mzee Kaduma kwa walio Dar es salaam zitatolewa kesho saa nne asubuhi hospitali ya Muhimbili kabla mwili wake kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Bagamoyo na kisha baada ya kuagwa saa nane mchana utapelekwa kijijini kwake Itamba, Iringa, kwa mazishi.

Wednesday, September 26, 2007

Ukweli kuhusu Sara aka Venus Hottentot





Mmewahi kusikia habari ya Saartje (Sara) Baartman, kutoka Afrika Kusini. Sara alifariki dunia mwaka 1815 nchini Ufaransa, lakini alizikwa mwaka 2002 kwao Afrika Kusini.

Alivyofariki mwaka 1815 akiwa na umri wa miaka 26, wanasayansi wa huko waligombania maiti yake. Walikata viungo vyake vya siri na kuviweka kwenye chupa za kuzihifadhi na kuwekewa kwenye nyumba ya maonyesha. Walisema eti mashavu ya huko mahala ni marefu.

Kisa cha kutokuzikwa miaka 187 ni kuwa Sara ndiye yule ambaye wazungu walikuwa wanamwita, 'Venus Hottentot'. Sara alikuwa na matako makubwa kweli kweli na wazungu walikuwa wanamshangaa. Kumbe kwa kabila lake ndo wanawake walivyo. (picha ya juu ni wax mold ya maiti yake, Aliwekwa kwenye circus na kutembezwa Ulaya kama mnyama kwenye zoo!

Wakati hayuko zoo walifanya ngono naye kwa ajili ya kutoka 'kuonja' maajabu yake!

Sara alichukuliwa ktoka kwao Afrika Kusini akiwa na miaka 21 kam mtumwa. Alipelekwa kwanza Uingereza na daktari fulani. Alifariki kwa ugonjwa na si ajbu ilikuwa ugonjwa wa zinaa!

Unaweza kusoma habari zake kwenye vitabu vilivyoandikwa kuhusu watu wa ajabu duniani kama yule Elephant Man, ambaye alikuwa na ugonjwa mbaya wa ngozi na mifupa.

Kuna michezo ya kuigiza kuhusu maisha ya Sara. Naona muda umefika watengeneze sinema kuhusu maisha yake na jinsi alivyoteswa na wazungu.

Mungu apumzishe roho yake mahali pema mbinguni. Amen.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.heretical.com/miscella/baker4.html

http://www.salon.com/books/review/2007/01/09/holmes/index_np.html


http://www.southafrica.info/ess_info/sa_glance/history/saartjie.htm

http://freaks.monstrous.com/the_hottentot_venus.htm

Marudio - Wapenzi wa Matako Makubwa


From my 12/2005 Blog:

Wapenzi wasomaji, leo nimeamua kuzungumzia suala ya matako makubwa. Tafadhali msione kama ni matusi lakini hapa USA ni issue kubwa, maana watu wanayachukia! Nimeona nizungumzie suala ya matako makubwa kwa vile jana kazini, mzungu aliyekondeana mno kasema ni mnene na akila keki eti yote itaenda matakoni. Nilishangaa na kusikitika sana.

Uzuri kwa wazungu ni kuwa na matako fleti kama vile yamepigwa pasi. Sijui kwa nini. Mtu anashepu ya mbao, mwanamke hana hips kakaa kama dume vile eti ndo uzuri. Kumbe ni kwa sababu hao models na wacheza sinema wako hivyo!Basi wasichana na akina mama wanajinyima chakula kusudi wakonde na eti wapendeze. Ndo maana magonjwa kama Bulimia na Anorexia zimeshamiri hapa.

Lakini ukitazama sinema za miaka ya nyuma kama za 1930's na 1940's, wanawake walikuwa na shepu na walikuwa wamejaa na hata wanaume wa kizungu walikuwa wanasifia. Mpaka 1950's kulikuwa na mcheza sinema Marilyn Monroe, alikuwa na zinga la figure 8, na wanaume wote walikuwa wanampapatikia. Ama kweli mambo yanabadilika. Hivi sasa wanasema eti walikuwa ni obese yaani wanene! Mbona mimi naona matako fleti kama chapati ni mabaya na hayapendezi? Au ni kwa sababu nimekulia Africa?

Brothas (waMarekani Weusi) wanapenda mwanamke awe na matako ya maana! Akipita mwanamke mwenye mbarikio utasikia brothas wakisifia, "umm, umm umm!"

