Saturday, October 27, 2007

Madereva waongea kuhusu ajali za Viongozi Bongo

Ukiendeshwa na dereva unaweka maisha yako mikononi mwake.

Miaka ya 80' kuna Prof wa Chuo Kikuu alikuwa kwenye ziara mikoani kukagua wanafunzi wake. Huyo Prof. alikuwa na briefcase imejaa malaki ya pesa. Ile gari land rover ilipinduka, Prof aliumia vibaya na pesa zile potea. Hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi ya yule dereva. Sasa kuna siku nilikuwa kwenye warsha sehemu za Kurasini. Kulikuwa na kundi la madereva wa wakubwa nje. Nilikuwa karibu nao. Nilimsikia yule dereva aliyekuwa na yule Prof. akitamba mbele ya madereva wengine jinsi alivyopindua ile gari na kuiba zile pesa! Yule dereva naamini alikuwa na matatizo ya akili maana hakuna mwenzake aliyesema kitu bali walimtazama kama yeye ni mwendawazimu.

Kweli madereva wa chunguzwe kabla ya kupewa kazi ya kuendesha mtu.

******************************************************************************

From Gazeti la Mwananchi:

Madereva wajitetea juu ya za ajali za viongozi

Frederick Katulanda, Mwanza

WAKATI taifa likiomboleza kifo cha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia aliyefarika katika ajali juzi mkoani Iringa, baadhi ya madreva wameeleza kuwa ajali nyingi zimekuwa zikiwakumba viongozi wa serikali zinatokana na baadhi yao kutoawajali madreva wao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana mjini hpa, baadhi ya madreva hao walisema ajali nyingi zimekuwa zikiwakumba viongozi kutokana na baadhi yao kuwafanyaisha kazi madreva wao wakiwa na njaa, usingizi, mawazo na hata matatizo ya kifamilia.

Akielezea ajali hizo dreva wa CCM mkoa Adamu Sudi, alisema kuwa viongozi wamekuwa wakiwatumia madreva bila ya kuwajali jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao kwa vile dreva kuendesha akiwa na njaa inaweza kusababishia ajali na hata kupoteza maisha.

"Mfano tatizo linaloweza kusabaisha ajali kwa viongozi ukiondoa uzembe wa madreva, ni viongozi kutowajali madreva wao, huwezi kuendeshwa na dreva mwenye njaa, ama unamfanyika kazi hadi usiku wa manane na kisha untaka alfajili akuendeshe, anahitaji kupumzika," alisema.

Dreva James Lisalaka alisema huku akitoa mfano kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwaangali madreva wao kama watu wasio na maana wakati wamekuwa wakilinda maisha yao katika safari na hivyo kusema kuwa wanapaswa kuwaangali na kujali afya zao.

"Madreva wanapokwenda safari baadhi ya viongozi wamekuwa wakishindwa kuwalipa hata posho, hatua ambayo imekuwa ikiwafanya baadhi yao kuishi katika mazingira magumu, wengine kulala katika magari, kushinda njaa," alisema.

Wamesema kuwa baadhi ya viongozi pia wamekuwa wakichukua madreva wasio na uzoefu mkubwa kutokana na kuwalipa gharama kubwa na matokeo yake kusababisha ajali.

No comments: