Monday, October 22, 2007

Tahadari mnaotaka kununua magari ya South Africa


Nimepata hii habari kwa e-mail. Imeandika na Dr. Anthony Masaka.

************************************************************************

Dear all,

Nimeona kwenye taarifa ya habari( ya ITV ya jana usiku) na magazeti jinsi wabongo 'walivyonunua' kesi za wizi wa magari ya south Africa.

Nafikiri sio mbaya kuelezana( kwa wasiofahamu) kamchezo fulani wanakofanya hawa wenzetu wa SA juu ya magari.

Hawa jamaa wa-SA, wanauza magari yao wenyewe kwenye agents(makampuni ya huuzaji na ununuaji magari), ili huwa ni 'deal' kati ya muuzaji(mwenye gari) , mnunuaji(kampuni) , na "corrupt polisi".

Ishu ni gari litauzwa kwa mteja wa nchi ya nje anayenunua gari SA( through kampuni ya uuzaji magari),likishauzwa na kuvuka boarder tu , mwenye gari anaenda polisi ku-report gari limeibiwa!!, anapewa polisi report, gari linatafutwa, insurance yake inamlipa( that means kauza gari mara2!!). au mengine yameibiwa SA,yanabadilishwa namba na rangi na kuvushwa nchi nyingine( Botswana, Zambia,Namibia, Angola etc hata Tanzania).

Kisheria ukinunua gari lolote kabla hujalisajili au kubadilisha Card, lazima upate clearance ya interpol . Kwenye nchi nyingi za Afrika tunatumia CID , wanaweka chasis number kwenye mtandao wa interpool, baada ya 36hours linakuwa cleared.

Nchi kama Botswana na SA huwezi kulipia ushuru hadi clearance ya interpol.

Process hizi huwa zinarukwa na baadhi ya watu au police wanahongwa au uzembe wa polisi kutohakiki gari interpol na kutoa clearance certificate.

Baada ya muda ndio mambo yanaibuka!!, unaambiwa gari liliibiwa miaka kadhaa iliyopita!!! Wakati wewe umenunua kihalali!! Na papers zote unazo!!

Linarudishwa kwa mwenyewe( wa SA), na wewe kununua kesi!! Unaambiwa kama una madai au swali uliza kwa aliyekuuzia, na kwa sasa wewe ni mtuhumiwa hadi ushahidi ukamilike!! Nafikiri ndio yaliyowapata baadhi ya ndugu zetu.

Na ndio maana kuna magari kama Benzi, BMW X5, Pajeros, RAV4 etc nyingi za ki-south ambazo zinauzwa bei nafuu!!,unaweza kupata X5 hata kwa 5mil tzsh , ni kamchezo ka wajanja tu!

Watu wengi wakinunua haya magari(bila kujua)wanakimbilia kwa mawakili ambao uthibitisho wanataka Card ya gari,unalipia, linakuwa lako!! Umeshanunua kesi!!

Take care.

Ishu hii nimepewa na jirani yangu m-SA, ambaye kamchezo haka amekafanya mara2.

Dr.A.A Masaka.


No comments: