Thursday, September 20, 2007

Mwivano Kupaza alivyouliwa na Ndugu yake Wisconsin


Marehemu Mwivano Kupaza

Polisi reconstruction ya uso wa marehemu


Muaji Peter Kupaza


Jana niliangalia Documentary kwenye Discovery Channel kuhusu jinsi wataalam wa forensics walivyo gundua kuwa vipande vya maiti yaliotupwa kwanye mto huko Wisconsin yalikuwa ya marehemu Mwivano Mwambashi Kupaza.

Nadhani baadhi yenu mnakumbuka pilipilika za wakati ule miaka ya 1999/2000. Kwa wasiojua nitawasimulia kwa kifupi mambo yalivyokuwa.

Mama moja mzungu na watoto wake walienda kufanya picnic kando ya mto. Walikuta vipande vya maiti vimetupwa ndani ya mifuko ya takataka. Waliita polisi. Polisi walishangaa mambo waliokuta. Maiti ilikuwa imechunwa ngozi, maiti imekatwa katwa viapnde kitaalamu hasa, lakini wali kuta kipande chenye nywele na kujua kuwa ni maiti ya mwanamke mwenye asili ya Afrika.

Polisi walichunguza database zao za watu ambao wamepotea. Hawakupata kitu waligonga ukuta.

Waliomba msaada wa wataalam wa forensics kusudi wajue huyo mwanamke alikuaje. Hata fuvu (skull) yake ilikuwa imebomolewa lakini waliweza kuijenga kwa kutumia kompyuta. Baada ya hapo walipeleka kwa mtaalamu wa kujenga uso (facial reconstruction) ndo ikapatikana ile picha ya juu enye picha nne.

Polisi huko Wisconsin walisambaza hiyo picha sehemu nyingi na katika vyomboa ya habari. Ndo mke wa Peter Kupaza na waTanzania wengine walipiga simu polisi na kusema kuwa hiyo picha inafanana na Mwivano Kupaza. Pia mke wa Peter alimwambia kuwa huko Tanzania mume wake aliwahi kufanya kazi kama bucha na alimsimulia sana jinsi ya kuchinja mnyama na kumchuna ngozi. Hapo sasa Peter kawa suspect namba moja. Polisi waliwahoji sana waTanzania huko Wisconsin wakati huo.

Polisi walimfuata Peter nyumbani kwake. Kwanza Peter alidai hamjui Mwivano. Baadaye alisema kuwa alirudi Tanzania na jamaa anaitwa Shadrack lakini hajui jina lake la pili eti. Polisi wa Wisconsin walipiga simu Tanzania na kuambiwa kuwa Mwivano bado yuko Marekani.

Sasa ingawa Peter walimshuku walishindwa kumkamata kwa sababu walikuwa bado hawana uhakika kuwa hiyo maiti ni ya Mwivano. Wakati huo Peter alikuwa anafanya kazi kama 'Employment and job-training counselor for the Wisconsin Department of Labor and Human Relations'. Alivyondoka Tanzania alikuwa mwalimu.

Polisi walijua wasipokuwa wajanja kesi itaishia hewani. Walichukua mbwa wa kunusa nusa (sniffer dog) na aligundua damu chini ya mabao bafuni. Walifanya DNA Test na kugundua kuwa damu ni ya Mwivano. Lakini hiyo haikutosha kumkamata Peter. Kilichohakikisha kuwa maiti ni ya Mwivano ni kuwa Peter alimpeleka kliniki kutoa mimba! Hiyo mimba ilikuwa ni ya Peter. Kumbe Peter alimgeuza ndugu yake mke mdogo. Mwivano alivyosign ile fomu ya kutoa mimba aliacha fingerprint. Ndo fingerprint hiyo waliomechisha na fingerprint kwenye maiti. Na mimi nasema roho ya kile kichanga kilichouliwa pale kliniki ndo kilimponza Peter Kupaza!

Peter alikamatwa na kesi ilipelekwa mahakamani. Huko mahakami Peter alidai kuwa Mwivano aliuliwa na mwanaume wa kizungu. Peter amefungwa maisha gerezani. Lakini jamaa alivyo mshenzi alijaribu kukata rufaa. Lakini hataachiwa. Huyo Peter Kupaza ataoza gerezani na kwa sasa ni moja wa wake wa Big Bubba huko.

Mungu amlaze roho ya Mwivano Kupaza mahali pema mbinguni. Amen.

* Kwa wasiofahamu mke wa Peter Kupaza, Shari Goss, anaigiza katika sinema ya TUSAMEHE!


KWA HABARI ZAIDI ZA MAUAJI YA MWIVANO KUPAZA SOMA:

Killing Cousins


Rebuilding victim's face key to arrest in killing

http://www2.jsonline.com/news/state/feb00/body03020200a.asp?format=print

Appeal ya Peter Kupaza 2006 (Mshenzi anataka aachiwe huru)

http://caselaw.lp.findlaw.com/scripts/getcase.pl?court=wi&vol=wisctapp2%5C2006%5C2005ap000101&invol=1

WISCONSIN VS. PETER KUPAZA

22 comments:

MOSONGA RAPHAEL said...

Chemi,
Samahani naomba nikurekebishe kidogo kuhusiana na maelezo yako chini ya (picha iliyochorwa na polisi) ya marehemu.

Ni:
'Polisi reconstruction ya uso wa marehemu' (sio uso wa maiti!!!)

Chemi Che-Mponda said...

Okay, asante kwa marekebisho. Ila niliona kuwa wakati huo walikuwa bado hawajajua ni nani.

Anonymous said...

Duh unyama huu wa binadamu.

Huyu Peter Kupaza angekuwa mkenya watu (pamoja na wewe chemi) mngesema "ooh! kweli wakenya si watu"

Haya sasa m-bongo huyo.

Je! wabongo si watu?

Anonymous said...

Lakini sasa huyu mwivano naye inakuwaje alikubali kupigwa miti na kaka yake?
Mambo mengine yanashangaza jamani. Kweli kaka yake ni mnyama, lakini! "it takes two to tangle".

Huyu mwivano naye (mungu amweke pema) kenge pia.

Chemi Che-Mponda said...

Walisema alikuwa ana bakwa usiku. Sijui lakini sikuwepo. Majungu niliyosikia kipindi kile, Shari aliwafukuza alipogundua nini inatokea. Walikuwa wanakaa pamoja kwenye hiyo fleti lakini Mwivano alikuwa hafanyi kazi na bills zote juu ya Peter.

Mungu na shetani waanajua kilichotokea huko.

Huyo Peter Kupaza ni MBongo na ni Mnyama na mshenzi pia. Hasthili hata kuitwa bindamu. Mpaka amekuwa case study hapa USA. Hebu fanya web search muone mpaka criminal profile yake.

Anonymous said...

Da Chemi asante sana kwa habari motomoto ila punguza kidogo hukumu Bado anastahili kuitwa mwanadamu. Shetwani lilimpanda lakini anasameheka. Atubu katika Jina la Yesu Kristo ataiona mbingu.

Nimepita kijijini kuona kama umetoa maoni yeyote juu ya hayo maandamano ya watu weusi dhidi ya double standards mahakamani.Siju ni State gani.

Nakutakia Siku njema

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 11:06am,

Nadhani unazungumzia kesi ile ya Jena 6 ya huko Louisiana. Inasikitisha kweli kuwa mwaka 2007, bado mambo ya ubaguzi wa enzi zile (Jim Crow)bado upo Marekani. Na waMarekani wanadai ndo polisi wa dunia. Wanahukumu nchi zingine zenye ubaguzi kumbe upo hapa hapa!

Anonymous said...

Kumpiga miti dadaako, au kupigwa miti na kakaako huu wote ni ushenzi na ukosefu wa miiko. Inawezekana kabisa hawa walikuwa wanapigana miti kwa makubaliano. Kama alikuwa anabakwa, huwezi kubakwa kila siku na ukakaa kimya tuu. Labda alikuwa anaiegesha kwa makusudi katika staili ya kaka "akinitongoza simpi lakini akinibaka nampa".

Wote wawili hawa wanastahili yaliyowakuta. Nyau hawa.

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 11:23am,

Hatuwepo huko, hatujui nini ilikuwa inatendeka. Marehemu alikuja Marekani kusomea Kiingereza Wisconsin English as a Second Language Institute huko Madison. Huenda hakujua kuwa kuna sehemu za kwenda kama anabakwa hivyo alivumilia. Huenda alikuwa na uoga kuwa kaka anaweza kumtendea mabaya akisema. Huenda alimwambia kuwa atamshitaki polisi ndo maana Peter aliamua kumwua...hatuwezi kujua.

Anonymous said...

huyo alikuwa kaka yake wa damu au binamu yake? maana binamu makabila mengine wanaita nyama ya hamu au nyama choma ila kama ni kaka yake kabisa hiyo ni mbaya sana ingawa hata binamu siisupport

Anonymous said...

hii kesi naikumbuka kipindi kila kla ukishika nipashe cha kwanza ni hicho!!ila hapo dada chemi umeongea!inawezekana kuwa hakuwa na la kufanya na alipozidiwa na kutaka kusema ndio akanyamazishwaaa!!kesho kiyama kuna kazi!!

Anonymous said...

Kwakweli inasikitisha sana

Egidio Ndabagoye said...

Duh! kuna watu balaa sana.Hivi inakuwaje mtu unamgeuza mwenzio bucha?
Inasikitisha kweli,hii kesi naikumbuka ila sikufatilia hatima ya Peter.

Anonymous said...

eeeh Mola wangu ilaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Nimesoma kwa masikitiko sana habari hiyo.

Kwa maoni yangu haijalishi marehemu aliridhia au alibakwa,ukweli unabaki pale pale.Kitendo alichokitenda huyo bwana pita sio cha kibinaadamu kabisa.

MWENYEZI MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.AMINA.

Anonymous said...

dada chemi nashukuru sana kw ahii information duh wabongo wengine ni makenge kweli huyu jamaa ni mbwa kweli wacha wamlambe kiboga uko gerezani arudi hapa anajamba jamba shenzi sana kw anini ukatili maisha ya kiumbe mwenzio hivi hivi ? uchi upewe bado na kuuwa uue inatia uchungu sana.

Anonymous said...

Du, inasikitisha kweli!hivi huyu ndiye yule Peter Kupaza aliyesoma Lutheran Junior Seminary Morogoro (nilikuwa nampiga chenga sana kwenye kale ka-uwanja pinde?) au namchanganya maana naona hata sura kama ni yake hivi. Samahani kama ni majina tu kufanana.
Vyovyote vile kumuua mwanadamu mwenzako ni hukumu ya hapa duniani na mbinguni.
Chemi sijaelewa vizuri ebu tueleze kidogo, huyo ex-wife wa Kupaza (Muigizaji) waliachana kwa ajili ya huyu dada marehemu au? samahani nimekuwa mvivu wa kufuatilia story yote kila sehemu mambo yao yalipoandikwa! nataka nami kuanza uforensiki blogu wangu juu ya kesi hii!!

Anonymous said...

Kupaza nasikia alikuwa anapenda kupiga TIGO
Kupaza ni firauni mkubwa sana,kwanini utoe ngozi
nimekasirika sana sana
na huyu Marehemu alikuwa anamakosa,kwanini akukubali ngono na binamu?,angerudi bongo

Anonymous said...

Huyo Peter alisoma Seminary na huyo mke wake mzungu alikuwa Missionary huko Bongo. Peter hakuridhika na mavitu aliyokuwa anapewa kutoka kwa mzungu ndo maana aliamua kuvunja mila na kutembea na ndugu yake. Aibu. Peter alikuwa na kazi ya maana kufanya kazi State siyo mchezo. Shauri zake, kama Da'Chemi anayosema Peter ni moja wa wake wa big Bubba sasa. Wacha aliwe. Ukimwona sasa anatembea kama mwanamke.

Anonymous said...

Jamani! Da'Chemi hajakosea. Peter Kupaza ni MNYAMA hasa. Mjue miguu ya Mwivano hayajapatikana hadi leo!

We also observe that the evidence supporting Kupaza's conviction for hiding Mwivano's corpse likewise provides support for the jury's finding that Kupaza caused Mwivano's death. See State v. Bettinger, 100 Wis. 2d 691, 698, 303 N.W.2d 585 (1981) (" vidence of criminal acts of an accused which are intended to obstruct justice or avoid punishment are admissible to prove a consciousness of guilt of the principal criminal charge."). Not only did Kupaza attempt to hide Mwivano's corpse by disposing of it in a river, he went through a great deal of trouble to impede identification of Mwivano's body. In gruesome fashion, Kupaza cut Mwivano's body into pieces and disposed of those pieces separately in the river. In fact, her feet were never found. Kupaza removed the skin from her skull, making identification extremely difficult. The jury could have inferred that the mutilation of Mwivano's body was also intended to obscure the cause of her death. Indeed, the pathologist was unable to determine the cause of death.

