Thursday, September 13, 2007

WaKenya Wana Mapafu Makubwa

MKenya Robert Cheruiyot aliyeshinda Boston Marathon mara tatu

Wikiendi iliyopita walifanya Block Party kwenye mtaa wetu. Ni mkusanyiko wa majirani na hasa nafasi ya kujuana zaidi.

Basi, kuna Bibi kizee wa kizungu alinishangaza sana. Aliposikia kuwa natoka Africa alisema, waKenya wanashinda Marathon kwa sababu wana mapafu makubwa (big lungs)! Nikamwuliza alikuwa na maana gani. Bi Kizee yule alisema na nanukuu " Wana mapfu makubwa kuliko watu wote kwa vile wanakimbia kwenye milima ya Serengeti"

Duh! Mbona niliblow! Nikamwambia kwanza waKenya na waafrika kwa ujumla wana mapafu sawa na bindamu wa rangi nyingine. Pili, Serengeti iko Tanzania na siyo Kenya. Tatu, ni mbuga ya wanyama watu hawakai huko. Ila watalii wanaenda na kukaa kwenye mhoteli ya fahari huko. Lakini yule bibi alinibishia. Alisema waKenya wanakimbia kwenye milima ya Serengeti tokea wadogo na ndo maana mapafu yao yanakuwa makubwa.

Na mimi nikwamwuliza kwa nini wazungu wakienda kwenye mbuga ya wanyama na wanaambiwa wasiguse hawasikii. Nikamwambia mzungu ataona nyoka, anasema, yule nyoka mzuri kweli, halafu atajaribu kumkamata na kucheza naye. Nexti unsikia mzungu kaumwa na huyo 'nyoka mzuri' na kafa. Au anaambiwa asimshike Tembo yule japo anaonekana mpole. Wanaenda kumshika na Tembo anamwua mzungu na mapembe yake.

Hapo yule mzungu alisema, kweli nakubali kuwa kuwa wazungu ambao ni wajinga na hawasikii. Halafu aliamua kuondoka na kjuongea na watu wengine. Na mimi nilishukuru maana hasiri zilikuwa zinaanza kunipanda.

Na mjue zamani kabla wafrika hawajaanza kushinda Marathon mara kwa mara wazungu walikuwa wanasema kuwa waafrika hawawezi kushinda hata siku moja. Walisema eti waafrika wameumbwa kukimbia mbio fupi, lakini mbio ndefu hawawezi!
Sasa mtoto akisikia hizo habari potofu anakuwa nazo. Kama hamjasikia kuna kampeni ya kupiga vita waKenya wasikimbie hiyo Boston marathon kwa vile wanashinda mara kwa mara.

3 comments:

Anonymous said...

pia ungemwelimisha kwamba serengeti ni savanah grasslands na siyo milima na ni tanzania isipokuwa the same uwanda grasslands huo unaextend mpaka kenya ambapo huko hujulikana kama masai mara

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 7:31am, asante. Nilimwambia ila nilishau kuandika kwenye story. Nilimwambia hakuna mlima Serengeti.

Kama alikuwa na akili baasa ya maongezei yale angenda kuangalia National Geographic Channel.

Anonymous said...

Chemi, wazungu siyo wajinga bali ni mashujaa sana hawa watu. "Na ndo maana wametutawala na wanaendelea kututawala".