Saturday, September 01, 2007

Aibu! Senator Ajiuzulu baada ya kufanya mambo ya kishoga chooni!



Makubwa! Kumbe huko chooni kwa wanaume kuna mambo. Ukiona mwanaume anagonga gonga mguu, au kupitisha mkono wake chini ya kitenganisho au kucheki nani kakaa kwenye choo ni ishara za kishoga!

Bila shaka mmesikia kuwa Senator Larry Craig, wa Idaho amejiuzulu leo baada ya skandali iliyompata. Akiwa safarini alipatwa na nyege choo huko kwenye uwanja wa ndege ya Minneapolis Minnesota. Sasa akawa anamtafuta mtu wa kumridhisha. Alidhani kampata kumbe anaopoa polisi aliyevaa kiraia! Polisi huyo alimkamata na Senator Craig alikiri mashtaka dhidi yake na kulipa faini na kukwepa kufunga jela. Alikiri kwa vile alidhani mambo yataisha pale. Kumbe kuna gazeti iliyokuwa inasaka habari zake. Ndo hao waliotoa habari za maovu yake na kukamtwa kwake huko Minneapolis.

Kichekesho zaidi, alidai kuwa aligonga mguu wa huyo polisi aliyekaa choo cha pili kwa vile, akisimama kukojoa anapanua miguu sana. Waandishi wa habri walifanya majribio na kuona haiwezekani hasa kama umeshusha suruali kwenye magoti!

Hayo mambo yapo sehemu nyingi hapa Marekani, lakini kitu ambacho nimechukia kuhusu Senator Craig ni kuwa ni Mnafiki mkubwa! Nasema ni mnafiki kwa sababu alikuwa anakashifu mambo ya kishoga na kupinga mambo ya ndoa za wasenge, na kujidai ni mtakatifu. Kumbe yeye ni moja wao. Hivyo yule shoga aliyejitokeza na kusema kuwa alifanya mapenzi na Senator Craig chooni Washington D.C. mwaka jana hakuwa mwongo.

Na mjue kuwa Republicans wenzake walimlazimisha kujiuzulu maana ni aibu kubwa, na hawataki kukosa kura kwenye uchaguzi ujao. Haya Senator Craig, sasa mambo yako wazi, hivyo vaa gauni, sidiria, na wigi na ufanye unavyotaka. Mambo yako hayako kwenye closet tena.

Kwa kweli lazima tuwahurumie familia yake, maana kwa hapa Marekani ni kashfa nzito. Ana mke, watoto na wajukuu.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.cnn.com/2007/POLITICS/09/01/craig.arrest/index.html


http://www.iht.com/articles/2007/09/01/america/31cndcraig.php


http://seattletimes.nwsource.com/html/politics/2003858123_craig29.html

5 comments:

Anonymous said...

Hebu nieleweshe vizuri dadaangu hivyo vyoo vilikuwa viko separated au vyoo vya wanaume ambavyo wanaonana? na alimgonga miguu akiwa na nia ya kumuomba yaani ni ishara za mashoga au asipanue miguu zaidi?

Anonymous said...

Jamani Jamani ushoga siupendi kwa dhati ya moyo wangu lakini have you ever asked your self mtoto wako akikuambia yeye ni shoga utafanyaje? utamfukuza, utamtenga?? kama ni mume thats a different story mtoto wa kuzaa mwenyewe. nina mtoto wa kiume ninamuomba mungu kila siku amuepeushe na balaa hilo lakini kumtenga hakusaidii sana sana kuwa karibu naye kunaweza kumbadilisha arudi katika hali ya kawaida. ukiangalia historia zao wengi wamekuwa hivyo bila wao kupenda na sistoshe mbaya zaidi wamesababishiwa na wanaume wenzao either baba zao ndugu zao jirani nk. kuruhusu kuoana si jambo zuri hata mimi nalipinga kwa sababu kuhalalisha kosa ndio kosa lenyewe kubwa kabisa.

Anonymous said...

Nimezisoma pamoja na hizo interviews zote, inaelekea hiyo kesi wamembambikia. Mtu pekee aliyemwona ni huyo polisi mmoja tu. Ni rahisi sana kupanga mtu kama huyo amtungie mtu mashtaka. Inaelekea wasenge walichukizwa na msimamo wa huyo mzee wakaamua kumfanyizia. Hapo kukiri mashtaka jamaa wamembana na yeye kwa kudhani akifanya hivyo yataisha(kila mara walikuwa wanamtishia na media, na hiyo inaweza kumvuruga sana mtu hata kama hana makosa). Yaani wamemuumiza sana mzee wa watu, lakini nadhani akijitetea vizuri anaweza akajiondoa kwenye aibu ya usenge, lakini useneta keshaukosa. Mbaya kweli!

Anonymous said...

Bush is goin down,damn,it's like every week the Repubs are lookin more n more like Clowns.

Anonymous said...

huyu Jamaa mpuuzi, wacha aondoke-tatizo lake eti alikiri mashtaka akidhani kuwa mambo yataisha. Mambo ya ushoga pembeni, sijawahi kuona senator mjinga kama huyu!!