Anonymous said...

Mungu ailaze roho ya Mwivano mahali pema peponi, Amina..nimefurahi kusikia huyo muuaji yuko jela.
Kwa kifupi, wengine mmemsema kuwa Mwivano naye ana makosa, ni mjinga n.k mimi kutokana na experience yangu nawaambia hivi: nilikuja nchi za nje, nikiwa nina wenyeji wangu wawili tu(sio ndugu zangu), basi watakalosema wao ndio hilohilo naliamini kwa maana sina ujanja mwingine, walinibania sana,,niliwaheshimu na kuwasikiliza sana, mpaka baadae nilipoanza kufunguka macho kuwa wenzangu hawakutaka nizoeane na watu wengine nisije nikawa mjanja zaidi, wao walikaa miaka mingi wakawa maisha bado magumu sana,na hata degree hawajazimaliza,,, hivi hawakutaka nije tu nyuma yao na niwazidi,,ndio wakawa wananibania,we umekuja juzi tu huwezi pewa nyumba bado, nilikuja kuamka baada ya kwenda shuleni na kibaruani, kukutana na watu katika kuongeaongea ndio unasikia kuwa hapa kuna sheria hii na hii, we una kibali cha kukaa hapa una haki hizi na zile, ndipo nilianza kufunguka macho na kujitahidi kwa bidii kusonga mbele sasa,,na nilipoanza kupiga hatua, wenyeji wangu hawakupendelea kabisa, bahati nzuri nilikuwa nishapata kibarua na nyumba pia hivyo nikaanza kujitegemeea,ikabakia kuheshimiana tu..fikiria mtu amekaa kwenye nchi miaka 6 kabla yako anakuambia eti shauri yako we jifanye tu unakazania shule sijui nani atakulisha,vibarua vizuri vyote viko asubuhi,,, nikaja kuambiwa mitaani na wengine kuwa watu kibao hapa wanasoma na kufanya kazi za jioni, huyo hataki usome wewe,,huyo mdada amenikazania tukae wote, ufanye kazi, wacha mi nisome nikikaribia kugraduate ndo nawewe ukazanie shule,,yaani mambo kibao,na nilipowaambia nimesaidiwa na watu nimepata kibarua cha jioni pia nimepata nyumba, wacha nisemwe,,sisi tumekupokea hapa, halafu unajifanya umewapata watu wa kukusaidia kupata vibarua n.k na blabla bla nyingi, nakuambiwa nilikasirikiwa haswa,, KWA KIFUPI, mi naweza kuthubutu kusema, Mwivano, alikuwa na heshima kwa mwenyeji wake(kumbukeni mtoto wa watu katoka nyumbani na maadili yake)hivi alimheshimu na kumsikiliza lolote analosema nduguye, na kuna zile za kuambiwa ukileta ushenzi ntakurudisha bongo, na kama hivyo unasikia alikuwa hafanyi kazi mtoto wa watu analipiwa bills zote, unataka kuniambia Peter alishindwa kumtafutia kibarua huyo binti, hata cha baby sitting,,nyie msalieni mtume jamani, mimi binti wa watu kama vile namuona alivyokuwa anatishwa na kutawaliwa na nduguye na alipoanza tu kuleta mdomo kuwa nitasema kwa ndugu au ntaenda kukushtaki mahali flani, ndo alipouwawa nahisi.Anyway, wote hatujui vizurti, ni assumptions tu.

Anonymous said...

Na huko kwao kwa huyo Peter Kupaza kama kuna missing persons au aunsolved murders. Huenda Peter alianza kuua watu tok Tanzania.

Deogratius A. Lyakurwa said...

tumepewa assignment ya kusoma hii kesi mara ya kwanza nilisoma iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ilikuwa inanichanganya sana, lakini baada ya hii nimepata kila kitu kwa ufasaha AKHANTE SANA, nadhani ni njia nzuri ya kusaidia wanafunzi wa SHERIA wanaozungumza KISWAHILI.