From my 12/2005 Blog:
Wapenzi wasomaji, leo nimeamua kuzungumzia suala ya matako makubwa. Tafadhali msione kama ni matusi lakini hapa USA ni issue kubwa, maana watu wanayachukia! Nimeona nizungumzie suala ya matako makubwa kwa vile jana kazini, mzungu aliyekondeana mno kasema ni mnene na akila keki eti yote itaenda matakoni. Nilishangaa na kusikitika sana.
Uzuri kwa wazungu ni kuwa na matako fleti kama vile yamepigwa pasi. Sijui kwa nini. Mtu anashepu ya mbao, mwanamke hana hips kakaa kama dume vile eti ndo uzuri. Kumbe ni kwa sababu hao models na wacheza sinema wako hivyo!Basi wasichana na akina mama wanajinyima chakula kusudi wakonde na eti wapendeze. Ndo maana magonjwa kama Bulimia na Anorexia zimeshamiri hapa.
Lakini ukitazama sinema za miaka ya nyuma kama za 1930's na 1940's, wanawake walikuwa na shepu na walikuwa wamejaa na hata wanaume wa kizungu walikuwa wanasifia. Mpaka 1950's kulikuwa na mcheza sinema Marilyn Monroe, alikuwa na zinga la figure 8, na wanaume wote walikuwa wanampapatikia. Ama kweli mambo yanabadilika. Hivi sasa wanasema eti walikuwa ni obese yaani wanene! Mbona mimi naona matako fleti kama chapati ni mabaya na hayapendezi? Au ni kwa sababu nimekulia Africa?
Brothas (waMarekani Weusi) wanapenda mwanamke awe na matako ya maana! Akipita mwanamke mwenye mbarikio utasikia brothas wakisifia, "umm, umm umm!"
Kuna siku nilisikia wanaume wa kizungu wakijadili sababu ya wanaume weusi kupenda matako makubwa, walisema ni "cultural thing". Kwa kweli ni culture yaani utamaduni wa mwafrikai! Kama umekulia katika mazingara ya kupenda kitu utakipenda. Na ndo maana kuna weusi USA wanataka kuwa na shepu iliyokondeana kama mzungu kumbe haiko katika 'genes' zake. Wajitahidi kupunguza mzigo lakini wapi, iko pale pale.
Sisi wanawake wenye asili ya Afrika tumebarikiwa huko nyuma. Yaani boxi, siha, wowowo, booty, na nasikia waGhana wanaita yokohama, matako makubwa yana majina mengi. Waafrika tunaona kama ni urembo, lakini wazungu na waliokulia uzunguni wanaona kinyaa. Wanasema eti ni dalili ya ulafi na uvivu! Lakini kama ni dalili ya ulafi mbona hata mwanamke mwembamba mwafrika anaweza kuwa na kamzigo huko nyuma?
Ubaya mwenye matako makubwa anaweza kubaguliwa kwa vile bosi anaweza kuona kuwa ni 'ugly' (mbaya) na mwenye nacho anachafua mazingira ya ofisi. Kweli kabisa! Hayo matako makubwa ni 'genes' za sisi waafrika. Lakini ajabu kuna siku nilisikia wazungu wakisema eti waafrika tuna matako makubwa kwa sababu ya utumwa. Eti mabibi zetu walinyimwa chakula hivyo matako ndo ilikuwa 'godown' ya mafuta ya akiba. Nadhani ni uzushi kama ile ya ngamia kuweka maji kwenye nundu zake!
Mimi mara nyingi nimeambiwa nina matako makubwa, niyapunguze kwa kwenda gym kufanya mazoezi. Hayo mazoezi haisadii kitu ni makubwa vile vile! Lakini msione kama naona haya, wala! Mtu akiniambia nina matako makubwa namwambia mbona kama ni madogo, na ningependa yawe makubwa zaidi! Wanabakia kushangaa hasa nikiwaambia kuwa Afrika, matako makubwa ni uzuri.Na amini usiamini kuna opresheni ya kuyapunguza inaitwa Liposuction.
Wanawake wengi weusi na wazungu wamefanya hiyo liposuction ya matako, akiwemo mwimbaji Janet Jackson. Ubaya, ni kuwa ukishafanya hiyo liposuction, mafuta yataenda kwingine mwilini, hivyo utakuwa na shepu ya ajabu!Sisi waafrika tunapenda kuringia huo mbarikio wa matako makubwa. Nilipokuwa nacheza ngoma shuleni na jeshini, tulikuwa tunatia nguo ndani ya bukta kusudi tuonekana na matako makubwa kweli kweli! Lakini, mara nyingi mitaani hapa USA, nimesikia akina dada wakifokewa, "You got a big a-s!"