Kuna siku nilisikia wanaume wa kizungu wakijadili sababu ya wanaume weusi kupenda matako makubwa, walisema ni "cultural thing". Kwa kweli ni culture yaani utamaduni wa mwafrikai! Kama umekulia katika mazingara ya kupenda kitu utakipenda. Na ndo maana kuna weusi USA wanataka kuwa na shepu iliyokondeana kama mzungu kumbe haiko katika 'genes' zake. Wajitahidi kupunguza mzigo lakini wapi, iko pale pale.

Sisi wanawake wenye asili ya Afrika tumebarikiwa huko nyuma. Yaani boxi, siha, wowowo, booty, na nasikia waGhana wanaita yokohama, matako makubwa yana majina mengi. Waafrika tunaona kama ni urembo, lakini wazungu na waliokulia uzunguni wanaona kinyaa. Wanasema eti ni dalili ya ulafi na uvivu! Lakini kama ni dalili ya ulafi mbona hata mwanamke mwembamba mwafrika anaweza kuwa na kamzigo huko nyuma?

Ubaya mwenye matako makubwa anaweza kubaguliwa kwa vile bosi anaweza kuona kuwa ni 'ugly' (mbaya) na mwenye nacho anachafua mazingira ya ofisi. Kweli kabisa! Hayo matako makubwa ni 'genes' za sisi waafrika. Lakini ajabu kuna siku nilisikia wazungu wakisema eti waafrika tuna matako makubwa kwa sababu ya utumwa. Eti mabibi zetu walinyimwa chakula hivyo matako ndo ilikuwa 'godown' ya mafuta ya akiba. Nadhani ni uzushi kama ile ya ngamia kuweka maji kwenye nundu zake!

Mimi mara nyingi nimeambiwa nina matako makubwa, niyapunguze kwa kwenda gym kufanya mazoezi. Hayo mazoezi haisadii kitu ni makubwa vile vile! Lakini msione kama naona haya, wala! Mtu akiniambia nina matako makubwa namwambia mbona kama ni madogo, na ningependa yawe makubwa zaidi! Wanabakia kushangaa hasa nikiwaambia kuwa Afrika, matako makubwa ni uzuri.Na amini usiamini kuna opresheni ya kuyapunguza inaitwa Liposuction.

Wanawake wengi weusi na wazungu wamefanya hiyo liposuction ya matako, akiwemo mwimbaji Janet Jackson. Ubaya, ni kuwa ukishafanya hiyo liposuction, mafuta yataenda kwingine mwilini, hivyo utakuwa na shepu ya ajabu!Sisi waafrika tunapenda kuringia huo mbarikio wa matako makubwa. Nilipokuwa nacheza ngoma shuleni na jeshini, tulikuwa tunatia nguo ndani ya bukta kusudi tuonekana na matako makubwa kweli kweli! Lakini, mara nyingi mitaani hapa USA, nimesikia akina dada wakifokewa, "You got a big a-s!"

Kuna siku nilikuwa kwenye kituo cha Subway hapa Boston, kapita mama fualni Mganda, aisei alikuwa amejaliwa kweli huko nyuma, mpaka nikaona wivu. Basi ungeona wazungu walivyokuwa wanamtazama kwa mshangao ungecheka. Ila nilishuhudia baba fulani Mmarekani Mweusi akimtazama kwa furaha na kawa kama vile anamezea mate.

Nampenda sana mecheza sinema, Whoopi Goldberg. Nilikuwa nasoma jinsi akienda kwenye audition au akiwa kwenye movie shoot, wazungu wanamwambia kuwa ana matako makubwa au avae nguo ya kuzificha. Yeye alichoka, na mwishowe kusema, " Mimi ni mwanamke mweusi, nina matako makubwa niache kama nilivyo!" Wanawake weusi wote tungedai heshima ya matako kama Whoopi nadhani wazungu wangeheshimu matako yetu makubwa.

Tatizo linigine la kuwa na matako makubwa USA ni kupata nguo. Ukienda kununua sketi au gauni uanweza kukuta mbele refu nyuma umepanda. Au unavaa hiyo nguo lakini kwenye hips na matako haipiti! Hii ni kwa sababu nguo imeshonwa kwa ajili ya wazungu wenye matako fleti. Na kupata Jeans inayofiti ni vigumu. Mtu ambaye atatengeneza nguo 'molded for the black woman' atapata wateja kweli kweli, maana tunalilia nguo kama hizo.

