Monday, September 10, 2007

Poleni Taifa Stars, lakini Mmejitahidi!


MAMBAS (Msumbiji) 1- TAIFA STARS - 0

Hiyo mechi ilikuwa kali na mlijitahidi sana. Mjipongeze kuwa mliweza kufika mbali safari hii!

WaTanzania na wapenzi wa Kandanda tusikate tamaa. Ni kweli moyo unauma, lakini Taifa Stars wameonyesha kuwa na sisi tumo katika ngazi na kimataifa kwa mchezo wa kandanda.

******************************************************************************
From ippmedia.com

Lawama sasa zamwandama Maximo

2007-09-10

By Mwandishi Wetu,

Baada ya timu ya taifa, JK Boys, kuchapwa bao 1-0 na timu ya taifa ya Msumbiji `Mambas` (nyoka wakali), baadhi ya wapenzi wa soka wameanza kumuangushia lawama nzito kocha mkuu, Marcio Maximo.

Hata hivyo, kabla ya lawama hizo kuanza kutolewa, Maximo tayari aliwataka Watanzania kuyapokea matokeo yoyote ya mechi hiyo pasipo kumlaumu yeyote. Wakizungumza mara baada ya mechi hiyo iliyochezwa juzi usiku, wapenzi hao akiwemo Shaaban Alexander `Chama`, amesema kitendo cha Maximo kuwakumbatia wachezaji anaowapenda na kuwapanga uwanjani bila msaada, ndicho kimechangia timu kufungwa.

``Kuna wachezaji ambao Maximo huwezi kumweleza kitu, atawapanga tu ingawa hawana msaada wowote...angalia Joseph Kaniki aliyeingizwa dakika chache alivyochangamsha,`` amedai Chama.

Aidha, amesema haungi mkono kitendo cha kocha Maximo kumuacha mshambuliaji Kudra Omari ambaye amekuwa kinara wa ufungaji mabao katika michuano ya ligi ndogo na ile ya Tusker. ``Sijui ni kigezo gani anachotumia huyu kocha kuchagua washambuliaji, inawezekana anashikwa masikio na watu, afanye kazi aliyoijia nchini bila kuelekezwa,`` amesema.

Naye shabiki mwingine, John Edward `Edu`, amelalamikia kitendo cha kocha huyo kushinikiza timu hiyo kwenda `kutalii` Ulaya wakati kulikuwa na timu nyingi za kiafrika zakuweza kupimana ubavu na JK Boys.

``Hakuwa na sababu ya kupeleka timu Ulaya, au timu za Afrika anaziogopa iwapo zingetufunga...hizo timu walizocheza na Stars Ulaya si lolote hazifahamiki kabisa,`` amehoji shabiki huyo. Tanzania imekosa nafasi ya kuingizwa katika `kapu` baada ya kipigo hicho, huku Senegal wakipanda ndege mwakani kuelekea moja kwa moja Ghana baada ya kushika nafasi ya kwanza kwa kuibugiza Burkina faso mabao 5-1.

5 comments:

Anonymous said...

Tatizo walienda kutalii ulaya. Pia walitembea na malaya kibao. Kabla ya mechi kama hiyo wanatakiwa wakose raha ya ngono kama mwezi moja hivi halafu kweli watakuwa wakali kama simba mwenye njaa!

Anonymous said...

Nilikuwa nasoma hiyo article ya ipp media nilipkutana na neno JK boys nikasikia kukinai fulani hivi. What a crap!! Nani kasema timu yetu nya taifa imesha badilishwa jina? I hate to read it in the IPP media. Waandishi mkibao jiandaeni kuface mashitaka mahakamani kwa irresponsible journalism JK wenu akisha maliza muda wake. Endeleeni kumlamba miguu. Shenzi type.

Anonymous said...

Samahani kutoa haya mawazo, hata bila kuangalia mechi-walioiona watanikosoa
1) Kama Bwana Ismail Aden Rage alivyosema hawa jamaa walivimba vichwa mno-nafikiri kiakili waliathirika. "too much distractions"

2) Pia wanasiasa wanaingilia mno, haya mambo ya kikwete kwenda kuwatembelea siku kabla ya mechi nafikiri yanaondoa focus,

3)pia walikatiwa cheki siku chache kabla ya mechi-je kuna sababu gani ya hawa wachezaji kupewa zawadi ya pesa eti kwa ushindi waliopata miezi kazaa iliyopita

projestus rwegarulila said...

Bi chemponda hujambo?
Napenda kukupongeza kwa jitihada zako za networking hata mie nilikuwa natafuta watanzania kama ninyi ili tuwasiliane na labda nasi hapa ughaibuni tutakuwa na kitu cha kujivunia kama wakenya walivyo na migahawa,club na hata magazeti yao. Kwanini siyo sisi?naomba niandikie rwegap@yahoo.com
au piga simu 3017687965. Tembelea blog ya Rwega.blogspot
Projestus

Anonymous said...

Mnatiwa nini? nyie mlitegemea nini