Kuna siku nilikuwa kwenye kituo cha Subway hapa Boston, kapita mama fualni Mganda, aisei alikuwa amejaliwa kweli huko nyuma, mpaka nikaona wivu. Basi ungeona wazungu walivyokuwa wanamtazama kwa mshangao ungecheka. Ila nilishuhudia baba fulani Mmarekani Mweusi akimtazama kwa furaha na kawa kama vile anamezea mate.
Nampenda sana mecheza sinema, Whoopi Goldberg. Nilikuwa nasoma jinsi akienda kwenye audition au akiwa kwenye movie shoot, wazungu wanamwambia kuwa ana matako makubwa au avae nguo ya kuzificha. Yeye alichoka, na mwishowe kusema, " Mimi ni mwanamke mweusi, nina matako makubwa niache kama nilivyo!" Wanawake weusi wote tungedai heshima ya matako kama Whoopi nadhani wazungu wangeheshimu matako yetu makubwa.
Tatizo linigine la kuwa na matako makubwa USA ni kupata nguo. Ukienda kununua sketi au gauni uanweza kukuta mbele refu nyuma umepanda. Au unavaa hiyo nguo lakini kwenye hips na matako haipiti! Hii ni kwa sababu nguo imeshonwa kwa ajili ya wazungu wenye matako fleti. Na kupata Jeans inayofiti ni vigumu. Mtu ambaye atatengeneza nguo 'molded for the black woman' atapata wateja kweli kweli, maana tunalilia nguo kama hizo.
Pamoja na yote haya sasa wazungu wameibuka na staili ya kuwa ka ka-butt. Yaani jeans inakuwa na pedi ndani kusudi mtu aonekana ana matako. Loh! Watu hawaridhiki! Sijui tuseme asante J-Lo (mwimbaji Jennfier Lopez) au nini. Kwanza walikuwa wanamcheka J-Lo na matako yake makubwa lakini naona watu wanaanza kuyapenda. Mpaka kuna opresheni sasa ya kuongeza matako.
Wacha wafanye haitapendeza kama matako natural tulyiozaliwa nayo waafrika.
Matako Makubwa Oyee!

9 comments:
mie nafikiri haya ni maswala ya utamaduni.
Mifano:
1) mzungu ukimuambia kuwa ana matiti madogo, basi ni kuwa umememtukana-wao wanapenda sana boobs-matati makubwa. Nafikiri mnakumbuka siku ile Janet Jackson alivyoonyesha chuchu yake wakati wa super bowl, basi ilikuwa "big deal" . Kwa mtu kama mimi muafrika sikuona kama ni big deal.
Nyumbani matiti makubwa yanaitwa mtindi-wakati matiti madogo yanapendwa (au yalikuwa yanapendwa).
2) kwa sisi waswahili kuonyesha sehemu za mwili chini ya kitovu ni big deal, wakati wazungu sio issue kabisa. Mimi bado huwa nikienda beach za wazungu huwa nabakia kushangaa shangaa, wao ni kawaida mradi umefunika maziwa basi!!!
3) nyumbani ukiambiwa ana matako ya pasi, ni tusi lakini wazungu wao wanaona poa tu au ndio uzuri wenyewe. Kinachoudhi ni kama unaweza kubaguliwa kama una matako makubwa!! Kwa bishara za hollwoood hiyo ni kawaida, kwa sababu sio matako tu, hata ukionekana una-figure, zile ambazo wengine hatuiti unene-bado unaweza usipate kazi.
4) hii topic ya matako naweza kuifananisha na kitambi kwa wanaume-nyumbani ukiwa na kitambi ndio watu wanasema kuwa mambo yake mazuri, lakini wazungu inaonekana kuwa unamatatizo ya kiafya.
ahsante kwa kirudisha hii topic.
Nafarijika mtu au kundi la watu wanapoamua kujikubali.
Ila hata mimi binafsi napenda sana hayo ma YOKOHAMA!!!
Hata kule bongo nakumbuka akipita dada na matako makubwa basii kama mnajadili siasa au soko ghafla network inakata.
Nilitaka kufafanua kwa undani umuhimu wa Tako katika utamaduni wa kiafrika,ila nitasubiri go ahead ya Swahili Times.
Adios
hata mimi nayapenda sana hayo mayokohama
Asante Dada Chemi kwa topic nzuri kama hii...