Pamoja na yote haya sasa wazungu wameibuka na staili ya kuwa ka ka-butt. Yaani jeans inakuwa na pedi ndani kusudi mtu aonekana ana matako. Loh! Watu hawaridhiki! Sijui tuseme asante J-Lo (mwimbaji Jennfier Lopez) au nini. Kwanza walikuwa wanamcheka J-Lo na matako yake makubwa lakini naona watu wanaanza kuyapenda. Mpaka kuna opresheni sasa ya kuongeza matako.

Wacha wafanye haitapendeza kama matako natural tulyiozaliwa nayo waafrika.

Matako Makubwa Oyee!

Tuesday, September 25, 2007

Happy Anniversary Michuzi Blogu - Inatimiza Miaka Miwili


Leo blogu ya Michuzi inatimiza miaka miwili. Kama wengi wenu mnafahamu blogu ya Michuzi ilileta mapinduzi katika kublogu Tanzania.

Asante Michuzi kwa kazi unayofanya, picha unazopiga na HONGERA!


Waziri wa Ulinzi Prof. Kapuya apata ajali Tabora



UPDATE - Prof. Kapuya na majeruhi wengine wameletwa Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.

(Photo kushoto from Michuzi Blog)



Prof. Kapuya apata ajali

2007-09-25 Na Abubakary Mlawa,Jijini

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Profesa Juma Kapuya amepata ajali mbaya na hivi sasa madaktari wanapigana kufa na kupona kuokoa maisha yake.
Katika ajali hiyo, watu watatu wamefariki dunia na wawili kati yao inadaiwa ni mabodigadi wa Profesa Kapuya.

Ajali hiyo mbaya ilitokea jana majira ya saa 1:00 usiku katika kijiji cha Kaliua wilayani Urambo na kulihusisha gari la Profesa Kapuya, ambalo lilipasuka gurudumu la mbele la kulia kabla ya kupinduka.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Muhidin Mshihiri, amesema watu hao waliokufa wanasadikiwa kuwa askari wa Jeshi la Wananchi, JWTZ.

Akieleza ajali hiyo, Kamanda Mshihiri ambaye amezungumza na Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi, amesema Waziri Kapuya alikuwa katika ziara ya kulitembelea jimbo la Urambo ambalo yeye ni mbunge wake.

Amesema akiwa umbali mfupi kabla ya kufika nyumbani kwake, ndipo ajali hiyo mbaya ilipotokea.

Hata hivyo, Kamanda Mshihiri amesema bado hajapata majina ya watu waliofariki.

Imeelezwa kuwa wawili wamekufa papo hapo wakati mwingine alifikia hospitali. Kwa mujibu wa Kamanda Mshihiri, mbali na Profesa Kapuya ambaye amejeruhiwa, wengine waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo ni watu wanne, ambao wote walikuwa abiria katika gari la Waziri. Imeelezwa gari hilo lilikuwa na watu wanane wakati linapata ajali.
`Hadi usiku wa jana, Mheshimiwa Waziri (Kapuya) na majeruhi wengine walikuwa wakiendelea na matibabu,` amesema Kamanda Mshihiri.

Hata hivyo, Kamanda Mshihiri amesema wanaendelea kufuatilia ili kuwatambua waliofariki na kujua hali za majeruhi.
`Naelekea hospitali ili kuwatambua waliofariki na pia kujua hali ya Mheshimiwa Waziri ambaye hadi sasa sijafahamu amejeruhiwa kwa kiasi gani,` akasema Kamanda Mshihiri.
Habari zilizolifikia gazeti hili wakati linakwenda mitamboni zinasema kulikuwa na mpango wa kumhamishia Waziri Kapuya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Photo Zaidi za Moto Sea Cliff Hotel Mjini Dar es Salaam













Nimetumiwa hizi picha na msomaji P.K. wa Ohio. Asante P.K.
*********************************************************************************

Team to probe Sea Cliff fire
Dailynews ReporterDaily News; Monday,September 24, 2007

THE management of the Sea Cliff hotel which was on Saturday evening gutted by fire has assured the public that they would rebuild the hotel and resume business soon.
The Managing Director of the hotel, Mr Ketan Patel, said yesterday that currently the management was reorganizing, including calculating the loss caused by the fire, so that they can start rebuilding the hotel to continue with services.
Earlier, the hotel’s Deputy General Manager, Mrs Nadine Atallah said that the three-storey hotel with 92 rooms had 72 guests at the time of the incident but no one was hurt. Mrs Atallah said that some guests were shifted to Moven Pick hotel while the French Embassy and British High Commission assisted with others.
“We will be back. It will be bigger and better. We are yet to establish the extent of damage and loss but initial estimates are in billions of shillings,” explained Patel.
He made the comments shortly after the Vice President, Dr Ali Mohamed Shein, toured the wreckage at what remains of the famed tourist hotel at Masaki Peninsula in Dar es Salaam. Kinondoni Regional Commander (RPC), Mr Jamal Rwambow, who has been at the scene since the fire broke out, and the hotel’s General Manager, Mr Kelvin Stender, could not establish cause of the fire.
They, however, said that they both suspect the fire was caused by an electric fault that started at the boiler room in the kitchen. The hotel’s, insisted that they will resume business soon because they had been fully insured. She would give further details about the insurance.
“Right now we are under the pressure and I cannot get into details about the insurance coverage but I must assure you that we are insured,” said Atallah. She also told this paper that all employees will continue to be in employment and no one would be affected by the devastation caused by the fire. Atallah said that even though the hotel was completely burnt, there were other activities to be taken care of by employees including business at the remaining buildings that did not catch fire.
The fire has completely destroyed the main part of the hotel except for a small wing on the Sea Cliff village that accommodates shops, restaurants and a gym. According to Mrs Atallah, more than 60 percent of the hotel has been completely destroyed.
Meanwhile the Vice President Dr Ali Mohamed Shein has said that the government was shocked by the incident because it has not only caused huge economic loss to the owners but also to the government. He said that the hotel used to accommodate various tourists who were visiting the country as well as international conferences.

Monday, September 24, 2007

Unapoguswa Gusika


Nimepokea hii shairi kwa E-mail. Ila haisema mtunzi ni nani.

Unapoguswa Gusika

Mtunzi?

Wengine hupenda chungulia, miguso isowahusu,
Na macho huyatoa kama mijusi, waonapo miguso,
Na sio tabia nzuri, kuchungulia yasowahusu,
Ni sharia ya mguso, unapoguswa gusika!!


Wawili wapendanapo, si ajabu kugusana,
Popote pale walipo, wazee hata vijana,
Ije mvua na upepo, mikono watashikana,
Fumbo kubwa la mguso, unapoguswa gusika!!


Wengine wanashituka, pale wao wanaguswa,
Pembeni wakaja ruka, kama wamekoswa koswa,
Wakabakia kucheka, hawajui la kupaswa,
Ni utamu wa mguso, unapoguswa gusika!!


Wapo wapenda mgongo, wakakigusa kiuno,
Kwa mbwembwe na kwa maringo, wakikenua na meno,
Wamejawa na usongo, yamewatoka maneno,
Mtetemo wa mguso, unapoguswa gusika!!


Wapo wapenda kifua, wakaligusa na tumbo,
Lengo lao twalijua, wanaamsha majambo,
Haraka wakipumua, utadhania mgambo,
Ladha kubwa ya mguso, unapoguswa gusika!!


Wapo wependa kugusa, visoguswa hadharani,
Wakayafanya makosa, wakajaitwa wahuni,
Mkitaka kuvigusa, mjifunguie chumbani,
Ni fahari ya mguso, unapoguswa gusika!!


Uguse aliye wako, karibu mshikilie,
U mguse atakako, asije akachukie,
Wa mwenzako huyo mwiko, tamaa usiwakie
Siri kubwa ya mguso, unapoguswa gusika!!


Ninawasihi wenzangu, msiogope kugusa,
Ni kipaji chake Mungu, ukiguswa nawe gusa,
Ukaondoa machungu, na machozi kupangusa,
Ni uhondo wa mguso, unapoguswa gusika!!

Sunday, September 23, 2007

Msikilize Kaka Ndesanjo Macha




DIGITAL CITIZENS


The second Digital Citizen Indaba took place on September 9, 2007 at Rhodes University in Grahamstown, South Africa. Discussions during the Indaba centered on issues of blogging, cyber-activism, language and identity. The first Indaba, which took place last year, provoked a heated debate about the racial composition of participants.

Ndesanjo Macha, a blogger and writer from Tanzania gave a Keynote adress on ' The Emergence of the Digital Citizen'.

************************************************************************

Kaka Ndesanjo Macha ndiye alinipa motisha ya kuanza ku-blogu.

Hivi karibuni alikuwa Keynote Speaker kwenye mkutano kuzungumzia habari ya internet na mablogu katika dunia ya leo. Mkutano ulifanyika Afrika Kusini.

Kaka Ndesanjo ana blogu yake JIKOMBOE. Unaweza kusoma habari zaidi za huo mkutano kwenye blogu yake. http://jikomboe.com/

Saturday, September 22, 2007

Bongoland II



Kwa habari zaidi za Bongoland II nenda:

KIBIRA FILMS
http://www.kibirafilms.com/index.html

Hoteli ya Sea Cliff Yaungua Moto Dar!


(Photo from Michuzi Blog)

Hoteli ya Sea Cliff umeungua moto usiku wa kuamkia leo.

Kwa habari zaidi nendendi Michuzi Blog.

Trailer ya Bongoland II sasa iko You Tube












Haya sasa! Mlio na kiu ya sinema ya Bongoland II - Nyumbani ni Nyumbani mnaweza kuona


Friday, September 21, 2007

Ubaguzi wa rangi bado upo Marekani


Hii picha hapo juu haijapigwa mwaka 1960. Umepigwa usiku wa kuamkia leo huko Louisiana!
Vijana wa kizungu walikuwa wanazunguka na hiyo pick-up enye 'noose' (kamba ya kunyonga watu weusi) katika mitaa ya Alexandria, Louisiana.
Weusi wengi walifika katika huo mji baada ya maandamano makubwa ya weusi kudai haki kwa ajili ywa vijana wa shule sita waliofungwa jela zaidi ya miezi tisa huko Jena, Louisiana. Walikuwa wanangojea mabasi ya kurudi makwao ndo hao vijana walianza kuwapita na kuwatishia! Polisi walikamata hiyo gari na vijana wa kizungu waliokuwemo. Vijana hao walisema kuwa wao pamoja na familia zao wako katika kile kikundi cha kigaidi hapa Marekani Ku Klux Klan (KKK). Hao KKK wameua maelefu na maelfu ya watu weusi Marekani bila kuchukuliwa hatua yoyote!
History ya Marekani kwa watu weusi ni mbaya na bado wanazidi kuonewa. Wanaume weusi wengi wamefungwa gerezani. Weusi wanapata elimu duni na pia wanabaguliwa hata katika kazi!

Kwa habari zaidi ya hiyo tukio someni:

Thursday, September 20, 2007

Mwivano Kupaza alivyouliwa na Ndugu yake Wisconsin


Marehemu Mwivano Kupaza

Polisi reconstruction ya uso wa marehemu


Muaji Peter Kupaza


Jana niliangalia Documentary kwenye Discovery Channel kuhusu jinsi wataalam wa forensics walivyo gundua kuwa vipande vya maiti yaliotupwa kwanye mto huko Wisconsin yalikuwa ya marehemu Mwivano Mwambashi Kupaza.

Nadhani baadhi yenu mnakumbuka pilipilika za wakati ule miaka ya 1999/2000. Kwa wasiojua nitawasimulia kwa kifupi mambo yalivyokuwa.

Mama moja mzungu na watoto wake walienda kufanya picnic kando ya mto. Walikuta vipande vya maiti vimetupwa ndani ya mifuko ya takataka. Waliita polisi. Polisi walishangaa mambo waliokuta. Maiti ilikuwa imechunwa ngozi, maiti imekatwa katwa viapnde kitaalamu hasa, lakini wali kuta kipande chenye nywele na kujua kuwa ni maiti ya mwanamke mwenye asili ya Afrika.

Polisi walichunguza database zao za watu ambao wamepotea. Hawakupata kitu waligonga ukuta.

Waliomba msaada wa wataalam wa forensics kusudi wajue huyo mwanamke alikuaje. Hata fuvu (skull) yake ilikuwa imebomolewa lakini waliweza kuijenga kwa kutumia kompyuta. Baada ya hapo walipeleka kwa mtaalamu wa kujenga uso (facial reconstruction) ndo ikapatikana ile picha ya juu enye picha nne.

Polisi huko Wisconsin walisambaza hiyo picha sehemu nyingi na katika vyomboa ya habari. Ndo mke wa Peter Kupaza na waTanzania wengine walipiga simu polisi na kusema kuwa hiyo picha inafanana na Mwivano Kupaza. Pia mke wa Peter alimwambia kuwa huko Tanzania mume wake aliwahi kufanya kazi kama bucha na alimsimulia sana jinsi ya kuchinja mnyama na kumchuna ngozi. Hapo sasa Peter kawa suspect namba moja. Polisi waliwahoji sana waTanzania huko Wisconsin wakati huo.

Polisi walimfuata Peter nyumbani kwake. Kwanza Peter alidai hamjui Mwivano. Baadaye alisema kuwa alirudi Tanzania na jamaa anaitwa Shadrack lakini hajui jina lake la pili eti. Polisi wa Wisconsin walipiga simu Tanzania na kuambiwa kuwa Mwivano bado yuko Marekani.

Sasa ingawa Peter walimshuku walishindwa kumkamata kwa sababu walikuwa bado hawana uhakika kuwa hiyo maiti ni ya Mwivano. Wakati huo Peter alikuwa anafanya kazi kama 'Employment and job-training counselor for the Wisconsin Department of Labor and Human Relations'. Alivyondoka Tanzania alikuwa mwalimu.

Polisi walijua wasipokuwa wajanja kesi itaishia hewani. Walichukua mbwa wa kunusa nusa (sniffer dog) na aligundua damu chini ya mabao bafuni. Walifanya DNA Test na kugundua kuwa damu ni ya Mwivano. Lakini hiyo haikutosha kumkamata Peter. Kilichohakikisha kuwa maiti ni ya Mwivano ni kuwa Peter alimpeleka kliniki kutoa mimba! Hiyo mimba ilikuwa ni ya Peter. Kumbe Peter alimgeuza ndugu yake mke mdogo. Mwivano alivyosign ile fomu ya kutoa mimba aliacha fingerprint. Ndo fingerprint hiyo waliomechisha na fingerprint kwenye maiti. Na mimi nasema roho ya kile kichanga kilichouliwa pale kliniki ndo kilimponza Peter Kupaza!

Peter alikamatwa na kesi ilipelekwa mahakamani. Huko mahakami Peter alidai kuwa Mwivano aliuliwa na mwanaume wa kizungu. Peter amefungwa maisha gerezani. Lakini jamaa alivyo mshenzi alijaribu kukata rufaa. Lakini hataachiwa. Huyo Peter Kupaza ataoza gerezani na kwa sasa ni moja wa wake wa Big Bubba huko.

Mungu amlaze roho ya Mwivano Kupaza mahali pema mbinguni. Amen.

* Kwa wasiofahamu mke wa Peter Kupaza, Shari Goss, anaigiza katika sinema ya TUSAMEHE!


KWA HABARI ZAIDI ZA MAUAJI YA MWIVANO KUPAZA SOMA:

Killing Cousins


Rebuilding victim's face key to arrest in killing

http://www2.jsonline.com/news/state/feb00/body03020200a.asp?format=print

Appeal ya Peter Kupaza 2006 (Mshenzi anataka aachiwe huru)

http://caselaw.lp.findlaw.com/scripts/getcase.pl?court=wi&vol=wisctapp2%5C2006%5C2005ap000101&invol=1

WISCONSIN VS. PETER KUPAZA

Wednesday, September 19, 2007

Sinema mpya - Pink Panther 2 - Nimo!




Jana nilifanya kazi kama background extra katika sinema ya Pink Panther 2. Stars wake ni Steve Martin, Jean Reno, Andy Garcia na Aishwarya Rai.

Sehemu kubwa ya hiyo sinema inapigwa mjini Boston. Boston Convention Center iligeuzwa kuwa uwanja wa ndege ya Charles De Gaulle -Paris. Set ilikuwa safi sana utadhani uko Ufaransa kweli, ila watu walikuwa wanaongea English.

Mimi nilikuwa Msafiri wa kiAfrika pamoja na akina mama wengine watatu. Niliambiwa niijifanye nimechelewa ndege halafu nikimbie ndani na kukutana na hao wengine walio kuwa ndani. Mbona extras wengine walinionea wivu! Ujue kupewa 'direction' katika sinema ya Hollywood kama wewe ni extra ni kitu kikubwa. Nangojea kuona kama nitaonekana kwenye sinema au vipi.

Steve Martin alinipita mara kadhaa. Alikuwa na make-up nyingi usoni, kiasi kwamba alionekana kama kavaa mask. Kwa vile ni star, alikuwa na stand-in na stunt man. Stand-in anafanya kazi wakiwa wanafanya scene set up. Stunt man anafanyakazi kama kuendesha gari ovyo, kukimbia, kuruka ukuta nini. Ama kweli wanatumia hela nyingi kwenye sinema za Hollywood. hako kagari kadogo kalikuwepo. Watu walikuwa wanapita barabarani na kuishangaa.

Bahati mbaya walitupiga maaruku kupiga picha za kumbukumbu.

Kwa habari zaidi za sinema ya Pink Panther 2, nenda:


Monday, September 17, 2007

Please Stay Tuned




STAY TUNED FOR MORE ON JOSIAH KIBIRA's NEW FILM BONGOLAND II!


Michuzi ameanzisha Site Mpya - Tanzania Times

DEAR FRIENDS

I AM PROUD AND PLEASED TO INTRODUCE YOU TO http://www.tztimes.com/ THE PORTAL FOR MODERN TIMES TANZANIA WHOSE MOTTO IS TO BE ONE STEP AHEAD IN AS FAR AS NEWS ABOUT TANZANIA, THE DIASPORA AND ANY OTHER THAT IS RELEVANT TO TANZANIA AND HER PEOPLE IS CONCERNED.

BASED ON A THREE YEAR RESEARCH IT HAS COME TO OUR REALISATION THAT SO FAR VERY FEW OUTLETS ATTEMPT NOT ONLY TO GATHER NEWS AND IMAGES OF HAPPENINGS BUT ALSO MOST ARE LATE IN DISSEMINATING IT TO CONSUMERS. OUR RESOLVE IS TO FILL THAT VACCUM.

OF COURSE, THIS IS NOT AN OVERNIGHT UNDERTAKING THAT WOULD BE PERFECTED IN NO TIME, RATHER IT IS THE FIRST STEP TOWARDS A LONG SAFARI WHOSE DESTINATION IS WHERE ALL NEWS CONSUMERS WORLDWIDE ARE. THEREFORE, AT THE OUTSET ALLOW ME TO SAY THAT WHATEVER GLITCH ENCOUNTERED IS NOT INTENTIONAL NOR A NORM BUT AN ATTEMPT TO ATTAIN PERFECTION. WE THEREFORE WELCOME VIEWS, CRITICISIM AS WELL AS NEWER IDEAS THAT WOULD HELP US THRIVE.

YOU ARE ALSO WELCOME TO CONTRIBUTE NEWS, IMAGES AND VIEWS IN ANY OF THE SUBJECTS AVAILABLE IN http://www.tztimes.com/ INITIALLY IN VOLUNTARY BASIS AND WHEN THE TIME IS RIPE WE CAN NEGOITIATE TERMS DEPENDING ON RELIABILITY AND CREDIBILITY OF MATERIAL SENT.

YOU WILL NOTE THERE IS A VIDEO COMPONENT WHICH WE ARE POISED TO FILL WITH STUFF THAT ARE RELEVANT. THAT AND OTHER PARTS ARE STILL WORKED ON AND AFTER THIS TRIAL PERIOD IS OVER, AND WHICH WE PLAN TO MAKE IT AS SHORT AS POSSIBLE, SAY TWO WEEKS, WE SHALL HAVE WHAT YOU HAVE BEEN CRAVING FOR IN TERMS OF LOCAL VIDEO CLIPS.

WITH A VIEW TO CATER FOR A WIDER AUDIENCE THE LANGUAGE USED IS BOTH KISWAHILI AND ENGLISH.

NEED I SAY MORE?

