Wednesday, September 19, 2007

Sinema mpya - Pink Panther 2 - Nimo!




Jana nilifanya kazi kama background extra katika sinema ya Pink Panther 2. Stars wake ni Steve Martin, Jean Reno, Andy Garcia na Aishwarya Rai.

Sehemu kubwa ya hiyo sinema inapigwa mjini Boston. Boston Convention Center iligeuzwa kuwa uwanja wa ndege ya Charles De Gaulle -Paris. Set ilikuwa safi sana utadhani uko Ufaransa kweli, ila watu walikuwa wanaongea English.

Mimi nilikuwa Msafiri wa kiAfrika pamoja na akina mama wengine watatu. Niliambiwa niijifanye nimechelewa ndege halafu nikimbie ndani na kukutana na hao wengine walio kuwa ndani. Mbona extras wengine walinionea wivu! Ujue kupewa 'direction' katika sinema ya Hollywood kama wewe ni extra ni kitu kikubwa. Nangojea kuona kama nitaonekana kwenye sinema au vipi.

Steve Martin alinipita mara kadhaa. Alikuwa na make-up nyingi usoni, kiasi kwamba alionekana kama kavaa mask. Kwa vile ni star, alikuwa na stand-in na stunt man. Stand-in anafanya kazi wakiwa wanafanya scene set up. Stunt man anafanyakazi kama kuendesha gari ovyo, kukimbia, kuruka ukuta nini. Ama kweli wanatumia hela nyingi kwenye sinema za Hollywood. hako kagari kadogo kalikuwepo. Watu walikuwa wanapita barabarani na kuishangaa.

Bahati mbaya walitupiga maaruku kupiga picha za kumbukumbu.

Kwa habari zaidi za sinema ya Pink Panther 2, nenda:


13 comments:

Jaduong Metty said...

Chemi,

Go Chemi! Go Chemi! It's your birthday! Natania. Unajua nini? Ukiwa na usongo na kitu, usikate tamaa. Nakupa pongezi kwa sababu unanyemelea destiny yako.

Chemi Che-Mponda said...

jaduong metty,

Asante sana. Ama kweli najifunza hii Hollywood Business. Naomba scwene yangu isiishie kwenye cutting room floor.

Simon Kitururu said...

Da Chemi , Moto huo huo. Wakikata hii kuna ambayo wewe ndio utakayekuwa Staa

MOSONGA RAPHAEL said...

Hongera sana Chemi, nimefurahi kusikia habari hii njema.
Haya ni mafanikio ya kujivunia si wewe pekee tu bali wa-TZ wote.
Iko siku utafanya makubwa zaidi ya hili na kuwa balozi wetu huko H/wood!
Kila la heri ...

Anonymous said...

hongera Da Chemi,
siku moja tutasikia umefika mbali-nafikiri hata kupata hiyo background sio mchezo

Egidio Ndabagoye said...

Da Chemi,
Lazima tukupongeze hata kama wakikata scene yako.Next time tutaluona red carpet

Kibunango said...

Hongera sana... umenipa hamu kubwa ya kuisubiri hiyo Pink Panther 2... Nipate kukuona na kulupukushani za kuchelewa ndege...

Anonymous said...

da chemi,
Hivyo vigali vidogo viko kibao hapa Uholanzi na vingine ni vya walemavu. Ni vizuri ktk mapambano ya packing!

Anonymous said...

jipe moyo utashinda!! Extraaaaa

Chemi Che-Mponda said...

Asanteni wote. Kwa kweli kwa sasa kazi za Extra ziko nyingi hapa Boston. Wanapiga sinema za The Bachelor 2, The Women, na Pink Panther 2, na mweza Novemba sinema zingine zinakuja.

Ila kuchaguliwa na kupewa direction ni kitu kikubwa badala ya extra unaitwa 'featured extra'. Hatua inayofuata ni kuwa 'day player'.

Anonymous said...

loh hongera sana tena sana, !!! big achievement !!! i really admire you !
hongera kwa moyo woooote, mdau from tanzania sinza kwa wajanja

Anonymous said...

chemi hongera sana si kwa sababau eti umepata nafasi ya kucheza ktk sinema ya holiwud kama extra no!
kwa sababu tuu unathubutu(sijui kama silabi ni sahii hapa)
na walau unajuhudi za kufuatilia na kujishughulisha katika passion yako.safi sana.wapo wengi saana wamrekani wenyewe huko holiwud wanfanya waiting (migahawani ) miaka nenda rudi na bado hawapaiti nafasi hata ya extra tuu kwenye BIG PRODUCTION ya FEATURE FILM wanaishia kwenye vikomesho vya studio ndogondogo tuu
hivyo nakupa changamoto wala usikate tamaa kuwa a BEATIFUL full figured woman kama wewe ulivyo ina nafasi yake na bado inahitajika wengi it may not necessarily be kwenye lead lakini kwenye nafasi nyingi ambAzo ni key
tena nakupa pongezi kama utaonekana kama extra kwa sababu wewe unafahamu vema kwamba hollywood big budget productions wana shoot several takes, tens of thousands of film feet! na baada ya hapo zinfanyiwa editing ya nguvu ya kuondoa zile amabazo hazileti muendelezo wa hadithi na zile amabzo kiufundi haizfai
hivyo basi kama wewe ni extra na umecheza vizuri convincingly na ukabaki kwenye release copy dada yangu nakupa hongera who know! kuna siku itakuja utapata nafasi muhimu zaidi na ya kukunufaisha zaidi kimapato,ki-talent na kiajira ya sinema
mimi pia nilishiriki kama extra ktk mall moja WEST EDMONTON MALL hapa edmonton ,mimi na my daughter tulirub shoulders na patrick shweiz na electra carmen
na tulilipwa dola 12 ya canada nilipaswa kumbeba binti yanagu mabegani tukijifannyia shopping ktk duka la nguo za wasichana jina la sinema ni CHRISTMAS IN THE WONDERLAND takes zilikuwa nyingi saana of the same scene na sina uhakika kama nitakuwepo kwenye final copy
but mostly nilikuwa naenda kujifunza na kuchunguza mambo ya teknikali behind the scenes mimi sina kipaji cha acting any way!
chemi kaza buti na wala usichoke
hata usipofanikiwa huko marekani kumbuka nyumbani tz tunakuhitaji sana !
hongera hongera
Raceznobar

Chemi Che-Mponda said...

Raceznbar,

Asante kwa maoni yako na kunitia moyo. Doh! Ulilipwa dola 12 za Canda kuwa Extra? Kumbe ndo maana hizi sinema za Hollywood wanapenda kupiga film Canada.

Kwa sasa hivi non-union wanalipwa dola $75 US na Union wanapata mara mbili ya hiyo. Day Player wanalipwa mara 10 ya hiyo ya Union Extra!

Kwa kweli hii ni sinema yangu ya tatu ya Hollywood. Zingine nilizofanya ni Gone Baby Gone (mimi ni Restaurant Customer), 21 (inatoka mwakani, mimi ni Mhudumu wa hoteli), na hii sasa ya Pink Panther 2. Pia kwenye TV History Channel nimecheza kama Mtumwa katika Aftershock. Ukisearch hapa kwenye blog utaona picha na trailer.

Kwa kweli hii kazi lazima uwe na moyo na hizi za holyywood ndo kabisa maana mnapiga take 20 na zaidi! Nimeona extras wengine wakiondoka kwenye seti kwa kuchoka na kusema hawarudii tena. Ni kazi kwa kweli.