Hasa ukizingatia ya kuwa huku UK tunaadhimisha mwezi 10 kama mwezi wa watu weusi, na mwaka huu ni muhimu sana sababu ndio imitimia miaka 200 ya kumalizika kwa utumwa. Cha kuchekesha zaidi ni kwamba kuna mjadala katika vyombo ya habari kuanzia majuzi kuhusu cream ya kujichubua, maalumu kwa ajili ya wanaume wa kihindi, cream yenyewe inaitwa " Fair and Handsome". Ndiyo, najua wasomaji wengi watashtushwa lakini kwa kweli hawa wazungu wametutawala sana hasa katika akili zetu, kiasi cha kwamba tuone kila kitu tulicho nacho ni kibaya... Sasa mimi huwa najiuliza mbona huku watu wanatumia hela nyingi sana kununua organics wakati sisi tukiwa na vibustani wanatucheka sana. Huku kuna mzungu amejenga nyumba ya udongo na kuezekwa na majani na wameipa thamani ya £700,000 eti ni organic... Jamani... na sisi tukiwa na nyumba organic?!?!?!
Kwa kifupi hii miili yetu ni organic maana tumeweza kustahimili vingi, watoto wengi hufa kabla ya miaka 5 na tumepata kila aina ya kinga ya magonjwa ya ASILI... Kumbuka AIDS siyo ugonjwa wa asili...
Nakumbuka zamani kidogo nilisoma ya kuwa hata wazungu walikuwa wakipenda watu wenye ma-pistol (hips) sababu kubwa ni kwamba kulingana na uwezo wa matibabu wakati ule(hapakuwepo na uwezo wa kupasuliwa kama vile ilivyo sasa), mwanamke ambaye alikuwa hana wowowo au ma-pistol alikuwa anapata taabu sana ktk kujifungua na kuweza hata kupoteza maisha. Hata ukiangalia wachoraji wa zamani km Picaso utakuta walikuwa wanawachora wanawake wanene wanene tu kuonyesha ndio wazuri.
Miaka miwili iliyopita, tulikwenda bongo kutembea, sasa binti yangu na bibi yake walikwa wakiangalia Miss World,- bahati nzuri binti yangu amejaliwa mwili wa Kiafrika ingali mdogo,wakati huo alikuwa na miaka 10 tu - bibi akawa anamwambia mjukuu wake itabidi uanze diet ili uweze kuja kushiriki kwenye masindano ya uzuri kama hayo... Mwanangu akamjibu, Bibi don't worry, I'll win for sure if they do Miss Africa like your Khanga Party, (Me to that - You go Girl!!!)
I am African and Proud! Cant wait for spring to start, coz from spring all through autmn/fall I wear only designer clothes, mind you African designer only. They are always colourful, airy, fit to measure, and made to flatter african figures...wewee!!! Acha tu!
Mungu awabariki wote,
Lilly.
Nafikiri tathmini yako si sahii kabisa. Tatizo la watanzania wakitoka kidogo wakaenda kwenye kakijiji kamoja huko nje basi kila kitu wanataka kukitazama kwa mtazamo wa hako hako kakijiji. Dunia hii ni pana na kuna mengi mno ya kujifunza. Tembea uone mambo. TAKO kubwa ni sifa kwa mwanamke popote pale. Achana na hizo kasumba uchwara.
Da Chemi yaani umenigusa sana ktk hii article yako. Napenda kusema kuwa hauko peke yako mwenye mtizamo huo. Kwa kukuthibitis hili nimeamua kunakiri maneno yangu mwenyewe(bila ruhusa ya Michuzi)kutoka katika blogu yake. Nilitoa comments zangu chini ya KICHWA CHA CHAKE CHA HABARI MISS EARTH; ANYWAY MIMI SIKUWA NAANZISHA ULE MJADALA WA KAMA RICHA ANAFAA AU HAFAI, KISHA JAMAA MMOJA AKANIRUKIA KUWA MIMI SIJUI HAYO MASHINDANO YA ULIMBWENDE NDIPO NILIPOMKANDAMIZA KWA JINA LA BABA YANGU. NAOMBA RADHI KWAMBA NI MAMBO MENGI NILIYOANDIKA LAKINI NIMEONA NIYAPOSTI NA HAPA KWAKO, WENYE KUFIKIRI NA WAFIKIRI WENYE KUTUONA WASHAMBA NA WASEME; NI MIMI NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO.
ENDELEA SASA UONE.
*****************************
COMMENTS ZANGU NO.1
Tarehe September 21, 2007 6:06:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous
KOKORIKOOOO!!
Hili nalo waulizwe hao waandaaji wa haya mashindano hivi MISI DUNIA sasa anahusikanaje na kuwa nusu uchi au nusu uvaaji? ningefurahi sana angetafutwa dada shujaa zaidi aliyeteitetea DUNIA NA MAZINGIRA YAKE KWA NGUVU NA AKILI ZAKE ZOTE KULIKO WENGINE.
Jina la Sanaa ya kutuletea Taswira za Mabinti namna hii iwe ni ya kumtafuta MISS SEMI-STRIPTEASE!!
Mataifa tunayopinga ukoloni wa kuhusianisha uzuri wa mabinti na kuwavua nguo adharani tuamke sasa, vinginevyo kujadili na kujishebedua eti tuna hasira na wanawake wanaovaa vi micro pico-pico mini-skirts na vitop mjinjo ni UNAFIKI MKUBWA. Maana hata mke wa rais ndiye anakwenda kuwafunda watoto wa watu kujiandaa kuja wakiwa nusu utupu halafu maelfu kwa mamia tunatinga VIP na kwingineko kula chabo tukio linalofafana na mtemi Mswati-wa Infinitive, kasoro tu ni kuwa, Lundenga yeye nadhani haendi nao kwake!
Ni nani aliyesema kuwa uzuri wa mwanamke ni mpaka abaki na chupi?? kwa nini sasa wasivue na hiyo kabisa?? Where are you TAMWA na mtandao wa kulinda haki za jinsia?
Mimi nitamwambia binti wangu sasa awe anatembea na chupi tu na sindiria iliyokatwa kidogo kuanzia makoko hadi mkendo street hadi mkwakwani hadi Kariakoo Dar na mtu aje amguse aone nitakavyomshughulikia kisheria kwa kosa la kumzuia Miss mtarajiwa akiwa MAZOEZINI.
SIPENDI KUTAWALIWA TENA NI MIMI NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO
*********************************
COMMENTS ZA MVAMIZI KWANGU
•Tarehe September 21, 2007 12:15:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous
Wewe (Anonymous wa Tarehe September 21, 2007 3:38:00 AM EAT, ) unaweza ukawa sio muelewa mzuri wa haya mashindano. Hakuna mtu anaye lazimishwa kuvaa chupi unaambiwa uvae vazi la ufukweni. Sasa kama wewe kwenu huwa unavaa vitenge au suti ukiwa ufukweni hakuna mtu atakaye kushangaa kwani ndio utamaduniwenu. Watu wanao vaa vichupi wakiwa ufukweni ndio wanao vaa hivyo kwenye mashindano na ndio maana kuna kuwa na mavazi ya jioni pia. Je wewe ukitoka jioni kwenda kwenye shufhuli au hafla unavaa traksuti?
tuwe waungawana sio mnato malalamiko bila kujua Mchezo wenyewe.
********************************
COMMENTS ZANGU NO.2
•Tarehe September 24, 2007 6:14:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous
WE MWANADAMU WA 21/9 12:15
UNAYEJIDAI KUSOMESHA WATU JUU YA MASHINDANO HAYA NA KUHUSU VAZI LA UFUKWENI HUJANISOMA VEMA KUHUSU CHANGAMOTO YA UNUSU UCHI. KWA HIYO KAMA NI HIVYO KWA MAELEZO YAKO VAZI LA HUYU 'MTANZANIA ASILIA'LA KWENDA UFUKWENI NI CHUPI???? NDO MAANA WATU WANASEMA SI MTANZANIA BASI MAANA WATAZANIA HATA HUJIFUNIKA KAKANGA HIVI!
USITAKE KUTETEA VITU KAMA HUJUI KINAELEZWA HAPA.
PILI TUNAPOLETEWA PICHA HII SASA JE KUSUDI NI KUONYESHA VAZI LA UFUKWENI AU NI KUMTANGAZA.
JE KULIKUWA NA ULAZIMA KUJITANGANZA KWA KACHUPI?? MBONA SIKU HIYO ALIVAA MAVAZI MENGI AMBAYO YALIWAVUTIA WATU ZAIDI LA HILO?
TATU KAMA SUALA NI KUONYESHA VAZI LA UFUKWENI BASI MTU ATAINGIA NA VAZI HILO AMENINGÍNIZA KWENYE 'HANGER'!!