THANK YOU,

SINCERELY

MUHIDIN ISSA MICHUZI
MANAGING DIRECTOR
EMEDIA (T) LIMITED

Thursday, September 13, 2007

Ujumbe kutoka Kaka Lazurus Mbilinyi 'Mawaidha kuhusu Ndoa'

Wapendwa wasomaji nimepata ujumbe huo kutoka kwa Kaka Lazarus Mbilinyi ambaye aliandika somo la NDOA NA UNYUMBA ambayo umeisoma kwenye blog hii:

http://swahilitime.blogspot.com/search/label/Mbilinyi

**************************************************************************
Dada Chemi,

Mimi ndo Lazarus Mbilinyi niliyeandaa hilo somo la ndoa na nyumba na kwa bahati mbaya nilikuwa sijui kama linaweza kusomwa na mtu yoyote kwani katika kuliandaa niliandaa katika mazingira ya Tanzania na hasa vijijini na sehemu ambazo mwanamume anafanya kazi (ameajiriwa) na mwanamke ni mama wa nyumbani (anayejishughulisha na kazi zingine) na pia limeegemea zaidi katika familia za kikristo.

Naamini maoni ninayopata kutokana na hilo somo basi nitayafanyia kazi na kama inawezekana siku nyingine nitoe kitabu cha Ndoa na nyumbaHata hivyo nashukuru sana kwa kueneza ujumbe kwa watu wote ili wajue ndoa ni nini hilo nashukuru.

Kwa sasa nipo Canada kwa ajili ya shule niemfika hapa tarehe 1 Sept 2007 na naamini tutazidi kuwasiliana na pia nimsomaji wa blog yako kwa muda mrefu.

Asante sana kwa kazi njema ya kuelimisha jamii:

--
Lazarus P. Mbilinyi

Hongera Mr. & Mrs. Mroki


Mpiga picha wa magazeti ya serikali Daily News na Habari Leo, Mroki Mroki aka Father Kidevu, amefunga pingu za maisha, na Bi Deborah Fute, wikiendi iliyopita.

Hongera Mr. & Mrs. Mroki. Nawatakia maisha mema. Zaeni matunda mema.

WaKenya Wana Mapafu Makubwa

MKenya Robert Cheruiyot aliyeshinda Boston Marathon mara tatu

Wikiendi iliyopita walifanya Block Party kwenye mtaa wetu. Ni mkusanyiko wa majirani na hasa nafasi ya kujuana zaidi.

Basi, kuna Bibi kizee wa kizungu alinishangaza sana. Aliposikia kuwa natoka Africa alisema, waKenya wanashinda Marathon kwa sababu wana mapafu makubwa (big lungs)! Nikamwuliza alikuwa na maana gani. Bi Kizee yule alisema na nanukuu " Wana mapfu makubwa kuliko watu wote kwa vile wanakimbia kwenye milima ya Serengeti"

Duh! Mbona niliblow! Nikamwambia kwanza waKenya na waafrika kwa ujumla wana mapafu sawa na bindamu wa rangi nyingine. Pili, Serengeti iko Tanzania na siyo Kenya. Tatu, ni mbuga ya wanyama watu hawakai huko. Ila watalii wanaenda na kukaa kwenye mhoteli ya fahari huko. Lakini yule bibi alinibishia. Alisema waKenya wanakimbia kwenye milima ya Serengeti tokea wadogo na ndo maana mapafu yao yanakuwa makubwa.

Na mimi nikwamwuliza kwa nini wazungu wakienda kwenye mbuga ya wanyama na wanaambiwa wasiguse hawasikii. Nikamwambia mzungu ataona nyoka, anasema, yule nyoka mzuri kweli, halafu atajaribu kumkamata na kucheza naye. Nexti unsikia mzungu kaumwa na huyo 'nyoka mzuri' na kafa. Au anaambiwa asimshike Tembo yule japo anaonekana mpole. Wanaenda kumshika na Tembo anamwua mzungu na mapembe yake.

Hapo yule mzungu alisema, kweli nakubali kuwa kuwa wazungu ambao ni wajinga na hawasikii. Halafu aliamua kuondoka na kjuongea na watu wengine. Na mimi nilishukuru maana hasiri zilikuwa zinaanza kunipanda.

Na mjue zamani kabla wafrika hawajaanza kushinda Marathon mara kwa mara wazungu walikuwa wanasema kuwa waafrika hawawezi kushinda hata siku moja. Walisema eti waafrika wameumbwa kukimbia mbio fupi, lakini mbio ndefu hawawezi!
Sasa mtoto akisikia hizo habari potofu anakuwa nazo. Kama hamjasikia kuna kampeni ya kupiga vita waKenya wasikimbie hiyo Boston marathon kwa vile wanashinda mara kwa mara.