Thursday, September 27, 2007

Rest in Peace Mzee Godwin Kaduma (1938-2007)

Hapa Mzee Kaduma anajadili mambo ya filamu Tanzania.


Nimepata habari za kusikitisha sana. Mzee Godwin Kaduma amefariki dunia. Nilikuwa namfahamu miaka mingi sana, alikuwa na kipaji ya ajabu katika usanii. Ninalia. Mungu Amlaze mahali pema mbinguni. AMEN.

*****************************************************************************

Dear Friends,

Mzee Godwin Zilaoneka Kaduma is no longer with us. Godwin Kaduma passed away at the Muhimbili National Hospital this afternoon the 27th September 2007 due to a severe stroke. I will update you with the funeral arrangements once I get information from relatives. May God rest him in eternal peace!

Ghonche Materego.

CEO - EATI
27th September 2007

************************************************************************
Habari za kusikitisha zilizotufikia ni kwamba gwiji la sanaa za maonyesho nchini Tanzania Mzee Godwin Zilaoneka Kaduma hatunaye tena duniani.Habari hizo zinazidi kupasha kwamba mauti imemfika Mzee Kaduma katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa ajili ya matibabu zaidi.Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza(stroke).

Msiba upo nyumbani kwake Bagamoyo jirani na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo. Heshima za mwisho kwa walio Dar-es-salaam zitatolewa kesho (Ijumaa) saa nne asubuhi habari zaidi zinasema heshima za mwisho kwa marehemu mzee Kaduma kwa walio Dar es salaam zitatolewa kesho saa nne asubuhi hospitali ya Muhimbili kabla mwili wake kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Bagamoyo na kisha baada ya kuagwa saa nane mchana utapelekwa kijijini kwake Itamba, Iringa, kwa mazishi.

4 comments:

Anonymous said...

Mzee wetu mpendwa,Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahala pema peponi,Amina.

Tunawaombea ndugu,jamaa na marafiki wawe na nguvu katika kipindi hiki kigumu tulichonacho cha majonzi.

Pumzika kwa amani.Amina

Simon Kitururu said...

R.I.P KADUMA!
Nasikitika tu kuwa Wazee wetu kama Kaduma, watunzao sanaa ya kitanzania, yenye asili ya Kitanzania , hawajulikani sana kwa wadau wadaio wanapenda utanzania na sio Miss Tanzania ambay asili yake si ya Kitanzania.

Mzee Kaduma , Hukwe Zawose ,na wote wengine, wengine tutajaribu kufuata nyayo zenu kutunza sanaa ya Kitanzania. Ingawa sasa hivi sanaa ya bongo ya asili, wengine wanaamini ni Ngwasuma na Bongo Fleva.

MIMI binafsi, nitafuatilia angalau Bagamoyo tuwe hata na Nguzo fulani iwatajao wewe na,,Hukwe Zawose, akina Morisi Nyunyusa na wote waliotumia nguvu yao kujaribu kukuza na kutunza utanzania katika sanaa ingawa bado tumemezwa ...
R.I.P Kaduma!

mloyi said...

Mzee wetu ametutoka, tumebaki na masikitiko ya upweke.
Chemi, samahani kwa kutoka nje ya mada, kuna picha nimezikuta mahali, zilipigwa terehe 2 dec, 1962, kama nimekumbuka sawa. Napenda uzione. nitazi-scan nikuwekee mahali uzipitie. surprise but realy, kama mlizipoteza utapata kumbukumbe moja kabambe.
Mloyi.

Chemi Che-Mponda said...

Mloyi,

Nitashukuru kama utanitumia. Nitazibandika kwenye blogu.

e-mail: chemiche3@yahoo.com

Asante