MPAKA KESHO, SUALA LA MJADALA WA KUONYESHA VICHUPI AU VIKANGA AU VIKOI N.K NI DEBATABLE KATIKA ANGA ZA JUU ZA MEDANI YA FANI HII. FANYA ASSIGNMENT ZAKO KATIKA BEAUTY PAGEANT STATS NA KATIKA ACADEMIC PAPERS WALIZOANDIKA WENZAKO WANADHUONI JUU YA SUALA HILO KABLA YA KUKURUPUKA NA KUFIKIRI KUWA NI ISSUE YA USHAMBA AU ETI MTU KUTOJUA MASHINDANO HAYA. HII NI FANI NA NI TAALUMA THAT WILL CONTINUE TO BE SHAPED TO UNCOVER UNNECESSARY BURDENS! HATA SUALA LA WEMBAMBA LINAJADILIWA SANA NA MPAKA SASA AKINA DADA ZETU WAMESHAONYWA KUWA WALE WANAOPEPESUKA NA UPEPO WATATUPWA NJE!! NA BADO USIFIKIRI MCHEZO; SWALI ZA MZURI NI NANI LAZIMA LIWE TOFAUTI NA SUALA LA NANI AMEVAA AU AMETENGENEZA VAZI ZURI, UPO HAPOO WEWE MSHAMBA.
NITAJIE CHUO CHAKO NIJE NIWAPE WALAU VIONJO VYA ADV. LECTURE OF MA. DEGREE IN MODELING, PEGEANTOPOLIS & MISSOSOLOGY (Hakuna cha bure Lundenga awalipie fee!) .
HAKUNA UBISHI KWAMBA MASHINDANO HAYA BADO YANA CHECHE ZA UKOLONI NA AU UTAMADUNI WA SEHEMU FULANI ZAIDI KULIKO WENGINE.
DID YOU KNOW THAT MISS WORLD STARTED AS THE FESTIVAL BIKINI CONTESTS & THAT MISS WORLD CHAIRPERSON JULIA MORLEY SCRAPPED THE SWIMSUIT COMPETITION FROM THE FINALS IN 1998 AND SHE SAID THAT BEACH WEARS MUST BE WON ON BEACHES ONLY?
NDUGU YANGU ACHA UJUVI MWOLOLO WA KUWAFIKIRI WADAU WA HII BLOGU ETI WOTE NI WASHAMBA AU KWAMBA HATUJUI TUNACHOANDIKA, UKILETA HAKO KASOMO KA BIKINI SCIENCE, G-STRINGOLOGY HATA WET -TSHIRT COMPETITIONS MBONA UTAKESHA HAPA MAANA HAPO UTATAKIWA UNIVUE 'Doctoraal' YANGU!!
NAKWAMBIA KUWA BADO YAKO MASWALI MENGI SANA JUU YA VIGEZO VYA KUMPATA MISS WORLD NA SASA TUNATAFUTA KUFUTA HIYO BEACH BEAUTY MAANA WENGINE TUNADAI IWEPO NA KITCHEN BEAUTY NA FARM BEAUTY N.K. KAMA SOMO HILI BADO HALIJAKUKUNA BASI KAULIZE KWA NINI HATA TZ PALIANZISHWA MISS BANTU??
HUWEZI KULAZIMISHA WATU WOTE KUKENUA MENO WAKATI MIFUPA ISIYO NA NYAMA INASUGUANA KAMA VILE HAINA MAFUTA MLAINISHO!! BINTI MREMBO KWA WENGINE NI YULE AMBAYE UKIMWANGA MAJI MGONGONI LAZIMA YATUAME KIDOGO NA SIO KUPITILIZA AU KWA MAELEZO MENGINE KIMWANA NI YULE MWENYE SIFA YA KUMBEBA MTOTO MGONGONI HATA BILA MBELEKO!
Kaka Michu tafadhali rusha hili gazeti langu likiwa ni somo la III kwa waosha toka kwangu,
Ni mimi, Nyakatakule Unyilisya Echalo
Hayo sio matako,mwanamke amezeeka na ana sura mbaya kama fisi.Matako ni yaleeeeee uliowekaga siku zileeeee demu mcheza tenis.Hii picha umenitia kichefuchefu ile mbaya.Yaani nilipoona marudio ya matako makubwa nilikimbilia ile mbaya lakini niliishiwa na hamu mara moja.
Wape salam wazee wa Boston hasa mbunge wa kutarajiwa wa mkuranga,mwambie baba yake alikua gavana mpaka leo katasi zimekataa?Maana amebakia story tu na email nyingi lakini haji nyumbani
Dada Chemi,
Hebu weka picha yako inayoonyesha jinsi 'ulivyojaaliwa'. Tuna hamu ya kuona 'mzigo' wako!
Wagiriama wa Pwani ya Kenya huoongeza matabara kusudi wawe na nyuma kubwa. Wenyewe wakiita 'Mahando'. e wasomali huongeza chochoe au ni hulka yao?
Post a Comment