Thursday, September 13, 2007

Ramadhani Njema


Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umefika. Nawatakia waislamu wote Ramadhani Njema.

********************************************************************************
Nimepata salamu hizi za Ramadhani kwe e-mail:

Asalaam alaiykum,

Mimi ni RAMADHANI, Nilimpa ujumbe Rajab akuletee, Nikamtuma na Shaaban akuambie kuwa nipo njiani.

NAKUJA na mke wangu SWAUMU na watoto wetu watatu: 1.Rhma, 2.Maghufira, na3.Tauba. Pia sijamuacha rafiki yangu wa damu QURAAN, na ndugu yake QIYAMU LAIL.

Sitokaa nawe kwa muda mrefu, nitakua nawe kwa mwezi mmoja tu, ukisha tutaondoka kumpisha, EID -EL-FITRI na hatimae Sitat – Shawwal, ambao watawasili kwa kupishana.
Utupokee kwa mapenzi yako yote, na ututunze kwa kipindi hiki kifupi kwani tukiagana huna uhakika wa kutuona tena mwakani.

RAMADHANI MUBARAK !!

“Enyi Mlioamini! Funga ya Ramadhani imefaradhishwa kwenu kama ilivyokafaradhishwa kwa wale waliokuwa kabla yenu ili mpate tauba” (QURAAN Surah Al-Baqarah 2:183) (Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumchamungu)

Nakutakia maandalizi ya funga njema ya mwezi mtukufu wa Ramadhan…shahar tauwba..

M.M. Juma

No comments: